data:post.body Oktoba 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU DALILI ZA KUPANDA KWA SUKARI KWA WAGONJWA WA KISUKARI.

Kupambana na kiasi cha Sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa kisukari ndio msingi mkuu wa matibabu ya ugonjwa wa kisukari kwani huepusha madhara makubwa yatokanayo na ugonjwa huu kama kuharibika kwa figo, ugonjwa wa presha, upofu. matatizo ya mishipa ya fahamu na kadhalika.
Kwa kawaida sukari ya mgonjwa ikiwa zaidi ya 7.1mmol/l baada ya saa 8 bila kula au zaidi ya 10mmol/l saa 2 baada ya kula hutambulika kitaalamu kama hyperglaicemia au sukari ya juu kwa wagonjwa hawa.

nini chanzo cha kupanda sukari kwa wagonjwa hawa?
wagonjwa wengi wa sukari hupata tatizo la sukari zao kupanda sana hata kama wako kwenye dawa na hii husababishwa na sababu zifuatazo.
kutomeza au kutochoma dawa kwa wakati: wagonjwa ambao hawamezi dawa au kuchoma sindano za sukari kama walivyoelekezwa na wataalamu wa afya huishia kupata tatizo la kupanda sukari juu kuliko kawaida.
kula wanga mwingi sana; kimsingi wagonjwa wa sukari wanatakiwa wale vyakula vya wanga kidogo sana na siku zingine ikiwezekana wasile kabisa.
Vyakula vya wanga kama ugali,wali, viazi, tambi, mihogo, chapati, mikate, maandazi, keki na kadhalika huongeza sukari sana ukilinganisha na vyakula vya protini na mafuta kama nyama, samaki, karanga, korosho, maziwa, mayai, na kadhalika.
kuugua; mgonjwa wa sukari akiuugua ugonjwa wowote yaani kama malaria, typhoid, u.t.i au magonjwa yeyote mengine unayojua wewe lazima sukari ipande hivyo kwa kipindi hiki hata kama anapewa dawa za sukari, kama ugonjwa haujafahamika basi sukari haiwezi kushuka.
msongo wa mawazo; msongo wa mawazo huchangia sana homoni zingine mwilini ambazo husababisha kupanda kwa sukari kwenye damu.
kua mvivu; kama wewe ni mtu wa kufanya shughuli mbalimbali kama kutembea, kwenda kazini, kufanya kazi za nyumbani, kwenda mazoezini na kadhalika kisha ikatokea ukaacha hizo shughuli na kushinda nyumbani basi uko kwenye hatari ya kupandisha sukari mwilini.

dalili za sukari kupanda ni zipi?
 • kusikia kiu sana
 • kichwa kuuma
 • kushindwa kutuliza akili sehemu moja.
 • kuona ukungu
 • kukojoa mara kwa mara 
 • kuishiwa nguvu
 • sukari kupanda zaidi ya 10mmo/l kwenye kipimo cha damu.
hali hii ikiendelea kwa muda mrefu husababisha
 • magonjwa ya ngozi ya mara kwa mara
 • kuchelewa kupona kwa vidonda
 • ganzi
 • choo ngumu sana au kuharisha.

matibabu ya hali yapi?
matibabu ya sukari kupanda yanategemea sana chanzo cha ugonjwa husika cha kupanda kwa sukari hiyo na huweza kufanyika nyumbani au hospitali kama ifuatavyo.
kunywa maji mengi; maji mengi husaidia sana kupunguza sukari mwilini kwa kuondoa sukari kupitia mkojo lakini pia huzuia kupungua kwa maji mwilini.
fanya mazoezi; mazoezi husaidia sana kupunguza sukari, lakini ikiwa sukari imepanda usifanye mazoezi kwanza bila kuhakikisha kwamba umepima mkojo, ni hatari sana kufanya mazoezi iwapo mkojo wako una vitu vinaitwa ketones.
badili mfumo wa chakula; epuka vyakula vya wanga na sukari na tumia muda mwingi kula vyakula vya ptotini na matunda ambayo hayana sukari.
badilisha dawa; wakati mwingine dawa hazikufai au dozi ni kidogo hivyo onana na daktari wako anaweza kukubadilishia mfumo wa kumeza au akaongeza dozi.
chukua vipimo; wakati mwingine ni ugonjwa mpya unakusumbua hivyo ni vizuri kwenda hospitali kupima magonjwa mbalimbali.

