data:post.body Januari 2021 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KIFO WAKATI WA TENDO LA NDOA.

 Hivi karibuni kumekua na ongezeko la vifo vingi vya watu hasa wanaume kwenye nyumba za kulala wageni ambapo inasemekana kwamba vifo hivo vilitokea wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Kumekua na hofu na imani za kishirikina kwamba huenda watu hao wamerogwa au wametegewa kitu cha kishirikina ndio maana wamekufa lakini mambo yote hayo hayana ushahidi.

                                                                        


Kitaalamu kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kuleta kifo wakati wa tendo la ndoa na mara nyingi huhusisha mfumo wa moyo kama ifuatavyo.

Magonjwa ya moyo; kuna wachezaji kadhaa wameshawahi kufia uwanjani wakati wa kucheza mpira, vifo hivi havina tofauti na vifo ambavyo vinatokea wakati wa tendo la ndoa.

Magonjwa ya moyo kitaalamu kama cardiomyopathies ndio yanayoongoza kwa vifo vya ghafla kwa vijana mpaka watu wazima hasa wakati wa mazoezi makali, magonjwa haya huja na kuvimba sehemu za ndani au chemba za moyo na kufanya ubadilishaji wa damu kutoka kwenye moyo kwenda sehemu zingine za mwili kua mgumu sana.

Vyanzo vya magonjwa haya hua ni kurithi kwa mzazi mmoja, ulevi wa kupitiliza, kuugua presha kwa muda mrefu, unene na magonjwa ya sukari,matumizi ya baadhi dawa za saratani,madhara ya ujauzito, madawa ya kulevya kama cocaine na kadhalika.

Dalili za magonjwa haya ni kuumwa kifua, kupumua kwa shida na kufa ghafla, mara nyingi magonjwa haya yanakua hayana dalili kabisa na mtu anaweza kukutwa na ugonjwa huu wakati wa vipimo vingine vya magonjwa mengine au uchunguzi baada ya kifo cha ghafla.

Magonjwa haya hayatibiki kabisa lakini kuna dawa malimbali za kupunguza makali au kubadilisha moyo kwa watu wenye uwezo huo.

dawa za kuongeza nguvu za kiume; Dawa maarufu kabisa inayotumika kutibu nguvu za kiume ni viagra kitaalamu kama sedenafil citrate, dawa hii inatakiwa iandikwe na kutumika chini ya uangalizi wa daktari na kwa lugha rahisi sio kila mtu anafaa kutumia dawa hii.

Viagra inafanya kazi kwa kutanua mishipa ya mwili ili kusukuma damu nyingi sana kwenye uume lakini faida hii inaambatana na madhara ya kushuka kwa presha ya damu, kitu hiki ni hatari sana kwa watu wenye presha ya kushuka na magonjwa mbali mbali ya moyo kwani hawezi kuvumilia tatizo hili na huweza kupelekea kifo cha ghafla kwa muhusika.

Kabla ya kutumia dawa hizi ni vizuri kuonana na wataalamu kwa ajili ya vipimo mbalimbali na kama wewe ni mgonjwa wa moyo tayari ni vizuri kukaa mbali kabisa na dawa hizi.

mwisho; Kila kitu kina wakati wake, kama wewe ni kijana na una uhakika una afya njema unaweza kufanya haya mashindano ya ngono lakini kama afya yako haiko sawa au umri umeenda sana basi kubali yaishe na ushiriki tendo hili kwa kiasi.Hakuna mtu amewahi kushinda chochote kwa kuonyesha umwamba wakati wa tendo la ndoa.

Maumivu ya sehemu ya moyo  na kushindwa kupumua wakati wa tendo la ndoa inaweza kua dalili ya kwanza ya kuelekea kusimama kwa moyo, ukifika hatua hii usiendelee na omba msaada wa haraka  kwani muda wowote unaanguka.

                                                            STAY ALIVE

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                  0653095635/0769846183

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA UUME NA MATIBABU YAKE.

 Saratani ya uume ni ugonjwa adimu kidogo lakini hua unatokea, saratani hii huweza kutokea sehemu yeyote kwenye uume lakini mara nyingi hutokea kwenye kichwa cha uume au kwenye ngozi ya mbele ya uume au govi kwa mtu ambaye hajatahiriwa au hutokea ndani ya mishipa ya damu ya uume..

                                                                        


Wataalamu hawajui chanzo cha uhakika wa saratani hii lakini lakini kuna mambo ambayo huleta hatari ya kupata ugonjwa huu kama..

  • Ugonjwa wa zinaa wa Human papiloma virus.
  • Kuvuta sigara
  • Ugonjwa wa ukimwi
  • Umri zaidi ya miaka 60
  • Mtu ambaye hajatahiriwa.
Dalili za saratani hii ni kama zifuatazo.
  • Kubadilika kwa unene na rangi ya ngozi.
  • Vipele kwenye uume.
  • Uvimbe kwenye uume.
  • Harufu mbaya chini ya ngozi kwa watu ambao hawajatahiliwa.
  • kidonda kwenye uume ambacho kinavuja damu kirahisi.
                                                    

Jinsi ya kutambua ugonjwa hospitali.
Sampuli ya uvimbe wa kwenye uume huchukuliwa na kwenda kupimwa maabara kuangalia kama kweli uvimbe huo ni saratani lakini pia vipimo vingine vya mionzo kama CT scan, utrasound, x ray na MRI hufanyika kuangalia saratani imesambaa kiasi gani mwilini.

