data:post.body Septemba 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI NA MATIBABU YAKE.

 Uke wa kawaida wa mwanamke lazima uwe na harufu fulani, sio rahisi kusema ni harufu gani lakini wanawake huweza kutofautiana harufu hiyo. Kwakawaida uke ni nyumbani kwa bacteria wengi sana huku kukiwa na gland ambazo hutoa majimaji ya uke ambayo yana tindikali kali sana.

                                                                


Kazi ya bacteria hao na glandi hizo ni kujaribu kutoa ulinzi mkali ili uke usishambuliwe na vijidudu hatarishi ambavyo huleta magonjwa. Ukiona mwanamke anapambana sana kutumia vitu mbalimbali na kufanya usafi mwingi uke wake usitoe harufu hata kidogo basi ujue anatafuta magonjwa.

Kwakawaida kuna magonjwa mawili ambayo yakianza yanakua tishio kubwa kwa mwanamke kwani huja na harufu kali kama ya kitu kilichooza na kutao uchafu wa kijani na njano, magonjwa haya kitaalamu ni bacterial vaginosisi na trichomonisis.

ugonjwa wa trichomoniasis ni upi?
huu ni ugonjwa  unaoshambulia sehemu za siri kwa jina la trichonomiasis na husababiswa na aina ya protozoa kwa jina la trichomona vaginalis.
huu ni ugonjwa unaoshambualia angalau 10% ya wanawake wote kwenye kipindi chote cha maisha yao,
maambukizi ni kwa njia ngono kati ya mwanaume na mwanamke lakini pia kuchangia nguo za ndani au mataulo kunaweza kuambukiza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
ugonjwa huu huweza kuambukiza watu wa jinsia zote lakini unawaathiri sana wanawake na mgonjwa asipotibiwa anaweza kuishi na ugonjwa huo kwa siku miaka kadhaa.
baada ya kuambukizwa ugonjwa huu, huchukua siku 5 mpaka 28 kuanza kuonyesha dalili zake waziwazi.

dalili za ugonjwa wa trichomoniasis
kuwashwa sana sehemu za siri
kuchubuka sehemu ya juu ya uke na mlango wa uzazi
maumivu wakati wa kukojoa
maumivu wakati wa tendo la ndoa
maumivu makali ya tumbo la chini
kutokwa uchafu wa kijani na njano wenye harufu kali kama ya kitu kilicho oza.
kwa wanaume ugonjwa huu mara nyingi hauna dalili lakini mara chache sana wanaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa

vipimo
daktari mzoefu anaweza kuujua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini pia kwa upande wa maabara uchafu unaotoka huchukuliwa na kupimwa kwa darubini...

matibabu
metronidazole au kwa jina lingine fragile 2g kwa wakati mmoja [vidonge kumi] au 400mg[vidonge viwili] kutwa mara tatu kwa siku tano.
tinidazole 2g kwa wakati mmoja
scenidazole 2g kwa wakati mmoja.
kumbuka dawa hizi hazipatani na pombe kabisa hivyo usitumie pombe ukitumia dawa hizi.

jinsi ya kuzuia
tumia kondom kila tendo na kwa usahihi
achana na ngono kama huwezi kondom
kua na mpenzi mmoja muaminifu
epuka kua na wapenzi wengi
epuka kuchangia chupi, taulo au nguo yeyote ya ndani.
                                                                         

  • Ugonjwa wa bacterial vaginosis unafanana sana dalili na ugonjwa trichomoniasis, tofauti ni kwamba chanzo chake ni kuzaliana sana kwa bacteria asilia ambao wanapatiakana kwenye uke.. chanzo kikiwa   matumizi ya marashi au dawa mbalimbali za kuondoa harufu asilia ya uke, kuosha sana uke, kua na wapenzi wengi au mpenzi mpya, na kupungua kwa ulinzi asilia sehemu za siri.
  •   Dalili, vipimo na matibabu hufanana lakini pia ni vizuri kujua kwamba kupuuzia magonjwa haya kuna madhara makubwa kama kuharibika mimba na magonjwa ya kizazi ambayo yanaweza kuleta ugumba.

                                                       STAY ALIVE


                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                 MAWASILIANO 0653095635/0769846183

TATIZO LA KUTORUDIA TENDO LA NDOA BAADA YA KUFIKA KILELENI.

Katika mambo ambayo yanaumiza sana vichwa wanaume walio wengi ni kushindwa kurudia tendo la ndoa kwa mara ya pili baada ya kufika mshindo kwa mara ya kwanza, wengi hudhani wana matatizo na kuanza kutafuta suluhisho ya matatizo yao kwa kutumia dawa za aina mbalimbali bila kujua kwamba wao hawana shida yeyote.


ukweli ni upi?

Kila mwanaume ana muda wake ambao anatakiwa kupumzika kabla ya kuendelea na tendo la ndoa kitaalamu kama refractory period, kuna ambao wanaweza kuendelea hapo hapo na kuna wengine wanahitaji mapumziko ya kwanzia nusu saa mpaka siku nzima.Tofauti na wanawake ambao huhitaji muda mfupi wa mapumziko au hua hawahitaji muda huu wa mapumziko kwani wao huweza kufika kileleni hata mara kumi kwa kulala na mtu mara moja kitaalamu kama multi orgasmic.

Tatizo ni nini? 

Wanaume wengi hutumia muda mchache sana kufika mshindo wa kwanza kitu ambacho kinaweza kumfanya mwanamke asiridhike kwa wakati huo, sasa kwasababu mwanamke hajaridhika na anataka kuendelea basi wanaume hawa hujilazimisha kuendelea bila kupata mapumziko hayo ambayo ni ya msingi sana.Matokeo yake wanaume hawa hupaniki kwa kuhisi kwamba watapata aibu na katika kupaniki huko muda wa kurudia ndio unazidi kua mrefu zaidi.

kwanini wanaume wako tofauti kwenye jambo hili?

  • umri; vijana wadogo wanakua na stamina sana lakini pia mfumo wao wa damu ni msafi sana hivyo wanaweza kurudia haraka.
  • kuvutiwa na mwanamke; mwanaume akilala na mwanamke ambaye anavutiwa naye kingono basi ana uwezo wa kurudia mara nyingi sana kuliko akilala na mwanamke yeyote na hii nikitu muhimu sana wakati wa kuoa, hakikisha unaoa mwanamke anayekuvutia sio yeyote tu.
  • uwezo wa mwanamke kitandani; baadhi ya wanawake wana uwezo na utundu sana wa kukufanya utake kuendelea baada ya muda mfupi tu.
  • magonjwa; baadhi ya magonjwa hasa presha na kisukari huweza kuchelewesha sana muda wa kurudia tendo la ndoa.
  • matarajio; ukiwa na matarajio makubwa ya kuendelea na tendo lingine baada ya kumaliza tendo la ndoa kwa hofu kwamba hujamridhisha basi ndio hupati kitu kabisa.
Nini cha kufanya?
Chelewa kufika mshindo wa kwanza; ukichelewa kufika kileleni kuna uwezekano mkubwa wa kufikishwa mwanamke kileleni zaidi ya mara moja na ukajikuta unapumzika naye baada ya wewe kumaliza pia  bila haraka kusubiri kuendelea mara ya pili au kutorudia kabisa kwani ameridhika.
Inaweza isiwe rahisi kuchelewa kufika kileleni lakini kuna njia za kufanya hivyo bonyeza hapa kusoma...http://www.sirizaafyabora.info/2014/08/kama-wewe-mwanaume-una-tatizo-la-kufika.html
jiweke vizuri kimwili; Fanya mazoezi mara kwa mara, hii huongeza mzunguko wa damu mwilini, hukupa stamina na uwezo wa kufanya ngono kwa muda mrefu zaidi.
tumia dawa zako kwa wakati; kama una ugonjwa wowote ambao unakuletea shida hii hasa magonjwa ya moyo, presha na sukari basji jitahidi kutumia dawa zako kwa wakati kupunguza makali ya ugonjwaa.
epuka mahusiano na mwanamke asiyekuvutia; anaweza kua hakuvutii wewe lakini kuna watu anawavutia, kua mkweli na nafsi yako na utafute mwanamke ambaye nafsi yako inaridhika naye na hapo utafurahia sana tendo la ndoa.

mwisho; mfumo wa maisha kama kunywa pombe sana, matumizi ya sigara na kupiga sana punyeto kunaweza kukufanya ushindwe kuendelea na tendo lingine kwa wakati.

