data:post.body JINSI YA KUJIOKOA KUTOKA KWENYE GARI AMBAYO INAZAMA KWENYE MAJI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JINSI YA KUJIOKOA KUTOKA KWENYE GARI AMBAYO INAZAMA KWENYE MAJI.

Siku chache zilizopita mama mmoja na na mtoto wake nchini kenya walizama kwenye maji na kupoteza maisha, inasemekana gari ile ilidondoka kutoka kwenye kivuko.
Kila mwaka zaidi ya ajali 10000 hutokea duniani kote, wengi hufariki na wachache huweza kujiokoa katika majanga kama hayo.
Wataalamu wanaamini kwamba dakika moja ya kwanza ndio inaamua kwamba wewe utakufa au utabaki hai, ukifanya makosa katika muda huu basi uwezekano wa kutoka hai haupo.
Kwenye makala hii ntaenda kuzungumzia mambo muhimu ya kufanya ili uweze kutoaka hai ndani ya gari linalozama kwenye maji kama ifuatavyo;
tulia kabisa bila kupaniki; sio rahisi kutumbukia kwenye maji bila kupaniki lakini jitahidi unavyoweza kujituliza ili kufanya maamuzi sahihi, ukianza kutumia nguvu nyingi ndio utaishiwa hewa na kufa mapema.
watu wengi wana tabia ya kuanza kuwapigia simu ndugu zao wa karibu na mwisho wa siku ndugu hao hawawezi kufika eneo hilo kwa wakati.
vunja kioo cha dirishani; gari ikizama kwenye maji, presha ya nje inakua kubwa sana kuliko presha ya ndnai kiasi kwamba huwezi kufungua mlango, mlango hufunguka baada ya muda fulani maji yakishajaa ndani ya gari hivyo kama muda huo utakua bado uko hai basi utatoka salama.
sasa kuliko kusubiri mlango ufunguke basi ni bora uvunje kioo kwa kutumia kitu chochote kigumu au kiwiko chako cha mkono.
Kioo ni kigumu kidogo hivyo kinahitaji nguvu ya ziada kukipasua kwa kiwiko cha mkono.
toka haraka dirishani: baada ya kupasua kioo maji huingia kwenye gari kwa kasi na gari haunza kuzama haraka, huu ni muda wa kutoka haraka dirishani na kuogelea kwenda juu ili uweze kupata msaada na kuokolewa.
kama una abiria; kama uko na abiria basi msipoteze muda kubushana nini cha kufanya, wape mpango wako kisha vunja kioo, mkianza kubishana nani anajua kuogelea na nani hajui basi mtakufa wote.
kama kuna mtoto basi mshike mkono utoke naye, kwa ambao hawajui kuogelea ni vizuri wakatoka hivyohivyo kwani maji yatawarudisha juu na pia ni rahisi kupata msaada kuliko kushuka na gari mpaka chini ya ziwa au bahari.
mwisho;majanga haya hutokea mara kwa mara, kama sio vibaya kua na boya la kuogelea kwa watu wasiojua kuogelea kwenye gari na kifaa chochote kigumu kama nyundo iwapo ikitokea shida kama  hii uweze kuokoka.

                                                                    STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                             0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni