data:post.body UFAHAMU UGONJWA ULIOUA WATU WENGI ZAIDI KWENYE HISTORIA YA DUNIA.(THE BLACK DEATH) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA ULIOUA WATU WENGI ZAIDI KWENYE HISTORIA YA DUNIA.(THE BLACK DEATH)

Mwishoni mwa mwezi octoba mwaka 1347 karne ya 14, meli 12 ziliwasili katika bandari ya messina mji wa sicily nchini Italia zikiwa zimetokea bahari nyeusi maarufu kama the black sea.
Sababu ilikua moja ya bandali kubwa ya kibiashara watu walisogea ili kupokea meli hizo na kupigwa na butwaa baada ya kukuta watu waliokua kwenye meli zile wengi walikua wamekufa na wengine walikua wagonjwa sana huku wakivuja usaa, damu na kutoa harufu kali milini mwao.
Viongozi wa mji ule walitoa amri haraka meli zile ziondolewe bandarini pale lakini walikua wameshachelewa.

Ndani ya miaka miwili ugonjwa uliua Zaidi ya watu milioni mia mbili ulaya, afrika na asia huku Zaidi ya 1\3 ya bara la ulaya lilikua limeuawa.
Ni moja ya vifo vingi kuwahi kutokea katika kipindi cha muda mfupi katika historia ya dunia, watu milioni mia mbili ni kama Tanzania nne.

Sababu ya uelewa mdogo wa biolojia kipindi hicho, watu hawakujua chanzo na jinsi ugonjwa huo unavyosambaa hivyo uliendelea kuua watu wegi zaidi na zaidi.
Ugonjwa ulisambaa ukaenda ufaransa, roma, uingereza, nchi za asia na afrika.
Kasi ya mauaji ilikatisha tamaa kwani mtu angeweza kulala usiku akiwa mzima kabisa na asubuhi akakutwa ashafariki.
Madakatari walikataa kuona wagonjwa, wachungaji walikataa kuzika na kuombea wafu na maduka mengi yakafungwa huku watu wakikimbia miji yao.

Lakini huu ni ugonjwa gani?
Huu ugonjwa ulifahamika kwa jina la plague, uliambukizwa na viroboto, aina fuani ya wadudu wanaoruka ambao walikua wanatoa ugonjwa kutoka kwenye panya kwenda kwa binadamu, bateria aliyekua anahusika kuleta ugonjwa huu alikua anaitwa Yersinia pestis hivyo ulikua uking'atwa na viroboto hawa unapata ugonjwa huu lakini pia kugusa mgonjwa, na kuchangia hewa  iikua ni tiketi ya moja kwa moja ya kuugua ugonjwa huu.

Je ilikua laana ya Mungu?
Wengi waliamini kwamba ilikua ni laana kutoka kwa mungu hivyo walijitahidi kutubu zambi zao na kuwaua watu ambao walidhaniwa kwamba ni wakosefu ndani ya jamii na ndio maana wahayahudi wengi sana waliokua wakiishi ulaya waliuawa sana kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha yesu lakini hizo zilikua ni Imani tu.

ugonjwa huu ulienda wapi?
Ugonjwa huu uliendelea kuja na kuondoka huku ukiua mamilioni ya watu mpaka karne ya 20 mwaka 1928 ambapo mwanasayansi alexander fleming aligundua antibayotiki ya kwanza ndipo ugonjwa huu ulianza kutibika kabisa, lakini pia kuongezeka kwa teknolojia na usafi wa hali ya juu majumbani ulitokomeza kabisa viroboto hasa kwenye mazingira ya mjini.
Mpaka leo ugonjwa huu bado upo kwa kiasi kidogo sana, shirika la marekani la magonjwa ya kuambukiza linaamini kila mwaka wagonjwa 600 hupatikana duniani kote lakini hatari ya kifo ni ndogo sana.

Tutegemee nini siku za usoni?
Kuna hatari kubwa sana ya magonjwa mengi ya ajabu kuja siku za usoni sababu antibayotiki nyingi tunazotegemea zimeanza kufeli sababu ya bacteria kuanza kubadilika na matumizi mabaya ya dawa hizo lakini pia virusi ambavyo mara nyingi havina dawa vimeanza kuishambulia dunia kwa kasi sana, ukiachana virusi vya ukimwi ambao mpaka sasa umeua watu Zaidi ya milioni 40, virusi vya ebola, virusi vya corona bado kuna Zaidi ya virusi milioni moja ambavyo viko kimya na kati ya hivyo watafiti wameweza kutambua kama virusi 700 tu.
Wakati huo huo baadhi ya nchi zinatumia virusi hivi kama silaha kwa kuvigeuza na kuvifanya vikali Zaidi huko maabara.

                                                                              STAY ALIVE

                                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                          0653095635/0769846183Maoni 2 :