                                                                STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                        0653095635/0769846183

TATIZO LA KUTOSIKIA HARUFU NA MATIBABU YAKE

Wengi wetu uwezo wa kusikia harufu fulani tunaona ni kitu cha kawaida sana na tunahisi ni haki yetu lakini ushawahi kujifikiria kukosa harufu kabisa? Kutosikia harufu kabisa kitaalamu tunaita anosmia, ni tatizo ambalo linakufanya usisikie harufu ya mafuta, maua, manukato, chakula na hata ladha ya chakula hubadilika.

                                                                   


Hali hii inaweza kukuweka kwenye mazingira hatarishi kama ukishindwa kusikia harufu ya moshi, gesi inayovuja, au chakula kilichoharibika au kuwekewa kemikali.

Kwa nchi ambazo zimeendelea, tatizo hili huwapeleka wagonjwa wengi hospitali hapa kwetu ni tofauti kidogo kwani watu wana tabia ya kuvumilia magonjwa kama haya. Bahati nzuri asilimia kubwa ya wagonjwa hawa ni sababu ya mafua makali lakini baadhi inaweza kua magonjwa makubwa sana ambayo yanahitaji uangalizi wa karibu.

Mwili wa binadamu unatambua vipi harufu?

Mwili wa binadamu una mshipa wa fahamu maalumu kwa jina la olfactory ambao unapeleka taarifa ya harufu kutoka puani kwenda kwenye ubongo kwa ajili ya kutoa tafsiri ya kujua hii ni harufu gani, sasa tatizo lolote ambalo linaingilia huo mfumo huu kama mafua makali, nyama za pua au kuharibika kwa mshipa huu wa fahamu basi linasababisha mtu akose uwezo wa kusikia harufu.

Chanzo cha tatizo hili..

kama nilivyosema hapo mwanzoni kwamba mafua makali na kamasi, aleji ya vitu na hali mbaya ya hewa ndio chanzo kikuu cha hali hii lakini vyanzo vingine ni...

  • nyama za pua kitaaalamu kama nasal polyp.
  • kuumia kwa pua na kichwa baada ya ajali au upasuaji.
  • harufu za kemikali kali.
  • baadhi ya dawa za moyo, msongo wa mawazo na antibayotiki.
  • matumizi ya dawa za kulevya kama cocaine
  • umri mkubwa hasa baada ya miaka 60.
  • mionzi ya kichwa na shingo
  • baadhi ya magonjwa kama ya homoni, magonjwa ya kuzaliwa, alzehmers, parnkison, na utapiamlo wa chakula.
  • ugonjwa wa homa kali ya mafua wa covid 19.
Dalili za ugonjwa.
Dalili kuu ni kukosa harufu ya kitu ambacho unafahamu harufu yake siku zote.

Jinsi ya kutambua ugonjwa.
Ukiona unashindwa kupata harufu kwa zaidi ya wiki mbili na hauna mafua basi ni vizuri kwenda hospitali kuonana na daktari bingwa wa pua, sikio na koo ili akufanyie vipimo zaidi kujua tatizo ni nini.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yanatakiwa yaelekezwe zaidi kwenye chanzo cha ugonjwa wenyewe, kama ni mafua makali basi ugonjwa unaweza kuisha wenyewe na kama unasumbua basi unaweza kumeza dawa za mafua kupna haraka.
Tatizo la nyama za pua linaweza kutibika kwa upasuaji na kuondoa nyama hizo, tatizo la covid19 huweza kuisha lenyewe baada ya ugonjwa kuisha.
Kama unahisi chanzo ni dawa fulani ambazo unatumia kwa ajili ya kutibu shida zako zingine za kila siku basi ongea na daktari wako akubadilishie dawa hizo.
Bahati mbaya kama tatizo hili linatokana na umri mkubwa likaua haliwezi kutibika kirahisi lakini kama unaweza ni vizuri kununua vifaa maalumu vya kupiga kelele hasa kwenye harufu ya moshi au gesi kukuepusha na hatari.

                                                                 STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                          0653095635/0769846183


TATIZO LA SARATANI YA UTUMBO MKUBWA NA MATIBABU YAKE.

 Baada ya kifo cha mkali wa filamu za kimarekani maarufu kama wakanda au chadwick bossman kumekua na utafutaji mkubwa sana mtandaoni kujua ugonjwa huu unasababishwa na nini na ni jinsi gani mtu anaweza kukwepa ugonjwa huu.


Saratani hii huanzia kwenye sehemu ya utumbo mkubwa, mara nyingi huanza kama viuvimbe vidogo ambavyo sio saratani kitaakamu kama benign tumours au polyp lakini baadae hubadilika na kua saratani kamili na wakati mwingine hujumuisha sehemu ya mwisho kabisa ya mfumo ya chakula na kuitwa kitaalamu kama colerectal cancer. Mara nyingi ugonjwa huu huanza bila dalili na baadae dalili huanza kutokana na eneo ambalo ugonjwa umeshambulia.

Dalili za saratani ya utumbo mkubwa.

  • kubadilika kwa mfumo wako wa kupata choo yaani kupata choo ngumu sana au kuanza kuharisha.
  • maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi au kujisikia vibaya tumboni.
  • kupata choo chenye damu au kujisaida tamu tupu.
  • kujisikia kama choo haitoki yote kila ukitoka chooni.
  • uchovu wa mara kwa mara 
  • kuanza kupungua uzito kwa kasi isiyo kawaida.
Chanzo cha ugonjwa huu.
Ugonjwa huu haufahamiki chanzo chake lakini inafahamika kwamba mabadiliko ya chembe za DNA ndio sababu ya saratani zote kitaalamu kama DNA mutation.
Lakini kinachofahamika kwa uhakika ni vitu ambavo vinachangia mtu kuugua ugonjwa huu kama ifuatavyo.
umri mkubwa; Saratani hii mara nyingi huwapata watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea lakini wataalamu wameanza kuona ongezeko hili kwa vijana chini ya miaka 50 na sababu hazifahamiki.
magonjwa mengine ya utumbo mkubwa; kama ushawahi kuugua magonjwa mengine ya utumbo mkubwa unaweza kua kwenye hatari ya kuugua. mfano; ulcerative colitis
mgonjwa kwenye ukoo wako; kama mzazi wako mmoja kaugua ugonjwa huu basi na wewe una hatari ya kuupata na kama kuna mtu zaidi ya mmoja kwenye ukoo wenu basi hatari ni kubwa zaidi.
chakula; ugonjwa wa huu umeonyesha kuathiri zaidi watu wanaokula sana diet ambazo asili yake ni dunia ya magharibi yaani vyakula vyenye mafuta mengi, na nyama nyingi nyekundu bila kula mboga za majani na matunda ya kutosha.
kutofanya mazoezi; watu ambao hawana tabia ya kufanya mazoezi wana hatari sana ya kuugua ugonjwa huu kuliko watu wenye tabia ya kufanya mazoezi au wanaofanya kazi ambazo zinatumia nguvu.
uzito mkubwa; watu wanene wana hatari ya kuugua na hata kufa haraka kutokana na ugonjwa huu.
sigara na pombe; watu wanaokunywa pombe sana  na kuvuta sigara wana hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu.
mionzi; watu ambao wanapigwa na mionzi ya kupima au kutibu magonjwa fulani fulani wanakua na hatari pia ya kupata ugonjwa huu.
wagonjwa wa kisukari na watu weusi; watu hawa pia wameonyesha kuugua zaidi ugonjwa huu lakini sababu maalumu haifahamiki.

jinsi ya kutambua ugonjwa.
Colonoscopy; Hichi ni kipimo ambacho kina camera ndogo na hupitishwa kwenye njia ya haja kubwa kuangalia kama kuna uvimbe wowote wa saratani, uvimbe ukionekana basi inachukuliwa sample kwenda kupimwa maabara ili kuhakikisha kama ni saratani lakini hata kama sio saratani uvimbe huo huondolewa ili usibadilike na kua saratani.
vipimo vya damu; baadhi ya kemikali huwezwa kupimwa ili kujua kama kuna saratani mwilini mwako kitaalamu kama carcinoembryonic antigen na ukianza matibabu kipimo hichi kinaweza kugundua kama maendeleo ni mazuri mwilini mwako.

matibabu ya saratani ya utumbo mkubwa.
Matibabu makubwa ya ugonjwa huu ni upasuaji, dawa za saratani na mionzi..katika kipindi cha mwanzo kabisa cha ugonjwa huu basi mgonjwa anaweza kupona kabisa kama sehemu hiyo ya saratani ikiondolewa kwa upasuaji.
Lakini wagonjwa wengine hufika hospitali kwa kuchelewa huku saratani ikiwa ishasambaa sehemu kubwa sana ya mwili na kuifanya isitibike kabisa.

jinsi ya kujikinga na saratani ya utumbo mkubwa.
  • kula vizuri; mboga za majani na matunda zina vitamini fulani ambazo zina uwezo wa kuzuia saratani za aina zote kwenye mwili wa binadamu, huku afrika tuna nafasi kubwa ya kupata vitu hivi kwa bei rahisi.
  • kunywa pombe kiasi na achana na uvutaji wa sigara.
  • fanya mazoezi angalau nusu saa mara tatu kwa wiki.
  • kaa kwenye uzito sahihi kulingana na urefu wako.
  • kama uko kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu fanya vipimo kila baada ya miaka miwili au mitatu ilia kama umeanza utibiwe mapema.
                                                                                 STAY ALIVE

                                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                                        0653095635/0769846183

TATIZO LA KUWASHWA BAADA YA KUOGA NA MATIBABU YAKE.(AQUAGENIC URTICARIA)

 Aquagenic urticaria ni hali ambayo sio ya kawaida ambayo hutokea pale mtu anapowashwa baada ya kuoga au kugusa maji, tafiti zinaonyesha kwamba hali hii inasababishwa na mgonjwa kua na allergy ya maji.                                                           


Mgonjwa huweza kuwashwa na maji ya bomba, bahari, ziwani, mto, mvua, machozi, jasho, na kadhalika.Baadhi ya watafiti huamini kwamba kuwashwa huko kunaweza kunasababishwa na kemikali ambazo huwekwaa ndani ya maji kuua bacteria mfano chlorine lakini maelezo haya hayajitoshelezi kwani kuna watu wanawashwa mpaka na maji ya mvua ambayo haya kemikali yeyote.

dalili ni zipi?

Unapopata allergy ya kitu chochote mwili wako hutoa kemikali moja inaitwa histamine kupambana na hicho kitu ambacho mwili wako unatafsiri kama adui na matokeo yake unawashwa. Kwa kawaida mtu hupata dalili za vipele, kuwashwa mwili mzima,ngozi nyekundu kwa watu weupe, na kwa dalili mbaya  sana mtu huweza kushindwa kupumua, kushindwa kumeza na kuanza kukoroma wakati wa kupumua.

jinsi ya kutambua ugonjwa

Daktari huchukua maelezo yako na kukagua ngozi yako lakini pia anafanya majaribio kwa kuweka maji kwenye mwili wako na kuangalia matokeo ambayo mara nyingi hutokea baada ya dakika 15. Dalili hizi zikianza baadhi ya vipimo vya damu kama full blood picture huweza kuonyesha kuongezeka kwa kiwango cha seli mwilini kinachohusika na allergy kitaalamu kama easinophil.

matibabu

Duniani kote hakuna dawa ya kutibu allergy na kuimaliza lakini kuna dawa za kuondoa dalili hizi za kuwashwa. Dawa kama aina ya anthistamine kama piriton au citrizine unaweza kumeza kidonge kimoja nusu saa kabla ya kuoga lakini pia badilisha mfumo wako wa maisha kwa kujiepusha na shughuli zote ambazo zinakuhusisha na kuloa maji.

                                                               STAY ALIVE 

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                             0653095635/076984613