Liposuction ni nini?
Hii ni aina ya upasuaji ambayo inatumika kuondoa Mafuta mwilini kwa watu wanene, mara nyingi hutumika kuondoa Mafuta tumbo, mapaja, shingo, kidevu, mgongo na mikono.
Mafuta huondolewa kwa Bomba Fulani maalumu ambalo huwekwa chini ya ngozi kisha presha kubwa sana hutumika kuvuta Mafuta hayo.
Nchini marekani hii ni moja ya upasuaji ambao unafanyika sana Sababu ya watu wengi huko kua wanene na data zinaonyesha kwamba zaidi ya watu laki tatu kila mwaka hufanyiwa upasuaji huo.
Je upasuaji huu unafaa watu wa aina gani?
Huu upasuaji sio wa kupunguza Uzito kwa watu wanene ila ni kwa ajili ya kuondoa Mafuta ya ziada sehemu mbali mbali za mwili hasa baada ya kushindikana kutoka kwa mazoezi na diet ya kupunguza Uzito.
Lakini pia mtu anaweza kua ni mwembamba lakini ana sehemu ya mwili ambayo ina mafuta mengi na ameshindwa kuyatoa kwa mazoezi na chakula.
Mafuta yanavutwa vipi?
kuna aina mbali mbali za kufanya upasuaji huu lakini mara nyingi upasuaji maarufu kitaalamu kama tumescent liposuction hufanyika kwa kumpa mgonjwa Dawa ya usingizi au Dawa ya ganzi kisha sehemu ambayo inatakiwa itolewe Mafuta inawekewa Maji maalumu(normal saline) na Dawa ya kukunja Mishipa ya damu(adrenaline) kisha Mafuta huvutwa nje.
Baada ya upasuaji sehemu zilizotolewa Mafuta huota huvimba kwa muda(inflammation) hivyo matokeo ya upasuaji yataonekana baada ya wiki nne uvimbe ukishapungua.
Nini kifanyike baada ya upasuaji?
Mgonjwa anatakiwa ajaribu kula vizuri baada ya upasuaji ili kuzuia kunenepa tena Kwani upasuaji huu hauzuii mtu kunenepa tena.
Watu wenye ngozi inayovutika hufaidi upasuaji huu kwani ngozi hujivuta kawaida lakini watu ambao hawana ngozi ya kuvutika huishia kua na ngozi kubwa iliyolala ambayo baadae itahitaji upasuaji mwingine.
Nini madhara ya upasuaji huu?
Kama ilivyo kwa upasuaji wa aina yeyoye, upasuaji huu pia una madhara kama kuvimba mwili kwa muda Mrefu, kuganda kwa damu, shepu kutoka vibaya, ganzi, au kifo kutokana na madhara ya dawa za usingizi.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183

0 maoni:
Chapisha Maoni