Mwezi wa 12 mwaka 2020 kirusi kipya cha corona kiligunduliwa na kutangazwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani na baada ya hapo virusi vingine vingi viliendelea kugunduiwa na kuzua maswali mbalilimbali, Je kwanini virusi hivi vinabadilika? je virusi hivi vinasambaa zaidi kuliko mwanzo? je virusi hivi ni hatari kuliko mwanzoni? Chanjo itafanya kazi? Kuna njia zingine mpya za kujikinga?
Kwanini virusi vya corona vinabadilika?
Virusi vya corona sio vya kwanza kubadilika, kuna virusi vingi sana ambvyo vinabadilika kila mwaka na kuleta changamoto ya matibabu na sababu kuu ya kubadilika ni pale vinapozidiwa nguvu au kubadili mazingira hivyo huja na umbo jipya kuweza kupambana na mazingira au kupambana na dawa mpya, mfano wa virusi ambavyo vimekua vikibadilika ni virusi vya ukimwi ambapo sasa kuna type 1 na type 2 lakini pia kuna subtypes zingine, virusi vya mafua hubadilika kila mwaka ndio maana marekani kila mwaka wanakua na chanjo mpya ya mafua kulingana na mabadiliko ya virusi hivo.
Kirusi kipya kilichogunduliwa uingereza kinaitwa B.1.1.7 ambacho kilisambaa mpaka nchini marekani na kusababisha zaidi ya 60% ya maambukizi mapya. virusi vingine vipya vimegunduliwa nchini brazili na afrika kusini.
Tofauti ya virusi hivi na vile vya mwanzo ni nini?
Kuna ushahidi wa wazi kwamba kirusi hiki kipya kinasambaa kwa kasi sana kuliko kile cha mwanzoni sababu ya maambukizi kua mengi eneo au nchi ambayo virusi hivi huingia lakini mpaka sasa hivi hakuna ushahidi wa kitaalamu kwamba virusi hivi ni hatari kuliko vile vya mwanzo ila kwasababu waathirika kwasasa ni wengi sababu ya kasi ya virusi ni wazi kwamba vifo vitaongezeka kuliko mwanzoni duniani kote.
Je kutatokea virusi vingine vya corona?
Ndio, kwasababu virusi hivi bado vinaendelea kusambaa duniani bado mabadiliko ya virusi hivi yataendelea na kuja na maumbo mapya. Tafiti nchini marekani zinaonyesha kwamba virusi vya mafua vipya hupatikana karibia kila wiki.
je chanjo hii itafanya kazi?
Kuna ushahidi kwamba baadhi ya chanjo hazitaweza kupambana na na virusi hivi vipya kwa 100% lakini vitatoa kinga ya uhakika kwa virusi vile vya zamani ndio maana pamoja na kutolewa kwa chanjo nchini uingereza na sehemu zingine duniani bado kuna nchi lockdown inaendelea lakini pia tahadhari za kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko, na kunawa mikono mara kwa mara zinaendelea.Nchini afrika kusini kuna chanjo ilizuiliwa wiki iliyopita baada ya kuona haitakua na msaada kwa aina ya virusi vilivyoko pale.
je kuna njia zingine mpya za kujikinga na virusi vipya?
Jibu ni hapana, kulingana na shirika la afya duniani WHO miongozo ni ileile kama kutumia sanitizer, kunawa mikono, kuvaa barakoa, na kuepuka mikusanyiko ya watu.
Ugonjwa huu utakuja kuisha?
Magonjwa mengi ya mlipuko huja na kuondoka na hata kama yakikaa kwa muda mrefu basi kinga za mwili huzoea magonjwa hayo na hivyo mwisho wa siku yanakua magonjwa ya kawaida tu. Ukichukulia ugonjwa wa spanish flu ambao uliua watu wengi zaidi karne ya 20 uliisha baada ya miaka miwili, Inakadiriwa kwamba watu milion 500 waliugua ugonjwa huu na watu zaidi milioni 100 waliuawa huku ugonjwa huo ukisabishwa na kirusi cha H1N1.Wana historia wanaamini kwamba ugonjwa wa spanish flu ulikua hauna nguvu sana wakati vita ya kwanza inaendelea sababu watu walikua wamejificha wengi lakini baada ya vita ya kwanza kutangazwa kuisha na watu kujaa mitaani kushangilia basi ugonjwa huu uliua zaidi ya watu milioni 50 wiki tano za kwanza.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni