data:post.body UFAHAMU UPASUAJI WA KUKATA UTUMBO KUPUNGUA UZITO.(GASTRIC BYPASS SURGERY) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UPASUAJI WA KUKATA UTUMBO KUPUNGUA UZITO.(GASTRIC BYPASS SURGERY)

Msanii mmoja wa maigizo kwa jina la Wema Sepetu inasemekana alifanya upasuaji wa kuondoa utumbo lakini yeye mwenyewe hajakubali wala hakuna ushahidi wa hilo.
Hivyo watu wengi wamekua wakijiuliza maswali mengi kwamba upasuaji huo unafanyika vipi, wapi na gharama za upasuaji huo zikoje.

Gastric by pass surgery ni nini?
Huu ni upasuaji wa ambao unabadilisha jinsi tumbo lako unavyopokea chakula na kukitumia, baada ya upasuaji tumbo lako litakua dogo na ukila chakula kidogo tu limejaa.
Baada ya upasuaji huu tumbo lako litakua linapokea chakula kidogo sana na baadhi ya sehemu za utumbo wako zitakua hazifikiwi na chakula hivyo ni chakula kidogo sana kitakua kinachukuliwa na mwili, hii itamfanya mtu apungue uzito mwingi sana.

upasuaji huu hufanyika kwa watu wa aina gani?
upasuaji huu hufanyika kwa watu ambao ni wanene sana na wameshindwa kujipunguza kwa njia za asili yaani mazoezi na diet.

upasuaji huu unafanyika vipi?
Hatua ya kwanza daktari atagawanya tumbo lako katika sehemu kuu mbili, sehemu ya chini kubwa na sehemu ya juu ndogo kisha atabakiza sehehemu ndogo ya juu. kawaida tumbo la binadamu lina uwezo wa kuchukua lita moja na nusu ya chakula lakini kwa sasa utakua na uwezo wa kuchukua kama theluthi tu ya lita moja.
Hatua ya pili daktari ataukata utumbo mdogo wa juu kitaalamu kama duedonum kisha atachukua utumbo wa katikati kwa jina juejonum na kuunganisha na tumbo lako dogo jipya hivyo utakua ukila chakula kinaingia kwenye tumbo dogo na kupitiliza moja kwa moja kwenye utumbo wa katikati.

upasuaji huu unafanyika wapi?
sina uhakika sana kama upasuaji huu unafanyika hapa nchini lakini nina uhakika madaktari wetu wanaweza kufanya kazi hii, gharama kwa nchi kama marekani ni shilingi milion 30 lakini kwa hapa kwetu inaweza kua chini ya hapo.

mwisho; kama ilivyo kwa aina zingine za upasuaji, uparesheni hii inaweza kua na madhara kama kuvuja damu nyingi, kupata henia, kupata makovu tumboni, kuziba kwa utumbo hata kifo japokua utafiti unaonyesha madhara yake wanapata watu chini ya 1% na vifo vikiwa 0.5%.

                                                                                STAY ALIVE

                                                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                              0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni