data:post.body Machi 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU UGONJWA WA MAFUA ULIOUA WATU WENGI ZAIDI KWENYE HISTORIA YA DUANIA.(H1N1 VIRUS)

Mwezi January mwaka 1918, miaka 102 iliyopita wakati vita kuu ya dunia ikielekea ukingoni dunia ilipigishwa magoti na ugonjwa mpya uliovamia ghafla.
Watu walianza kua na dalili za mafua, kichwa kuuma, homa, kikohozi na kuishiwa nguvu.
Wanahistoria wanaamini kwamba ugonjwa huu ulianzia ufaransa ambapo majeshi ya uingereza yalikua yameweka vikosi vyao kwa utitiri wa askari wengi sehemu moja.
                                                                     
Lakini ugonjwa huu ulipewa jina la Spanish flu, sababu uliripotiwa sana nchini Hispania, nchi nyingi ambazo zilikua zinapigana vita zilificha idadi ya wafu wao ili kumficha adui na kuongeza morali ya vita.

Ugonjwa huu ulikua ni ugonjwa hatari zaidi wa mafua kuwahi kutokea duniani na pia ni ugonjwa ulioua watu wengi  kwa mpigo karne  ya 20, ukisababishwa na virusi vya H1N1.
 Ugonjwa huu ulishambulia moja ya tatu  ya dunia yaani watu milion 500 waliugua ugonjwa huku ukiua watu Zaidi ya milion 100.

Tofauti na ugonjwa wa COVID 19 ambao unaua sana wazee na watu ambao kinga zao ziko chini kama wagonjwa wa sukari na saratani...ugonjwa huu uliua watoto chini ya miaka mitano, vijana umri wa miaka 20 mpaka 40, na watu wazima Zaidi ya miaka 65.

Kukiwa hakuna chanjo, dawa ya kutibu ugonjwa, wala antibayotiki ya kuzuia bacteria wengine kushambulia… ugonjwa ndani ya miaka miwili ugonjwa ulikua umeshaua watu wengi sana huku ukisambaa kwa kasi sana na kushambulia dunia nzima.

Mwaka 1920 ugonjwa huu ulipotea na  baadae tena mwaka  2009 ugonjwa huu ulirudi tena sehemu mbalimbali duniani na kushambulia watu billion moja na laki nne huku ukiacha vifo laki tano.
Shirika la afya duniani wanaamini ugonjwa bado upo ila kwa kiasi kidogo lakini una tabia ya kulipuka kila baada ya muda Fulani.
Bahati nzuri chanjo yake ipo na dawa za kutibu ugonjwa huu kwa sasa zipo japokua wakati mwingine virusi vinakua vikali kuliko dawa na bado mtu anakufa.

Historia ya dunia imeandikwa kwa kalamu yenye damu nyingi sana, watu wengi sana wamepoteza Maisha kwa mgonjwa mbalimbali, vita, ajali na matetemeko makubwa ya dunia huku magonjwa na vita yakiua watu wengi Zaidi.

                                                                 STAY ALIVE

                                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

SABABU 1 KWANINI NI MUHIMU KUPIMA UKIMWI KIPINDI HICHI CHA CORONA.

Tangu ugonjwa huu wa corona umeanza kuishambulia dunia tumekua tukisikia habari za uhakika kutoka shirika la afya duniani yaani WHO kuhusu wahanga wakubwa wa ugonjwa huu ni watu wa aina gani.

Wataalamu wanasema kwamba watu ambao kinga zao za mwili ziko chini kama wazee sana na watu wenye magonjwa ambayo yanashusha kinga ya mwili kama kisukari na saratani wako kwenye hatari kubwa ya kua wahanga wakuu.

Lakini kwa hapa kwetu Tanzania na Africa kwa ujumla magonjwa yanayoshusha kinga sio hayo tu ila kuna ugonjwa wa ukimwi na utapiamlo pia.
Swala la virusi vya ukimwi ni hatari zaidi kwani kwani kuna watu wengi wameathirika, kinga zao zimeshuka na hawana habari kama wao ni wahanga.

Ripoti ya shirika la ukimwi duniani UNSAID  mwaka 2013 inaonyesha kwamba kati ya watu milion 35 ambao wameathirika dunia nzima, milioni 19 hawajui kama wamethirika na kama tunavyofahamu kwamba wagonjwa wengi wa ukimwi wanaishi afrika basi huenda hata wewe msomaji wa Makala hii hujui afya yako au umepima zamani sana.

Ugonjwa wa corona unaweza usiwe hatari kwa wagonjwa wa ukimwi ambao wamepima na wanatumia dawa sababu kinga zao kwa sasa ziko imara ila ni hatari kwako ambaye hujui afya yako.

Nitoe nafasi hii kutoa wito kwa watu ambao hawajui afya zao hasa wanaume kwani wao ndio wagumu sana kupima, ni vizuri kupima na kujua afya yako.
Kama ulipima mwaka jana basi huu ni muda muafaka tena kupima kwani miezi kadhaa imepita na huenda majibu yako ya mwaka jana sio majibu yako ya mwaka huu.
Sio kwamba natishia, lakini naamini hata kama hauna sasa hivi basi utajiamini na kuendelea kujikinga Zaidi.

                                                       STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0653095635/0769846183

SABABU 3 KWANINI UGONJWA WA CORONA VIRUS UNAWEZA USIWE NA MADHARA MAKUBWA AFRIKA.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa habari za BBC na CNN utagundua kwamba taarifa zinasema kwamba ni 2%  pekee ya wagonjwa wanaopata corona wanafariki dunia na habari zinaongeza kusema watu wengi wanaokufa ni umri wa miaka 81 na kuendelea na wengine ni wale wenye magonjwa sugu ambayo yanashusha kinga kama kisukari, magonjwa ya moyo,saratani na wavutaji sigara wa muda mrefu.
                                                                 
Kitakwimu 42.2% ya vifo ni umri wa miaka  80 mpaka 89, 32.4% umri wa miaka 70 mpaka 79,  8.4% umri wa miaka 60 mpaka 69 na 2.8% miaka 50 mpaka 59. Hizi  ni takwimu za vifo nchini Italy.
sasa kwa akili ya kawaida mambo yafuatayo yanaweza yakasababisha ugonjwa huu uwe wa kawaida Africa.
umri wa waafrika; kama umesoma jiographia kwenye topic ya idadi ya watu duaniani au population utagundua kwamba idadi kubwa ya waafrika ni vijana huku ikiwa na wazee wachache sana lakini pia idadi ya wazee nchi zilizoendelea ni kubwa kuliko vijana au inalingana na vijana kitu ambacho kinafanya waathirike zaidi.
chati hiyo hapo chini kushoto inaonyesha idadi ya waafrika kulingana na umri kwamba watoto na vijana ni wengi Zaidi wakati hiyo ya kulia ya ulaya inaonyesha watoto, vijana na wazee wanataka kulingana huku wakiwa na tofauti ndogo sana. 
kinga imara ya waafrika; Siku zote jamii inayopigwa na magonjwa mengi kwa muda mrefu inatengeneza kinga yenye nguvu sana, Afrika ni sehemu ambayo huwezi kuishi kama wewe ni legelege kiafya kwani utakufa tu, wataalamu wanaita survival of the fittest.
Mtu akifikisha miaka mitano tu afrika anakua amekwepa mikuki mingi ya magonjwa kuliko watu wanaokulia ulaya.
Mfano halisi ni mafua ya influenza ambayo inakadiriwa kwamba yanaua watu laki sita na elfu hamsini kila mwaka duniani na nchi nyingi ulaya zinatoa chanjo za mafua haya kila mwaka kuwalinda watu wake, chakushangaza ni kwamba chanjo hiyo haitolewi afrika kwa watu wazima na hakuna mtu ashawahi kushuhudia mafua yanamuua mwafrika.
hali ilivyo mpaka sasa hivi; kwa ushahidi wa macho yaani evidence based medicine inaonekana hatari ni ndogo sana, wakati Italy wakirekodi mpaka vifo 2000 kwa siku sisi hapa kwetu hakuna kifo wala hakuna nchi ya afrika iliyorekodi vifo vingi hivyo.
Yule mgonjwa wa kwanza Tanzania anaendelea vizuri kitu ambacho kinaleta matuamaini makubwa sana.
Lakini pia wagonjwa ambao wameripotiwa mpaka sasa hivi ni wachache afrika ukilinganisha na nchi za ulaya, japokua shirika la afya duniani WHO limekosoa na kusema kwamba afrika hakuna vipimo vya kutosha kwa hiyo hakuna uhakika wa namba zinapotajwa kwa tafsiri nyingine ni kwamba hata kama wapo hawana dalili na hawajafa na hiyo dalili nzuri.
mwisho; sijasema kwamba watu wasichukue tahadhari bali nimeandika kupunguza hofu na taharuki ambayo imeletwa na watu wengi wanaosambaza habari za uongo kuhusu ugonjwa huu.
Watu wengi wamepaniki sana lakini hakuna sababu ya kupaniki, kikubwa kusikiliza maelekezo ya shirika la afya duniani na wizara ya afya.

