data:post.body MAMBO 8 YANAYOWEZA KUHARIBU MUONEKANO MZURI WA MWANAWAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MAMBO 8 YANAYOWEZA KUHARIBU MUONEKANO MZURI WA MWANAWAKE.

Ukiumuona mwanamke baada ya kuvunja ungo basi utagundua kweli mungu aliweka kitu cha ziada au aliweka uzuri wa asili ambao kila mwanamke anao hapa duniani.
Bahati mbaya ni wanawake wachache sana wanaweza kuuendeleza uzuri au muonekano ule hata kwa miaka mitano au kumi tu.
Wengi huingia kwenye mfumo wa maisha ambao unaanza kuharibu kabisa mionekano yao na wakati mwingine kuonekana wana umri mkubwa sana kuliko umri wao halisi.
                                                                       
       
Kimsingi mwanamke akijitunza vizuri ana uwezo wa kuonekana mbichi mpaka miaka 45 au 50 ambapo siku zake za mwezi zinasimama na hapo ndio ana haki ya kuanza kuonekana kwamba ameanza kubadilika sana lakini kabla ya hapo mwanamke anaweza kubaki katika hali hiyo hiyo ya muonekano mzuri kwa miaka mingi tu.
Leo naenda kuzungumzia mambo ambayo yanaweza kumchosha mwanamke na kuonekana mkubwa sana kabla ya umri wake.
kula vibaya; wanawake wengi huharibika kwa kula vyakula ambavyo sio vya kiafya kabisa hasa mikaango na vyakula vya haraka maarufu kama fast food, sukari na wanga mwingi.
vyakula hivi huwanenepesha sana, kuwapa vitambi mpaka wanapoteza kabisa ile shepu asilia ambayo walikua nayo hapo mwanzo.
lakini pia mwanamke anaweza kuchoka kwa kukosa chakula cha kutosha hasa kutokana na ugumu wa maisha.
kutofanya mazoezi; mazoezi yanachangia sana kumfanya mwanamke abaki na misuli iliyokaza na kutokua nyama uzembe kitaalamu kama muscle tone.
unaweza kua unakula vizuri na sio mnene lakini baadhi ya maeneo ya mwili wako yamejikunja kunja kama mzee sababu ya kukosa mazoezi kabisa.

kutumia vipodozi wasivyovifahamu; kuna vipodozi vingi sana sokoni ambavyo huwafanya wanawake wanaonekane warembo ndani ya muda mfupi sana lakini mara nyingi vipodozi vile hua na madhara ya muda mrefu ambayo wakati mwingine hayatoki.
ukikutana na mwanamke ambaye alijichubua miaka kumi iliyopita na baadae akaacha mara nyingi utaona kabisa ngozi yake imeungua na imeshindwa kurudi katika hali yake ya zamani, lakini pia vipodozi vya nywele vingine ni hatari na huunguza ngozi ya nywele.

msongo wa mawazo; katika karne hii ambayo dunia ina mambo mengi sana ambayo yanaleta msongo wa mawazo hasa ukosefu wa ajira na mahusiano mabovu ya kimapenzi basi wanawake wengi hutumia muda mwingi sana kuwaza mwisho wao.
Siku zote mtu akifika kwenye hali hii basi hawezi kula vizuri na kupata mahitaji yake muhimu na matokeo yake huonekana kabisa amechoka na kudhoofu.

kutoshiriki tendo la ndoa; tendo la ndoa kwa wanawake lina faida nyingi za kiurembo kama kufanya ngozi kung'aa sana kwani damu nyingi huenda kwenye ngozi wakati wa tendo la ndoa na kupeleka hewa ya oxgen na virutubisho vingine.
lakini pia wakati wa tendo la ndoa mwanamke anatoa homoni nyingi ikiwemo oxytocin na oestrogen ambazo ndio msingi mkuu unaomfanya mwanamke awe na shepu nzuri na ngozi laini kwanzia kuvunja ungo mpaka mwisho.
mwanamke asiyeshiriki tendo la ndoa hapati faida hizi.
ulevi na uvutaji wa sigara; siku hizi wanawake ni walevi sana kama wanaume, kimsingi pombe hupunguza maji mwilini kitaalamu kama deuresis na kuifanya ngozi kukosa maji na kua mbaya lakini pia sigara huweka kemikali kitaalamu kama nicotine kwenye ngozi.
Kemikali hii hufanya ngozi kua nyeusi na kupoteza muonekano wake wa awali.

magonjwa; ukiachana na magonjwa ya mwili kama saratani, ukimwi,sukari ambayo huchosha mwili kabisa baadhi ya magonjwa kama ugumba na magonjwa ya kizazi huathiri sana saikolojia ya wanawake.
Hali hii huwakondesha, kuwachosha na kuwazeesha kabisa.

kazi ngumu; miili ya wanawake haikuandaliwa kufanya kazi ngumu kama za wanaume, miili ya wanaume iliumbwa kwa ajili ya kazi ngumu hivyo sio kitu cha ajabu ila mwanamke akijikita kwenye kazi ngumu hupoteza kabisa muonekano wake wa awali na anaweza kuanza kuonekana kama mwanaume.                                                              
 Mwisho; wawake wengi hasa wa afrika huamini kwamba swala la muonekano mzuri ni bahati tu, wakisahau kua kwamba wao pia wanachangia kwa asilimia kubwa kua katiaka muonekano huo, mambo mengi ya urembo na muonekano yapo ndani ya uwezo wako ni swala la kuchukua hatua tu.

                                                                        STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni