data:post.body MAKOSA MATANO UNAYOFANYA WAKATI WA KUPIMA UZITO. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MAKOSA MATANO UNAYOFANYA WAKATI WA KUPIMA UZITO.

Kujipima uzito ni muhimu sana ukiwa unataka kupunguza, kuongezeka au kubaki na uzito wako wa kila siku, kimsingi kila mtu anatakiwa awe na mzani wake hasa kipindi hiki ambacho watu wengi wana uzito mkubwa na lengo kuu ni kupungua uzito.
Swala la kupima tu uzito peke yake lina umuhimu sana kisaikolojia na linaweza kukufanya ukate tamaa au upate moyo wa kuendelea na diet au mazoezi unayofanya.
makosa yenyewe ni kama ifuatavyo...
                                                             
kupima uzito jioni; kupima uzito mchana au jioni ni makosa sana kwani hakuonyeshi uhalisia, maana muhusika anakua ameshakula na kunywa maji mengi.
inategemea na kiasi ulichokula na kunywa lakini kumbuka lita moja ya maji ni sawa na kilo moja kwenye mzani hivyo muda mzuri wa kupima uzito ni asubuhi ukiwa haujala chochote yaani umeshakaa saa Zaidi ya 8 ukiwa umelala bila kula chakula chochote.
Hivyo ukiamka asubuhi kojoa kwanza na kama unasikia haja kubwa basi kajisaidie kisha pima uzito.
kupima uzito kila siku; kupungua au kuongezeka uzito sio safari ya siku moja bali ni safari ya muda mrefu sana ambayo inataka nidhamu kubwa, baadhi ya vyakula vinaweza kukufanya uonekane umepungua uzito na vingine vikaonesha umeongezeka.
mfano ukiacha sukari, vyakula vya chumvi na wanga ghafla utaonekana umepungua ndani ya siku moja lakini ni maji ndio yamepungua Zaidi na sio mafuta kwani vyakula ulivyoacha vinakufanya uhifadhi maji mengi Zaidi mwilini.
Baadhi ya diet kama ketogenic diet hukufanya ukojoe sana na kupunguza maji mwilini na hii itakufanya uhisi umepungua, kimsingi unatakiwa upime uzito angalau mara moja au mbili kwa wiki baada ya kuanza diet mpya hii inaupa mwili muda wa kufanya regulations na kutoa majibu ya kweli.
Wataalamu wa lishe wanaamini binadamu anatakiwa apungue nusu kilo au kilo moja kwa wiki hivyo kupima kila siku kunaweza kukufanya uhisi uko pale pale au unaongezeka kumbe umeanza kupungua ila mwili wako bado haujaanza kuonyesha kwenye mzani hasa kama unakunywa maji mengi kwenye diet yako.
kutumia mizani tofauti; mizani mingi ina formula tofauti, tafiti zimeonyesha kwamba kunaweza kua na tofauti ya hata kilo moja au mbili kwa kila mzani.
hivyo epuka tabia ya kupima uzito barabarani au kupima uzito nyumbani kisha ukienda gym tena unapima uzito.
chukua mzani mmoja na upime kwenye huo huo kila mara ili kuangalia maendeleo yako.
kupima uzito na nguo; kitaalamu mzani unatakiwa ukae bafuni, sehemu ambayo unapima ukiwa hujavaa nguo yeyote, ile tabia ya kufika sehemu kisha  unapanda mzani ukiwa na simu, pochi, nguo,begi na funguo sio nzuri..tafiti zimeonyesha tabia ile inaweza kuongeza uzito mpaka kilo moja au nusu kilo ambazo si zako.
kupima uzito baada ya mazoezi; ukiingia gym kufanya mazoezi utatokwa na jasho jingi sana mpaka nusu lita au lita moja, ukimaliza ukapima uzito utaona umepungua lakini ukweli ni kwamba umepungua maji tu na uzito wa kweli utaaupata baada ya siku mbili au tatu.

                                                                        STAY ALIVE

                                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                 0769846183/06530956350 maoni:

Chapisha Maoni