                                                               STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

FAHAMU KUHUSU MAJI YANAYOMWAGIKA KUTOKA KWA MWANAMKE AKIFIKA KILELENI.(squrting)

Squrting ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke kumwaga maji kutoka sehemu za siri wakati anafika kileleni, hii huambatana na msisimko mkali wa kuishiwa nguvu, kutetemeka hata kukaa chini.
kuna aina mbili za mwanamke kufika kileleni, moja ni hiyo niliyoandika hapo juu na ya pili ni ile mwanamke anatoa kama utando mweupe ambao unaonekana kusambaa  kwenye uume  wakati tendo hili la ndoa likiendelea, lakini maada hii itazungumzia maji yanayoruka wakati mwanamke anafika kileleni.

jee ni hali ya kawaida?
Hii ni hali ya kawaida kabisa japokua watu wengi hua hawapendi kuizungumzia, kwa miaka mingi watafiti walidhani kwamba huenda wanawake wanaomwaga yale maji wanakua na tatizo la fistula na wengine walidhani maji yale yanatoka ukeni.
Lakini utafiti uliofanyika mwaka 2014 uligundua kwamba hali ile ni ya kawaida na maji yale yanatoka kwenye kibofu cha mkojo.
Utafiti ulifanyika kwa kipimo cha utrasound ambapo mwanamke aliambiwa akakojoe ili kuondoa mkojo wote ndani ya kibofu cha mkojo kisha alianza kujichua huku kipimo cha utrasound kikiangalia hali ya kibovu cha mkojo.
utafiti ulionyesha kwamba, wakati mwanamke anaendelea kujichua maji yalianza kujaa tena kwenye kibovu cha mkojo na alipofika kileleni na kumwaga maji kama kawaida, picha ya utrasound ilionyesha kupotea kwa maji yale, hii ilionyesha kweli maji yale yanatoka kwenye kibofu cha mkojo bila mwanamke kuyatoa mwenyewe kwa hiari.

wanawake wangapi wanafika kileleni kwa staili hii?
Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia kumi mpaka hamsini wanafika kileleni kwa kumwaga maji, lakini wataalamu wanaamini kwamba wapo ambao wanaishia kwenye hatua ya kujaza maji kwenye kibovu lakini yale maji hayatoki.
utafiti uliofanyika kwa wanawake 233 ulibaini kwamba 14% walifika kileleni kwa kumwaga maji kila wakati wakilala na wanawake huku 54% walisema hali kama hiyo ishawahi kuwakuta mara moja au mbili.
Utafiti pia unaonyesha kwamba hali ya mwanamke kumwaga maji vile hutegemea na hisia alizonazo kwa mtu huyo na uwezo wa mwanaume huyo kumkuna vizuri anapotaka yeye.

je kuna tofauti kati ya mkojo na maji yanayotoka wakati wa kufika kileleni?
Ndio, maji yanayotoka wakati wa kufika kileleni hua hayana rangi kabisa pia kuna maji yale yana kiasi kikubwa cha sukari aina ya fructose ambayo husaidia mbegu za kiume kusafiri haraka pale mwanaume anapomwaga mbegu kwenye uke huo.

mwisho; kuna wanawake wengi sana ambao wanahisi kwamba hali ile ya kumwaga maji sio yao lakini huenda hawajakutana na watu sahihi ambao wana uwezo wa kuwafanya hivyo.
badhi ya wanawake hali hii walikutana nayo baadae sana baada ya kuingia kwenye mahusiano mengine.

HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYE UKE WA MWANAMKE KULEGEA NA KUA MKUBWA.

Katika mambo ambayo yamepotoshwa sana kwenye jamii yetu ni kuhusu kulegea na kutanuka kwa uke wa mwanamke.
Jamii yote inaamini kwamba kulegea kwa uke kunasabishwa na mwanamke kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, kulala na wanaume wengi au kulala na mwanaume mwenye uume mkubwa, kitu ambacho hakina ushahidi wowote kitaalamu.
                                                             
 
Ni kweli uke una tabia ya kulegea katika hatua fulani ya maisha ya mwanamke lakini kuna sababu zingine ambazo zinahusika kama ifuatavyo.
umri; kadri umri unavyozidi kwenda misuli yote ya mwili inaanza kuishiwa nguvu na ngozi kuanza kutoa makunyazi.
Katika umri wa miaka 40 mara nyingi kiwango cha homoni za uzazi ambazo zinahusika na shughuli za uke huanza kupungua na uke unaanza kulegea na kupungua kiasi cha maji.
Katika umri wa miaka 50 ambapo mara nyingi hedhi husimama, uke hua mkavu kabisa na kua mdogo mno kiasi kwamba hata tendo la ndoa linaanza kua gumu.

