data:post.body Februari 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA CORONA VIRUS NA MATIBABU YAKE.(COVID-19)

Corona virus ni ugonjwa ambao ulionekana mara ya kwanza mwaka 1960 lakini ulikua ugonjwa wa kawaida kama mafua tu, lakini desemba  mwaka 2019 wakati shirika la afya duniani linatangaza hali ya hatari basi watafiti walikua wamegundua aina nyingine ya kirusi hicho ambacho kilikua ni hatari sana kiasi cha kusababisha kifo.
Ugonjwa ulipewa jina jipya  COVID-19, Ulisambaa haraka sana nchini china hata kwenda nchi jirani kama japan, south korea, uingereza, marekani, italia na kadhalika.
Mpaka sasa hivi ugonjwa huu umeua Zaidi ya watu 2000 nchini china huku wengine Zaidi ya 70000 wakiwa wagonjwa.
Nchi za afrika imekua ngumu sana kwa ugonjwa huu kufika sababu ya hali ya joto ambayo haipatani na virusi hivyo.

dalili za ugonjwa huu.
dalili za ugonjwa huu hutokea siku ya 2 mpaka 14 baada ya kuambukizwa virusi hivi na huanza kama mafua ya kawaida kisha mgonjwa hupata homa, kikohozi na kushindwa kupumua.

maambukizi 
ugonjwa huu huambukizwa kwa hewa yaani kukohoa na kupiga chafya lakini pia kugusa vitu ambavyo mgonjwa amegusa kama kitasa cha mlango, kikombe na kadhalika na ndio maana wagonjwa hutengwa ili kuzuia kuambukiza wengine.

vipimo
vipimo vya damu huweza kuchukuliwa na mjibu hutoka ndani ya siku moja.

matibabu
hakuna dawa wala chanjo ya ugonjwa huu, kinachotibiwa ni dalili za ugonjwa huu mpaka mgonjwa atakapo pata nafuu, mgonjwa hupewa dawa za homa kupunguza joto, oxygen kama anapumua kwa shida na kuongezewa maji mengi kwa dripi.

jinsi ya kuzuia ugonjwa
  • Nawa mikono kwa maji safi na salama
  • usiguse pua, mdomo na macho
  • kaa mbali na wagonjwa.
chanzo cha kifo
watu wengi wanaokufa ni wazee sababu ya kinga ndogo ya mwili na watu wenye magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili kama wagonjwa wa saratani na ukimwi.
Ugonjwa huu husababisha kushindwa kupumua, kichomi cha mapafu au pneumonia na kupungua uwezo wa damu kuzunguka mwilini kitaalamu kama shock na hichi ndio chanzo cha kifo.

                                                               STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0653095635/0769846183

                                                                 

CHANJO MPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHINDWA VIBAYA KWENYE MAJARIBIO.

Huko nchini south Africa matumaini ya chanjo mpya ya virusi vya ukimwi yamefeli vibaya baada ya chanjo hiyo ambayo ndio ilikua tumaini la watafiti kushindwa kufanya kazi.
Watafiti hao wameonyesha masikitiko makubwa sana lakini wakaongeza kwamba utafiti wa chanjo hiyo lazima uendelee.

utafiti ulifanyika vipi?
Utafiti huo ambao uliwahusisha watu 5000 ulionyesha kwamba watu 252 waliathirika baada ya muda Fulani.
Dr Antony Fauci kutoka kituo hicho cha utafiti anasema kwamba kipindi hichi ambacho dunia inaumia kwa kuwepo kwa wagonjwa wengi sana wa ukimwi huku ukiacha yatima na wajane wengi na kuharibu uchumi, chanjo ya ukimwi ni muhimu sana" aliongea kwa masikitiko.
Kawaida chanjo hii hutolewa kwa watu Fulani kisha wanaachwa waendelee na Maisha yao ya kawaida kisha huenda tena kupimwa baada ya muda Fulani, kitaalamu kama cohort study.
South Africa ikiwa na wagonjwa milioni tano na laki sita mwaka 2016 ndio inaongoza duniani kwa kua na wagonjwa wengi Zaidi.

kwa sasa ugonjwa huu unaweza kuzuiliwa vipi?
Kwa sasa njia pekee ya kuzuia ugonjwa huu ni kumeza aina Fulani ya dawa ambayo inazuia ukimwi lakini tofauti na chanzo za kawaida, dawa hii inataikiwa kumezwa kila siku ili ifanye kazi.
Nchini Tanzania dawa hii inapewa Zaidi wa watu ambao wana hatari sana ya kupata ugonjwa huu kama wanawake wanaojiuza na watumiaji wa madawa ya kulevya.
Kwa nchi ambazo hazina dawa hizi basi matumizi ya condom na kujizuia kufanya ngono ndio njia pekee ya kuzuia ukimwi kwani kuamini wenza bado kumeambukiza watu wengi virusi hivi.

                                                              
                                                              STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183
                                                               

FAHAMU VIGEZO MUHUHIMU VYA KUCHANGIA MBEGU ZA KIUME.(SPERM DONOR)

Kuchangia  mbegu za kiume ni moja ya shughuli kubwa na muhimu sana kwenye nchi ambazo zimeendelea na inaweza ikakupa kipato kizuri iwapo ukikidhi vigezo vya kuchangia mbegu hizo mara kwa mara, sina uhakika kuhusu hapa kwetu.
Kwa kawaida mwanaume mchangiaji hulipwa dola 70 kwa kila sampuli anayopeleka na hii ni sawa na shilingi laki na sitini za kitanzania  au milioni moja na laki mbili kwa mtu anayechangia mara mbili kwa wiki kila mwezi.

Inaweza kuonekana ni pesa rahisi lakini kuna vigezo vingi ambavyo unatakiwa uvipitie ili uweze kukidhi mahitaji na kama haukidhi mbegu zako hazitachukuliwa kama ifuatavyo.
                                                                               
hatua ya kwanza, historia ya mchangiaji; Hapa utaulizwa historia ya ukoo wenu kwanzia bibi na babu zako mpaka wazazi, baba mkubwa na baba wadogo  na watoto wa ukoo wenu.
Kama kuna magonjwa yeyote ya kurithi kama siko seli basi mchangiaji atapoteza uwezo wa kuchangia hapo hapo lakini pia tabia kama za kushiriki tendo na wanaume, kutumia madawa ya kulevya, uhalifu, kuchora tatoo au kupigwa na mionzi yeyote utakua haukidhi vigezo.

hatua ya pili, uchunguzi wa mwili mzima; Daktari atakuchunguza mwili mzima kwanzia kwenye nywele mpaka vidole kuangalia kama una tatizo lolote kisha atachukua sampuli ya damu na mkojo kupima magonjwa yote hatari ya kurithi na magonjwa ya kuambukizwa kama ukimwi na homa mbali mbali za maini kitaalamu kama hepatitis.

Hatua ya tatu, kutoa sampuli ya kwanza; baada ya hapa utatoa sampuli ya kwanza ambayo itapimwa vitu mbalimbali kama umbo la mbegu, kasi ya kukimbia, na afya ya mbegu zako kwa ujumla kisha vitahifadhiwa kwa muda wa miezi sita na kama muda huo ukipita mbegu zako hazijaharibika basi utakua umekidhi vigezo na kuanza kutoa angalau sampuli mbili au tatu kwa wiki.
kumbuka sampuli hizi unazitoa kituoni kwenye chombo maalumu na sio unaleta kutokea nyumbani.

vigezo vingine; kabla ya kuanza kupimwa ili kuonekana kama unafaa au hufai basi mchangiaji anatakiwa awe na umri wa miaka 18 mpaka 40, yuko chuo kikuu au kamaliza tayari, awe na urefu sahihi na na muonekano wa kuvutia kwa wateja, na awe kwenye afya njema.

                                                                           STAY ALIVE
                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                     0769846183/0653095635