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

0653095635/ 0769846183







FAHAMU JINSI MAGONJWA YANAVYOTENGENEZWA MAABARA KUUA WATU.(BIOTERRORISM)

Bioterrorism ni nini?
Hii ni njia ya kuachia virusi, bacteria au fangasi kwenye jamii ya watu, mazao au mifugo ili kuweza kuwaambukiza kwa makusudi ugonjwa fulani na kuua kila kitu chenye uhai kwenye sura ya ardhi.
Hii inawezekana kwa kutumia mabomu maalumu, chakula, maji, dawa za kupuliza na kuchoma sindano.
Silaha hizi ni moja ya silaha hatari zaidi duniani kwani zikitupwa sehemu zinahakikisha hakuna uhai unaobaki, hata samaki na wadudu wa kwenye maji hufariki.
Kumekua na tetesi nyingi sana kwamba huenda ugonjwa wa corona virus umetengenezwa makusudi kuua watu au umewaponyoka maabara lakini hakuna ushahidi wa kutosha japokua hatuwezi kupinga kwani hilo linawezekana kwa asilimia mia moja na historia ya dunia imeonyesha mataifa yalioyofanya hivyo wakati wa vita Fulani Fulani.

magonjwa haya yanatengenezwa vipi?
Gene therapy ni teknolojia ambayo ililetwa mahususi kwa ajili ya kutumika kusaidia kutibu magonjwa kama siko seli, saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya kuvuja damu na hata ukimwi kwa kubadilisha vimelea au gene ambazo zinachochea magonjwa hayo na kuweka gene mpya ambazo zinazuia magonjwa hayo.
Mpaka sasa hivi wagonjwa wengi wamefaidika na teknolojia hiyo lakini ka upande wa pili teknolojia hiyo inatumika vibaya kutengeneza magonjwa hatari na ya kutisha.
Wanasayansi huchukua vimelea au DNA ya  bacteria, virusi au fangasi kisha hutengeneza wadudu wengine wengi wa aina hiyo hiyo  kitaalamu kama cloning kisha huwabadilisha maumbile wadudu hao na kuwafanya wasiweze kutibika na dawa zilizopo.
mfano kama bacteria Fulani alikua na uwezo wa kutibiwa kwa kuharibu gamba lake la nje kitaalamu kama cell wall basi gamba lile huondolewa kwa teknolojia ya gene therapy  na kumfanya bacteria yule kushindwa kutibika.

kwanini corona virusi haitibiki sasa hivi?
Ugonjwa wa corona ulikuepo tangu mwaka 1960, na ulikua sio ugonjwa hatari lakini ghafla ulibadilika mwaka 2019 na kua ugonjwa tishio kitu ambacho kinaleta mashaka kwamba huenda virusi hao wamebadilishwa na kuongezewa nguvu maabara.
Mpaka sasa hivi hakuna mtu aliyekubali kuhusika na ugonjwa huo japokua kuna mashaka kwamba ugonjwa huu umetengenezwa.

Nchi ambazo zilitengeneza magonjwa kwenye historia ya dunia.
Mwaka 1944 wakati ya vita kuu ya pili ya dunia nchi za marekani, uingereza, urusi, china na wenzake walitengeneza maabara kubwa za kutengeneza bacteria wa anthrax, brucellosis, na sumu botulism kwa ajili ya kupambana na wapinzani wake wa japan, ujeruman na italia lakini bahati nzuri vita iliisha kabla ya silaha hizo za kibiologia hazijatumika.

Wakati wa vita ya pili ya dunia japan iliweka bacteria wa kupindupindu kwenye mito 1000 ya maji nchini china na kuua Zaidi ya watu 30000, ugonjwa huo uliendelea kuua watu hata baada ya kuisha kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Mwaka 1979 maabara moja nchini urusi iliachia virusi vya anthrax bahati mbaya na kuua watu 66, serikali ya nchi hiyo ilipinga swala hilo lakini baadae ilikubali.

Mwaka 2001 barua ilitumwa nchini marekani ikiwa na bacteria wa anthrax ndani yake na kuua watu watano, haikufahamika barua ile ilitoka wapi.

Wakati wa vita ya mungolia, askari wake walitupa maiti zilizouawa na ugonjwa wa plague kwa wapinzani  ili kusambaza  ugonjwa huo sehemu mpya, hii ni moja ya sababu ya kuchelewa sana kuisha wa ugonjwa huo.

Tutarajie nini miaka ijayo?
kuna uwezekano mkubwa silaha hizi kutumika sana dunia hii ya sasa sababu ya kukua sana kwa teknolojia ya kutengeneza magonjwa haya na mbinu za kupambana kiuchumi kwa mataifa mbalimbali kwani vita ya silaha za kawaida zina athiri sana miundombinu, nyumba za kuishi, viwanda na miji mikubwa iliyojengwa kwa miaka mingi.

                                                                 STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183

UFAHAMU UGONJWA ULIOUA WATU WENGI ZAIDI KWENYE HISTORIA YA DUNIA.(THE BLACK DEATH)

Mwishoni mwa mwezi octoba mwaka 1347 karne ya 14, meli 12 ziliwasili katika bandari ya messina mji wa sicily nchini Italia zikiwa zimetokea bahari nyeusi maarufu kama the black sea.
Sababu ilikua moja ya bandali kubwa ya kibiashara watu walisogea ili kupokea meli hizo na kupigwa na butwaa baada ya kukuta watu waliokua kwenye meli zile wengi walikua wamekufa na wengine walikua wagonjwa sana huku wakivuja usaa, damu na kutoa harufu kali milini mwao.
Viongozi wa mji ule walitoa amri haraka meli zile ziondolewe bandarini pale lakini walikua wameshachelewa.

Ndani ya miaka miwili ugonjwa uliua Zaidi ya watu milioni mia mbili ulaya, afrika na asia huku Zaidi ya 1\3 ya bara la ulaya lilikua limeuawa.
Ni moja ya vifo vingi kuwahi kutokea katika kipindi cha muda mfupi katika historia ya dunia, watu milioni mia mbili ni kama Tanzania nne.

Sababu ya uelewa mdogo wa biolojia kipindi hicho, watu hawakujua chanzo na jinsi ugonjwa huo unavyosambaa hivyo uliendelea kuua watu wegi zaidi na zaidi.
Ugonjwa ulisambaa ukaenda ufaransa, roma, uingereza, nchi za asia na afrika.
Kasi ya mauaji ilikatisha tamaa kwani mtu angeweza kulala usiku akiwa mzima kabisa na asubuhi akakutwa ashafariki.
Madakatari walikataa kuona wagonjwa, wachungaji walikataa kuzika na kuombea wafu na maduka mengi yakafungwa huku watu wakikimbia miji yao.

Lakini huu ni ugonjwa gani?
Huu ugonjwa ulifahamika kwa jina la plague, uliambukizwa na viroboto, aina fuani ya wadudu wanaoruka ambao walikua wanatoa ugonjwa kutoka kwenye panya kwenda kwa binadamu, bateria aliyekua anahusika kuleta ugonjwa huu alikua anaitwa Yersinia pestis hivyo ulikua uking'atwa na viroboto hawa unapata ugonjwa huu lakini pia kugusa mgonjwa, na kuchangia hewa  iikua ni tiketi ya moja kwa moja ya kuugua ugonjwa huu.

Je ilikua laana ya Mungu?
Wengi waliamini kwamba ilikua ni laana kutoka kwa mungu hivyo walijitahidi kutubu zambi zao na kuwaua watu ambao walidhaniwa kwamba ni wakosefu ndani ya jamii na ndio maana wahayahudi wengi sana waliokua wakiishi ulaya waliuawa sana kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha yesu lakini hizo zilikua ni Imani tu.

ugonjwa huu ulienda wapi?
Ugonjwa huu uliendelea kuja na kuondoka huku ukiua mamilioni ya watu mpaka karne ya 20 mwaka 1928 ambapo mwanasayansi alexander fleming aligundua antibayotiki ya kwanza ndipo ugonjwa huu ulianza kutibika kabisa, lakini pia kuongezeka kwa teknolojia na usafi wa hali ya juu majumbani ulitokomeza kabisa viroboto hasa kwenye mazingira ya mjini.
Mpaka leo ugonjwa huu bado upo kwa kiasi kidogo sana, shirika la marekani la magonjwa ya kuambukiza linaamini kila mwaka wagonjwa 600 hupatikana duniani kote lakini hatari ya kifo ni ndogo sana.

