data:post.body Desemba 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

KUOSHA SEHEMU ZA SIRI BAADA YA TENDO LA NDOA HUONGEZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.(TAFITI)

Kwa miaka mingi imekua ikifahamika kwamba kuosha sehemu za siri baada ya tendo la ndoa kuna zuia magonjwa ya zinaa kama kaswende, pangusa na mengine ambayo huambukizwa kwa tendo la ndoa, hii imekua ni kweli kwasababu magonjwa ya aina hiyo huhitaji muda wa kutosha kuweza kuanzisha makoloni yao sehemu za siri ili kuleta ugonjwa.
hivyo maji maji yenye ugonjwa huo yakishaoshwa yanasimamisha mfumo mzima wa kuanzisha ugonjwa husika.


Lakini hii imeonekana ni tofauti linapokuja swala la virusi vya  ukimwi kwani kuosha sehemu za siri hasa kwa wanawake na wanaume ambao hawajatahiriwa kumeonekana kuongeza maambukizi badala ya kupunguza.
Utafiti huu ulifanyika nchini Uganda ulichukua wanaume ambao hawajatahiriwa ambao wanatabia hiyo kisha kuchukua wanaume ambao hawana tabia hiyo na kuwafuatilia kwa muda Fulani( cohort studies) na majibu yakionyesha kuongezeka kwa maambukizi kwa 2.3% kwa wale wenye tabia ya kuosha uume wao muda mfupi tu baada ya tendo la ndoa.
Lakini utafiti mwingine ulifanyika nchini kenya kwa muda wa miaka kumi kwa wanawake 1270 na majibu yalionyesha kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 2.6% kwa wale walio osha sehemu zao za siri pale pale ukilinganisha na wale waliochelewa na kuosha baada ya dakika kumi mpaka 20.

je chanzo cha maambukizi haya ni nini?
Hakuna majibu ya uhakika wa swali hili lakini wataalamu wamekuja na ababu ambazo huenda ndio zinachangia kutokea kwa jambo hili kama ifuatavyo.
kuongeza ukali wa virusi; sehemu za siri za mwanamke zina maji maji ambayo yana tindikali ambayo kazi yake ni kuua wadudu ambao wanaingia ndani ya uke, sasa ukimwaga maji pale ile tidikali inaishiwa nguvu na kuwapa virusi wale nguvu.
kuongeza michubuko; baadhi ya watu huosha na sabuni au dawa mbalimbali,yale maumivu kidogo unayosikai baada ya kumwaga maji au kupaka sabuni ni kuongezeka kwa michubuko ambayo inatoa nafasi zaidi kwa virusi vya ukimwi kufanya mashambulizi.
kuvipa virusi uwezo wa kuishi na kusafiri; kwa kawaida virusi huishiwa nguvu au kufa pale maji maji yanayovizunguka yanapokauka, kuosha na maji na kuongeza maji maji na kuvihamisha sehemu zingine za sehemu za siri ambazo huenda zina michubuko Zaidi.
mwisho;Kwa lugha nyingine sio vizuri kuosha sehemu za siri muda mfupi tu baada ya tendo la ndoa, jipe muda wa kutosha kitandani na mtu wako kama dakika 10 au 20 ukiwa umepumzika au unafanya mambo mengine kisha unaweza kwenda kunawa.


                                                                        STAY ALIVE

                                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                 0653095635/0769846183

UFAHAMU UPASUAJI WA KUKATA UTUMBO KUPUNGUA UZITO.(GASTRIC BYPASS SURGERY)

Msanii mmoja wa maigizo kwa jina la Wema Sepetu inasemekana alifanya upasuaji wa kuondoa utumbo lakini yeye mwenyewe hajakubali wala hakuna ushahidi wa hilo.
Hivyo watu wengi wamekua wakijiuliza maswali mengi kwamba upasuaji huo unafanyika vipi, wapi na gharama za upasuaji huo zikoje.

Gastric by pass surgery ni nini?
Huu ni upasuaji wa ambao unabadilisha jinsi tumbo lako unavyopokea chakula na kukitumia, baada ya upasuaji tumbo lako litakua dogo na ukila chakula kidogo tu limejaa.
Baada ya upasuaji huu tumbo lako litakua linapokea chakula kidogo sana na baadhi ya sehemu za utumbo wako zitakua hazifikiwi na chakula hivyo ni chakula kidogo sana kitakua kinachukuliwa na mwili, hii itamfanya mtu apungue uzito mwingi sana.

upasuaji huu hufanyika kwa watu wa aina gani?
upasuaji huu hufanyika kwa watu ambao ni wanene sana na wameshindwa kujipunguza kwa njia za asili yaani mazoezi na diet.

upasuaji huu unafanyika vipi?
Hatua ya kwanza daktari atagawanya tumbo lako katika sehemu kuu mbili, sehemu ya chini kubwa na sehemu ya juu ndogo kisha atabakiza sehehemu ndogo ya juu. kawaida tumbo la binadamu lina uwezo wa kuchukua lita moja na nusu ya chakula lakini kwa sasa utakua na uwezo wa kuchukua kama theluthi tu ya lita moja.
Hatua ya pili daktari ataukata utumbo mdogo wa juu kitaalamu kama duedonum kisha atachukua utumbo wa katikati kwa jina juejonum na kuunganisha na tumbo lako dogo jipya hivyo utakua ukila chakula kinaingia kwenye tumbo dogo na kupitiliza moja kwa moja kwenye utumbo wa katikati.

upasuaji huu unafanyika wapi?
sina uhakika sana kama upasuaji huu unafanyika hapa nchini lakini nina uhakika madaktari wetu wanaweza kufanya kazi hii, gharama kwa nchi kama marekani ni shilingi milion 30 lakini kwa hapa kwetu inaweza kua chini ya hapo.

mwisho; kama ilivyo kwa aina zingine za upasuaji, uparesheni hii inaweza kua na madhara kama kuvuja damu nyingi, kupata henia, kupata makovu tumboni, kuziba kwa utumbo hata kifo japokua utafiti unaonyesha madhara yake wanapata watu chini ya 1% na vifo vikiwa 0.5%.

                                                                                STAY ALIVE

                                                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                              0653095635/0769846183

UFAHAMU UPASUAJI WA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI,(liposuction)

Liposuction ni nini?
Hii ni aina ya upasuaji ambayo inatumika kuondoa Mafuta mwilini kwa watu wanene,  mara nyingi hutumika kuondoa Mafuta tumbo, mapaja, shingo, kidevu, mgongo na mikono.
Mafuta huondolewa kwa Bomba Fulani maalumu ambalo huwekwa chini ya ngozi kisha presha kubwa sana hutumika kuvuta Mafuta hayo.
Nchini marekani hii ni moja ya upasuaji ambao unafanyika sana Sababu ya watu wengi huko kua wanene na data zinaonyesha kwamba zaidi ya watu laki tatu kila mwaka hufanyiwa upasuaji huo.
                                                                         
Je upasuaji huu unafaa watu wa aina gani?
Huu upasuaji sio wa kupunguza Uzito kwa watu wanene ila ni kwa ajili ya kuondoa Mafuta ya ziada sehemu mbali mbali za mwili hasa baada ya kushindikana kutoka kwa mazoezi na diet ya kupunguza Uzito.
Lakini pia mtu anaweza kua ni mwembamba lakini ana sehemu ya mwili ambayo ina mafuta mengi na ameshindwa kuyatoa kwa mazoezi na chakula.

