data:post.body Septemba 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

MAMBO 8 YANAYOWEZA KUHARIBU MUONEKANO MZURI WA MWANAWAKE.

Ukiumuona mwanamke baada ya kuvunja ungo basi utagundua kweli mungu aliweka kitu cha ziada au aliweka uzuri wa asili ambao kila mwanamke anao hapa duniani.
Bahati mbaya ni wanawake wachache sana wanaweza kuuendeleza uzuri au muonekano ule hata kwa miaka mitano au kumi tu.
Wengi huingia kwenye mfumo wa maisha ambao unaanza kuharibu kabisa mionekano yao na wakati mwingine kuonekana wana umri mkubwa sana kuliko umri wao halisi.
                                                                       
       
Kimsingi mwanamke akijitunza vizuri ana uwezo wa kuonekana mbichi mpaka miaka 45 au 50 ambapo siku zake za mwezi zinasimama na hapo ndio ana haki ya kuanza kuonekana kwamba ameanza kubadilika sana lakini kabla ya hapo mwanamke anaweza kubaki katika hali hiyo hiyo ya muonekano mzuri kwa miaka mingi tu.
Leo naenda kuzungumzia mambo ambayo yanaweza kumchosha mwanamke na kuonekana mkubwa sana kabla ya umri wake.
kula vibaya; wanawake wengi huharibika kwa kula vyakula ambavyo sio vya kiafya kabisa hasa mikaango na vyakula vya haraka maarufu kama fast food, sukari na wanga mwingi.
vyakula hivi huwanenepesha sana, kuwapa vitambi mpaka wanapoteza kabisa ile shepu asilia ambayo walikua nayo hapo mwanzo.
lakini pia mwanamke anaweza kuchoka kwa kukosa chakula cha kutosha hasa kutokana na ugumu wa maisha.
kutofanya mazoezi; mazoezi yanachangia sana kumfanya mwanamke abaki na misuli iliyokaza na kutokua nyama uzembe kitaalamu kama muscle tone.
unaweza kua unakula vizuri na sio mnene lakini baadhi ya maeneo ya mwili wako yamejikunja kunja kama mzee sababu ya kukosa mazoezi kabisa.

kutumia vipodozi wasivyovifahamu; kuna vipodozi vingi sana sokoni ambavyo huwafanya wanawake wanaonekane warembo ndani ya muda mfupi sana lakini mara nyingi vipodozi vile hua na madhara ya muda mrefu ambayo wakati mwingine hayatoki.
ukikutana na mwanamke ambaye alijichubua miaka kumi iliyopita na baadae akaacha mara nyingi utaona kabisa ngozi yake imeungua na imeshindwa kurudi katika hali yake ya zamani, lakini pia vipodozi vya nywele vingine ni hatari na huunguza ngozi ya nywele.

msongo wa mawazo; katika karne hii ambayo dunia ina mambo mengi sana ambayo yanaleta msongo wa mawazo hasa ukosefu wa ajira na mahusiano mabovu ya kimapenzi basi wanawake wengi hutumia muda mwingi sana kuwaza mwisho wao.
Siku zote mtu akifika kwenye hali hii basi hawezi kula vizuri na kupata mahitaji yake muhimu na matokeo yake huonekana kabisa amechoka na kudhoofu.

kutoshiriki tendo la ndoa; tendo la ndoa kwa wanawake lina faida nyingi za kiurembo kama kufanya ngozi kung'aa sana kwani damu nyingi huenda kwenye ngozi wakati wa tendo la ndoa na kupeleka hewa ya oxgen na virutubisho vingine.
lakini pia wakati wa tendo la ndoa mwanamke anatoa homoni nyingi ikiwemo oxytocin na oestrogen ambazo ndio msingi mkuu unaomfanya mwanamke awe na shepu nzuri na ngozi laini kwanzia kuvunja ungo mpaka mwisho.
mwanamke asiyeshiriki tendo la ndoa hapati faida hizi.
ulevi na uvutaji wa sigara; siku hizi wanawake ni walevi sana kama wanaume, kimsingi pombe hupunguza maji mwilini kitaalamu kama deuresis na kuifanya ngozi kukosa maji na kua mbaya lakini pia sigara huweka kemikali kitaalamu kama nicotine kwenye ngozi.
Kemikali hii hufanya ngozi kua nyeusi na kupoteza muonekano wake wa awali.

magonjwa; ukiachana na magonjwa ya mwili kama saratani, ukimwi,sukari ambayo huchosha mwili kabisa baadhi ya magonjwa kama ugumba na magonjwa ya kizazi huathiri sana saikolojia ya wanawake.
Hali hii huwakondesha, kuwachosha na kuwazeesha kabisa.

kazi ngumu; miili ya wanawake haikuandaliwa kufanya kazi ngumu kama za wanaume, miili ya wanaume iliumbwa kwa ajili ya kazi ngumu hivyo sio kitu cha ajabu ila mwanamke akijikita kwenye kazi ngumu hupoteza kabisa muonekano wake wa awali na anaweza kuanza kuonekana kama mwanaume.                                                              
 Mwisho; wawake wengi hasa wa afrika huamini kwamba swala la muonekano mzuri ni bahati tu, wakisahau kua kwamba wao pia wanachangia kwa asilimia kubwa kua katiaka muonekano huo, mambo mengi ya urembo na muonekano yapo ndani ya uwezo wako ni swala la kuchukua hatua tu.

                                                                        STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183

TATIZO LA KONDO LA NYUMA KUSHINDWA KUTOKA BAADA YA KUJIFUNGUA(RATAINED PLACENTA)

Wanawake wengi huamini kwamba safari ya uzazi huisha pale mtoto anapozaliwa, kitu ambacho mara nyingi sio kweli na ukweli ni kwamba safari hii huisha pale kondo la nyuma linapokua limetoka lote kitaalamu kama third stage of labour.

retained placenta ni nini?
Hii ni hali ambayo kondo la nyuma linashindwa kutoka nje ya kizazi nusu saa baada ya kujifungua, ni hali hatari kwa mama kwani anaweza akavuja damu mpaka kifo.

nini chanzo cha kondo la nyuma kukataa kutoka?
kuna sababu mbalimbali za kondo la nyuma kukataa kutoka kama ifuatavyo..
uchungu kidogo; hii hutokea pale baada ya kujifungua mtoto  ambapo uchungu unakua mdogo sana na kondo la nyuma linashindwa kutoka lenyewe.
kukamatwa kwa kondo la nyuma; kondo la nyuma huweza kunaswa na kushindwa kutoka hata kama uchungu upo,mara nyingi husabishwa na kufunga kwa mlango wa uzazi.
kunasa kwenye kizazi; wakati mwingine kondo la nyuma hunasa kabisa kwenye misuli ya kizazi na mara nyingi husabishwa na historia ya kuzaa kwa upasuaji.

watu gani wako kwenye hatari ya kupata tatizo hili?

  • kuzaa baada ya umri wa miaka 30
  • kuzaa kabla ya miezi tisa ya mimba.
  • uchungu kuchukua muda mrefu
  • mtoto kufia tumboni.
  • historia ya kuzaa kwa upasuaji.
dalili za tatizo hili ni zipi kwa mama mjamzito?
  • homa kali
  • maumivu makali
  • harufu sehemu za siri
  • kuvuja damu nyingi
  • kutokwa na vipande vya nyama ukeni.
matibabu
Matibabu makubwa ya hali hii ni kuhakikisha kondo la nyuma linatoka kwa njia yeyote ile, njia zinazotumika hospitalini ni kuchoma sindano ya uchungu, kuingiza mkono kwenye uke na kuondoa kawaida, au kufanyiwa upasuaji mkubwa kama kondo limenasa kwenye kizazi na kuondoa kizazi.(accreta)

                                                       STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183

FAHAMU KWANINI MIHOGO NI SUMU KALI KWA BINADAMU.

Pamoja kwamba mihogo ni zao la tatu duniani kwa ajili ya chakula cha aina ya wanga huku likiwa na virutubisho vingine kama madini, vitamin A,B  na C lakini ni moja ya mazao hatari sana kwa binadamu.
Tarehe 10 mwezi wa tatu mwaka 2005 watoto 27 walifariki nchini ufilipino huku wengine 100 wakinusurika baada ya kula mihogo.
Watoto hao walikula mihogo ya kukaangwa wakati wa chakula cha asubuhi baada ya kununuliwa kwa mtu wa mtaani aliyekua anatembeza.
                                   