Matibabu ya saratani ya uume
Matibabu ya saratani ya uume hutegemea hatua ambayo saratani imefika na katika hatua za mwanzo kabisa kuna cream za kutumia, matibabu ya barafu kali kitaalamu kama cryotherapy, matibabu ya kuua seli kwa kutumia laser na kutahiliwa kama saratani bado iko kwenye ngozi ya govi.

Matibabu katika hatua kubwa kabisa ya ugonjwa huu basi huhusisha dawa za saratani au chemotherapy, mionzi na upasuaji wa kuondoa uume kabisa na matoki yake kitaalamu kama penectomy.
Matibabu ya mionzi na dawa za saratani huweza kupunguza nguvu za kiume kwa mgonjwa ambaye uume hautaondolewa hivyo ni vizuri kujua mapema.
                                                   

           

Njia za kuzuia saratani ya uume
  • Hakikisha unatailiwa na hata kabla ya kutailiwa hakikisha usafi wa uume wako.
  • Epuka matumizi ya sigara.
  • Tumia kondomu kuepuka magonjwa ya zinaa pamoja na ukimwi.

                                                      STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183

FAHAMU TATIZO LA SARATANI YA KOO NA MATIBABU YAKE.

Saratani ya kooni ni aina ya saratani inayoshambulia njia yako ya chakula ambayo husafirisha chakula kwanzia mdomoni mpaka tumboni, ugonjwa huu huanzia ndani ya koo kisha kusambaa sehemu mbalimbali za mwili. 

Saratani ya koo ni ya sita duniani kwa kusababisha vifo na wahanga wengi wa ugonjwa huu ni wanaume kuliko wanawake..Nchini Tanzania wagonjwa hawa wapo wengi hasa kwenye hospitali kubwa za rufaa lakini waathirika wakubwa ni watu wazima kwanzia Miaka 50 kwenda mbele.

                                                    


Nini chanzo cha ugonjwa huu?

Kama ilivyo kwa aina zote za saratani duniani mara nyingi chanzo halisi hua hakifahamiki mambo hatarishi ambayo huchangia kuanza kwa ugonjwa huu kama ifuatavyo.

  • kuvuta sigara
  • unywaji wa pombe kupitiliza.
  • kiungulia cha muda mrefu
  • unene
  • kula vyakula vya moto sana
  • kutokula matunda na mboga za majani.
  • magonjwa mengine ya koo mfano achalasia.
dalili za saratani ya koo
  • kushindwa kumeza chakula;  mara nyingi mgonjwa huanza na kushindwa kumeza chakula kigumu kama ugali, baadae hushindwa uji, kisha hushindwa maji ya kunywa na mwisho kabisa hushindwa kabisa hata kumeza mate.
  • kukohoa na sauti kukoroma; dalili hii mara nyingi hutokea mwishoni kwani koo linakua limetoboka na chakula kinaingia kwenye njia ya hewa lakini pia mishipa ya fahamu ya sauti inakua imeingiliwa na saratani
  • kupungua uzito sana.
  • maumivu ya kifua.
  • kiungulia kikali.
jinsi ya kutambua ugonjwa.
Kipimo cha endoscopy au OGD ambacho kina mpira wenye camera maalumu hupitishwa kooni mpaka tumboni kuangalia saratani hiyo lakini pia kipimo hiko hiko hutumika kutoa nyama kitaalamu kama biopsy na kwenda kupima maabara.
Vipimo vingine kama PET scan,CT scan na broncoscopy hufanyika kuangalia ugonjwa umesambaa kiasi gani.

Matibabu ya saratani ya koo.
Matibabu ya ugonjwa huu hutegemea na hatua ya ugonjwa husika, katika hatua ya kwanza mpaka ya tatu ya ugonjwa ambayo ugonjwa unakua bado uko ndani ya koo upasuaji huweza kufanyika kuondoa vimbe za saratani hizo kitaalamu kama oesophagectomy lakini ugonjwa ukishasambaa kwenye hatua ya nne ya ugonjwa basi panakua hapawezekani tena kupasua, mgonjwa anaweza kutumia dawa za saratani kama chemotherapy kuongeza muda wa kuishi.

maisha baada ya saratani.
Ugonjwa huu ukiwahiwa unaweza kutibiwa kabisa kwa upasuaji na kupona lakini kwenye hatua za mwisho mgonjwa atapewa tu ushauri na kupewa dawa za kupunguza maumivu ili aendelee kuishi muda uliobaki bila maumivu lakini pia atawekewa koo bandia ambalo litamsaidia kula kama alikua amefika hatua ambayo hawezi kula tena.
Uwezekano wa kuishi miaka zaidi ya miaka mitano kwa saratani kwanzia steji ya kwanza mpaka ya 3 yaani inakua bado iko kwenye koo ni asilimia 47%, ikisambaa sehemu za pembeni ya koo kma kwenye mishipa ya damu na sehemu za kifua ni asilimia 25% lakini ikisambaa mwili mzima ni asilimia 5% tu.
Ni vizuri ndugu na mgonjwa kukubali ukweli mapema kuliko kutumia pesa nyingi kwa waganga wa kienyeji au hata kwenda nje ya nchi kwani hakuna faida yeyote ya kufanya hivo.

                                                             STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183