data:post.body SABABU 1 KWANINI NI MUHIMU KUPIMA UKIMWI KIPINDI HICHI CHA CORONA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

SABABU 1 KWANINI NI MUHIMU KUPIMA UKIMWI KIPINDI HICHI CHA CORONA.

Tangu ugonjwa huu wa corona umeanza kuishambulia dunia tumekua tukisikia habari za uhakika kutoka shirika la afya duniani yaani WHO kuhusu wahanga wakubwa wa ugonjwa huu ni watu wa aina gani.

Wataalamu wanasema kwamba watu ambao kinga zao za mwili ziko chini kama wazee sana na watu wenye magonjwa ambayo yanashusha kinga ya mwili kama kisukari na saratani wako kwenye hatari kubwa ya kua wahanga wakuu.

Lakini kwa hapa kwetu Tanzania na Africa kwa ujumla magonjwa yanayoshusha kinga sio hayo tu ila kuna ugonjwa wa ukimwi na utapiamlo pia.
Swala la virusi vya ukimwi ni hatari zaidi kwani kwani kuna watu wengi wameathirika, kinga zao zimeshuka na hawana habari kama wao ni wahanga.

Ripoti ya shirika la ukimwi duniani UNSAID  mwaka 2013 inaonyesha kwamba kati ya watu milion 35 ambao wameathirika dunia nzima, milioni 19 hawajui kama wamethirika na kama tunavyofahamu kwamba wagonjwa wengi wa ukimwi wanaishi afrika basi huenda hata wewe msomaji wa Makala hii hujui afya yako au umepima zamani sana.

Ugonjwa wa corona unaweza usiwe hatari kwa wagonjwa wa ukimwi ambao wamepima na wanatumia dawa sababu kinga zao kwa sasa ziko imara ila ni hatari kwako ambaye hujui afya yako.

Nitoe nafasi hii kutoa wito kwa watu ambao hawajui afya zao hasa wanaume kwani wao ndio wagumu sana kupima, ni vizuri kupima na kujua afya yako.
Kama ulipima mwaka jana basi huu ni muda muafaka tena kupima kwani miezi kadhaa imepita na huenda majibu yako ya mwaka jana sio majibu yako ya mwaka huu.
Sio kwamba natishia, lakini naamini hata kama hauna sasa hivi basi utajiamini na kuendelea kujikinga Zaidi.

                                                       STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni