data:post.body FAHAMU JINSI UGONJWA WA CORONA UNAVYOUA.(COVID19) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU JINSI UGONJWA WA CORONA UNAVYOUA.(COVID19)

Elimu ya msingi ya ugonjwa wa COVID19 ishatolewa na jinsi gani ugonjwa huu unavyosambazwa na jinsi gani ugonjwa huu unavyoweza kuzuilika kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Lakini kuna watu bado hawafahamu ni jinsi gani kirusi hiko kinaingia mwilini na kuua mtu ndani ya muda mfupi kiasi hicho wakati virusi vingine kama vya ukimwi huchukua miaka kuua.

Virusi vya corona virus huingia mwilini kupitia mifumo ya hewa yaani pua na mdomo baada ya hapo huanzisha dalili kama za mafua na homa kwa mgonjwa na hii ni hatua ya kwanza ya ugonjwa huu, baadhi ya watu ugonjwa huu huweza kuishia hapa na wakapona lakini kwa watu wengine ugonjwa huu huendelea mpaka kwenye mapafu na kumfanya mgonjwa kushindwa kupumua vizuri.

Hatua hii ikifika basi mwili wa binadamu hujaribu kupambana na virusi hawa kwa kutoa chembechembe nyeupe za damu kama askari wa mwili kupambana na hali hii baadhi ya watu huweza kupona katika hatua hii lakini kwa bahati mbaya mwili unaweza ukapambana na virusi kwa nguvu nyingi kiasi cha kuharibu mapafu yenyewe.

Kipindi hiki hali ya mgonjwa huzidi kua mbaya kwani mapafu hujaa maji na mgonjwa huendelea kupumua kwa shida sana, lakini pia bacteria hupata nafasi ya kushambulia na kufanya hali ya mgonjwa iwe mbaya zaidi.

Wakati huu sasa mgonjwa anahitaji huwekewa mashine za ventilator ambazo kazi yake ni kupuliza hewa ya oxygen kwenye mapafu na kumsaida mgonjwa kuvuta hewa ndani na kutoa hewa nje kwani yeye mwenyewe anakua hana uwezo wa kupumua mweyewe.

Pamoja na matibabu yote hayo, kifo hutokea pale sehemu kubwa ya mapafu yanapokua yameathirika na mgonjwa anakua hawezi tena kupumua hata kwa msaada wa ventilator,(acute respiratory failure) lakini pia kifo hutokea pale bacteria wanaposambaa mwili mzima na kuathiri vitu vingine kama ubongo, moyo, mishipa ya damu na figo.
Hatua hii mgonjwa tunaweza kusema anakua nje ya uwezo wa madaktari kumtibu hivyo hupoteza maisha.

mwisho; Tuendelee kujikinga na maambukizi kwa kufuata maelekezo ya serikali na kufuata masharti, kama hauna kitu cha msingi cha kufanya nje ya nyumba basi usisubiri marufuku ya serikali.
wewe mwenyewe kaa ndani.

                                                                   STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0769846183/0653095635

0 maoni:

Chapisha Maoni