data:post.body Agosti 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAUME NA MATIBABU YAKE.

Fangasi sugu za kwenye korodani za wanaume limekua moja ya matatizo sugu siku hizi za usoni, baadhi wamekua wakitumia dawa bila mfanikio yeyote na hii ni kwasababu ya kushindwa kuelewa chanzo na jinsi ya kupambana na hatari za kupata ugonjwa huu.

                                                                        


chanzo cha ugonjwa.

ugonjwa huu husababishwa na aina ya fangasi mwenye jina la trichopyton rubrum na waathirika wakubwa  vijana,tabia kuvaa nguo za ndani zinazobana, kua mzito sana, kinga iliyoshuka kwa ukimwi, saratani, utapiamlo au kisukari, na kutokwa na jasho sana.

dalili za ugonjwa.

 • kuwashwa sana kwenye sana kwenye korodani.
 • korodani kua nyekundu hasa kwa watu weupe
 • korodani kuanza kutoa kama magamba kwenye ngozi.

jinsi ya kutambua ugonjwa
Daktari anaweza kutambua ugonjwa wako wa kusikiliza maelezo yako tu au kuchukua sehemu ya mabaka ya ngozi na kwenda kupima maabara,

Matibabu ya ugonjwa huu.
Kuna dawa nyingi sana za kutibu ugonjwa huu, dawa ya terbinifine ya kumeza ni moja ya dawa bora sana kwa ugonjwa huu.
Zingine ni cotrimazole, ketoconazole, gresiofulvin, na miconazole.
kumeza na kupaka kwa wakati mmoja kumeonyesha matokeoa mazuri zaidi. 
Sasa jambo la msingi kabisa kuzingatia ambalo linafanya watu wengi wasipone ni kutumia dawa hizi muda mfupi, dawa hizi zinatakiwa zitumike wiki sita na sio chini ya hapo.


Mambo mengine ya kuzingatia..

kua mkavu; baada ya kuoga hakikisha umekausha mwili mzima kwa taulo safi kabla ya kuvaa nguo zingine lakini pia kausha miguu mwishoni kuzuia kuhamisha fangasi za vidoleni kwenda sehemu zingine za mwili.
vaa nguo safi: wanaume wengi wana tabia ya kuvaa nguo ya ndani moja kwa siku nyingi, jaribu kuvaa moja kila siku na kubadilisha hii itakupunguzia maambukizi yanayojirudia na hakikisha nguo za mazoezi unazitumia mara moja na kufua.
epuka nguo zinazobana sana; Vaa nguo za ndani ambazo zinakutosha ili kufanya maeneo hayo yapate hewa ya kutosha na kuepuka unyevunyevu.
usiazime nguo; epuka kuchangia taulo au nguo zako na watu wengine kwani hii itakuletea maambukizi mapya kila siku.
tibu fangas za vidole; kama una fangasi za kwenye vidole vya miguu hakikisha zinatibiwa na kupona ili kuepusha kuzisambaza mwili mzima.

                                                              STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0653095635/0769846183
FAHAMU JINSI UNENE UNAVYOWEZA KUSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKE.

 Kama wewe ni mwanamke mnene au una tumbo kubwa  na umekua ukisumbuliwa na tatizo la kutobeba mimba basi ni vizuri kwanza ukaacha kuhangaika na waganga na dawa mbalimbali ambazo umeambiwa zitakusaidia na kuweka nguvu nyingi kwenye kupungua uzito.

                                                                                 

Tafiti zinaonnyesha kwamba kadri unavyoondoka kwenye uzito wako wa kawaida yaani body mass index ya 24 ndio uwezekano wako wa kubeba mimba unazidi kua mdogo na ukiwa mnene kabisa ndio hali inazidi kua mbaya kabisa.

Mwanamke akiwa mnene au mwenye kitambi kikubwa anakua na kiwango kikubwa cha homoni inaitwa leptin ambayo hutengenezwa na mafuta yaliyoko mwilini, kiwango hichi cha homoni huingilia mfumo wa homoni za uzazi na kuuvuruga.Unene unavyozidi au tumbo linavyokua kubwa zaidi ndio hali hii inazidi kua mbaya zaidi.

Pamoja na unene kuvuruga mfumo wa homoni wanawake wanene hupata shida ya kutoa yai kitaalamu kama ovulation yaani yai linaweza lisitoke kabisa au likatoka likiwa halina ubora wa kutunga mimba hivyo huishia kuharibika.Lakini pia wanawake wa aina hii hata wakijaribu kuzaa kwa njia za kisasa yaani yai kurutubishwa nje na kupandizwa kitaalamu kama IVF bado uwezekano wa mimba kufika mwisho ni mdogo.

Dalili kuu ya hali hii ni kukosa siku zako za hedhi au kupata siku zako bila mpangilio maalumu na kwa kawaida hakuna dawa ambayo inaweza kukusaidia hapa bila ya wewe mwenyewe kuamua kupunguza uzito kwa mazoezi na chakula,

                                                                  STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                              0653095635/0769846183

FAHAMU JINSI UNENE NA KITAMBI UNAVYOPUNGUZA NGUVU ZA KIUME.

Tunafahamu kwamba unene huambatana na magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na kushindwa kupata usingizi wakati wa usiku lakini tatizo lingine la unene ni kupungua nguvu za kiume, kitu ambacho mara nyingi watu hawa wanene au wenye vitambi hawako wazi kukizungumzia.

                                                                      

Tafiti zinasemaje?

Shirika la kimarekani maarafu kama AUA au American urology association wanasema kwamba asilimia 53% ya wanaume wenye umri kati ya miaka 40 mpaka 70 wana tatizo la nguvu za kiume ambalo husababishwa na umri, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, unene na kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara na kiwango kidogo cha homoni za kiume yaani testosterone.

Hebu tuone uume unavyosimama.

Uume husimama pale damu inapoingia kwenye mishipa ya damu ya uume na kufanya uume ujae damu, mishipa ya damu hutoa kitu kinaitwa nitric oxide ambayo hufanya uume ubaki kwenye hali ile mpaka mwanaume atakapofika mshindo.(dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume huwekewa kemikali hii). Kitu chochote ambacho kinaweza kuharibu sehemu ya ndani ya mishipa ya damu ya uume husabisha uume kuishiwa nguvu.

Unene huathiri vipi nguvu za kiume?

 Mtu akiwa mnene mishipa ya damu pia inakua na mafuta kwa ndani ambayo yanakua yameganda kwenye kuta za mishipa ya damu kitaalamu kama atherosclerosis, hali hii hufanya damu kupita kwa shida kwenda kwenye uume na lakini pia mfumo wa kutengeneza nitric oxide ambayo kazi yake ni kurelax misuli ya uume ili uweze kusimama unaingiliwa.

Sababu nyingine ni ongezeko la  mafuta yaliyopo tumboni au kitambi ambayo hubadilisha homoni ya testosterone kua oestrogen..homoni ya testosterone ndio homoni kuu ya kiume ambayo huleta mabadiko ya yote ya kiume wakati wa kubalehe na huhusika sana na ukubwa na nguvu za kiume na kupungua kwa homoni hii humaliza au kupunguza sana nguvu za kiume.

Mwisho; habari njema ni kwamba wanaume wengi wanene huweza kurudi kwenye hali zao za zamani kwa kupungua uzito tu japokua kama ukipungua bado shida haijaisha basi kuna uwezekano mkubwa homoni zako za testosterone zilipungua na utahitaji dawa za kumeza kuzisahihisha, kumbuka kwamba kupungua uzito sio rahisi lakini ni muhimu sana.

Wengi wenu mmejaribu kupungua uzito maisha yenu yote bila mafanikio kwa kufuata diet na programu mbalimbali bila mafanikio ni vizuri sasa mkawaona wataalamu waweze kuwapa utaalamu sahihi kwa ajili ya kupungua uzito.


                                                                 

                                                                        STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO..MD

                                                              0653095635/0769846183
FAHAMU CHANZO CHA TATIZO LA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA UKIWA SAFARINI.(MOTION SICKNESS)

 Tatizo la kutapika kwenye safari ya gari, meli au ndege ni tatizo ambalo liko miaka mingi hata kabla ya kukua kwa teknolojia na ukisoma vitabu kigiriki na kiroma pia tatizo hilo lilionekana sana miaka hiyo. Mtu yeyote anaweza kupata tatizo hili japokua liko zaidi kwa watoto na mama wajawazito, bahati nzuri sio tatizo la kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.                               

chanzo ni nini? Tatizo hili hutokea pale ubongo unapopata taarifa zinazochanganya kutoka kwenye mwili mmoja yaani macho yanatoa taarifa tofauti, mwili taarifa tofauti na masikio taarifa tofauti. Mfano uko kwenye ndege mwili unatoa taarifa kwenye ubongo kwamba uko unasogea lakini macho yanatoa taarifa kwamba umekaa tu lakini pia maskio ambayo yanahusika sana na kubalance usimame kwenye mstari ulionyooka yanatoa taarifa kwamba umekaa tu, na huu mchanganyiko wa taarifa au signals kwenye ubongo ndio unakufanya utapike.

dalili za hali hii.

 • kichefuchefu
 • mdomo kujaa mate
 • kizungungu
 • kutapika
mambo ya kufanya kupunguza hali hii.
 • pumzika na uangalie sehemu mmoja kwa muda mrefu, vuta pumzi ndefu na na epuka kupepesa macho, kufunga macho pia kunasaidia.
 • angalia vitu ambavyo havitembei, kama uko kwenye boti angalia mawingu na kama uko kwenye gari angalia kioo cha gari.
 • epuka kula kabla ya safari.
 • epuka kuvuta sigara wakati wa safari au harufu nzito.
 • epuka kunywa pombe kabla au wakati wa safari.
dawa za kutumia..
kama hii hali inakusumbua mara kwa mara basi kuna dawa zinaitwa promethazine unaweza kumeza kidonge kimoja saa moja kabla ya safari kisha ukaendelea kumeza kila baada ya nne au sita wakati safari inaendelea.
Kwa kawaida hali hii inatakiwa kuisha baada ya safari, ukiendelea kuugua baada ya safari basi huo ni ugonjwa mwingine muone daktari.

                                                              STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                         0653095635/0769846183