data:post.body Novemba 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

UZAZI WA MPANGO WA KUCHOMA SINDANO KWENYE UUME KUANZA KUTUMIKA.

Kwa miaka mingi njia za uzazi wa mpango zimekua zikitumika kwa wanawake tu, isipokua njia moja ya upasuaji kitaalamu kama vasectomy ndio ilikua ikutumika kwa wanaume na kwasababu njia hiyo ukiitumia huwezi kuzalisha tena basi wanaume wengi walikua wanaikwepa.
                                                                             
Njia hii mpya ya uzazi wa mpango itahusika kuchoma sindano kwenye uume imefanikiwa kwenye majaribio kwenye shirika la utafiti huko nchini india.
Akiongea na gazeti la Hindustan nchini india, Mwenyekiti wa shirika hilo la utafiti Dr.Sharma amesema kwamba dawa hiyo iko tayari inasubiri kibali cha serikali.
Utafiti huo ambao ulitumia awamu tatu, uliwahusisha watu 303 na matokeo yalionyesha kwamba dawa ilikua na uwezo wa 97.3% na ilikua na uwezo wa kudumu na kufanya kazi mpaka miaka 13.
Kitaalamu dawa hii itachomwa kwemye mirija inayotoka kwenye korodani kwenda kwenye uuume kitaalamu kama vas difference.

Wakati huohuo huko nchi marekani dawa ya uzazi wa mpango kwa wanaume kwa ajili ya kumeza imeshagunduliwa na kufanyiwa majaribio.
Watafiti wanaamini kwamba itakua tayari baada ya miaka kumi.

                                                          STAY ALIVE
                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                               0769846183/0653095635

WAGONJWA WA UKIMWI KUANZA KUCHOMWA SINDANO MOJA KILA MWEZI BADALA YA VIDONGE.

Moja ya changamoto kubwa ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi ni kushindwa kumeza vidonge  vya ARV kila siku na wakati uleule  kwa maisha yako yote.
Watu wengi huchoka kumeza kutokana na madhara mbalimbali ya dawa, kumeza kwa kujificha na kushindwa hata kuhifadhi dawa hizo nyumbani sababu ya unyanyapaa mkubwa.
Hali hii hufanya wagonjwa wengi kutoanza dawa au kuacha kabisa dawa na kusubiri kufa tu baada ya kukata tamaa.

Lakini kwa sasa tumaini jipya liko njiani baada ya watafiti kugundua dawa za ARV ambazo zitatolewa kwa mfumo wa sindano badala ya vidonge.
Utafiti huo uliwasilishwa katika mkutano mkuu wa virusi vya ukimwi uliofanyika jijini paris ulionyesha kwamba dawa hizo za kuchomwa zilikua zina uwezo sawa na zile za kumeza.
Utafiti huu ulifanyika  kwa watu 1000 katika nchi 16 dunaini ambapo dawa za ARV kwa jina la  cabotegravir rilpivirine zilionyesha uwezo wake mzuri wa kufanya kazi.

Sindano hizi zitaweza kutumika kama pre exposure yaani unaweza kuchoma kama hujaathirika na kukaa mwezi mmoja bila kua na hatari ya kuambukizwa au post exposure ambayo unaweza kuchomwa baada ya kulala na muathirika au kujichoma sindano ambayo inahisiwa kua na damua ya muathirika.
Utafiti huu unaamini kupunguza sana maambukiziya ukimwi kwani kuriuka dozi moja tu ya kumeza inahatarisha sana maambukizi kwa mwenza wa mgonjwa lakini pia inawapa uhuru sana kwamba badala ya kua na siku 365 za kumeza dawa kwa mwaka sasa watakua na siku 12 tu kwa mwaka yaani sindano moja kila mwezi.
Mfumo huu wa kumeza vidonge pia ulileta changamoto hat kwa watoto wadogo ambao wengi wanashindwa kueza dawa hizo kutokana na uchungu au ladha mbaya na kushindwa kufuata ratiba zake vizuri.

