data:post.body 2020 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

WANAWAKE KULAMBWA UKE HUWEZA KUSABISHA MAGONJWA YA UKE, KIZAZI NA UGUMBA.TAFITI

Jarida moja nchini marekani kwa jina la PLOS limechapisha tafiti mpya ambayo inasema kwamba tabia ya kulamba uke wakati wa tendo la ndoa linachangia sana wanawake kupata maambukizi ya fangasi na magonjwa mengine ya uke mara kwa mara hali ambayo huweza kusababisha usugu na kushindwa kutibika kabisa..Dalili za magonjwa haya ni kama kuwashwa, kutoka uchafu na harufu kali kutoka ukeni.


Ugonjwa wa uke kitaalamu kama vaginosis huweza kupanda mpaka kwenye kizazi na kusababisha magonjwa ya kizazi kama PID ambayo hupelekea ugumba mara nyingi.

Chanzo ni nini? 

Kiasilia uke una aina fulani ya bacteria ambao huulinda ili usiweze kuambukizwa magonjwa mbalimbali lakini pia kuna hali ya tindikali au acid ambayo pia ni kama njia ya ulinzi wa uke, sasa uke unavyonyonywa au kulambwa kuna bacteria wengi wa mdomoni ambao wakiwa mdomoni hawana shida lakini wakifika kwenye uke husababishwa magonjwa.

Bacteria wa fusobacterium ambao hupatikana kwenye mate mdomoni ni moja ya bacteria ambao wameonekana kuhusika sana na magonjwa ya uke lakini pia ulambaji wa uke hupunguza kiasi cha tindikali ambacho kinalinda uke na kusababisha magonjwa ya kuwashwa mara kwa mara ambayo ndio fangasi.

Tafiti hizi zinakuja baada ya tafiti za mwanzo ambazo zilionyesha kwamba walambaji wa sehemu za siri yaani uke au uume wana hatari ya kuugua saratani ya koo ambayo hupatikana kwa kulamba virusi vya HPV ambavyo hupatikana sehemu hizo.

Virusi vya HPV husabisha saratani ya shingo ya uzazi lakini vikilambwa na kwenda kwenye koo husababisha saratani ya koo.

Ushauri; Wataalamu wanashauri kutolamba sehemu za siri za mtu yeyote hata kama ni mke wako au mme wako kwani tafiti zinaonyesha kuongezeka kwa magonjwa ambayo yanatokana na tabia hizo.

                                                            STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE.

                                                0769846183/0653095635


SINDANO MPYA ZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI ZATOA MATUMAINI MAKUBWA.

Shirika la ukimwi duniani, UNAIDS limepata matuaini makubwa baada ya dawa mpya ya ukimwi kwa jina la cabotegravir ambayo inatolewa kwa sindano kila baada ya miezi miwili kuzuia maambukizi ya ukimwi kuonyesha matumaini makubwa.

Utafiti huu mpya umeonyesha kwamba dawa hiyo ilifanikiwa kuzuia maambukizi kwa 89% ukilinganisha na iliyokuepo ambayo ilikua ikitolewa kwa vidonge kila siku maarufu kama  PreP.
Matokeo haya ni ni muhimu sana, UNAIDS imekua ikitafuta kinga nzuri zaidi ya kuzuia maambukizi ya ukimwi hasa kwa wanawake na ugunduzi huu utakua na mchango mkubwa sana kuzuia maambukizi ya ukimwi. “Kama nchi tajiri zikiwekeza kutoa misaada na kuhakikisha watu ambao wako kwenye hatari ya maambukizi kupata sindano hizi kila baada ya miezi miwili basi kutakua na upungufu mkubwa wa maambukizi mapya”. Anaongea mkurugenzi  wa UNAIDS, Winnie Byanyima.

Utafiti huu ulihusisha wanawake  3200 wenye umri wa miaka 18 mpaka 45 ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi yaani wanaojiuza na watumiaji wa madawa ya kulevya.Utafiti ulihusisha nchi za Botswana,Kenya,Malawi,Uganda na Zimbabwe. Kati ya watu 3200 waliotumia sindano ya kuzuia virusi vya ukimwi ni wanne tu walioambukizwa huku kati ya 3200 waliotumia vidonge vya kila siku watu 34 waliambukizwa.

 Kwa hali kawaida yaani bila vidonge wala sindano za kuzuia maambukizi ni zaidi ya 61% huambukizwa, yaani katika watu 3200 basi watu 1952 huweza kuambuizwa nchini humo.

Shirika la ukimwi duniani linawashukuru watu wote walioshiriki kwenye ugunduzi wa dawa hizi katika mbio za kuhakikisha hakuna maambukizi mapya ya ukimwi,hakuna unyanyapaa na hakuna vifo vitokanavyo na ukimwi mpaka mwaka 2030.

Nchini Tanzania dawa za kuzuia maambukizi ya ukimwi za vidonge ambazo humezwa kila siku hutolewa katika kliniki za ukimwi lakini pia watu walioko kwenye hatari kama wanaojiuza, mashoga na watumia madawa ya kulevya hupelekewa mpaka majumbani ili kupunguza maambukizi mapya.

 

                                      STAY ALIVE

 

           DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.MD

                          0653095635/0769846183

TATIZO LA WATOTO WACHANGA KUINGIA HEDHI NA MATIBABU YAKE (FALSE MENSES)

Moja ya vitu vya kuogopa na kushtukiza kwa wamama ni kutoka kwa damu ya hedhi kwa mtoto mchanga ambaye ayezaliwa ndani ya kama siku mbili mpaka kumi hapo, na anaweza kukimbia hospitali haraka huku amechanganyikiwa.

                                                                 


chanzo ni nini?

Mama akiwa mjamzito homoni za uzazi yaani oestrogen na progesterone zinakua juu sana kiasi kwamba wakati mwingine zinakua zinamuathiri mpaka mtoto, moja ya kazi ya homoni ya oestrogeni ni kujenga ukuta wa seli ndani ya kizazi kitaalamu kama endometrial hyperplasia. Baada ya kujifungua homoni zile hushuka ghafla kwenye mwili wa mtoto na kufanya ukuta ule kushindwa kustahimili hivyo kuanguka kwa kutoa damu ambayo hutoka kama hedhi. Asilimia tano ya watoto wanaozaliwa hupata hali hii.

Nini cha kufanya?

Damu ili haitatoka kwa siku kadhaa kama hedhi zingine lakini itatoka tu ndani ya muda mfupi cha msingi endelea kumkagua na kumfanyia usafi na mara nyingi damu hiyo huisha yenyewe. Kama damu zikiendelea kutoka nyingi au kuanza kutoa harufu basi mpeleke mtoto hospitali.

                                                                        STAY ALIVE 

                                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                                  0653095635/0769846183

TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI NA MATIBABU YAKE.

 Uke wa kawaida wa mwanamke lazima uwe na harufu fulani, sio rahisi kusema ni harufu gani lakini wanawake huweza kutofautiana harufu hiyo. Kwakawaida uke ni nyumbani kwa bacteria wengi sana huku kukiwa na gland ambazo hutoa majimaji ya uke ambayo yana tindikali kali sana.

                                                                


Kazi ya bacteria hao na glandi hizo ni kujaribu kutoa ulinzi mkali ili uke usishambuliwe na vijidudu hatarishi ambavyo huleta magonjwa. Ukiona mwanamke anapambana sana kutumia vitu mbalimbali na kufanya usafi mwingi uke wake usitoe harufu hata kidogo basi ujue anatafuta magonjwa.

Kwakawaida kuna magonjwa mawili ambayo yakianza yanakua tishio kubwa kwa mwanamke kwani huja na harufu kali kama ya kitu kilichooza na kutao uchafu wa kijani na njano, magonjwa haya kitaalamu ni bacterial vaginosisi na trichomonisis.

ugonjwa wa trichomoniasis ni upi?
huu ni ugonjwa  unaoshambulia sehemu za siri kwa jina la trichonomiasis na husababiswa na aina ya protozoa kwa jina la trichomona vaginalis.
huu ni ugonjwa unaoshambualia angalau 10% ya wanawake wote kwenye kipindi chote cha maisha yao,
maambukizi ni kwa njia ngono kati ya mwanaume na mwanamke lakini pia kuchangia nguo za ndani au mataulo kunaweza kuambukiza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
ugonjwa huu huweza kuambukiza watu wa jinsia zote lakini unawaathiri sana wanawake na mgonjwa asipotibiwa anaweza kuishi na ugonjwa huo kwa siku miaka kadhaa.
baada ya kuambukizwa ugonjwa huu, huchukua siku 5 mpaka 28 kuanza kuonyesha dalili zake waziwazi.

dalili za ugonjwa wa trichomoniasis
kuwashwa sana sehemu za siri
kuchubuka sehemu ya juu ya uke na mlango wa uzazi
maumivu wakati wa kukojoa
maumivu wakati wa tendo la ndoa
maumivu makali ya tumbo la chini
kutokwa uchafu wa kijani na njano wenye harufu kali kama ya kitu kilicho oza.
kwa wanaume ugonjwa huu mara nyingi hauna dalili lakini mara chache sana wanaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa

vipimo
daktari mzoefu anaweza kuujua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini pia kwa upande wa maabara uchafu unaotoka huchukuliwa na kupimwa kwa darubini...

matibabu
metronidazole au kwa jina lingine fragile 2g kwa wakati mmoja [vidonge kumi] au 400mg[vidonge viwili] kutwa mara tatu kwa siku tano.
tinidazole 2g kwa wakati mmoja
scenidazole 2g kwa wakati mmoja.
kumbuka dawa hizi hazipatani na pombe kabisa hivyo usitumie pombe ukitumia dawa hizi.

jinsi ya kuzuia
tumia kondom kila tendo na kwa usahihi
achana na ngono kama huwezi kondom
kua na mpenzi mmoja muaminifu
epuka kua na wapenzi wengi
epuka kuchangia chupi, taulo au nguo yeyote ya ndani.
                                                                         

 • Ugonjwa wa bacterial vaginosis unafanana sana dalili na ugonjwa trichomoniasis, tofauti ni kwamba chanzo chake ni kuzaliana sana kwa bacteria asilia ambao wanapatiakana kwenye uke.. chanzo kikiwa   matumizi ya marashi au dawa mbalimbali za kuondoa harufu asilia ya uke, kuosha sana uke, kua na wapenzi wengi au mpenzi mpya, na kupungua kwa ulinzi asilia sehemu za siri.
 •   Dalili, vipimo na matibabu hufanana lakini pia ni vizuri kujua kwamba kupuuzia magonjwa haya kuna madhara makubwa kama kuharibika mimba na magonjwa ya kizazi ambayo yanaweza kuleta ugumba.

                                                       STAY ALIVE


                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                 MAWASILIANO 0653095635/0769846183

TATIZO LA KUTORUDIA TENDO LA NDOA BAADA YA KUFIKA KILELENI.

Katika mambo ambayo yanaumiza sana vichwa wanaume walio wengi ni kushindwa kurudia tendo la ndoa kwa mara ya pili baada ya kufika mshindo kwa mara ya kwanza, wengi hudhani wana matatizo na kuanza kutafuta suluhisho ya matatizo yao kwa kutumia dawa za aina mbalimbali bila kujua kwamba wao hawana shida yeyote.


ukweli ni upi?

Kila mwanaume ana muda wake ambao anatakiwa kupumzika kabla ya kuendelea na tendo la ndoa kitaalamu kama refractory period, kuna ambao wanaweza kuendelea hapo hapo na kuna wengine wanahitaji mapumziko ya kwanzia nusu saa mpaka siku nzima.Tofauti na wanawake ambao huhitaji muda mfupi wa mapumziko au hua hawahitaji muda huu wa mapumziko kwani wao huweza kufika kileleni hata mara kumi kwa kulala na mtu mara moja kitaalamu kama multi orgasmic.

Tatizo ni nini? 

Wanaume wengi hutumia muda mchache sana kufika mshindo wa kwanza kitu ambacho kinaweza kumfanya mwanamke asiridhike kwa wakati huo, sasa kwasababu mwanamke hajaridhika na anataka kuendelea basi wanaume hawa hujilazimisha kuendelea bila kupata mapumziko hayo ambayo ni ya msingi sana.Matokeo yake wanaume hawa hupaniki kwa kuhisi kwamba watapata aibu na katika kupaniki huko muda wa kurudia ndio unazidi kua mrefu zaidi.

kwanini wanaume wako tofauti kwenye jambo hili?

 • umri; vijana wadogo wanakua na stamina sana lakini pia mfumo wao wa damu ni msafi sana hivyo wanaweza kurudia haraka.
 • kuvutiwa na mwanamke; mwanaume akilala na mwanamke ambaye anavutiwa naye kingono basi ana uwezo wa kurudia mara nyingi sana kuliko akilala na mwanamke yeyote na hii nikitu muhimu sana wakati wa kuoa, hakikisha unaoa mwanamke anayekuvutia sio yeyote tu.
 • uwezo wa mwanamke kitandani; baadhi ya wanawake wana uwezo na utundu sana wa kukufanya utake kuendelea baada ya muda mfupi tu.
 • magonjwa; baadhi ya magonjwa hasa presha na kisukari huweza kuchelewesha sana muda wa kurudia tendo la ndoa.
 • matarajio; ukiwa na matarajio makubwa ya kuendelea na tendo lingine baada ya kumaliza tendo la ndoa kwa hofu kwamba hujamridhisha basi ndio hupati kitu kabisa.
Nini cha kufanya?
Chelewa kufika mshindo wa kwanza; ukichelewa kufika kileleni kuna uwezekano mkubwa wa kufikishwa mwanamke kileleni zaidi ya mara moja na ukajikuta unapumzika naye baada ya wewe kumaliza pia  bila haraka kusubiri kuendelea mara ya pili au kutorudia kabisa kwani ameridhika.
Inaweza isiwe rahisi kuchelewa kufika kileleni lakini kuna njia za kufanya hivyo bonyeza hapa kusoma...http://www.sirizaafyabora.info/2014/08/kama-wewe-mwanaume-una-tatizo-la-kufika.html
jiweke vizuri kimwili; Fanya mazoezi mara kwa mara, hii huongeza mzunguko wa damu mwilini, hukupa stamina na uwezo wa kufanya ngono kwa muda mrefu zaidi.
tumia dawa zako kwa wakati; kama una ugonjwa wowote ambao unakuletea shida hii hasa magonjwa ya moyo, presha na sukari basji jitahidi kutumia dawa zako kwa wakati kupunguza makali ya ugonjwaa.
epuka mahusiano na mwanamke asiyekuvutia; anaweza kua hakuvutii wewe lakini kuna watu anawavutia, kua mkweli na nafsi yako na utafute mwanamke ambaye nafsi yako inaridhika naye na hapo utafurahia sana tendo la ndoa.

mwisho; mfumo wa maisha kama kunywa pombe sana, matumizi ya sigara na kupiga sana punyeto kunaweza kukufanya ushindwe kuendelea na tendo lingine kwa wakati.

                                                                STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                        0653095635/0769846183

TATIZO LA KUTOSIKIA HARUFU NA MATIBABU YAKE

Wengi wetu uwezo wa kusikia harufu fulani tunaona ni kitu cha kawaida sana na tunahisi ni haki yetu lakini ushawahi kujifikiria kukosa harufu kabisa? Kutosikia harufu kabisa kitaalamu tunaita anosmia, ni tatizo ambalo linakufanya usisikie harufu ya mafuta, maua, manukato, chakula na hata ladha ya chakula hubadilika.

                                                                   


Hali hii inaweza kukuweka kwenye mazingira hatarishi kama ukishindwa kusikia harufu ya moshi, gesi inayovuja, au chakula kilichoharibika au kuwekewa kemikali.

Kwa nchi ambazo zimeendelea, tatizo hili huwapeleka wagonjwa wengi hospitali hapa kwetu ni tofauti kidogo kwani watu wana tabia ya kuvumilia magonjwa kama haya. Bahati nzuri asilimia kubwa ya wagonjwa hawa ni sababu ya mafua makali lakini baadhi inaweza kua magonjwa makubwa sana ambayo yanahitaji uangalizi wa karibu.

Mwili wa binadamu unatambua vipi harufu?

Mwili wa binadamu una mshipa wa fahamu maalumu kwa jina la olfactory ambao unapeleka taarifa ya harufu kutoka puani kwenda kwenye ubongo kwa ajili ya kutoa tafsiri ya kujua hii ni harufu gani, sasa tatizo lolote ambalo linaingilia huo mfumo huu kama mafua makali, nyama za pua au kuharibika kwa mshipa huu wa fahamu basi linasababisha mtu akose uwezo wa kusikia harufu.

Chanzo cha tatizo hili..

kama nilivyosema hapo mwanzoni kwamba mafua makali na kamasi, aleji ya vitu na hali mbaya ya hewa ndio chanzo kikuu cha hali hii lakini vyanzo vingine ni...

 • nyama za pua kitaaalamu kama nasal polyp.
 • kuumia kwa pua na kichwa baada ya ajali au upasuaji.
 • harufu za kemikali kali.
 • baadhi ya dawa za moyo, msongo wa mawazo na antibayotiki.
 • matumizi ya dawa za kulevya kama cocaine
 • umri mkubwa hasa baada ya miaka 60.
 • mionzi ya kichwa na shingo
 • baadhi ya magonjwa kama ya homoni, magonjwa ya kuzaliwa, alzehmers, parnkison, na utapiamlo wa chakula.
 • ugonjwa wa homa kali ya mafua wa covid 19.
Dalili za ugonjwa.
Dalili kuu ni kukosa harufu ya kitu ambacho unafahamu harufu yake siku zote.

Jinsi ya kutambua ugonjwa.
Ukiona unashindwa kupata harufu kwa zaidi ya wiki mbili na hauna mafua basi ni vizuri kwenda hospitali kuonana na daktari bingwa wa pua, sikio na koo ili akufanyie vipimo zaidi kujua tatizo ni nini.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yanatakiwa yaelekezwe zaidi kwenye chanzo cha ugonjwa wenyewe, kama ni mafua makali basi ugonjwa unaweza kuisha wenyewe na kama unasumbua basi unaweza kumeza dawa za mafua kupna haraka.
Tatizo la nyama za pua linaweza kutibika kwa upasuaji na kuondoa nyama hizo, tatizo la covid19 huweza kuisha lenyewe baada ya ugonjwa kuisha.
Kama unahisi chanzo ni dawa fulani ambazo unatumia kwa ajili ya kutibu shida zako zingine za kila siku basi ongea na daktari wako akubadilishie dawa hizo.
Bahati mbaya kama tatizo hili linatokana na umri mkubwa likaua haliwezi kutibika kirahisi lakini kama unaweza ni vizuri kununua vifaa maalumu vya kupiga kelele hasa kwenye harufu ya moshi au gesi kukuepusha na hatari.

                                                                 STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                          0653095635/0769846183


TATIZO LA SARATANI YA UTUMBO MKUBWA NA MATIBABU YAKE.

 Baada ya kifo cha mkali wa filamu za kimarekani maarufu kama wakanda au chadwick bossman kumekua na utafutaji mkubwa sana mtandaoni kujua ugonjwa huu unasababishwa na nini na ni jinsi gani mtu anaweza kukwepa ugonjwa huu.


Saratani hii huanzia kwenye sehemu ya utumbo mkubwa, mara nyingi huanza kama viuvimbe vidogo ambavyo sio saratani kitaakamu kama benign tumours au polyp lakini baadae hubadilika na kua saratani kamili na wakati mwingine hujumuisha sehemu ya mwisho kabisa ya mfumo ya chakula na kuitwa kitaalamu kama colerectal cancer. Mara nyingi ugonjwa huu huanza bila dalili na baadae dalili huanza kutokana na eneo ambalo ugonjwa umeshambulia.

Dalili za saratani ya utumbo mkubwa.

 • kubadilika kwa mfumo wako wa kupata choo yaani kupata choo ngumu sana au kuanza kuharisha.
 • maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi au kujisikia vibaya tumboni.
 • kupata choo chenye damu au kujisaida tamu tupu.
 • kujisikia kama choo haitoki yote kila ukitoka chooni.
 • uchovu wa mara kwa mara 
 • kuanza kupungua uzito kwa kasi isiyo kawaida.
Chanzo cha ugonjwa huu.
Ugonjwa huu haufahamiki chanzo chake lakini inafahamika kwamba mabadiliko ya chembe za DNA ndio sababu ya saratani zote kitaalamu kama DNA mutation.
Lakini kinachofahamika kwa uhakika ni vitu ambavo vinachangia mtu kuugua ugonjwa huu kama ifuatavyo.
umri mkubwa; Saratani hii mara nyingi huwapata watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea lakini wataalamu wameanza kuona ongezeko hili kwa vijana chini ya miaka 50 na sababu hazifahamiki.
magonjwa mengine ya utumbo mkubwa; kama ushawahi kuugua magonjwa mengine ya utumbo mkubwa unaweza kua kwenye hatari ya kuugua. mfano; ulcerative colitis
mgonjwa kwenye ukoo wako; kama mzazi wako mmoja kaugua ugonjwa huu basi na wewe una hatari ya kuupata na kama kuna mtu zaidi ya mmoja kwenye ukoo wenu basi hatari ni kubwa zaidi.
chakula; ugonjwa wa huu umeonyesha kuathiri zaidi watu wanaokula sana diet ambazo asili yake ni dunia ya magharibi yaani vyakula vyenye mafuta mengi, na nyama nyingi nyekundu bila kula mboga za majani na matunda ya kutosha.
kutofanya mazoezi; watu ambao hawana tabia ya kufanya mazoezi wana hatari sana ya kuugua ugonjwa huu kuliko watu wenye tabia ya kufanya mazoezi au wanaofanya kazi ambazo zinatumia nguvu.
uzito mkubwa; watu wanene wana hatari ya kuugua na hata kufa haraka kutokana na ugonjwa huu.
sigara na pombe; watu wanaokunywa pombe sana  na kuvuta sigara wana hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu.
mionzi; watu ambao wanapigwa na mionzi ya kupima au kutibu magonjwa fulani fulani wanakua na hatari pia ya kupata ugonjwa huu.
wagonjwa wa kisukari na watu weusi; watu hawa pia wameonyesha kuugua zaidi ugonjwa huu lakini sababu maalumu haifahamiki.

jinsi ya kutambua ugonjwa.
Colonoscopy; Hichi ni kipimo ambacho kina camera ndogo na hupitishwa kwenye njia ya haja kubwa kuangalia kama kuna uvimbe wowote wa saratani, uvimbe ukionekana basi inachukuliwa sample kwenda kupimwa maabara ili kuhakikisha kama ni saratani lakini hata kama sio saratani uvimbe huo huondolewa ili usibadilike na kua saratani.
vipimo vya damu; baadhi ya kemikali huwezwa kupimwa ili kujua kama kuna saratani mwilini mwako kitaalamu kama carcinoembryonic antigen na ukianza matibabu kipimo hichi kinaweza kugundua kama maendeleo ni mazuri mwilini mwako.

matibabu ya saratani ya utumbo mkubwa.
Matibabu makubwa ya ugonjwa huu ni upasuaji, dawa za saratani na mionzi..katika kipindi cha mwanzo kabisa cha ugonjwa huu basi mgonjwa anaweza kupona kabisa kama sehemu hiyo ya saratani ikiondolewa kwa upasuaji.
Lakini wagonjwa wengine hufika hospitali kwa kuchelewa huku saratani ikiwa ishasambaa sehemu kubwa sana ya mwili na kuifanya isitibike kabisa.

jinsi ya kujikinga na saratani ya utumbo mkubwa.
 • kula vizuri; mboga za majani na matunda zina vitamini fulani ambazo zina uwezo wa kuzuia saratani za aina zote kwenye mwili wa binadamu, huku afrika tuna nafasi kubwa ya kupata vitu hivi kwa bei rahisi.
 • kunywa pombe kiasi na achana na uvutaji wa sigara.
 • fanya mazoezi angalau nusu saa mara tatu kwa wiki.
 • kaa kwenye uzito sahihi kulingana na urefu wako.
 • kama uko kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu fanya vipimo kila baada ya miaka miwili au mitatu ilia kama umeanza utibiwe mapema.
                                                                                 STAY ALIVE

                                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                                        0653095635/0769846183

TATIZO LA KUWASHWA BAADA YA KUOGA NA MATIBABU YAKE.(AQUAGENIC URTICARIA)

 Aquagenic urticaria ni hali ambayo sio ya kawaida ambayo hutokea pale mtu anapowashwa baada ya kuoga au kugusa maji, tafiti zinaonyesha kwamba hali hii inasababishwa na mgonjwa kua na allergy ya maji.                                                           


Mgonjwa huweza kuwashwa na maji ya bomba, bahari, ziwani, mto, mvua, machozi, jasho, na kadhalika.Baadhi ya watafiti huamini kwamba kuwashwa huko kunaweza kunasababishwa na kemikali ambazo huwekwaa ndani ya maji kuua bacteria mfano chlorine lakini maelezo haya hayajitoshelezi kwani kuna watu wanawashwa mpaka na maji ya mvua ambayo haya kemikali yeyote.

dalili ni zipi?

Unapopata allergy ya kitu chochote mwili wako hutoa kemikali moja inaitwa histamine kupambana na hicho kitu ambacho mwili wako unatafsiri kama adui na matokeo yake unawashwa. Kwa kawaida mtu hupata dalili za vipele, kuwashwa mwili mzima,ngozi nyekundu kwa watu weupe, na kwa dalili mbaya  sana mtu huweza kushindwa kupumua, kushindwa kumeza na kuanza kukoroma wakati wa kupumua.

jinsi ya kutambua ugonjwa

Daktari huchukua maelezo yako na kukagua ngozi yako lakini pia anafanya majaribio kwa kuweka maji kwenye mwili wako na kuangalia matokeo ambayo mara nyingi hutokea baada ya dakika 15. Dalili hizi zikianza baadhi ya vipimo vya damu kama full blood picture huweza kuonyesha kuongezeka kwa kiwango cha seli mwilini kinachohusika na allergy kitaalamu kama easinophil.

matibabu

Duniani kote hakuna dawa ya kutibu allergy na kuimaliza lakini kuna dawa za kuondoa dalili hizi za kuwashwa. Dawa kama aina ya anthistamine kama piriton au citrizine unaweza kumeza kidonge kimoja nusu saa kabla ya kuoga lakini pia badilisha mfumo wako wa maisha kwa kujiepusha na shughuli zote ambazo zinakuhusisha na kuloa maji.

                                                               STAY ALIVE 

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                             0653095635/076984613

TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAUME NA MATIBABU YAKE.

Fangasi sugu za kwenye korodani za wanaume limekua moja ya matatizo sugu siku hizi za usoni, baadhi wamekua wakitumia dawa bila mfanikio yeyote na hii ni kwasababu ya kushindwa kuelewa chanzo na jinsi ya kupambana na hatari za kupata ugonjwa huu.

                                                                        


chanzo cha ugonjwa.

ugonjwa huu husababishwa na aina ya fangasi mwenye jina la trichopyton rubrum na waathirika wakubwa  vijana,tabia kuvaa nguo za ndani zinazobana, kua mzito sana, kinga iliyoshuka kwa ukimwi, saratani, utapiamlo au kisukari, na kutokwa na jasho sana.

dalili za ugonjwa.

 • kuwashwa sana kwenye sana kwenye korodani.
 • korodani kua nyekundu hasa kwa watu weupe
 • korodani kuanza kutoa kama magamba kwenye ngozi.

jinsi ya kutambua ugonjwa
Daktari anaweza kutambua ugonjwa wako wa kusikiliza maelezo yako tu au kuchukua sehemu ya mabaka ya ngozi na kwenda kupima maabara,

Matibabu ya ugonjwa huu.
Kuna dawa nyingi sana za kutibu ugonjwa huu, dawa ya terbinifine ya kumeza ni moja ya dawa bora sana kwa ugonjwa huu.
Zingine ni cotrimazole, ketoconazole, gresiofulvin, na miconazole.
kumeza na kupaka kwa wakati mmoja kumeonyesha matokeoa mazuri zaidi. 
Sasa jambo la msingi kabisa kuzingatia ambalo linafanya watu wengi wasipone ni kutumia dawa hizi muda mfupi, dawa hizi zinatakiwa zitumike wiki sita na sio chini ya hapo.


Mambo mengine ya kuzingatia..

kua mkavu; baada ya kuoga hakikisha umekausha mwili mzima kwa taulo safi kabla ya kuvaa nguo zingine lakini pia kausha miguu mwishoni kuzuia kuhamisha fangasi za vidoleni kwenda sehemu zingine za mwili.
vaa nguo safi: wanaume wengi wana tabia ya kuvaa nguo ya ndani moja kwa siku nyingi, jaribu kuvaa moja kila siku na kubadilisha hii itakupunguzia maambukizi yanayojirudia na hakikisha nguo za mazoezi unazitumia mara moja na kufua.
epuka nguo zinazobana sana; Vaa nguo za ndani ambazo zinakutosha ili kufanya maeneo hayo yapate hewa ya kutosha na kuepuka unyevunyevu.
usiazime nguo; epuka kuchangia taulo au nguo zako na watu wengine kwani hii itakuletea maambukizi mapya kila siku.
tibu fangas za vidole; kama una fangasi za kwenye vidole vya miguu hakikisha zinatibiwa na kupona ili kuepusha kuzisambaza mwili mzima.

                                                              STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0653095635/0769846183
FAHAMU JINSI UNENE UNAVYOWEZA KUSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKE.

 Kama wewe ni mwanamke mnene au una tumbo kubwa  na umekua ukisumbuliwa na tatizo la kutobeba mimba basi ni vizuri kwanza ukaacha kuhangaika na waganga na dawa mbalimbali ambazo umeambiwa zitakusaidia na kuweka nguvu nyingi kwenye kupungua uzito.

                                                                                 

Tafiti zinaonnyesha kwamba kadri unavyoondoka kwenye uzito wako wa kawaida yaani body mass index ya 24 ndio uwezekano wako wa kubeba mimba unazidi kua mdogo na ukiwa mnene kabisa ndio hali inazidi kua mbaya kabisa.

Mwanamke akiwa mnene au mwenye kitambi kikubwa anakua na kiwango kikubwa cha homoni inaitwa leptin ambayo hutengenezwa na mafuta yaliyoko mwilini, kiwango hichi cha homoni huingilia mfumo wa homoni za uzazi na kuuvuruga.Unene unavyozidi au tumbo linavyokua kubwa zaidi ndio hali hii inazidi kua mbaya zaidi.

Pamoja na unene kuvuruga mfumo wa homoni wanawake wanene hupata shida ya kutoa yai kitaalamu kama ovulation yaani yai linaweza lisitoke kabisa au likatoka likiwa halina ubora wa kutunga mimba hivyo huishia kuharibika.Lakini pia wanawake wa aina hii hata wakijaribu kuzaa kwa njia za kisasa yaani yai kurutubishwa nje na kupandizwa kitaalamu kama IVF bado uwezekano wa mimba kufika mwisho ni mdogo.

Dalili kuu ya hali hii ni kukosa siku zako za hedhi au kupata siku zako bila mpangilio maalumu na kwa kawaida hakuna dawa ambayo inaweza kukusaidia hapa bila ya wewe mwenyewe kuamua kupunguza uzito kwa mazoezi na chakula,

                                                                  STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                              0653095635/0769846183

FAHAMU JINSI UNENE NA KITAMBI UNAVYOPUNGUZA NGUVU ZA KIUME.

Tunafahamu kwamba unene huambatana na magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na kushindwa kupata usingizi wakati wa usiku lakini tatizo lingine la unene ni kupungua nguvu za kiume, kitu ambacho mara nyingi watu hawa wanene au wenye vitambi hawako wazi kukizungumzia.

                                                                      

Tafiti zinasemaje?

Shirika la kimarekani maarafu kama AUA au American urology association wanasema kwamba asilimia 53% ya wanaume wenye umri kati ya miaka 40 mpaka 70 wana tatizo la nguvu za kiume ambalo husababishwa na umri, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, unene na kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara na kiwango kidogo cha homoni za kiume yaani testosterone.

Hebu tuone uume unavyosimama.

Uume husimama pale damu inapoingia kwenye mishipa ya damu ya uume na kufanya uume ujae damu, mishipa ya damu hutoa kitu kinaitwa nitric oxide ambayo hufanya uume ubaki kwenye hali ile mpaka mwanaume atakapofika mshindo.(dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume huwekewa kemikali hii). Kitu chochote ambacho kinaweza kuharibu sehemu ya ndani ya mishipa ya damu ya uume husabisha uume kuishiwa nguvu.

Unene huathiri vipi nguvu za kiume?

 Mtu akiwa mnene mishipa ya damu pia inakua na mafuta kwa ndani ambayo yanakua yameganda kwenye kuta za mishipa ya damu kitaalamu kama atherosclerosis, hali hii hufanya damu kupita kwa shida kwenda kwenye uume na lakini pia mfumo wa kutengeneza nitric oxide ambayo kazi yake ni kurelax misuli ya uume ili uweze kusimama unaingiliwa.

Sababu nyingine ni ongezeko la  mafuta yaliyopo tumboni au kitambi ambayo hubadilisha homoni ya testosterone kua oestrogen..homoni ya testosterone ndio homoni kuu ya kiume ambayo huleta mabadiko ya yote ya kiume wakati wa kubalehe na huhusika sana na ukubwa na nguvu za kiume na kupungua kwa homoni hii humaliza au kupunguza sana nguvu za kiume.

Mwisho; habari njema ni kwamba wanaume wengi wanene huweza kurudi kwenye hali zao za zamani kwa kupungua uzito tu japokua kama ukipungua bado shida haijaisha basi kuna uwezekano mkubwa homoni zako za testosterone zilipungua na utahitaji dawa za kumeza kuzisahihisha, kumbuka kwamba kupungua uzito sio rahisi lakini ni muhimu sana.

Wengi wenu mmejaribu kupungua uzito maisha yenu yote bila mafanikio kwa kufuata diet na programu mbalimbali bila mafanikio ni vizuri sasa mkawaona wataalamu waweze kuwapa utaalamu sahihi kwa ajili ya kupungua uzito.


                                                                 

                                                                        STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO..MD

                                                              0653095635/0769846183
FAHAMU CHANZO CHA TATIZO LA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA UKIWA SAFARINI.(MOTION SICKNESS)

 Tatizo la kutapika kwenye safari ya gari, meli au ndege ni tatizo ambalo liko miaka mingi hata kabla ya kukua kwa teknolojia na ukisoma vitabu kigiriki na kiroma pia tatizo hilo lilionekana sana miaka hiyo. Mtu yeyote anaweza kupata tatizo hili japokua liko zaidi kwa watoto na mama wajawazito, bahati nzuri sio tatizo la kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.                               

chanzo ni nini? Tatizo hili hutokea pale ubongo unapopata taarifa zinazochanganya kutoka kwenye mwili mmoja yaani macho yanatoa taarifa tofauti, mwili taarifa tofauti na masikio taarifa tofauti. Mfano uko kwenye ndege mwili unatoa taarifa kwenye ubongo kwamba uko unasogea lakini macho yanatoa taarifa kwamba umekaa tu lakini pia maskio ambayo yanahusika sana na kubalance usimame kwenye mstari ulionyooka yanatoa taarifa kwamba umekaa tu, na huu mchanganyiko wa taarifa au signals kwenye ubongo ndio unakufanya utapike.

dalili za hali hii.

 • kichefuchefu
 • mdomo kujaa mate
 • kizungungu
 • kutapika
mambo ya kufanya kupunguza hali hii.
 • pumzika na uangalie sehemu mmoja kwa muda mrefu, vuta pumzi ndefu na na epuka kupepesa macho, kufunga macho pia kunasaidia.
 • angalia vitu ambavyo havitembei, kama uko kwenye boti angalia mawingu na kama uko kwenye gari angalia kioo cha gari.
 • epuka kula kabla ya safari.
 • epuka kuvuta sigara wakati wa safari au harufu nzito.
 • epuka kunywa pombe kabla au wakati wa safari.
dawa za kutumia..
kama hii hali inakusumbua mara kwa mara basi kuna dawa zinaitwa promethazine unaweza kumeza kidonge kimoja saa moja kabla ya safari kisha ukaendelea kumeza kila baada ya nne au sita wakati safari inaendelea.
Kwa kawaida hali hii inatakiwa kuisha baada ya safari, ukiendelea kuugua baada ya safari basi huo ni ugonjwa mwingine muone daktari.

                                                              STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
                                                         0653095635/0769846183FAHAMU JINSI YA KUTAMBUA DALILI ZA MWANZO ZA MTOTO MGONJWA KABLA HAJAZIDIWA ZAIDI.

Watoto wadogo hasa chini ya mwaka mmoja au miwili hawana uwezo wa kuongea hivyo wakianza kuugua unaweza usijue mpaka mtoto azidiwe kabisa ndio unaanza kukimbia usiku kutafuta msaada, sasa watoto wale ni rahisi sana kufariki kuliko watu wazima hivyo kugundua dalili za ugonjwa mapema ni vizuri zaidi kuliko kusubiri dalili za wazi..

Wazazi wengi hasa wazazi wapya wanakua wanafahamu kwamba dalili za kuugua mtoto zinakua wazi kama za watu wote kwa maana nyingine husubiri mpaka mtoto atapike, aharishe,ashindwe kupumua au apate degedege ndio ujue anaumwa.
Kuna dalili za mwanzo kabisa ambazo ukiziona ni vizuri kwenda hospital mapema, hii itamfanya mtoto atibiwe mapema na kuepusha adha zingine kama kulazwa, kutumia gharama kubwa za matibabu, kuugua sana na kupata madhara au kifo.
Mtoto wa kawaida hua na hamu nzuri ya kula, analala vya kutosha, anakua na nguvu na anakua mtundu na mchunguzi sana kwenye mazingira yanayomzunguka.
dalili za kwanza za mtoto mgonjwa ni kama ifuatavyo.......
 • kulia sana hata akiguswa kidogo tu.
 • kuacha kucheza.
 • kua mkimya sana.
 • kuonekana mchovu sana
 • kukataa kula 
 • joto la mwili kuanza kubadilika.
Mara nyingi hizi ni dalili za mwanzo kabisa na ukizipuuzia mtoto huingia kweye hatua ya pili ambayo huzidiwa sana na kuhatarisha maisha yake hivyo ni vizuri kuwahi hospital.
usitoe dawa yeyote kwa mtoto mgonjwa hata kama ni panado, hiyo sio dawa ya kutibu na huweza kuficha dalili za ugonjwa halisi na kumpa shida daktari.

                                                                STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          0769846183/0653095635

FAHAMU TATIZO LA MWANAMKE KUA NA UKE MKAVU NA MATIBABU YAKE.

Tatizo la uke mkavu lipo kwa baadhi ya wanawake japo sio wote, ni tatizo ambalo kimsingi linaweza kuleta msongo wa mawazo kwa wahusika, maumivu wakati wa tendo ndoa,kukosa hamu ya tendo la ndoa,au kuvunja mahusiano kabisa, kupata vidonda ukeni hata kuvuja damu.
Ni tatizo ambalo linaweza kua chanzo cha aibu kwa wanawake na kushindwa kujieleza tatizo hilo kwa wataalamu wa afya kwa kuogopa aibu.

Kushuka kwa kiwango cha homoni ya oestrogen mwilini hasa mwanamke anapofikisha umri wa miaka 40 kwenda mbele ndio chanzo kikuu cha kukauka kwa uke na dalili hizo hua wazi kabisa mwanamke anapofikika menopause au mwisho wa kuona siku zake za mwezi lakini kuna vyanzo vingine kama 
 • msongo wa mawazo
 • kunyonyesha
 • kuvuta sigara
 • baadhi ya magonjwa mfano hypothyrodism
 • mazoezi makali
 • uzazi
 • matibabu ya saratani
 • upasuaji wa kuondoa mayai ya mama.
 • baadhi ya dawa
 • kutokua na hisia na mwenza husika.
Nini cha kufanya?
ukipata tatizo hili unaweza ukamuona mtaalamu wa afya ambaye atakuchukua maelezo marefu na baadae atakupa suluhisho la matatizo yako kulingana na chanzo ambacho atakiona.
Lakini pia kwa wanawake ambao wanapata ukavu huu sababu ya umri basi kuna dawa mbalimbali za kupaka ambazo hua zina homoni ya oestrogen ndani yake ambayo huweza kusaidia tatizo hili, kumbuka tumia dawa tu ambayo imeelekezwa kwa kazi hii kwani baadhi ya dawa zimechanganywa na vitu mbalimbali kama perfume, na vitu asilia ambavyo sio salama kwa uke.

                                                            STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO(MD)
                                                   0653095635/0769846183


YAFAHAMU MAZOEZI 10 BORA SANA KWA AJILI YA KUPUNGUA UZITO.

Kama unasoma makala hii huenda wewe ni mdau wa mazoezi na fitness au una nia ya kupunguza uzito hivyo makala kama hizi zinakuvutia.
Pamoja kwamba ulaji wa chakula unachangia sana mtu kupungua uzito, mazoezi pia yana nafasi yake katika kupungua uzito na kukupa muonekano bomba.
Unaweza kupungua kwa chakula tu lakini utakua kama umekonda yaani hautakua na muonekano mzuri kama mtu ambaye kapungua kwa chakula na mazoezi.