Tutegemee nini siku za usoni?
Kuna hatari kubwa sana ya magonjwa mengi ya ajabu kuja siku za usoni sababu antibayotiki nyingi tunazotegemea zimeanza kufeli sababu ya bacteria kuanza kubadilika na matumizi mabaya ya dawa hizo lakini pia virusi ambavyo mara nyingi havina dawa vimeanza kuishambulia dunia kwa kasi sana, ukiachana virusi vya ukimwi ambao mpaka sasa umeua watu Zaidi ya milioni 40, virusi vya ebola, virusi vya corona bado kuna Zaidi ya virusi milioni moja ambavyo viko kimya na kati ya hivyo watafiti wameweza kutambua kama virusi 700 tu.
Wakati huo huo baadhi ya nchi zinatumia virusi hivi kama silaha kwa kuvigeuza na kuvifanya vikali Zaidi huko maabara.

                                                                              STAY ALIVE

                                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                          0653095635/0769846183



MAKOSA MATANO UNAYOFANYA WAKATI WA KUPIMA UZITO.

Kujipima uzito ni muhimu sana ukiwa unataka kupunguza, kuongezeka au kubaki na uzito wako wa kila siku, kimsingi kila mtu anatakiwa awe na mzani wake hasa kipindi hiki ambacho watu wengi wana uzito mkubwa na lengo kuu ni kupungua uzito.
Swala la kupima tu uzito peke yake lina umuhimu sana kisaikolojia na linaweza kukufanya ukate tamaa au upate moyo wa kuendelea na diet au mazoezi unayofanya.
makosa yenyewe ni kama ifuatavyo...
                                                             
kupima uzito jioni; kupima uzito mchana au jioni ni makosa sana kwani hakuonyeshi uhalisia, maana muhusika anakua ameshakula na kunywa maji mengi.
inategemea na kiasi ulichokula na kunywa lakini kumbuka lita moja ya maji ni sawa na kilo moja kwenye mzani hivyo muda mzuri wa kupima uzito ni asubuhi ukiwa haujala chochote yaani umeshakaa saa Zaidi ya 8 ukiwa umelala bila kula chakula chochote.
Hivyo ukiamka asubuhi kojoa kwanza na kama unasikia haja kubwa basi kajisaidie kisha pima uzito.
kupima uzito kila siku; kupungua au kuongezeka uzito sio safari ya siku moja bali ni safari ya muda mrefu sana ambayo inataka nidhamu kubwa, baadhi ya vyakula vinaweza kukufanya uonekane umepungua uzito na vingine vikaonesha umeongezeka.
mfano ukiacha sukari, vyakula vya chumvi na wanga ghafla utaonekana umepungua ndani ya siku moja lakini ni maji ndio yamepungua Zaidi na sio mafuta kwani vyakula ulivyoacha vinakufanya uhifadhi maji mengi Zaidi mwilini.
Baadhi ya diet kama ketogenic diet hukufanya ukojoe sana na kupunguza maji mwilini na hii itakufanya uhisi umepungua, kimsingi unatakiwa upime uzito angalau mara moja au mbili kwa wiki baada ya kuanza diet mpya hii inaupa mwili muda wa kufanya regulations na kutoa majibu ya kweli.
Wataalamu wa lishe wanaamini binadamu anatakiwa apungue nusu kilo au kilo moja kwa wiki hivyo kupima kila siku kunaweza kukufanya uhisi uko pale pale au unaongezeka kumbe umeanza kupungua ila mwili wako bado haujaanza kuonyesha kwenye mzani hasa kama unakunywa maji mengi kwenye diet yako.
kutumia mizani tofauti; mizani mingi ina formula tofauti, tafiti zimeonyesha kwamba kunaweza kua na tofauti ya hata kilo moja au mbili kwa kila mzani.
hivyo epuka tabia ya kupima uzito barabarani au kupima uzito nyumbani kisha ukienda gym tena unapima uzito.
chukua mzani mmoja na upime kwenye huo huo kila mara ili kuangalia maendeleo yako.
kupima uzito na nguo; kitaalamu mzani unatakiwa ukae bafuni, sehemu ambayo unapima ukiwa hujavaa nguo yeyote, ile tabia ya kufika sehemu kisha  unapanda mzani ukiwa na simu, pochi, nguo,begi na funguo sio nzuri..tafiti zimeonyesha tabia ile inaweza kuongeza uzito mpaka kilo moja au nusu kilo ambazo si zako.
kupima uzito baada ya mazoezi; ukiingia gym kufanya mazoezi utatokwa na jasho jingi sana mpaka nusu lita au lita moja, ukimaliza ukapima uzito utaona umepungua lakini ukweli ni kwamba umepungua maji tu na uzito wa kweli utaaupata baada ya siku mbili au tatu.

                                                                        STAY ALIVE

                                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                 0769846183/0653095635