kuzaa watoto; kipindi cha kuzaa mtoto, uke wa mwanamke hutanuka sana ili mtoto aweze kupita vizuri, wanawake wengine huzaa watoto wakubwa kuliko wegingine.
Sasa uharibifu unaosababishwa na mtoto kutoka ni mkubwa, japokua uke hurudi kwenye hali yake ya zamani baada ya kuzaa lakini hautaweza kua kama mwanzo kabisa.

maumbile asili; kuna watu ambao wameumbwa hivyo, kwamba maumbile yao ya kike ni makubwa yaani kama jinsi wanaume wanavyokua na maumbile tofauti.
Ukisikia mwanamke anapenda uume mkubwa basi ujue maumbile yake ndio yanaridhishwa na aina hiyo lakini kuna wanawake wengine ambao uume mkubwa kwao ni mateso na maumivu makali.

mwisho; kuna mazoezi ya kubana uke yanafahamika kama kegel, kama umezaa watoto au umri umeenda na unataka kuendelea kua mbichi basi unaweza kuyafanya na misuli yako ya uke ikawa na nguvu kama mwanzo.
mazoezi haya hufanyika kwa kubana msuli ambao unafanya kazi ya kuzuia na kuachia mkojo mara kwa mara.

                                                                     STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                    0653095635/0769846183
                                                             

YAFAHAMU MATIBABU YA UKOSEFU WA MAZIWA BAADA YA KUJIFUNGUA.

Baada ya kujifungua, baadhi ya akina mama hutoa maziwa kidogo sana kwa ajili ya watoto wao na wengine hukosa kabisa maziwa.
Hali hii huleta changamoto kubwa kwani mtoto huanza kulia sana na wakati mwingine kuishiwa maji mwilini na kuchemka.
Kitaalamu baada ya kujifungua homoni nyingi za uzazi zinapungua kisha homoni zingine kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa kitaalamu kama prolactin hutengenezwa, sasa kuchelewa kwa kwa hatua hii kunaweza kuleta shida hii.
Lakini pia zipo sababu zingine za tatizo hili na unaweza kuzisoma hapa.......http://www.sirizaafyabora.info/2016/09/sababu-kumi-za-kuishiwa-au-kukaukiwa.html

mambo gani unaweza kufanya kutibu tatizo hili?
usiishiwe na maji mwilini: hakikisha unakunywa maji ya kutosha angalau glass nane kwa siku ili kuongeza kiasi cha maji mwilini mwako.
kumbuka maziwa yako kwenye mfumo wa kimiminika hivyo maji mengi yanahitajika kuyatoa.
kula mlo kamili; ungeza ulaji wako wa zamani kwa zaidi kidogo, vyakula vya protini kama mayai, nyama,maziwa nay ng'ombe samaki na mboga za majani husaidia sana sana kuzalisha maziwa ya kutosha ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya mtoto.
tumia virutubisho; taasisi  nyingi za kiafya zinashauri matumizi ya madini ya clacium, vitamin D, Iron, na folic acid kama kiungo muhimu sana katika kumuandaa mama kuzalisha maziwa mengi na yenye virutubisho vya kutosha ndani yake.
nyonyesha mara kwa mara; hata kama maziwa ni kidogo sana jitahidi kumnyonyesha mtoto mara nyingi sana iwezekanavyo yaani mara 10 mpaka 12 ndani ya saa 24 au kila anapohitahi na hii itasaidia sana kutengeneza homoni ya oxytocin ambayo husaidia sana kutengeneza maziwa.
nyonyesha ziwa moja moja; ukimpa mtoto ziwa moja mpaka maziwa yakaaisha kabisa, taarifa hutumwa kwenye ubongo kwamba maziwa yameisha kabisa hivyo ziwa lingine litajazwa maziwa haraka wakati mtoto anamalizia kunyonya ziwa lingine.
matumizi ya dawa; wakati mwingine baadhi ya dawa hutumika hasa pale kiwango cha homoni inayohusika na maziwa inapoenekana iko chini sana na haiwezi kuongeza kiwango cha maziwa.
dawa ya dompiredone huweza kutumika kwa dozi ya 10mg kutwa mara nne na kuongeza mpaka kiwango cha mwisho cha 20mg kutwa mara nne.
Mama anaweza kupunguza dozi na kuacha kabisa kama maziwa yakipatikana, ila ikitokea maziwa yanapungua tena basi ataanza dozi na kuendelea nayo mpaka atakapomuanzishia mtoto vyakula vingine, mara nyingi baada ya miezi sita.
mwisho; wakati mwingine mama anaweza asipate nafuu pamoja nakutumia dawa zote, huenda sababu ya vyanzo vingine ambavyo vinakua nje ya matibabu kama historia ya upasuaji wa matiti na kadhalika hivyo anaweza kutumia maziwa mbadala ya lactogen au maziwa ya ng'ombe ambayo mchanganyiko wake umetajwa hapa.....http://www.sirizaafyabora.info/2015/05/jinsi-ya-kutengeneza-maziwa-ya-mtoto.html