                                                           STAY ALIVE
                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            0653095635/0769846183

VIRUSI VIPYA VYA UKIMWI VYAGUNDULIWA.

Moja ya changamoto kubwa wakati wa kutafuta dawa ya ukimwi ni kubadilika badilika kwa kirusi hicho kwenye mifumo na maumbo mbalimbali.
Wanasayansi nchini marekani wamegundua kirusi kipya cha ukimwi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.
Kirusi hicho ni sehemu ya familia ya kile kirusi cha zamani ambacho kimeathiri na kuua wengi duniani kote kwa ujumla kitaalamu kwa jina la HIV-1 Group M.
M ikisimama kwa maana ya major kwani imeathiri watu wengi sana duniani kote kwa ujumla.

Sampuli za damu ambazo zimekutwa na virusi hivi vya ukimwi zilichukuliwa nchini congo kati ya mwaka 1980 mpaka 2001.
“Bahati nzuri utafiti huu unaonyesha kwamba dawa zilizopo zina uwezo wa kutumika kutibu kirusi hiki lakini hakuna uhakika kama vipimo vinavyotumika kwa sasa vina uwezo wa kuwatambua wagonjwa wenye virusi hivi’.Anasema Dr.Antony Fauci kiongozi kitengo cha magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani.

‘Ugunduzi wa kirusi hiki unatukumbusha kwamba kumaliza ugonjwa wa ukimwi bado tunahitaji teknolojia ya hali ya juu kuvielewa virusi hivi’, anasema Dr Marry Rodgers.
Kitengo cha kupambana na kuzuia na magonjwa maarufu kama CDC nchini marekani kinaamini kwamba kuna zaidi ya wagonjwa milioni 40 walioathirika na ugonjwa huu duniani kote huku zaidi ya wagonjwa milioni moja wakiishi marekani na 14% duniani kote hawajua kama ni waathirika.

                                                                             STAY ALIVE

                                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                0653095635/0769846183

HUYU NDIO MGONJWA WA UKIMWI MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI.

Ugojwa wa ukimwi ulipogunduliwa mara ya kwanza miaka ya 1980 uliua watu wengi kwa kasi ya kutisha na wengi waliogunduliwa na ugonjwa huu walisubiri kufa tu kwani palikua hakuna tumaini lolote.
Miaka kadhaa baadae baada ya kugundulika dawa za kupunguza makali, tafiti zilionyesha kwamba mgonjwa asingeweza kuzidi miaka 20 baada ya kuambukizwa.
Kama hatakufa kwa matatizo ya ugonjwa wenyewe basi atakufa kwa madhara ya dawa hizi kama kuharibika kwa maini,figo na kadhalika.

Siku za karibuni mambo yamebadilika kidogo ambapo tafiti zinaonyesha kwamba tofauti ya mtu mwenye virusi na asiyekua navyo ni miaka 13 tu kwa maana nyingine ni kwamba kama mtu ambaye hana virusi anaishi miaka 73 basi mwenye virusi anaweza kuishi miaka 60, hesabu hii imeletwa hivi kulingana na kutofautiana kwa urefu wa maisha wa nchi tofauti.

Mtu mmoja kutoka ureno kwa jina la miguel amekua binadamu wa kwanza kufikisha umri mkubwa sana akiwa na virusi vya ukimwi.
Miguel aligunduliwa na virusi hivi miaka 16 iliyopita akiwa na umri wa miaka 84 na kwa wakati huo vipimo vilionyesha kwamba alikua ameugua kwa muda mrefu kabla bila kujua kwani alikua katika hatu ya 3 ya ugonjwa huu.

Wakati anagunduliwa na ugonjwa huu kulitokea mvutano kati ya madaktari kama kweli dawa zingemsaidia kwani umri ulikua umeenda sana lakini baadae madaktari waliamua kumpa dawa aanze.
Miguel anasema ile ilikua kama bahati kwani dawa hazikuwahi kumsumbua na sasa amefikisha miaka 100 akiwa na ugonjwa huu.
Miguel anasema kwamba hajawahi kuacha wala kuruka maumizi ya dawa tangu alipogunduliwa na ugonjwa huu.

