data:post.body Julai 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU JINSI YA KUTAMBUA DALILI ZA MWANZO ZA MTOTO MGONJWA KABLA HAJAZIDIWA ZAIDI.

Watoto wadogo hasa chini ya mwaka mmoja au miwili hawana uwezo wa kuongea hivyo wakianza kuugua unaweza usijue mpaka mtoto azidiwe kabisa ndio unaanza kukimbia usiku kutafuta msaada, sasa watoto wale ni rahisi sana kufariki kuliko watu wazima hivyo kugundua dalili za ugonjwa mapema ni vizuri zaidi kuliko kusubiri dalili za wazi..

Wazazi wengi hasa wazazi wapya wanakua wanafahamu kwamba dalili za kuugua mtoto zinakua wazi kama za watu wote kwa maana nyingine husubiri mpaka mtoto atapike, aharishe,ashindwe kupumua au apate degedege ndio ujue anaumwa.
Kuna dalili za mwanzo kabisa ambazo ukiziona ni vizuri kwenda hospital mapema, hii itamfanya mtoto atibiwe mapema na kuepusha adha zingine kama kulazwa, kutumia gharama kubwa za matibabu, kuugua sana na kupata madhara au kifo.
Mtoto wa kawaida hua na hamu nzuri ya kula, analala vya kutosha, anakua na nguvu na anakua mtundu na mchunguzi sana kwenye mazingira yanayomzunguka.
dalili za kwanza za mtoto mgonjwa ni kama ifuatavyo.......
  • kulia sana hata akiguswa kidogo tu.
  • kuacha kucheza.
  • kua mkimya sana.
  • kuonekana mchovu sana
  • kukataa kula 
  • joto la mwili kuanza kubadilika.
Mara nyingi hizi ni dalili za mwanzo kabisa na ukizipuuzia mtoto huingia kweye hatua ya pili ambayo huzidiwa sana na kuhatarisha maisha yake hivyo ni vizuri kuwahi hospital.
usitoe dawa yeyote kwa mtoto mgonjwa hata kama ni panado, hiyo sio dawa ya kutibu na huweza kuficha dalili za ugonjwa halisi na kumpa shida daktari.

                                                                STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          0769846183/0653095635

FAHAMU TATIZO LA MWANAMKE KUA NA UKE MKAVU NA MATIBABU YAKE.

Tatizo la uke mkavu lipo kwa baadhi ya wanawake japo sio wote, ni tatizo ambalo kimsingi linaweza kuleta msongo wa mawazo kwa wahusika, maumivu wakati wa tendo ndoa,kukosa hamu ya tendo la ndoa,au kuvunja mahusiano kabisa, kupata vidonda ukeni hata kuvuja damu.
Ni tatizo ambalo linaweza kua chanzo cha aibu kwa wanawake na kushindwa kujieleza tatizo hilo kwa wataalamu wa afya kwa kuogopa aibu.

Kushuka kwa kiwango cha homoni ya oestrogen mwilini hasa mwanamke anapofikisha umri wa miaka 40 kwenda mbele ndio chanzo kikuu cha kukauka kwa uke na dalili hizo hua wazi kabisa mwanamke anapofikika menopause au mwisho wa kuona siku zake za mwezi lakini kuna vyanzo vingine kama 
  • msongo wa mawazo
  • kunyonyesha
  • kuvuta sigara
  • baadhi ya magonjwa mfano hypothyrodism
  • mazoezi makali
  • uzazi
  • matibabu ya saratani
  • upasuaji wa kuondoa mayai ya mama.
  • baadhi ya dawa
  • kutokua na hisia na mwenza husika.
Nini cha kufanya?
ukipata tatizo hili unaweza ukamuona mtaalamu wa afya ambaye atakuchukua maelezo marefu na baadae atakupa suluhisho la matatizo yako kulingana na chanzo ambacho atakiona.
Lakini pia kwa wanawake ambao wanapata ukavu huu sababu ya umri basi kuna dawa mbalimbali za kupaka ambazo hua zina homoni ya oestrogen ndani yake ambayo huweza kusaidia tatizo hili, kumbuka tumia dawa tu ambayo imeelekezwa kwa kazi hii kwani baadhi ya dawa zimechanganywa na vitu mbalimbali kama perfume, na vitu asilia ambavyo sio salama kwa uke.

                                                            STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO(MD)
                                                   0653095635/0769846183


YAFAHAMU MAZOEZI 10 BORA SANA KWA AJILI YA KUPUNGUA UZITO.

Kama unasoma makala hii huenda wewe ni mdau wa mazoezi na fitness au una nia ya kupunguza uzito hivyo makala kama hizi zinakuvutia.
Pamoja kwamba ulaji wa chakula unachangia sana mtu kupungua uzito, mazoezi pia yana nafasi yake katika kupungua uzito na kukupa muonekano bomba.
Unaweza kupungua kwa chakula tu lakini utakua kama umekonda yaani hautakua na muonekano mzuri kama mtu ambaye kapungua kwa chakula na mazoezi.

Kuna mazoezi mengi sana ya kupungua uzito na yote yanafanya kazi lakini yanatofautina kasi ya kupungua uzito.
watu wengi wanaamini mazoezi ya kukimbia au aerobic yanapunguza uzito haraka ni kweli yanachoma mafuta hapo hapo lakini mazoezi ya kubeba uzito yanaendelea kukupunguza uzito masaa mpaka siku baada ya mazoezi hayo.
Leo tutaangalia mazoezi kumi ambayo ynapunguza uzito haraka kulingana na wingi wa calories au uzito kumbuka calorie 7700 ni sawasawa na kilo moja ya uzito na upunguaji hutegemea na uzito yaani mtu mwenye uzito mkubwa anachoma calories nyingi kwa kufanya mazoezi sawa na mtu mwenye uzito mdogo.
kubeba chuma; haya ni mazoezi ambayo sio hupunguza tu uzito lakini hujenga na misuli pia na kama nilivyosema hapo mwanzo mazoezi haya huchoma calories 250 mpaka 300 kwa saa lakini kwasaabu shughuli ya kuendelea kuchoma huendelea hata ukiwa ushatoka mazoezini ni kwamba unaweza kuchoma zaidi sababu yaani kesho yake 200, kesho kutwa 100 na kadhalika kwani mwili wako utaendelea kuhitaji oygen nyingi kwa ajili ya misuli hiyo.
kuruka kamba:Ni zoezi ambalo unaweza kulifanya kwenye mazingira yeyote hata kama kuna hali mbaya ya hewa na kifaa chako ni kamba tu na eneo la kurukia..inaweza kua chumbani au sebuleni.
kwa kasi ya kuruka mara 120 kwa kwa dakika unaweza kuchoma calories 667 mpaka 990 kwa saa kulingana na uzito wako.
kukimbia kupanda mlima; ukifanya mazoezi ya kukimbia na kupanda mlima yanachoma mafuta zaidi kuliko kukimbia kawaida kwenye mstari ulionyooka au tumambalale.
kwa kupanda mlima na kushuka unaweza kuchoma calories 639 mpaka 946 kulingana na uzito wako.

mazoezi ya kupigana au kick boxing; sio mazoezi ya watu wengi hasa hap kwetu kwasababu ni mchezo ambao unachukuliwa kwamba ni wa ugomvi tu lakini wanaofanya mazoezi haya huchoma calories 582 mpaka 864.

kuendesha baiskeli; kuendesha baiskeli hasa maeneo yenye muinuko kidogo huku ukichochea kwa kasi sana kunachoma mafuta zaidi kuliko kuendesha taratibu sehemu zenye miteremko.
mazoezi haya yanakadiliwa kuchoma calories 568 mpaka 841.

kukimbia tambalale; mazoezi ya kukimbia uwanjani au mtaani ni moja ya mazoezi pendwa na watu wengi, na yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupungua na kua fit.
mazoezi haya yanakadiriwa kuchoma calories 566 mpaka 839 ukikimbia umbali wa kilometa 16 ndani ya saa moja  kwa mwendo wa kawaida japokua ukikimbia kwa kasi zaidi unachoma zaidi.

mashine ya baiskeli; hii ni ile baiskeli ambayo ni maalumu kwa ajili ya mazoezi, huweza kutumika sehemu yeyote na kukupa majibu mazuri.
naweza kuchoma calories 498 mpaka 738 kama ukiendesha kwa kasi ndani ya saa moja, kumbuka kuongeza ugumu wa baiskeli kwa matokeo chanya zaidi.

mazoezi ya kupanda ngazi; ni mazoezi mazuri hasa kwa watu ambao wanaishi sehemu zenye maghorofa au viwanja vikubwa , unaweza kuamua usitumie lift mara moja moja ukitoka kazini na kupanda kwa ngazi mpaka nyumbani kwako.
mazoezi haya huchoma caories 452 mpaka 670 kwa kila ngazi 77 unazozopanda hasa ukiwa kwa mwendo wa haraka.
planking; haya ni mazoezi ya kukunja mikono kama unalala chini kisha unabaki hivohivo kwa muda fulani mpaka unapochoka na kuachia, zoezi hili ni gumu kidogo lakini unaweza kufanya muda mwingi zaidi kadri unavyozoe na hukadiriwa kuchoma calories 4 mpaka 5 kwa dakika.
                                                   
mwisho; haya ni mazoezi ambayo unaweza kuyafanya kama unataka kupungua haraka lakini kama wewe ni mnene sana au una sababu za kiafya za kushindwa mazoezi haya unaweza ukaanza kwa kutembea kwanza kwani mazoezi ya kutembea pia yana uwezo wa kumpunguza mtu na kumpa afya njema.
                                                                 STAY ALIVE

                                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO (MD)
                                                          0653095635/0769846183