Kuna mazoezi mengi sana ya kupungua uzito na yote yanafanya kazi lakini yanatofautina kasi ya kupungua uzito.
watu wengi wanaamini mazoezi ya kukimbia au aerobic yanapunguza uzito haraka ni kweli yanachoma mafuta hapo hapo lakini mazoezi ya kubeba uzito yanaendelea kukupunguza uzito masaa mpaka siku baada ya mazoezi hayo.
Leo tutaangalia mazoezi kumi ambayo ynapunguza uzito haraka kulingana na wingi wa calories au uzito kumbuka calorie 7700 ni sawasawa na kilo moja ya uzito na upunguaji hutegemea na uzito yaani mtu mwenye uzito mkubwa anachoma calories nyingi kwa kufanya mazoezi sawa na mtu mwenye uzito mdogo.
kubeba chuma; haya ni mazoezi ambayo sio hupunguza tu uzito lakini hujenga na misuli pia na kama nilivyosema hapo mwanzo mazoezi haya huchoma calories 250 mpaka 300 kwa saa lakini kwasaabu shughuli ya kuendelea kuchoma huendelea hata ukiwa ushatoka mazoezini ni kwamba unaweza kuchoma zaidi sababu yaani kesho yake 200, kesho kutwa 100 na kadhalika kwani mwili wako utaendelea kuhitaji oygen nyingi kwa ajili ya misuli hiyo.
kuruka kamba:Ni zoezi ambalo unaweza kulifanya kwenye mazingira yeyote hata kama kuna hali mbaya ya hewa na kifaa chako ni kamba tu na eneo la kurukia..inaweza kua chumbani au sebuleni.
kwa kasi ya kuruka mara 120 kwa kwa dakika unaweza kuchoma calories 667 mpaka 990 kwa saa kulingana na uzito wako.
kukimbia kupanda mlima; ukifanya mazoezi ya kukimbia na kupanda mlima yanachoma mafuta zaidi kuliko kukimbia kawaida kwenye mstari ulionyooka au tumambalale.
kwa kupanda mlima na kushuka unaweza kuchoma calories 639 mpaka 946 kulingana na uzito wako.

mazoezi ya kupigana au kick boxing; sio mazoezi ya watu wengi hasa hap kwetu kwasababu ni mchezo ambao unachukuliwa kwamba ni wa ugomvi tu lakini wanaofanya mazoezi haya huchoma calories 582 mpaka 864.

kuendesha baiskeli; kuendesha baiskeli hasa maeneo yenye muinuko kidogo huku ukichochea kwa kasi sana kunachoma mafuta zaidi kuliko kuendesha taratibu sehemu zenye miteremko.
mazoezi haya yanakadiliwa kuchoma calories 568 mpaka 841.

kukimbia tambalale; mazoezi ya kukimbia uwanjani au mtaani ni moja ya mazoezi pendwa na watu wengi, na yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupungua na kua fit.
mazoezi haya yanakadiriwa kuchoma calories 566 mpaka 839 ukikimbia umbali wa kilometa 16 ndani ya saa moja  kwa mwendo wa kawaida japokua ukikimbia kwa kasi zaidi unachoma zaidi.

mashine ya baiskeli; hii ni ile baiskeli ambayo ni maalumu kwa ajili ya mazoezi, huweza kutumika sehemu yeyote na kukupa majibu mazuri.
naweza kuchoma calories 498 mpaka 738 kama ukiendesha kwa kasi ndani ya saa moja, kumbuka kuongeza ugumu wa baiskeli kwa matokeo chanya zaidi.

mazoezi ya kupanda ngazi; ni mazoezi mazuri hasa kwa watu ambao wanaishi sehemu zenye maghorofa au viwanja vikubwa , unaweza kuamua usitumie lift mara moja moja ukitoka kazini na kupanda kwa ngazi mpaka nyumbani kwako.
mazoezi haya huchoma caories 452 mpaka 670 kwa kila ngazi 77 unazozopanda hasa ukiwa kwa mwendo wa haraka.
planking; haya ni mazoezi ya kukunja mikono kama unalala chini kisha unabaki hivohivo kwa muda fulani mpaka unapochoka na kuachia, zoezi hili ni gumu kidogo lakini unaweza kufanya muda mwingi zaidi kadri unavyozoe na hukadiriwa kuchoma calories 4 mpaka 5 kwa dakika.
                                                   
mwisho; haya ni mazoezi ambayo unaweza kuyafanya kama unataka kupungua haraka lakini kama wewe ni mnene sana au una sababu za kiafya za kushindwa mazoezi haya unaweza ukaanza kwa kutembea kwanza kwani mazoezi ya kutembea pia yana uwezo wa kumpunguza mtu na kumpa afya njema.
                                                                 STAY ALIVE

                                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO (MD)
                                                          0653095635/0769846183

UFAHAMU UGONWA WA TEZI DUME NA MATIBABU YAKE.

Tezi dume ni nini?
Huu ni ugonjwa unaotokea baada ya kuvimba kwa tezi inayofahamika kwa jina la prostate gland, tezi hii huanza kuvimba mwanaume anapofikisha miaka arobaini na kuendelea na tafiti zinaonyesha kwamba nusu ya wanaume wa miaka 50 na kuendelea wana tatizo hili.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
Homoni za kiume; homoni maarufu kwa jina la testosterone ni homoni ambazo humfanya mtu aitwe mwanaume kwanzia kubalehe, uzazi wa mwanaume na muonekano wake.
Tafiti zinaonyesha kwamba homoni hii ni moja ya chanzo kikuu kwani wanaume ambao wana tatizo hili kwani wanaume ambao waliondolewa korodani walionyesha kutougua ugonjwa huu.
chakula; Tafiti zinaonyesha kuna mahusiano kati ya aina vya chakula na ugonjwa huu, watu wanaoishi mjini na kula nyama kwa wingi huathirika zaidi kuliko wale ambao wanakula vyakula vya ambavyo vina protini kidogo maeneo ya vijijini.
umri; kuna misuli ambayo inazuguka tezi dume muda wote, umri unavyozidi kwenda basi misuli ile inazidi kuchoka na kuipa nafasi tezi hiyo kuvimba.

dalili za ugonjwa huu.
 • kukojoa mara kwa mara
 • kuamka usiku kukojoa mara kwa mara
 • kushindwa kuzia mkojo ukibana
 • kujikojolea usiku
 • maumivu wakati wa kukojoa 
jinsi ya kugundua tatizo hili
 Tatizo hili linaweza kugunduliwa kwa historia ya mgonjwa, ukaguzi wa kitaalamu au physical examination na kuchukua baadhi ya vipimo.
kipimo cha utrasound huweza kugundua tatizo husika kupima ni kiasi gani tezi hiyo imeongezeka kwa ukubwa.
 Vipimo vingine huchukuliwa kuangalia magonjwa ambayo yameambatana, yanafanana au yameletwa na ugonjwa huu mfano ni kipimo cha sukari, kipimo cha uwezo wa figo kufanya kazi na kipimo cha satatani ya tezi dume kitaalamu kama PSA.

 matibabu; 
matibabu ya tezi dume yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, kuna matibabu ya dawa na matibabu ya upasuaji.
mgonjwa kwa mara ya kwanza utatibiwa na dawa kama finastreride, doxazosin, terazosin na kadhalika na pia atawekewa mpira wa kuondoa mkojo kama atashindwa kukojoa vizuri.
Lakini kama matibabu haya yasipofanya kazi nzuri basi mgonjwa huyu atafanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi hiyo.

Aina hizi za upasuaji zimegawanyika katika sehemu mbalimbali kutokana na teknolojia inayotumika sehemu husika.
Madhara ya upasuaji ni kama kutokwa damu nyingi, kushindwa kutoa mbegu, kuishiwa nguvu za kiume na kuumia kwa njia ya mkojo.


                                                     STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183


ZIJUE SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA VIPIMO VIONYESHE UNA UKIMWI WAKATI HAUNA.(FALSE POSITIVE)

Japokua uwezo wa vipimo vya ukimwi kugundua ukimwi ni mkubwa sana, lakini uwezo huo sio 100%,  vipimo vya ukimwi wakati mwingine huweza kuonyesha kwamba mtu ana ukimwi wakati hana.
Kipindi ambacho kitatumika kujaribu kuthibitisha ni kweli kama mtu huyo sio mgonjwa kunaweza kumuacha katika hali mbaya sana ya kisaikolojia muhusika ambaye tayari anahisi ameambukizwa na hata kuvunja mahusiano.
                                                       
Kulingana na muongozo wa shirika la afya duniani(WHO), mgonjwa hatakiwi kupewa majibu ya kua ameathirika na ukimwi mpaka apimwe na vipimo vya aina tofauti ambavyo vinahakikisha kweli ana maambukizi ya ukimwi.
shirika la doctor without borders(MSF) lilifanya utafiti  na kugundua kwamba vipimo havifanani nguvu hivyo kuleta makosa katika utoaji wa majibu na msisitizo mkubwa ukiwa katika watu ambao wanapewa majibu kwamba wameathirika wakati hawajaathirika.
ushahidi wa hili ni upi?
Data za shirika hilo la msf zinasema kwamba damu ilikusanywa kutoka kwa wagonjwa 2785 wa ukimwi ambao walikua wanahudhuria katika kliniki  mbalimbali za nchini kenya, uganda, congo, guinea na cameroon.
damu hiyo ilihifadhiwa vizuri na kutumwa ubeligiji kwa ajili ya vipimo vya ukimwi ili kuweza kuhakiki kama kweli wale watu ni wagonjwa wa ukimwi.
kati ya watu 2785 ambao damu zao zilichukuliwa, watu 140 walikua hawana ukimwi.
kwa maana nyingine hawa watu 140 wamekua wakimeza dawa za ukimwi kwa muda wote huo kimakosa.
Baada ya kupewa majibu mapya wengine walifurahi, wengine walisikitika kwani walikiua tayari kwenye mahusiano na waathirika wenzao na wengine walikua wameachwa na wake au wame zao sababu ya majibu hayo yenye utata.
sababu za majibu hayo kuja tofauti ni kama ifuatavyo....
magonjwa mengine; vipimo vya ukimwi kitaalamu kama antibody test havipimi virusi moja kwa moja bali hupima antibodies ambayo ni aina fulani ya protini inayotengenezwa kujaribu kupambana na virusi vya ukimwi wakati mtu ameathirika.
Bahati mbaya kwa baadhi ya watu protini hiyo huweza kuonekana kwenye magonjwa mengine kama kichocho, ugonjwa trypanasoma, lupus na aina fulani ya mafua yasababishwao na virusi.kitaalamu tunaita cross reactivity.
mpimaji kutokua na uzoefu; wakati mwingine mtu anaweza kujipima tu nyumbani na kuyapokea yale majibu kabla ya kwenda kupima kwenye vipimo zaidi kuhakikisha, vipimo vingi ambavyo watu wanatumia kujipima nyumbani haviruhusiwi kuthibitisha maambukizi ya ukimwi mpaka mgonjwa apimwe na vipimo vingine kuthibitisha hilo. lakini pia wakati mwingine mtoa huduma anaweza asiwe mzoefu sana kutoa majibu sahihi hasa kama kuna mstari unakuja unafifia.
Kawaida majibu ya ukimwi yanatakiwa yasomwe ndani ya dakika 15 mpaka tu baada ya hapo majibu hayo sio halali tena.
Sasa mtu anaweza kupima nyumbani akaonekana hana akaamua kuhifadhi kipimo, baadae jioni mstari wa pili unaonekana anaanza kuchanganyikiwa.
vipimo vilivopita muda wake wa matumizi; Vipimo hivi hupoteza ubora waka mara tu muda wake wa matumizi unapoisha, hivyo majibu yanayotoka baada ya hapo sio ya kuyaamini hata kidogo kwani hayana uhakika wa kutosha.
Mwisho; majibu ya aina hii ni changamoo sana hasa sehemu ambazo zina uhaba wa vifaa vya kupimia, lakini kwa sehemu ambazo wana mashine za kupima wingi wa virusi baada ya mgonjwa huhisiwa ameathirika, majibu yanaweza kutiliwa mashaka na kuhakikishwa tena na vipimo vikubwa kama PCR.