Kwasababu ya unyayapaa ambao bado unaendelea dhidi ya wagonjwa wa ukimwi, Miguel hakupenda sura yake iwekwe hadharani lakini pia jina lake halikutajwa lote.
Historia hii inatoa mwanga kwa jamii yetu ya wagonjwa na ambao sio wagonjwa wa ukimwi kwamba kuna matumaini makubwa ya kuishi miaka mingi na kumeza dawa kwa wakati ni njia bora ya kufika huko.

                                                                             STAY ALIVE

                                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                 0653095635/0769846183

HIVI NDIO UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI UNAVYOWEZA KUUA MTU.

Kwa wagonjwa wa kisukari, tatizo la kushuka sana kwa sukari ni hatari zaidi kuliko tatizo la kupanda kwa sukari.
Kwa hali ya kawaida sukari ikishuka huweza kuua ghafla lakini sukari ya kupanda haiwezi kumuua mtu ghafla, hali hii iko zaidi kwa watoto wadogo na wagonjwa wa kisukari.
Sababu mbalimbali huweza kuchangia kushuka kwa sukari ghafla ikiwemo kuchoma dawa nyingi ya kushusha sukari, kuchelewa kula, kufanya mazoezi sana,kunywa pombe na saratani za kongosho.
Wakati sukari inashuka kuna dalili za mwanzo na dalili za mwishoni, kua makini sana na dalili za mwanzoni kwani kipindi hicho ndio unakua una uwezo wa kujiokoa lakini baada ya hapo unakua huwezi tena kujiokoa bila msaada kutoka kwa watu wengine.

dalili za mwanzo za sukari kushuka.

 • kizunguzungu
 • kutokwa jasho
 • njaa kali
 • wasiwasi
 • kichwa kuuma
 • kuloanisha mashuka kwa jasho wakati wa usiku
 • kuota ndoto za ajabu
dalili za mwisho baada ya sukari kushuka sana
 • degedege
 • misuli kuishiwa nguvu
 • kushindwa kuongea
 • kuchanganyikiwa
 • kupoteza fahamu
 • kuona ukungu.
vipimo
kwenye kipimo cha sukari au glucometer, pale inapokua chini ya 3.0mmol/l basi ni dalili kwamba sukari imeshuka sana na inaelekea kubaya.
matibabu
mgonjwa katika dalili za mwanzo anaweza kunywa glucose, juice au soda na kupata nafuu kisha kutafuta chakula na kukila, lakini mgonjwa wa dalili za mwisho anatakiwa akimbizwe hospitali kuwekewa sukari kwa njia ya mishipa au dripu.
ni vizuri mgonjwa wa kisukari kuwaambia ndugu zake kuhusu dalili hizi ili waweze kumsaidia ikitokea hajiwezi kabisa.

jinsi ya kuzuia hali hii.
usichelewe kula; baada ya kuchoma dawa ya kushusha sukari au insulin basi hakikisha umekula kwa wakati ili kuzuia kuporomoka sana kwa kiwango cha sukari.
pima kiwango cha sukari; kupima mara kwa mara ni njia pekee ya kujua kiwango chako cha sukari kikoje, sio kwa ajili ya kuogopa sukari inayoshuka tu ila hata ile ya kupanda ni hatari kwa afya yako kama ikiwa imepanda muda wote.
kunywa pombe na chakula; sukari hushuka sana mgonjwa anapokunywa pombe bila chakula hivyo hakikisha umekula kwanza kabla ya kunywa pombe.
mazoezi yako yaendane na dawa unayotumia; ukifanya mazoezi sana hakikisha unapunguza dozi ya dawa unayotumia kwani mazoezi hupunguza sana sukari mwilini.

                                                                              STAY ALIVE
                                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                0653095635/0789846183