                                                              STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0769846183/0653095635

JINSI YA KUJIOKOA KUTOKA KWENYE GARI AMBAYO INAZAMA KWENYE MAJI.

Siku chache zilizopita mama mmoja na na mtoto wake nchini kenya walizama kwenye maji na kupoteza maisha, inasemekana gari ile ilidondoka kutoka kwenye kivuko.
Kila mwaka zaidi ya ajali 10000 hutokea duniani kote, wengi hufariki na wachache huweza kujiokoa katika majanga kama hayo.
Wataalamu wanaamini kwamba dakika moja ya kwanza ndio inaamua kwamba wewe utakufa au utabaki hai, ukifanya makosa katika muda huu basi uwezekano wa kutoka hai haupo.
Kwenye makala hii ntaenda kuzungumzia mambo muhimu ya kufanya ili uweze kutoaka hai ndani ya gari linalozama kwenye maji kama ifuatavyo;
tulia kabisa bila kupaniki; sio rahisi kutumbukia kwenye maji bila kupaniki lakini jitahidi unavyoweza kujituliza ili kufanya maamuzi sahihi, ukianza kutumia nguvu nyingi ndio utaishiwa hewa na kufa mapema.
watu wengi wana tabia ya kuanza kuwapigia simu ndugu zao wa karibu na mwisho wa siku ndugu hao hawawezi kufika eneo hilo kwa wakati.
vunja kioo cha dirishani; gari ikizama kwenye maji, presha ya nje inakua kubwa sana kuliko presha ya ndnai kiasi kwamba huwezi kufungua mlango, mlango hufunguka baada ya muda fulani maji yakishajaa ndani ya gari hivyo kama muda huo utakua bado uko hai basi utatoka salama.
sasa kuliko kusubiri mlango ufunguke basi ni bora uvunje kioo kwa kutumia kitu chochote kigumu au kiwiko chako cha mkono.
Kioo ni kigumu kidogo hivyo kinahitaji nguvu ya ziada kukipasua kwa kiwiko cha mkono.
toka haraka dirishani: baada ya kupasua kioo maji huingia kwenye gari kwa kasi na gari haunza kuzama haraka, huu ni muda wa kutoka haraka dirishani na kuogelea kwenda juu ili uweze kupata msaada na kuokolewa.
kama una abiria; kama uko na abiria basi msipoteze muda kubushana nini cha kufanya, wape mpango wako kisha vunja kioo, mkianza kubishana nani anajua kuogelea na nani hajui basi mtakufa wote.
kama kuna mtoto basi mshike mkono utoke naye, kwa ambao hawajui kuogelea ni vizuri wakatoka hivyohivyo kwani maji yatawarudisha juu na pia ni rahisi kupata msaada kuliko kushuka na gari mpaka chini ya ziwa au bahari.
mwisho;majanga haya hutokea mara kwa mara, kama sio vibaya kua na boya la kuogelea kwa watu wasiojua kuogelea kwenye gari na kifaa chochote kigumu kama nyundo iwapo ikitokea shida kama  hii uweze kuokoka.

                                                                    STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                             0653095635/0769846183

JINSI YA KUEPUKA MICHUBUKO WAKATI WA TENDO LA NDOA ILI KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.

Sio kila anayefanya ngono na mgonjwa wa ukimwi anapata maambukizi, kuna watu wameishi na wagonjwa wa ukimwi miaka na kuzaa watoto lakini bado hawakupata maambukizi haya ya virusi vya ukimwi.
                               
         
Tafiti zinaonyesha kwamba ukilala na muathirika wa ukimwi basi uwezekano wakupata maambukizi ni asilimia 0.002 mpaka asilimia 1, kwa maana nyingine ni kwamba kati ya watu 100 mpaka 500 wanaolala na waathirika wa ukimwi ni mmoja anayepata maambukizi.
Hatari ya maambukizi huongezeka kwa asilimia 1 mpaka 1.4 kwa watu ambao wanafanya ngono kinyume na maumbile.
Kama ingekua kila anayelala na muathirika wa ukimwi na yeye anapata basi watu wangeisha kwani sisi wote tumeunganishwa kwenye mnyororo mmoja wa ngono bila kujuana.
Pamoja kwamba mnaweza kupima kabla ya kuanza mahusiano kitu ambacho kweli ni muhimu, bado Kuna haja ya kuendelea kua makini kwani watu wengi sio waaminifu na waathirika wengi ni wanandoa  na watu ambao wako kwenye mahusiano sababu yakuaminiana sana.
yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya kuzuia michubuko na kukuepusha maradhi ya mbalimbali ikiwemo ukimwi.
maandalizi mazuri; Hakikisha mwanamke ameloa vya kutosha muda wote wa tendo la ndoa na hii ni matokeo mazuri ya kumuandaa vizuri kabla ya tendo la ndoa na ukiona ukavu umeanza basi sitisha na muandae tena, kamwe usikubali kuendela na tendo la ndoa wakati unasikia uke ni mkavu kabisa au unasikia maumivu.
tumia vilainishi; watu wengi wanaamini vilainishi ni kwa ajili ya kuingiliwa kinyume na maumbile kitu ambacho sio kweli.
kama mwanamke unaona umeshindwa kuloana kwa sababu ambao ziko nje ya uwezo wako basi unaweza kutumia vilainishi hivi kuepuka michubuko.
kama wewe ni kijana ambaye hua unashiriki tendo la ndoa basi sio vibaya kua nayo nyumbani.
epuka ngono ya kukomoa; kama mwanaume achana na mawazo yakumkomesha mwanaume, huwezi kumkomesha mwanamke kwa sex, ile sehemu mtoto anapita, wewe ni nani? fanya mambo yako kaa pembeni.
Ni rahisi sana kumridhisha mwanamke kwa round moja tu au mbili, ukizidi hapo mara nyingi anakua mkavu na kukauka.
ndio maana maambukizi yako juu kwa vijana kuliko wazee ambao hawana muda wala nguvu za kukomesha.
fanya taratibu; usidanganywe na video za ngono, mwanamke anaweza kuridhika sana kwa tendo la ndoa la taratibu kuliko ile ya fujo ambayo umeaminishwa kuiamini.
kufanya ngono taratibu kunaongeza msisimko, maji mengi ukeni na kupunguza uwezekano wa kuchubuka kwani unatumia nguvu kidogo sana kuingia na kutoka.
kua msikivu; kama kuna staili ambayo unaona ukimuweka mwenza wako anasikia maumivu au analalamika basi achana nayo, mwanamke akianza kusikia maumivu anakosa hamu ya tendo na kukauka haraka huku akisubiri umalize tu avae nguo.
hakikisha anafika kileleni; jaribu kua mtundu na kuhakikisha mwenza wako anafika kileleni siku zote, kumfikisha kileleni siku zote kunamfanya mwanamke aloane sana na kupunguza sana uwezekano wa kuchubuka.
bahati nzuri mwanamke anaweza kuingia kileleni hata mara nne au tano wakati mwanaume akifika kileleni mara moja au mbili.
usioshe uke na maji kama bado unaendelea; mwanamke anaweza kuosha uke wake kabla ya tendo la ndoa, sio kitu kibaya kwani maandalizi hayajaanza.
Lakini kwenda kuosha tena baada ya mshindo wa kwanza unapafanya kule kua kugumu na kukavu kwani maji sio laini, hivyo utaleta ukavu ambao haukuepo mwanzoni.
usilazimishe; kama mwanamke amechoka au ana sababu nyingine yeyote ya kutojisikia kufanya ngono basi usitumie nguvu kwani utajikuta umelala na mtu mkavu, mara nyingi watu ambao wanabakwa au kubaka huambukizwa maambukizi ya ukimwi sababu ya kufanya ngono na watu ambao hawakua tayari.
mwisho; tendo la ndoa sio vita, jipe muda wa kutosha kujiandaa kiakili na kimwili kabla ya kushiriki, hii itakuletea raha na kukuzuia na magonjwa mbalimbali ambayo ni hatari sana kwa mwili wako.