data:post.body Juni 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

UFAHAMU UGONWA WA TEZI DUME NA MATIBABU YAKE.

Tezi dume ni nini?
Huu ni ugonjwa unaotokea baada ya kuvimba kwa tezi inayofahamika kwa jina la prostate gland, tezi hii huanza kuvimba mwanaume anapofikisha miaka arobaini na kuendelea na tafiti zinaonyesha kwamba nusu ya wanaume wa miaka 50 na kuendelea wana tatizo hili.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
Homoni za kiume; homoni maarufu kwa jina la testosterone ni homoni ambazo humfanya mtu aitwe mwanaume kwanzia kubalehe, uzazi wa mwanaume na muonekano wake.
Tafiti zinaonyesha kwamba homoni hii ni moja ya chanzo kikuu kwani wanaume ambao wana tatizo hili kwani wanaume ambao waliondolewa korodani walionyesha kutougua ugonjwa huu.
chakula; Tafiti zinaonyesha kuna mahusiano kati ya aina vya chakula na ugonjwa huu, watu wanaoishi mjini na kula nyama kwa wingi huathirika zaidi kuliko wale ambao wanakula vyakula vya ambavyo vina protini kidogo maeneo ya vijijini.
umri; kuna misuli ambayo inazuguka tezi dume muda wote, umri unavyozidi kwenda basi misuli ile inazidi kuchoka na kuipa nafasi tezi hiyo kuvimba.

dalili za ugonjwa huu.
  • kukojoa mara kwa mara
  • kuamka usiku kukojoa mara kwa mara
  • kushindwa kuzia mkojo ukibana
  • kujikojolea usiku
  • maumivu wakati wa kukojoa 
jinsi ya kugundua tatizo hili
 Tatizo hili linaweza kugunduliwa kwa historia ya mgonjwa, ukaguzi wa kitaalamu au physical examination na kuchukua baadhi ya vipimo.
kipimo cha utrasound huweza kugundua tatizo husika kupima ni kiasi gani tezi hiyo imeongezeka kwa ukubwa.
 Vipimo vingine huchukuliwa kuangalia magonjwa ambayo yameambatana, yanafanana au yameletwa na ugonjwa huu mfano ni kipimo cha sukari, kipimo cha uwezo wa figo kufanya kazi na kipimo cha satatani ya tezi dume kitaalamu kama PSA.

 matibabu; 
matibabu ya tezi dume yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, kuna matibabu ya dawa na matibabu ya upasuaji.
mgonjwa kwa mara ya kwanza utatibiwa na dawa kama finastreride, doxazosin, terazosin na kadhalika na pia atawekewa mpira wa kuondoa mkojo kama atashindwa kukojoa vizuri.
Lakini kama matibabu haya yasipofanya kazi nzuri basi mgonjwa huyu atafanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi hiyo.

Aina hizi za upasuaji zimegawanyika katika sehemu mbalimbali kutokana na teknolojia inayotumika sehemu husika.
Madhara ya upasuaji ni kama kutokwa damu nyingi, kushindwa kutoa mbegu, kuishiwa nguvu za kiume na kuumia kwa njia ya mkojo.


                                                     STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183


ZIJUE SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA VIPIMO VIONYESHE UNA UKIMWI WAKATI HAUNA.(FALSE POSITIVE)

Japokua uwezo wa vipimo vya ukimwi kugundua ukimwi ni mkubwa sana, lakini uwezo huo sio 100%,  vipimo vya ukimwi wakati mwingine huweza kuonyesha kwamba mtu ana ukimwi wakati hana.
Kipindi ambacho kitatumika kujaribu kuthibitisha ni kweli kama mtu huyo sio mgonjwa kunaweza kumuacha katika hali mbaya sana ya kisaikolojia muhusika ambaye tayari anahisi ameambukizwa na hata kuvunja mahusiano.
                                                       
