data:post.body MBEGU ZA WANAUME WAFU KUANZA KUTUMIKA KUZALISHA WANAWAKE.(UTAFITI) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MBEGU ZA WANAUME WAFU KUANZA KUTUMIKA KUZALISHA WANAWAKE.(UTAFITI)

Mwaka 2017 nchini uingerza watoto 2345 walizaliwa baada kutumika kwa mbegu kutoka kwa wanaume waliochangia kwenye benki za mbegu, lakini kumekua na upungufu mkubwa sana wa upatikanaji wa mbegu hizo kutokana na sheria kali sana nchini humo.
                                                                         
Lakini utafiti unaonyesha kwamba kuna uwezekano wa kuvuna mbegu za watu waliokufa muda mfupi baada ya kifo kama inavyofanyika kwenye kuvuna viungo vingine kama figo, maini na mapafu iwapo mbegu hizo zikichukuliwa ndani ya masaa 48 baada ya kifo.

Pamoja na jambo hili kuwezekana bado kuna changamoto ya kisheria kwa wafu hao kwani sheria hairuhusu kitu hiko kifanyike kama muhusika mwenyewe hakukubali wakati akiwa hai.
Dr Nathan Hodson kutoka uingereza ameshauri mfumo wa watu kujaza fomu kukubali viungo vyao kutumika baada ya kifo uletwe pia kwenye swala la mbegu za kiume kupunguza uhaba huo.

Kwa sheria za nchi hiyo, mtoaji mbegu anatakiwa azitoe kwa ruhusa yake na watoto watakaozaliwa baada ya yeye kutoa mbegu basi wanaruhusiwa kuwasiliana naye baada ya kufikisha umri wa mika 18.
Mwaka 1995 mwanamke mmoja nchini uingereza alifiwa na mme wake baada ya kuugua ghafa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.
Mume wa marehemu kwa jina la Stephen blood alipoteza fahamu na kufariki kabla ya kutoa ruhusa ya mbegu zake kutumika lakini kabla hajafa mke wake aliomba mbegu zake zichukuliwe na kuhifadhiwa.
Pamoja na kufanya hivyo uongozi wa kitengo kinachohusiana na mambo ya uzazi ulikataa mwanamke yule asitumie mbegu zile, mpaka alipoenda mahakamani na kushinda kesi hiyo mwaka 1997.
Mwaka 2002 alijifungua salama mtoto wake kwa jina la joel.

                                                                       STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183
                                            

0 maoni:

Chapisha Maoni