data:post.body FAHAMU VIGEZO MUHUHIMU VYA KUCHANGIA MBEGU ZA KIUME.(SPERM DONOR) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU VIGEZO MUHUHIMU VYA KUCHANGIA MBEGU ZA KIUME.(SPERM DONOR)

Kuchangia  mbegu za kiume ni moja ya shughuli kubwa na muhimu sana kwenye nchi ambazo zimeendelea na inaweza ikakupa kipato kizuri iwapo ukikidhi vigezo vya kuchangia mbegu hizo mara kwa mara, sina uhakika kuhusu hapa kwetu.
Kwa kawaida mwanaume mchangiaji hulipwa dola 70 kwa kila sampuli anayopeleka na hii ni sawa na shilingi laki na sitini za kitanzania  au milioni moja na laki mbili kwa mtu anayechangia mara mbili kwa wiki kila mwezi.

Inaweza kuonekana ni pesa rahisi lakini kuna vigezo vingi ambavyo unatakiwa uvipitie ili uweze kukidhi mahitaji na kama haukidhi mbegu zako hazitachukuliwa kama ifuatavyo.
                                                                               
hatua ya kwanza, historia ya mchangiaji; Hapa utaulizwa historia ya ukoo wenu kwanzia bibi na babu zako mpaka wazazi, baba mkubwa na baba wadogo  na watoto wa ukoo wenu.
Kama kuna magonjwa yeyote ya kurithi kama siko seli basi mchangiaji atapoteza uwezo wa kuchangia hapo hapo lakini pia tabia kama za kushiriki tendo na wanaume, kutumia madawa ya kulevya, uhalifu, kuchora tatoo au kupigwa na mionzi yeyote utakua haukidhi vigezo.

hatua ya pili, uchunguzi wa mwili mzima; Daktari atakuchunguza mwili mzima kwanzia kwenye nywele mpaka vidole kuangalia kama una tatizo lolote kisha atachukua sampuli ya damu na mkojo kupima magonjwa yote hatari ya kurithi na magonjwa ya kuambukizwa kama ukimwi na homa mbali mbali za maini kitaalamu kama hepatitis.

Hatua ya tatu, kutoa sampuli ya kwanza; baada ya hapa utatoa sampuli ya kwanza ambayo itapimwa vitu mbalimbali kama umbo la mbegu, kasi ya kukimbia, na afya ya mbegu zako kwa ujumla kisha vitahifadhiwa kwa muda wa miezi sita na kama muda huo ukipita mbegu zako hazijaharibika basi utakua umekidhi vigezo na kuanza kutoa angalau sampuli mbili au tatu kwa wiki.
kumbuka sampuli hizi unazitoa kituoni kwenye chombo maalumu na sio unaleta kutokea nyumbani.

vigezo vingine; kabla ya kuanza kupimwa ili kuonekana kama unafaa au hufai basi mchangiaji anatakiwa awe na umri wa miaka 18 mpaka 40, yuko chuo kikuu au kamaliza tayari, awe na urefu sahihi na na muonekano wa kuvutia kwa wateja, na awe kwenye afya njema.

                                                                           STAY ALIVE
                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                     0769846183/0653095635

Maoni 1 :