Kulingana na muongozo wa shirika la afya duniani(WHO), mgonjwa hatakiwi kupewa majibu ya kua ameathirika na ukimwi mpaka apimwe na vipimo vya aina tofauti ambavyo vinahakikisha kweli ana maambukizi ya ukimwi.
shirika la doctor without borders(MSF) lilifanya utafiti  na kugundua kwamba vipimo havifanani nguvu hivyo kuleta makosa katika utoaji wa majibu na msisitizo mkubwa ukiwa katika watu ambao wanapewa majibu kwamba wameathirika wakati hawajaathirika.
ushahidi wa hili ni upi?
Data za shirika hilo la msf zinasema kwamba damu ilikusanywa kutoka kwa wagonjwa 2785 wa ukimwi ambao walikua wanahudhuria katika kliniki  mbalimbali za nchini kenya, uganda, congo, guinea na cameroon.
damu hiyo ilihifadhiwa vizuri na kutumwa ubeligiji kwa ajili ya vipimo vya ukimwi ili kuweza kuhakiki kama kweli wale watu ni wagonjwa wa ukimwi.
kati ya watu 2785 ambao damu zao zilichukuliwa, watu 140 walikua hawana ukimwi.
kwa maana nyingine hawa watu 140 wamekua wakimeza dawa za ukimwi kwa muda wote huo kimakosa.
Baada ya kupewa majibu mapya wengine walifurahi, wengine walisikitika kwani walikiua tayari kwenye mahusiano na waathirika wenzao na wengine walikua wameachwa na wake au wame zao sababu ya majibu hayo yenye utata.
sababu za majibu hayo kuja tofauti ni kama ifuatavyo....
magonjwa mengine; vipimo vya ukimwi kitaalamu kama antibody test havipimi virusi moja kwa moja bali hupima antibodies ambayo ni aina fulani ya protini inayotengenezwa kujaribu kupambana na virusi vya ukimwi wakati mtu ameathirika.
Bahati mbaya kwa baadhi ya watu protini hiyo huweza kuonekana kwenye magonjwa mengine kama kichocho, ugonjwa trypanasoma, lupus na aina fulani ya mafua yasababishwao na virusi.kitaalamu tunaita cross reactivity.
mpimaji kutokua na uzoefu; wakati mwingine mtu anaweza kujipima tu nyumbani na kuyapokea yale majibu kabla ya kwenda kupima kwenye vipimo zaidi kuhakikisha, vipimo vingi ambavyo watu wanatumia kujipima nyumbani haviruhusiwi kuthibitisha maambukizi ya ukimwi mpaka mgonjwa apimwe na vipimo vingine kuthibitisha hilo. lakini pia wakati mwingine mtoa huduma anaweza asiwe mzoefu sana kutoa majibu sahihi hasa kama kuna mstari unakuja unafifia.
Kawaida majibu ya ukimwi yanatakiwa yasomwe ndani ya dakika 15 mpaka tu baada ya hapo majibu hayo sio halali tena.
Sasa mtu anaweza kupima nyumbani akaonekana hana akaamua kuhifadhi kipimo, baadae jioni mstari wa pili unaonekana anaanza kuchanganyikiwa.
vipimo vilivopita muda wake wa matumizi; Vipimo hivi hupoteza ubora waka mara tu muda wake wa matumizi unapoisha, hivyo majibu yanayotoka baada ya hapo sio ya kuyaamini hata kidogo kwani hayana uhakika wa kutosha.
Mwisho; majibu ya aina hii ni changamoo sana hasa sehemu ambazo zina uhaba wa vifaa vya kupimia, lakini kwa sehemu ambazo wana mashine za kupima wingi wa virusi baada ya mgonjwa huhisiwa ameathirika, majibu yanaweza kutiliwa mashaka na kuhakikishwa tena na vipimo vikubwa kama PCR.

                                                                STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                    0653095635/0769846183

HAYA NDIO MAGONJWA SABA YA ZINAA YANAYOWEZA KUAMBUKIZWA KWA KULAMBA SEHEMU ZA SIRI.