Mafuta yanavutwa vipi?
kuna  aina mbali mbali za kufanya upasuaji huu lakini mara nyingi upasuaji maarufu kitaalamu kama tumescent liposuction hufanyika kwa kumpa mgonjwa Dawa ya usingizi au Dawa ya ganzi kisha sehemu ambayo inatakiwa itolewe Mafuta inawekewa Maji maalumu(normal saline) na Dawa ya kukunja Mishipa ya damu(adrenaline) kisha Mafuta huvutwa nje.
Baada ya upasuaji sehemu zilizotolewa Mafuta huota huvimba kwa muda(inflammation) hivyo matokeo ya upasuaji yataonekana baada ya wiki nne uvimbe ukishapungua.
                                       
Nini kifanyike baada ya upasuaji?
Mgonjwa anatakiwa ajaribu kula vizuri baada ya upasuaji ili kuzuia kunenepa tena Kwani upasuaji huu hauzuii mtu kunenepa tena.
Watu wenye ngozi inayovutika hufaidi upasuaji huu kwani ngozi hujivuta kawaida lakini watu ambao hawana ngozi ya kuvutika huishia kua na ngozi kubwa iliyolala ambayo baadae itahitaji upasuaji mwingine.

Nini madhara ya upasuaji huu?
Kama ilivyo kwa upasuaji wa aina yeyoye, upasuaji huu pia una madhara kama kuvimba mwili kwa muda Mrefu, kuganda kwa damu, shepu kutoka vibaya, ganzi, au kifo kutokana na madhara ya dawa za usingizi.
                                                                            STAY ALIVE

                                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                          0653095635/0769846183
                                                           
                       

UFAHAMU UTAPELI WA DAWA ZA KUHARISHA ILI KUPUNGUA UZITO.

Kumekua na ongezeko kubwa la watu wanene na vitambi ambao wanahitaji sana kupungua uzito, lakini tatizo kubwa liko palepale kwamba watu wanataka kupungua haraka kuliko kawaida.
Yaani unene uliopatikana kwa miaka miwili mpaka kumi mtu anataka kuupunguza kwa siku moja au wiki kitu ambacho sio cha kawaida na huweza kua hatari kiafya.
Kuna dawa maarufu sana ambazo zinauzwa sana mtaani huku zikidai kwamba zinaweza kupunguza uzito kwa muda mfupi tu.
Inasemekana baada ya kunywa dawa hizo mteja huharisha mafuta yote na baadae anakua mwembamba.

Dawa hizo ni hazina ukweli wowote na mtu anayetumia anakua haelewi kabisa jinsi mwili unavyofanya kazi na anahatarisha maisha yake kama ifuatavyo.
mtu hapungui unene ila anakonda na kusinyaa; siku zote ukiharisha unakua unatoa maji mwilini, kihesabu lita moja ya maji ni sawa na kilo moja ya uzito hivyo ukiharisha lita tano ni sawa umepungua kilo tano,na kwasababu sehemu kubwa ya mwili wa binadamu ni maji basi utasinyaa na kua mdogo.
Kwa matokeo ya haraka mtu ataona uzito umepungua lakini ni maji ndio yamepungua mwilini sio Mafuta na baada ya hapo uzito utarudi kwani utaanza kunywa maji na kurudisha yaliyopotea.
unahatarisha maisha; kuharisha sio hali ya kawaida mwilini ndio maana watu wakiugua kipindupindu hua wanakufa, kuharisha kunapoteza kiasi kikubwa cha madini ya potassium ambayo inasaidia sana misuli ya mwili na moyo.
Hali hii humfanya mgonjwa kuishiwa nguvu sana, mapigo ya moyo kutokwenda kawaida na hata kusimama kabisa kwa mapigo ya moyo na kifo.
mafuta yako hayako kwenye utumbo; hata kama kweli ingekua ukiharisha mafuta yanatoka, mafuta ambayo yanakufanya uonekane mnene yasingetoka kwani yapo chini ya ngozi yako na sio ndani ya utumbo.
Huwezi kutoa mafuta ya usoni, mgongoni na kifuani, mapajani, kifuani na tumboni kwa kuharisha tu.
mwisho; njia bora kabisa ya kupungua uzito ni kupunguza ulaji wa chakula hasa wanga na sukari, mazoezi na kupungua taratibu angalau kilo mbili kwa mwezi lakini mwisho wa siku hata ukishapungua lazima mfumo wako wa maisha ubadilike kwani mfumo wako wa maisha ya zamani ndio umekufikihsa hapa ulipo leo.
                                                                         STAY ALIVE

                                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                    O653095635/0769846183