                                                                STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                    0653095635/0769846183

HAYA NDIO MAGONJWA SABA YA ZINAA YANAYOWEZA KUAMBUKIZWA KWA KULAMBA SEHEMU ZA SIRI.

85% ya vijana umri wa miaka 18 mpaka 44 hushiriki aina ya ngono inayohusisha kulamba sehemu za siri au oral sex.

wengi hudhani kulamba sehemu hizo bila kushiriki tendo la ndoa huweza kuzuia magonjwa ya zinaa kitu ambacho hakina ukweli.
kwa kifupi ni kwamba;
 • unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa mdomoni kwako au kooni kwako kwa kulamba uume, uke au maumbile ya nyuma wa mgonjwa wa zinaa.
 • unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kwa kulambwa sehemu zako za siri na mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa mdomoni kwake au kooni.
 • unaweza kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa sehemu mbili kwa mpigo yaani mdomoni na sehemu za siri.
 • magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa njia ya mdomo yanaweza kusambaa mwili mzima kama yanavyosambaa haya ya kawaida.
 • kulamba sehemu za siri kama mkundu kunaweza kukusababishia magonjwa mengine kama ya ini na minyoo mfano hepatitis A na minyoo ya amiba.
 • ugonjwa wa zinaa unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu ambaye hana dalili hata moja sababu magonjwa mengi za zinaa hayana dalili kabisa.
 • kunyonya sehemu za siri kunaweza kuhamisha virusi fulani ambavyo hukaa sehemu za siri na kukusababishia saratani ya koo.

magonjwa yafuatayo ya zinaa huweza kuambukizwa kwa njia ya kulamba sehemu za siri au oral sex.
ugonjwa wa ukimwi; japokua hatari ya maambukizi ya ukimwi ni ndogo kwa aina hii ya ngono lakini uwezekano upo hasa kwa watu wanaotokwa na damu kwenye fidhi, wenye vidonda mdomoni au sehemu za siri, au watu wenye magonjwa ya zinaa, kwni maji maji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke na sehemu za siri za mwanaume yanakua na virusi vingi sana vya ukimwi.

kisonono; huu ni ugonjwa unaosabbishwa na aina ya bacteria kwa jina la naisseria gonorhea, ni ugonjwa wa zinaa uliokua ukiambukizwa kwa ngono ya kawaida tu lakini tangu kuanza kutumika kwa mdomo pia ugonjwa huu unaweza kukutwa mdomoni na moja ya madhara makubwa ya ugonjwa huu ni ugumba kwa wanawake.
kaswende; huu ni ugonjwa ambao huanza na kidonda kisichokua na maumivu sehemu iliyoathirika...inaweza kua mdomoni, au sehemu za siri baadae hufuatwa na upele mwili mzima, na hata ganzi hatua za mwishoni.
ugonjwa huu hushambulia mishipa ya fahamu hivyo huweza kufika mpaka kwenye ubongo na kuleta ukichaa.
herpes; huu ni ugonjwa unaosababishwa na aina fulani ya virusi kwa jina la herpes simplex type 2, virusi hushambulia sehemu za siri za binadamu lakini vikilambwa huenda kukaa mdomoni, ugonjwa huu huweza kuambatana na virusi vya HPV ambavyo huleta saratani ya koo.

warts; hii na aina fulani ya uvimbe inayotokea sehemu za siri na huweza kuvuja damu sana kama ikijeruhuhiwa, ugonjwa huu hutibiwa kwa kuchomwa na aina fulani ya dawa au upasuaji kuuondoa sehemu husika.
Hepatitis; Huu ni mchnganyiko wa magonjwa ya ini ambayo huambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kugusa majimaji au damu ya mgonjwa, kula uchafu na kadhalika.
Ni moja a magonjwa hatari sana ambayo huleta saratani ya ini ambayo kimsingi haitibiki.

chylamydia; huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unaweza kuambukizwa kwa njia ya tendo la ndoa la kawaida au lulamba sehemu za siri.
huweza kuvamia mlango wa kizazi, kizazi chenyewe na mirija ya uzazi.

Mwisho; kulamba sehemu za siri sio mbadala wa kukimbia magonjwa ya zinaa, kama unaitaka huduma hii basi ni vizuri uwe na mpenzi mmoja ambaye ni muaminifu lakini kama una mahusiano mengi basi ni bora uwe mvaaji mzuri wa kondomu na usikubali kulamba wala kulambwa.
baadhi ya magonjwa ya zinaa hayana dalili kabisa na utakuja kujua siku unatafuta mtoto humpati.

                                                                     STAY ALIVE

                                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                               0653095635/0769846183

JINSI UNAVYOWEZA KUPUNGUA UZITO KIRAHISI KIPINDI HIKI CHA CORONA.

Kipindi hichi ambacho watu wengi wanakaa nyumbani ni kipindi muhimu sana cha kubadlisha maisha yako ya kimwili na kiakili kama ukiamua kufanya hivyo kutoka moyoni.
kuna sababu nyingi ambazo zimekua zikiwazuia watu kupungua uzito kama kukosa muda wa mazoezi sababu ya kazi, kushindwa kufanya diet sababu ya kula nje ya nyumbani muda mwingi, kukosa nidhamu ya kula sababu ya presha ya marafiki kwenda kunywa pombe na kula vyakula mahotelini na bar siku za mwisho wa wiki ambapo kwa kiasi kikubwa imekua ikirudisha nyuma juhudi zao za kupungua.
Lakini kwa kipindi hiki ambacho muda mwingi unautumia nyumbani basi kuna mabadiliko makubwa ya kimuonekano unaweza kufanya afya yako iwe bora zaidi.
kuna mambo matatu ya msingi unaweza kufanya sasa hivi kama ifuatavyo.
chakula; punguza ulaji wa mazoea na uanze kula kama mtu anayetaka kupungua uzito kweli, kuna diet za aina nyingi sana kikubwa chukua moja ambayo unaiweza na uende nayo taratibu mpaka utakapopata matokeo.
Na kwasababu uko nyumbani sasa hivi basi unaweza kupika diet yeyote unayotaka, kama huna diet chukua hii http://www.sirizaafyabora.info/2018/01/ufahamu-mpangilio-bora-wa-chakula.html usitamani wanachokula wenzako ambao ni wembamba, wewe ndio unajua unataka nini hivo fuata malengo yako.
mazoezi; sasa hivi una muda mwingi sana wa mazoezi kiasi kwamba unaweza ukafanya asubuhi na jioni kwa masaa mengi kwasababu huna pakwenda, hata ukichoka sana kesho utalala mpaka usingizi uishe.
Tafuta kampani ya mazoezi hapo hapo nyumbani ili kupata motisha, unaweza kuruka kamba au kukimbia na yote ni sawa.
kipindi hiki sio salama sana kwenda gym hivyo fanya mazoezi nyumbani.

.weka malengo rasmi ya kupungua uzito; watu wengi wanaotaka kupungua uzito hawana malengo, mara nyingi wanaamka na kiu kubwa ya kupungua kisha kiu hiyo inaisha baada ya wiki moja.
kwa diet ya kawaida kabisa ambayo haina stress sana unaweza kupungua kilo mbili kwa mwezi, kwa maneno rahisi ni kwamba ukikomaa upungue kilo mbili kila mwezi basi utapungua kilo 24 kwa mwaka hivyo hata kama una uzito kiasi gani baada ya muda utaisha tu. kwa mtu wenye kitambi tu ila sio mnene anahitaji miezi mitatu tu kukimaliza.

weka malengo ya siku, wiki,mwezi na mwaka kisha yafuate na mabadiliko utayaona, kumbuka huwezi kubadilisha chochote kwenye maisha yako kwa kuishi kwa mazoea lazima ubadilishe kitu ili upate kitu.

                                                                STAY ALIVE

                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.(MD)
                                                     0653095635/0769846183

NAMNA 4 YA KUFADIKA NA KARANTINI.David Duncan Kipeta


Dunia imevamiwa na adui ambaye kwa kiasi kikubwa sisi kama wakazi wa dunia yetu hatukuwa tumejiandaa kubabiliana naye. Ametumavia na kutupiga na kisha kutusambaratisha kila mtu na kwake, watu wamejifungia na hawathubutu kutoka nje huku baadhi ya mataifa watu wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi za kila siku lakini wakiwa na hofu na wenye tahadhari kubwa wakiogopa kukutana na huyu adui mkubwa na mbaya mwenye kusababisha watu kupata homa kali, mafua makali, vichwa kuuma na mbaya zaidi wanapata homa kali sana ya mapafu yenye kusababisha mfumo wa upumuaji kuwa wa shida. Hali inakuwa mbaya sana kwa ndugu zetu wenye magonjwa ya muda mrefu na yenye kuathiri sana mfumo wa kinga wa mwili. Magonjwa kama kisukari, kifua kikuu, shinikizo la damu, virusi vya ukimwi/Ukimwi yanaongeza hatari ya madhara yatokanayo na adui yetu huyu. Huyu adui anaitwa CORONA VIRUS INFECTION DISEASE OF 2019 (COVID19).


COVID19 ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya corona ambayo huambukizwa haswa kwa kushika au kugusa majimaji yanayotoka kwa mtu mwenye maambukizi hayo. Ugonjwa huu ulianzia na kugunduliwa huko nchini China katika mji wa Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019 na ulianza kushamili kuanzia mwezi wa Disemba mwaka huo. Ugonjwa huu uligunduliwa na Daktari Lee Chen ambaye alifarika hapo baadaye kwa maambukizi ya COVID19. Njia zinazosababisha kuenea kwa ugonjwa huu ni kuvuta hewa yenye viini vya virusi vya corona, kushikana mikono, kugusa nguo za muathirika wa virusi vya corona, kushika vitu vilivyoshikwa na mtu mwenye virusi vya corona.

NAMNA YA KUJIKINGA NA COVID19
Nchi nyingi zimeweka namna ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kwa kuzuia mikusanyiko ya wananchi, kusisitiza kanuni bora za afya hasa kwa kunawa mikono na sabuni au vitakasa mikono(hand sanitizer), kuvaa barakoa (face masks) na zuio la kuchangamana (social distancing). Lakini jambo kubwa na muhimu linalofanywa kwa watu wanaohisiwa kuwa na maambukizi ni kuzuiwa kuchangamana na watu wasiohisiwa kuwa kuwa na maambukizi. Njia hii inatambulika kama karantini.

Karantini ni kitendo cha kuzuia au kujizuia kutokuchagamana na watu wengine ikiwa mtu fulani amehisiwa au anahisi kwamba amepata maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwa tiba au chanjo ya ugonjwa huo haijapatikana. Wikipedia kamusi inaeleza kuwa “karantini inamaanisha kuzuia miendo ya watu ambao wanaweza kuathiriwa na ugonjwa wa kuambukiza ilhali ugonjwa kwao haukuweza kuthibitishwa bado… karantini hutumiwa pia kama mgonjwa anazuiliwa kukutana na watu wengine ili kuzuia uenezaji wa ugonjwa hatari. Karantini inaweza kutumika kwa wanadamu, lakini pia kwa wanyama wa aina mbalimbali, na wote kama sehemu ya udhibiti wa mpakani na ndani ya nchi”.
Ingawa karantini hufanana zaidi na kutengwa, maneno haya mawili yanamaana tofauti. Kutengwa ni kitendo cha kumuweka mtu aliyethibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa kuambukiza mbali na watu wengine ili kuzuia maambukizi yasienee.
 Kikawaida karantini huwekwa kwa muda wa siku arobaini
(40) Japokuwa inaweza kuwa muda wa siku kadhaa kuanzia saba (7) na kuendelea.


NAMNA YA KUFAIDIKA NA KARANTINI
 Katazo la kutembea na kuchanganyika na watu lina faida sana kwa nchi ili kuzuia kuenea kwa maambukizi na hivyo kufanya mamlaka za afya kuwa na mzigo mdogo katika kushughulikia watu wachache wenye maambukizi na wenye dalili za maambukizi. Karantini husaidia katika kufuatilia mienendo ya watu na kufuatilia visa vya maambukizi kwa urahisi na umakini mkubwa. Hii husaidia pia katika kupunguza matumizi ya vifaa tiba ambavyo vingetumika kwa watu wengi ambao wangeambukizwa.
 Pamoja na faida zote hizo kwa nchi au jamii fulani pia mtu mmoja mmpoja anaweza kufaidika sana kwa uwepo wa karantini. Faida hizo zaweza kuwa za kiafya, kiuchumi, kimahusiano au kijamii. Katika makala hii tutangalia namna unavyoweza kufaidika na karantini.

Sura ya Kwanza

AFYA

Karantini inaweza kuwa na faida sana kwa mtu binafsi ikiwa ataliangalia jambo hili kama nafasi ya pekee ya kujenga afya njema ya mwili wake. Kabla ya karantini watu wengi hawajali afya zao kama inavyotakiwa kwani watu hawalali kwa muda wa kutosha, kula vizuri na kwa kutulia, kupata muda mwingi wa kujisomea na hata kufanya mazoezi na kadharika lakini wakati wa karantini unaweza kumsaidia mtu kujenga afya bora ya mwili wake ikiwa ataliangalia jambo hili katika mtazamo chanya. Afya bora wakati huu wa karantini inaweza kujengwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

Kupata muda wa kutosha wa kupumzika.
Kitabibu mtu mzima anatakiwa kupata muda usiopungua masaa nane (8) ili kupumzika. Muda huu unatakiwa kutumiwa hasa kwa kulala. Watu wengi wanakosa muda wa kutosha ili mkulala wakati wa usiku. Kulala masaa nane wakati wa usiku ni muhimu sana ili kujenga afya bora ya akili,mfumo wa uzazi, mfumo wa kinga, mfumo wa utoaji taka mwili na hata mmeng’enyo bora wa chakula.
 Kukosa muda wa kutosha wa kulala husababisha kutengenezwa kwa kemikali kama cortisol ambayo huharibu sana afya ya akili na hata viungo vingi vya mwili ikiwemo moyo, maini, figo na hata viungo vya uzazi kutokana na uwingi wa kemikali hii katika damu. Ubongo huanza kukosa kupumzika na hivyo huweza pia kumfanya mtu akose usingizi na baada ya muda mrefu mtu anaweza kupata magonjwa ya akili ikiwemo hasira za karibu zisizo na sababu, kiharusi, msongo wa mawazo na hata sonona.

Mfumo wa kinga huathiriwa sana ukosefu wa usingizi kwa sababu ya uwepo mkubwa wa kemikali ya cortisol ambayo huathiri na hta kuua seli lindaji (white blood cells) zinatotumika kulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hivyo ili kuwa na mfumo wa kinga ulio boira na imara ni muhimu sasna kupata muda mwingi wa kulala.
Kukosa muda wa kulala wa kutosha huathiri sana mfumo wa uzazi. Na hii ni moja kati ya sababu kubwa sana za upungufu wa nguvu za kiume, kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na wanaume na hata kukosa kufurahia tendo la ndoa. Tafiti mbali mbali zimefanyika na kuonyesha kwamba ukosefu wa usingizi hupunguza uzalishaji wa homoni ya kiume iitwayo testosterone ambayo ndio hufanya kazi ya kuongeza msukumo au hamu ya kufanya tendo la ndoa. Homoni hii ipo kwa uwingi sana kwa wanaume na kwa kiwango kidogo kwa wanawake. Homoni hii pia hujulikana sana kama sexual driver yaani kiamshi au kisukumo cha kufanya tendo la ndoa. Hivyo ukitaka kuwa na afya njema ya mfumo wa uzazi na kufanya vizuri na kufurahia tendo la ndoa, usingizi ni muhimu sana. Kipindi hiki cha karantini ni kipindi cha wewe kuirudisha na kujenga heshima katika kitanda chako na mwezi wako lakini tu itafanyika hivyo ukipata muda mwingi wa kupumzika kila siku.
Hizo pamoja na athari zingine kama mmeng’enyo mbaya wa chakula, kuharibika kwa mfumo wa utoaji takamwili ambao huathiri sana figo na maini zinasababishwa kukosa muda wa kutosha wa kulala hivyo katika kipindi hiki cha karantini ni muhimu sana kupata muda wa kutosha kupumzika kwa kulala usingizi si chini ya masaa nane (8) kwa mtu mzima na mtoto kuanzia masaa kumi (10). Usingizi ni Afya.

Kula Vizuri
 Chakula ni afya. Ili kuwa na afya bora ni muhimu kuzifuata kanuni za afya ikiwepo kula chakula bora. Kabla ya karantini watu wengi hula vyakula visivyo vizuri na visivyo na virutubisho vya kutosha ili kujenga afya bora. Vyakula maarufum kama fast foods au junk food mfano wa chips zinazouzwa, vinapoliwa mara kwa mara na kwa muda mrefu hudhoofisha afya kwa kuzorotesha mifumo mbali ya mwili wa binadamu. Vyakula vya kujenga mwili, vyakula vya kulinda mwili na vya kuupa mwili nguvu hutakiwa kutumiwa kwa uwingi kwa kipindi hiki cha karantini.
 Vyakula vya kujenga mwili kama maziwa, mayai, samaki, nyama, maharage na mboga za majani pamoja na vile vya kulinda mwili kama maini, samaki, mboga za majani, matunda ni muhimu na vinahitajika kwa kiwango kikubwa sana kwa kipindi hiki cha karantini bila kusahau vyakula vya kuupa mwili nguvu ili kuendelea na shughuli nyine muhimu za nyumbani.

Kufanya Mazoezi
Katika kuhakikisha umuhimu wa mazoezi katika kipindi hiki cha karantini, hivi karibuni Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Mseveni alionekana katika picha na mitandao ya kijamii akiwa nyumbani kwake akifanya mazoezi mbalimbali ya viungo ikiwemo push up. Alifanya hivi ili kuhimiza umma kuhusu umuhimu wa mazoezi ya viungo huku wakiendelea kubakia ndani katika makazi yao na si kufanyia mazoezi nje kwenye umati wa watu kama gym na hata katika viwanja vya mazoezi au kukimbia nje. Jambo hili la kufanya mazoezi nje au mbali na makazi huweza kuongea hatari ya kupata maambukizi ya vizuri vya COVID19. Uwepo wa katazo la kutoka nje na kuchangamana na watu kwa sababu ya kuogopa kuenea kwa COVID19 sio sababu na isiwe sababu ya kuacha kufanya mazoezi ya viungo. Unaweza kufanya mazoezi ya kutosha hata katika chumba chako cha kulala. Hivyo naomba nikusihi kuendelea kufanya mazoezi ya viungo kila siku na katika makazi yako. Mwanasaikolojia na mwandishi wa kitabu cha The Barbarians at the PTA anashauri kuwa “Endelea kufanya mazoezi na rafiki zako. Ikiwa unapata uvivu kufanya mazoezi peke yako, unaweza kupanga ratiba na rafiki zako ili kufanya mazoezi kama yoga na mengineyo kwa njia ya video katika muda mmoja”[1]
Kumbuka: Afya yako ni mtaji wako na mtaji huu hujengwa na mkukuzwa kwa kula chakula bora, kulala vizuri na kufanya mazoezi.
 Nakutakia heri katika kuendelea kujenga mtaji wako.


Sura ya Pili

UCHUMI

Kipindi inapotanghazwa karantini ni kipindi ambacho hofu ya kudorora kwa uchumi huwa kubwa sana. Uchumi hudorora kwa kwa watu binafsi, makampuni na hivyo hata kwa taifa. Hofu hii huwa kubwa kutokana na ukweli kwamba watu hupunguza kwenda kazini na wengine huacha kabisa. Kutokana na kutofanyika kwa shughuli za kiuchumi, watu huweza kuwa na hali mbaya kiuchumi hasa wale wasio na ajira za kudumu au waliojiajiri wenyewe. Lakini kwa shghuli zisizohamishika au zinazohitaji uwepo wa mtu husika mahali pa kazi hali yaweza kuwa mbaya zaidi tofauti na zile zinazoweza kuhamishika.

Pamoja na ukweli huu wa mabadiliko ya kiuchumi bado tunaweza kuwa na tumaini la kufanya kazi kama kawaida lakini kwa mfumo mwingine. Natamani uangalie mfano wa Mwandishi wa habari na mchekeshaji wa kipindi cha televisheni cha The Daily Show cha nchini Marekani Ndugu Trevor Noah. Yeye ameendelea na shughuli zake za kutoa habari na kuchekesha huku akisalia katika makazi yake. Muongozaji na mchekeshaji wa kipindi cha The Hellen Show, Hellen amekua akiendelea na kazi zake kama kawaida lakini akiwa katika makazi yake. Lakini pia mmiliki wa kampuni ya Zoom Video Communications inayoongoza kwa utoaji wa huduma ya mikutano kwa njia ya video (Video teleconferencing) ndugu Eric Yuan amekuwa akiendelea kufanya kazi na mikutano yake kwa njia ya video. Njia hii ni njia maarufu ikiwa kuna vizingiti kama hivi ya karantini au kutokana na umbali wa wahusika. Pia kulingana na aina za kazi hasa za kiofisi, watu hufanya kazi zao majumbani katika kompyuta na kuzituma katika ofisi zao. Hivyo kufanya shughuli zao kama kawaida.

Kipindi hiki cha karantini kikitumiwa vizuri kinaweza kuwa cha faida kubwa kwa mtu mmoja mmoja. Kuna mambo mengi ambayo mtu anaweza kuyafanya ambayop yakaleta faida kubwa kwa uchumi binafsi na kwa nchi nzima kwani watu wengi hukaa nyumbani. Mambo haya ni kama yafuatayo:

Kuongeza ujuzi wa kiuchumi
Kipindi hiki cha karantini kinaweza kutumiwa katika kuongeza ujuzi katika fani mbali mabali za maisha kwani watu wengi wanakuwa huru na hawajabanwa na majukumu mengi. Ujuzi huu huweza kuongezwa kwa kusoma vitabu au kutembelea tovuti mbalimbali zenye kufundisha maudhui ya kazi fulani na hata namna bora ya kufanya uwekezaji.

Biashara za mitandaoni na uwekezaji (Online marketing and investments).
Hizi ni aiana za biashara ambazo hufanyika kwa njia ya mtandao na mara zote haihitaji wahusika kukutana kwani mnunuzi huagiza mahitaji yake na kuyalipia kwa njia ya mtandao na kisha mahitaji yake hayo hutumwa kwa njia ya posta au kuletewa hadi katika makazi yake na mtu mwingine ambaye hufanya kazi ya kubeba mizigo.
Uwekezaji wa mitandaoni ni njia nzuri pia kwa kipindi hiki kwani huweza kufanya uchumi wako baada ya kipindi cha karantini ya COVID19 kuwa mzuri. Uwekezaji huu huweza kutumia mitandao kama Expert option

Tahadhari: Ni muhimu kutambua kwamba katika kipindi hiki ni muhimu kuwa na fedha ya akiba ili kuweza kuhudumia mahitaji ya familia. Hivyo tahadhari zote za kiuchumi inabidi zichukuliwe ili kuhakikisha kwamba hupati shida katika kipindi hiki kigumu.

Kutoa elimu au kozi mbalimbali kwa njia ya video au mitandao ya kijamii
Ikiwa una ujuzi au utaalamu juu ya kitu fulani basi usikate tamaa, kipindi hiki cha karantini unaweza kuendelea kutoa elimu kwa kupitia mitandao ya kijamii na hata baadhi ya mada kuwafikia watu wengi zaidi kuliko kipindi kingine chochcote kwani watu wako huru na wana muda wa kutosha kusoma na kujifunza zaidi kwa kupitia mitandao hii ya kijamii.

Kununua Hisa
Baadhi ya makampuni ya biashara yanaendelea kufanya vizuri katika masoko yake kutoka na utengenezaji bora wa bidhaa na huduma zingine zitolewazo. Makampuni haya yanauza hisa na ikiwa una akiba ya kutosha ni muhimu kuwekeza katika kununua hisa ili kuendelea kupata faida ambayo itakusaidia kuinuka kiuchumi baada ya karantini ya COVID19 kuisha.

Kufanya kazi za muda wa kujitegemea (freelancing)
Hizi ni kazi ambazo mtu fulani hufanya kwa muda wake aliojipangia na baada ya kumaliza hupata ujira wake hivyo anaweza kuendelea au akaacha baada ya malipo. Mtu mmoja huweza kujifanya kazi mbalimbali kwa kujipangia muda wake mwenyewe. Njia hii huweza kuingiza kipato kikubwa kwa muda mfupi. Baadhi ya programu tumizi (application) kama Freelancer na zinginezo ni nzuri kwa kazi hizi kwa kipindi kama hiki.Sura ya Tatu

MAHUSIANO
Mahusianona wengine ni jambo la kwanza kwa kiumbe chochote. Hii ni zawadi kubwa ya Mungu toka kuumbwa kwetu. Mahusiano baina ya watu ni jambo la msingi ambalo linatakiwa kuendelezwa katika kipindi hiki kigumu cha karantini.

Katika kipindi hiki, Mahusiano yanaweza kujengwa na kuwa mahusiano thabiti na imara au yanaweza kuharibika kwa sababu mbalimbali. Mahusiano yanajengwa na ukaribu wa watu katika muda fulani. Watu wengi huwa na mahusiano mazuri kwa sababu wanaonana mara kwa mara na hivyo huwasiliani kwa ukaribu. Lakini katika kipindi hiki, watu hawaonani na hivyo hupunguza mawasiliano na hata mahusiano yao hulegea.

Baadhi ya mahusiona yalijengwa kwa sababu watu wanaonana mara kwa mara na hivyo katika kipindi hiki mahusiano yao yako katika kipimo ili kujua uimara wake. Katika kipindi hiki, watu wengi wanakuwa huru na hawajabanwa na majukumu yao ya kila siku kama katika kipindi kabla ya katazo la mikusanyiko ana kuchangamana hivyo ni kipindi kizuri zaidi cha kujenga mahusiano na wenzi wao, watoto, familia na hata ndugu na marafiki wengine kwani hakuna mtu mwenye majukumu mengi sana yanayowafanya kukosa muda wa kuzungumzia mambo yao ya msingi. Zifuatazo ni namna za kujenga mahusiano na watu wengine katika kipindi hiki;

a)       Matumizi sahihi ya muda na watu tunaowapenda
Kipindi hiki cha karantini, watu wengi hawatokina kwenda shemu za mabali na makazi yao hivyo hupata muda mwingi wa kuzungumza na watu wanaowapenda hasa watu wa familia yao kama wazazi, kaka na dada, wenzi wetu, watoto wetu, ndugu, jamaa na marafiki. Kabla ya katazo la kutembea nje au mbali na makazi yetru, watu wengi walikosa muda wa kuzungumza na watu tunaowapenda hivyo katika kipindi hiki tunamuda wa kutosha ili kuzungumza na kuyajenga mahusiano yetu.
b)        Kuzungumza kwa kupitia vyombo vya mawasiliano kama simu, Kompyuta (tarakirishi)
Katika kipindi hiki cha zuio la mikusanyiko na kutotoka nje, tunaweza kuendelea kujenga, kuimarisha na kuendeleza mawasiliano na watu wetu wa karibu kwa kutumia simu au tarakirishi kutumiana ujumbe wa maandishi (meseji na barua pepe) au hata ujumbe wa sauti na hivyo kuendeleza maisha yetu na mahusiano na watu wengine.

c)        Kuzungumza kwa njia ya video
Katika kipindi hiki tunaweza kuendelea na mahusiano yetu na ndugu, jamaa na hata marafiki kwa kutumia mawasiliano ya video. Mitandao mbalimbali ya kijamii kama Instagram, Skype, Viber, FaceBook, WhatsApp, WeChat, SnapChat, Telegram,MySpace, Tumblr, Twitter, Qzone, zoom  na mingine mingi hutoa huduma ya mawasiliano kwa njia ya video maarufu kama Video Chat au Video Conference.

Njia hizi na nyingine nyingi zinaweza kutumika katika kuimarisha mahusiano na watu tunaowapenda na hata kuanzisha mahusiano mapya na watu wengine ili kubadirishana uzoefu katika shughuli mbalimbali na nyanja mbalimbali za maisha.
Sura ya Nne

ELIMU NA MAARIFA
 Karantini ni kipindi ambacho watu wanapata muda ,mwingi kufanya shughuli zaqo nyingi ambazo walikosa kuzifanya kwa usahihi au hawakuweza kuzifanya kabisa kutokana na kutingwa na majukumu mengine. Hivyo katika kipindi hiki, matumizi mazuri ya muda yanaweza kuwa na manufaa makubwa ikiwa tutaishi kwa malengo yakinifu.
 Katika kipindi hiki ambacho shule, vyuo na maktaba mbalimbali zimefungwa ni kipindi ambacho tunaweza kujifunza maarifa tuliyokuwa tunatamani kuyapat kutokana na kuweli kwamba tuna muda mwingi sana wa kuyafanya hayo. Hiki ni kipindi ambacho tunatakiwa kusoma baadhi ya vitabu tunavyovitamani kuvisoma, kurudia vitu ambavyo hatukuvielewa vizuri tukiwa darasani na tukajifunza zaidi kwa kutulia ili kuvielewa.
Karantini inakupa nafasi kubwa zaidi ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo huweza kuwa msaada kwa maisha yako binafsi na hata kwa jamii inayokuzunguka. Kusoma vitabu, kutazama tamthilia, kujifunza maarifa kama kuchora, kupamba, kuandika, kutengeneza programu tumizi, kuandika vitabu au  makala, kuandaa na kufundisha kozi fulani kwa njia ya mitandao, Kuchonga vitu na vingine vingi tunaweza kujifunza namna ya kuvifanya katika kipindi hiki muhimu. Zifuatazo ni njia za kupata na kutoa elimu aua maaraifa fulani:

a)       Kusoma vitabu, tafiti na makala mbalimbali
Karibu ya asilimia 99.99% ya kila kitu hapa duniani kimeandikwa katika vitabu na makala mbalimbali kwa kutumia tafiti au uelewa wa watu fulani juu ya jambo au kitu fulani. Hivyo ili kujifunza zaidi katika kitu fulani tunachokitamani ni muhimu kusoma vitabu, makala na tafito mbalimbali ili kupata ujuzi stahiki juu ya vitu hivyo.

b)       Kuwauliza watu wenye ujuzi wa kitu fulani
Kipindi hiki cha zuio la makusanyiko na kutembea bila sababu za msingi, kinaweza kutumiwa kujifunza ikiwa tutawauliza watu fulani wenye ujuzi juu ya mambo fulanai tunayotaka kuyajua. Tunaweza kuwauliza kwa kutumia barua pepe, mitandao ya kijamii, vikao vya video, ujumbe mfupi au hata kwa kuwapigia simu na njia ya ujumbe wa sauti.

c)        Kutazama video katika mitandao ya kijamii kama Instagram, FaceBook na YouTube.
 Watu wengi hutoa elimu na wengine hujifunza kwa kutazama video mbalimbali na kupata maarifa wayatakayo kwa kutumia njia hii ya mitandao ya kijamii. Waandaaji wa video hizi hufanya hivyo ili kutoa elimu kwa jamii na hivyo ukihitaji elimu hii unapaswa kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili ujifunze mambo mengi mbalimbali.

Njia hizi na nyinginezo nyingi zinawezaa kutumika na hivyo baada ya kipindi cha karantini uinaweza kuwa mtu mwenye mafanikio zaidi kuliko ulivyo leo.

Ninakutakia mapumziko mema na hakikisha unachukua hatua stahiki ili kujilinda na COVID19. Kumbuka; COVID19 inazuilika, jilinde na walinde watu wote wa karibu yako.
Ahsante.
David Duncan Kipeta
Instagram:davidduncankipeta
FaceBook: David Kipeta
+255 659711891(WhatsApp)
+255 753 736983