Wakati wa vita ya pili ya dunia wajapani wengi walikimbilia brazili kutafuta maisha mazuri, kutokana na ugumu wa maisha huko walipewa ardhi yenye ukame hivyo walipanda mihogo ili kuweza kuishi.
Historia inaonyesha ni watatu tu ndio waliobaki baada ya vita ya pili ya dunia kuisha baada ya kuishi kwa kutumia chakula hicho, wengi walikufa kwa sumu ya mihogo.

Sehemu zingine duniani ambazo watu hula mihogo kama afrika na sehemu zingine hua inatokea ghafla tu na kuua watu kadhaa na mara nyingi hapa Tanzania vifo husababishwa kwa kuliwa kwa majani ya mihogo maaruufu kama kisamvu.
Familia kadhaa nchini Tanzania zimewahi kufa kwa kula kisamvu tu ambacho pia hua na kemikali hiyo hasa kisipoiva vizuri.
Kwasasa baadhi ya serikali duniani kama japan zilishapiga marufuku matumizi ya mihogo na majani yake yote kama chakula.

nini chanzo cha sumu kwenye mihogo?
Mihogo ina kemikali moja kwa jina ya linamarin, mara nyingi muhogo ukiliwa mbichi kemikali hii hubadilishwa kwenye tumbo la binadamu na kua sumu kwa jina la cyanide.
Hizi ni moja ya sumu hatari zaidi duniani ambayo inaua ndani ya sekunde chache sana.
Kitaalamu ni kipande kidogo tu cha muhogo kina dozi ya kutosha kumuondoa mtu.


unaweza kuutambua muhogo wenye sumu?
Sio rahisi kuutambua, japokua tafiti zinaonyesha muhogo mchungu una sumu zaidi kuliko ule mtamu.

Pamoja na mbinu mbali mbali za kuloeka mihogo na kupunguza sumu zake bado wataalamu wana amini mihogo ina sumu zingine ambazo hata kama hazikuui basi zinakuumiza taratibu kwenye mfumo wa ubongo, maini na figo ndio maana baadhi ya nchu duniani ziliamua kupiga marufuku zao hilo kwani kuna vyakula vingi mbadala kama wali, ugali, viazi na ngano.

                                                                     STAY ALIVE

                                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                             0769846183/0653095635

HII NDIO SABABU MAFUTA YA MZAITUNI NI BORA KIFYA.(OLIVE OIL)

Mafuta ya mzaituni ni mafuta ambayo kitaalamu huitwa monosaturated yaani hua kwenye mfumo wa kimiminika kwenye joto la kawaida na huaminika kua na faida za kiafya sana mwilini.
                                                                    

Ukiacha  kutumia mafuta ambayo huitwa saturated au ambayo yanakua mgando wakati wa hali ya hewa ya kawaida na kuanza kutumia mafuta ya haya ya mzaituni basi afya yako itapata faida zaidi.

Mafuta ya mzaituni hupunguza sana hatari ya kuugua magonjwa ya moyo kwani yameonyesha kupunguza sana kiasi cha lehemu au cholestrol mwilini ambayo ndio moja ya chanzo kikuu cha ugonjwa wa moyo.

Tafiti zingine zimeonyesha kwamba mafuta haya yana uwezo wa kupunguza kiwango cha sukari mwilini hivyo ni faida sana kwa watu wenye hatari sana ya kupata magonjwa ya kisukari, lakini pamoja na faida zake hizo hutakiwi kutumia mengi kwani yana nguvu au calories nyingi ambazo huweza kukunenepesha.

siku zote chagua mafuta ambayo yako kwenye mfumo wa kimiminika badala ya mafuta ambayo yako kwenye mfumo wa mgando.
lakini pia kumbuka huwezi kuvifanya vyakula ambavyo sio vizuri kwa afya hasa vyakula vya kukaangwa sana eti kwasababu umeongezea  au umetumi mafuta haya kuandaa vyakula hivyo.

                                                               STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0653095635/0769846183