data:post.body SABABU KWANINI UACHE SIGARA, BANGI NA SHISHA KIPINDI HIKI CHA CORONA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

SABABU KWANINI UACHE SIGARA, BANGI NA SHISHA KIPINDI HIKI CHA CORONA.

Kati ya waathirika wakubwa wa covid19 ni wavuta sigara, bangi na shisha ambao shirika la afya duniani limewataja kama moja ya watu ambao wanakufa sana kutokana na ugonjwa huu.
Sababu kubwa ikiwa ni kudhoofu kwa mapafu yao na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kushindwa kupambana na ugonjwa iwapo wakipata maambukizi ya virusi vya corona. kwenye picha chini ni mapafu ya mvutaji kulia  na mapafu ya mtu asiyevuta kushoto.kwanini watu hawa ni wahanga?
uvutaji wa vitu hivi huambatana na uingiaji wa kemikali nyingi sana kwenye mapafu ambazo hushusha sana kinga ya mapafu,huleta makovu kwenye mapafu na kupunguza uwezo wake wa kuingiza na kutoa hewa na kumfanya mgonjwa kuwepo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya mapafu.
Hata hivyo kemikali hizo haziishii hapo, husambazwa na damu inayotoka kwenye mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kuathiri viungo vya mwili mzima kama figo, moyo, ubongo na hata mirija ya uzazi.

kwanini uache kuvuta sasa hivi?
Masaa 12 tu baada ya kuacha sigara, kiwango cha hewa chafu ya carbon monoxide hupungua kwa kiasi kikubwa mwilini, uwezo wa mapafu kufanya kazi huongezeka baada ya miezi miwili mpaka mitatu na vinyweleo vidogo ambavyo hulinda mapafu huota baada ya miezi tisa.
maana yake ni kwamba ukiacha sasa hivi ndani ya masaa 12 unakua umeweka mwili wako kwenye mazingira salama na siku zinavyozidi kwenda unazidi kujiokoa.
Kama huwezi kuacha kuvuta kwa ajili yako mwenyewe basi acha kwa ajili ya ndugu zako ambao watabaki wanakulilia ukifa.
Kumbuka huu sio muda wa kupunguza, ni muda wa kuacha.

                                                                   STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni