data:post.body TATIZO LA KUWASHWA BAADA YA KUOGA NA MATIBABU YAKE.(AQUAGENIC URTICARIA) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

TATIZO LA KUWASHWA BAADA YA KUOGA NA MATIBABU YAKE.(AQUAGENIC URTICARIA)

 Aquagenic urticaria ni hali ambayo sio ya kawaida ambayo hutokea pale mtu anapowashwa baada ya kuoga au kugusa maji, tafiti zinaonyesha kwamba hali hii inasababishwa na mgonjwa kua na allergy ya maji.                                                           


Mgonjwa huweza kuwashwa na maji ya bomba, bahari, ziwani, mto, mvua, machozi, jasho, na kadhalika.Baadhi ya watafiti huamini kwamba kuwashwa huko kunaweza kunasababishwa na kemikali ambazo huwekwaa ndani ya maji kuua bacteria mfano chlorine lakini maelezo haya hayajitoshelezi kwani kuna watu wanawashwa mpaka na maji ya mvua ambayo haya kemikali yeyote.

dalili ni zipi?

Unapopata allergy ya kitu chochote mwili wako hutoa kemikali moja inaitwa histamine kupambana na hicho kitu ambacho mwili wako unatafsiri kama adui na matokeo yake unawashwa. Kwa kawaida mtu hupata dalili za vipele, kuwashwa mwili mzima,ngozi nyekundu kwa watu weupe, na kwa dalili mbaya  sana mtu huweza kushindwa kupumua, kushindwa kumeza na kuanza kukoroma wakati wa kupumua.

jinsi ya kutambua ugonjwa

Daktari huchukua maelezo yako na kukagua ngozi yako lakini pia anafanya majaribio kwa kuweka maji kwenye mwili wako na kuangalia matokeo ambayo mara nyingi hutokea baada ya dakika 15. Dalili hizi zikianza baadhi ya vipimo vya damu kama full blood picture huweza kuonyesha kuongezeka kwa kiwango cha seli mwilini kinachohusika na allergy kitaalamu kama easinophil.

matibabu

Duniani kote hakuna dawa ya kutibu allergy na kuimaliza lakini kuna dawa za kuondoa dalili hizi za kuwashwa. Dawa kama aina ya anthistamine kama piriton au citrizine unaweza kumeza kidonge kimoja nusu saa kabla ya kuoga lakini pia badilisha mfumo wako wa maisha kwa kujiepusha na shughuli zote ambazo zinakuhusisha na kuloa maji.

                                                               STAY ALIVE 

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                             0653095635/076984613

Maoni 7 :

 1. Kwahiyo hiyo tiba yakuwashwa mwili baada yakuoga haipo

  JibuFuta
 2. Tatizo hili la kuwashwa limeanza toka Nina miaka 5 mpaka leo nina 30 nateseka kiasi cha kupata ukichaa ndan ya dakika 20 mpaka 40 hiv

  JibuFuta
 3. Mmh mm nadhan ugonjwa ndo inazid kuongezeka
  Maana nawashwa had na kuchanganyikiwa
  Sasa limezuka jipya na sisimka ovyo ovyo
  Sitaman kuona hata nilipoogea.

  JibuFuta
 4. Kwakwel hili ni tatizo yaan mm akiniongelesha mtu baada ya kuoga nataman nmpige kibao maana akili inahamia kweny kujikuna yaan n shda kabsa

  JibuFuta
  Majibu
  1. Mwee hili tatizo nilijua niko peke angu linanitesa na mimi daah!!..🥺

   Futa