85% ya vijana umri wa miaka 18 mpaka 44 hushiriki aina ya ngono inayohusisha kulamba sehemu za siri au oral sex.

wengi hudhani kulamba sehemu hizo bila kushiriki tendo la ndoa huweza kuzuia magonjwa ya zinaa kitu ambacho hakina ukweli.
kwa kifupi ni kwamba;
  • unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa mdomoni kwako au kooni kwako kwa kulamba uume, uke au maumbile ya nyuma wa mgonjwa wa zinaa.
  • unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kwa kulambwa sehemu zako za siri na mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa mdomoni kwake au kooni.
  • unaweza kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa sehemu mbili kwa mpigo yaani mdomoni na sehemu za siri.
  • magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa njia ya mdomo yanaweza kusambaa mwili mzima kama yanavyosambaa haya ya kawaida.
  • kulamba sehemu za siri kama mkundu kunaweza kukusababishia magonjwa mengine kama ya ini na minyoo mfano hepatitis A na minyoo ya amiba.
  • ugonjwa wa zinaa unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu ambaye hana dalili hata moja sababu magonjwa mengi za zinaa hayana dalili kabisa.
  • kunyonya sehemu za siri kunaweza kuhamisha virusi fulani ambavyo hukaa sehemu za siri na kukusababishia saratani ya koo.

magonjwa yafuatayo ya zinaa huweza kuambukizwa kwa njia ya kulamba sehemu za siri au oral sex.
ugonjwa wa ukimwi; japokua hatari ya maambukizi ya ukimwi ni ndogo kwa aina hii ya ngono lakini uwezekano upo hasa kwa watu wanaotokwa na damu kwenye fidhi, wenye vidonda mdomoni au sehemu za siri, au watu wenye magonjwa ya zinaa, kwni maji maji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke na sehemu za siri za mwanaume yanakua na virusi vingi sana vya ukimwi.

kisonono; huu ni ugonjwa unaosabbishwa na aina ya bacteria kwa jina la naisseria gonorhea, ni ugonjwa wa zinaa uliokua ukiambukizwa kwa ngono ya kawaida tu lakini tangu kuanza kutumika kwa mdomo pia ugonjwa huu unaweza kukutwa mdomoni na moja ya madhara makubwa ya ugonjwa huu ni ugumba kwa wanawake.
kaswende; huu ni ugonjwa ambao huanza na kidonda kisichokua na maumivu sehemu iliyoathirika...inaweza kua mdomoni, au sehemu za siri baadae hufuatwa na upele mwili mzima, na hata ganzi hatua za mwishoni.
ugonjwa huu hushambulia mishipa ya fahamu hivyo huweza kufika mpaka kwenye ubongo na kuleta ukichaa.
herpes; huu ni ugonjwa unaosababishwa na aina fulani ya virusi kwa jina la herpes simplex type 2, virusi hushambulia sehemu za siri za binadamu lakini vikilambwa huenda kukaa mdomoni, ugonjwa huu huweza kuambatana na virusi vya HPV ambavyo huleta saratani ya koo.

warts; hii na aina fulani ya uvimbe inayotokea sehemu za siri na huweza kuvuja damu sana kama ikijeruhuhiwa, ugonjwa huu hutibiwa kwa kuchomwa na aina fulani ya dawa au upasuaji kuuondoa sehemu husika.
Hepatitis; Huu ni mchnganyiko wa magonjwa ya ini ambayo huambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kugusa majimaji au damu ya mgonjwa, kula uchafu na kadhalika.
Ni moja a magonjwa hatari sana ambayo huleta saratani ya ini ambayo kimsingi haitibiki.

chylamydia; huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unaweza kuambukizwa kwa njia ya tendo la ndoa la kawaida au lulamba sehemu za siri.
huweza kuvamia mlango wa kizazi, kizazi chenyewe na mirija ya uzazi.

Mwisho; kulamba sehemu za siri sio mbadala wa kukimbia magonjwa ya zinaa, kama unaitaka huduma hii basi ni vizuri uwe na mpenzi mmoja ambaye ni muaminifu lakini kama una mahusiano mengi basi ni bora uwe mvaaji mzuri wa kondomu na usikubali kulamba wala kulambwa.
baadhi ya magonjwa ya zinaa hayana dalili kabisa na utakuja kujua siku unatafuta mtoto humpati.

                                                                     STAY ALIVE

                                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                               0653095635/0769846183