data:post.body Oktoba 2021 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA PINGILI ZA MGONGO NA MATIBABU YAKE.(ANKYLOSING SPONDYLITIS)

 Ankylosing spondylitis ni ugonjwa unaoshambulia mifupa ya uti wa mgongo kwa kuifanya mifupa ya mgongo kushikana na kua na ugumu badala ya mifupa hiyo kuachiana nafasi kama inavyotakiwa kua. Ugonjwa huu huwapata zaidi vijana na wazee lakini waathirika ni wanaume zaidi kuliko wanawake.

                                                          


Dalili za ugonjwa huu.

maumivu ya mgongo; Mgonjwa hua na maumivu makali sana ya mgongo ambayo hupungua kwa kufanya mazoezi ya hapa na pale na huongezeka zaidi kwa kukaa tu bila shughuli yeyote, maumivu hua makali zaidi asubuhi kuliko jioni na pia maumivu huweza kusambaa sehemu ya makalio mpaka miguuni na kuleta ganzi sababu ya kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu. Dalili hizi huja na taratibu na kuendelea kwa kipindi kirefu, kwa watu wengine dalili hizi huweza kuja na kuondoka lakini kwa watu wengine dalili hizi huendelea kua kali muda unavyozidi kwenda.

Maumivu ya joint zingine za mwili; ugonjwa huu huambatana na maumivu mengine ya joint zingine za mwili kama za miguu na nyonga na maumivu haya hutokea zaidi wakati wa kuhamisha joint hizo.

uchovu wa kupitiliza; Hii nikawaida kwa ugonjwa huu kwamba mgonjwa anakua mchovu sana na kushindwa kufanya kazi.

Ugonjwa huu pia huja na dalili za kushindwa kuona vizuri na kushindwa kuvuta hewa kwa nguvu sababu ya maumivu ya mgongo.


Chanzo cha ugonjwa huu.

Haifahamiki chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu lakini ugonjwa huu umehusishwa na mambo yafuatayo.

urithi; Kama wazazi wako wana tatizo hili basi na wewe una nafasi kubwa sana ya kupata ugonjwa huu sababu tafiti zimeonyesha kwamba ugonjwa huu unafuata koo.

Human leukocytes antigen; Tafiti zinaonyesha kati ya watu kumi wenye ugonjwa huu, tisa wanaubeba ugonjwa huu. Kama una antigen hii haimaanishi kwamba utaugua ugonjwa huu lakini una nafasi kubwa sana ya kuugua ugonjwa huu.


Vipimo vinavyofanyika;

Mara nyingi vipimo vinavyofanyika kugundua ugonjwa huu ni X ray, Utrasound na MRI lakini pia vipimo vya damu kupima human leukocytes antigen huweza kufanyika japo sio kipimo cha kutegemea sana.


Matibabu;

Hakuna matibabu ya kuutibu ugonjwa huu mpaka ukapona kabisa lakini kuna matibabu ya kupunguza makali na kumfanya mgonjwa aishi maisha ya kawaida kama watu wengine kwa kutumia dawa za maumivu, virutubisho vya mifupa na dawa za kurelax misuli ya mgongo.

Matibabu mengine yasiyohusisha dawa na mazoezi binafsi, mazoezi kutoka kwa wataalamu kama physiotherapy, hydrotherapy yaani kutumia maji ya moto kukanda au kuoga kusaidia mzunguko a damu na mishipa ya fahamu, kupunguza uzito kwa watu wanene, na kunyoosha mgongo wakati wa kutembea. Wazee wengi wakiafrika hupinda mgongo na kutembea kwa fimbo kwa kukwepa maumivu makali ya kunyoosha mgongo na wengi hufariki bila kutibiwa.


Mara nyingi wagonjwa wengi hupata nafuu kwa matibabu ya dawa tu lakini kwa hali ikiwa mbaya zaidi yaani maumivu makali na mifupa kuharibika zaidi basi upasuaji hufanyika kuleta nafuu ya ugonjwa huu. Katika hatua kubwa kabisa za ugonjwa huu, ugonjwa huweza kusababisha kupata ngazi sana, kushindwa kuzuia mkojo na choo kubwa na kushindwa kutembea kabisa kitaalamu kama cauda equina syndrome.

                                                       STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                             0769846183/0653095635

FAHAMU TATIZO LA KUKABWA NA JINAMIZI WAKATI WA KULALA LA MATIBABU YAKE.(SLEEPING PARALYSIS)

Watafiti wa usingizi wanasema kwamba mara nyingi kuhisi unakabwa na jinamizi na kushindwa kuinua hata kidole wakati wa kulala ni dalili kwamba mwili wako umeshindwa kufuata hatua za usingizi wa utaratibu maalumu, mara chache huweza kua sababu ya magonjwa ya akili.

                                                             


Kwa vizazi vingi hali hii imekua ikihusishwa sana na uchawi, majini na mashetani kwenye jamii mbalimbali na baadhi ya watu wenye imani hukemea kimoyomoyo kwa imani zao hali hii ikiwakuta lakini wataalamu wanaamini hali hii haina mahusiano na mambo giza..

Hali hii inatokeaje?

 Katika hali ya kawaida wakati mtu anasinzia mwili wote hulegea kwanza na kuishiwa nguvu kisha anapotelea usingizini lakini katika hali isiyo ya kawaida mwili unalegea na kuishiwa nguvu lakini ubongo unakua bado uko macho. wakati huu unakua hujiwezi kwa chochote, unahisi kuna mtu yuko chumbani kwako, unahisi kukabwa na kusukumwa kwenda chini na unakua na hofu kubwa.

Chanzo ni nini?

Haifamiki chanzo cha moja kwa moja cha shida hii lakini huambatana na vitu vifuatavyo.

 • Tatizo la kukosa usingizi.
 • ratiba ngumu ya kulala hasa kwa watu wanofanya kazi usiku na wakati mwingine mchana mfano walinzi na wahudumu wa afya.
 • magonjwa ya akili.
 • matatizo ya wasiwasi
 • kumbukumbu mbaya ya siku za zamani hasa kwa wanajeshi walioenda vitani, watu waliobakwa au waliokutana na matukio magumu zamani.(PTSD).
 • Historia ya shida hii kwenye familia.
Matibabu
Hakuna dawa ya moja kwa moja ya kutibu hali hii lakini unaweza kutibiwa kulingana na chanzo cha tatizo kama kukosa usingizi, wasiwasi, magonjwa ya akili na kumbukumbu mbaya kwa kupewa dawa za usingizi au dawa za kupunguza msongo wa mawazo.

Jinsi ya kuzuia shida hii.
 • Pata usingizi wa kutosha yaani masaa 6 mpaka 8.
 • Fanya mazoezi mara kwa mara.
 • Lala muda ule ule kila siku na kuamka muda uleule.
 • Epuka milo mikubwa, pombe, sigara na kahawa kabla ya kulala.
 • usilale kwa mgongo kwani wengi hupata hii shida kwa kulala hivi.
                                                            STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                   0653095635/0769846183