data:post.body TATIZO LA KUTOSIKIA HARUFU NA MATIBABU YAKE ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

TATIZO LA KUTOSIKIA HARUFU NA MATIBABU YAKE

Wengi wetu uwezo wa kusikia harufu fulani tunaona ni kitu cha kawaida sana na tunahisi ni haki yetu lakini ushawahi kujifikiria kukosa harufu kabisa? Kutosikia harufu kabisa kitaalamu tunaita anosmia, ni tatizo ambalo linakufanya usisikie harufu ya mafuta, maua, manukato, chakula na hata ladha ya chakula hubadilika.

                                                                   


Hali hii inaweza kukuweka kwenye mazingira hatarishi kama ukishindwa kusikia harufu ya moshi, gesi inayovuja, au chakula kilichoharibika au kuwekewa kemikali.

Kwa nchi ambazo zimeendelea, tatizo hili huwapeleka wagonjwa wengi hospitali hapa kwetu ni tofauti kidogo kwani watu wana tabia ya kuvumilia magonjwa kama haya. Bahati nzuri asilimia kubwa ya wagonjwa hawa ni sababu ya mafua makali lakini baadhi inaweza kua magonjwa makubwa sana ambayo yanahitaji uangalizi wa karibu.

Mwili wa binadamu unatambua vipi harufu?

Mwili wa binadamu una mshipa wa fahamu maalumu kwa jina la olfactory ambao unapeleka taarifa ya harufu kutoka puani kwenda kwenye ubongo kwa ajili ya kutoa tafsiri ya kujua hii ni harufu gani, sasa tatizo lolote ambalo linaingilia huo mfumo huu kama mafua makali, nyama za pua au kuharibika kwa mshipa huu wa fahamu basi linasababisha mtu akose uwezo wa kusikia harufu.

Chanzo cha tatizo hili..

kama nilivyosema hapo mwanzoni kwamba mafua makali na kamasi, aleji ya vitu na hali mbaya ya hewa ndio chanzo kikuu cha hali hii lakini vyanzo vingine ni...

 • nyama za pua kitaaalamu kama nasal polyp.
 • kuumia kwa pua na kichwa baada ya ajali au upasuaji.
 • harufu za kemikali kali.
 • baadhi ya dawa za moyo, msongo wa mawazo na antibayotiki.
 • matumizi ya dawa za kulevya kama cocaine
 • umri mkubwa hasa baada ya miaka 60.
 • mionzi ya kichwa na shingo
 • baadhi ya magonjwa kama ya homoni, magonjwa ya kuzaliwa, alzehmers, parnkison, na utapiamlo wa chakula.
 • ugonjwa wa homa kali ya mafua wa covid 19.
Dalili za ugonjwa.
Dalili kuu ni kukosa harufu ya kitu ambacho unafahamu harufu yake siku zote.

Jinsi ya kutambua ugonjwa.
Ukiona unashindwa kupata harufu kwa zaidi ya wiki mbili na hauna mafua basi ni vizuri kwenda hospitali kuonana na daktari bingwa wa pua, sikio na koo ili akufanyie vipimo zaidi kujua tatizo ni nini.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yanatakiwa yaelekezwe zaidi kwenye chanzo cha ugonjwa wenyewe, kama ni mafua makali basi ugonjwa unaweza kuisha wenyewe na kama unasumbua basi unaweza kumeza dawa za mafua kupna haraka.
Tatizo la nyama za pua linaweza kutibika kwa upasuaji na kuondoa nyama hizo, tatizo la covid19 huweza kuisha lenyewe baada ya ugonjwa kuisha.
Kama unahisi chanzo ni dawa fulani ambazo unatumia kwa ajili ya kutibu shida zako zingine za kila siku basi ongea na daktari wako akubadilishie dawa hizo.
Bahati mbaya kama tatizo hili linatokana na umri mkubwa likaua haliwezi kutibika kirahisi lakini kama unaweza ni vizuri kununua vifaa maalumu vya kupiga kelele hasa kwenye harufu ya moshi au gesi kukuepusha na hatari.

                                                                 STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                          0653095635/0769846183


Maoni 7 :

 1. Asante sana maana nimepata majibu ya maswali yangu

  JibuFuta
 2. Kwangu mim sjawah kuskia harufu tangu nizaliwe sjui inakuaj hii

  JibuFuta
 3. Unapatikana wp

  JibuFuta
 4. Mimi sihisi harufu kea mda wa miez sana lakini asaiv nahisi harufu lakini ni tofauti na ile niliyozoea

  JibuFuta
 5. Mimi sijui harufu kabisa

  JibuFuta
 6. Mimi toka mwaka 2016 sihisi harufu ya kitu chochote na nikinama pua inauma hadi machozi yanatoka tatizo nini jamani

  JibuFuta
 7. Mm Toka nimezaliwa harufu mzur sijawh ila harufu Kali iloyo karibu naskia ikiniumiza pia  JibuFuta