data:post.body FAHAMU AINA ZA VIRUSI VYA UKIMWI NA TOFAUTI ZA MAKALI YAKE MWILINI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU AINA ZA VIRUSI VYA UKIMWI NA TOFAUTI ZA MAKALI YAKE MWILINI.

Unaweza kushangaa mtu anapata ukimwi leo lakini anakufa baada ya mwaka mmoja au miwili pamoja na kufuata masharti yote na kutumia dawa zote kwa uaminifu.
Hii ni kwasababu virusi vya ukimwi havifanani, kuna ambavyo vikikupata vinakushambulia na kusambaa kwa kasi lakini vingine haviwezi.

je kuna aina ngapi ya virusi vya ukimwi?
Kuna aina mbili za virusi vya ukimwi kwa jina la HIV-1 na HIV-2 vyote husababisha maambukizi ya ukimwi lakini hutofautiana.
HIV-1 ndio aina ya virusi ambavyo vinapatikana zaidi, zaidi ya asilimia tisini ya wagonjwa wameathirika na virusi hivi,ni vikali sana, vinaambukizwa kirahisi, huchukua muda mfupi kutoka kwenye HIV kwenda kwenye AIDS na vimeua watu wengi sana duniani, yaani kwa haraka haraka ukisikia mtu ni mgonjwa wa ukimwi basi uwezekano mkubwa yuko na hivi.
Virusi hivi vina makundi manne yaani M,N,O na P lakini pia vikundi hivi vimegawanyika katika vikundi vingine vidogo vidogo zaidi na mara nyingi daktari anaweza kukutibu vizuri kama akijua ni aina gani ya hivyo vikundi vidogo vidogo unavyo kwani baadhi ya vikundi havisikii kabisa dawa fulani na vingine vinasikia, na bahati mbaya ni nchi zilizoendelea tu  ndio zina uwezo wa kutambua iana ya ukimwi ulionao.

HIV-2 ni aina ya virusi ambavyo vinashambulia watu wachache sana, mara nyingi hupatikana maeneo ya ya afrika magharibi.
Virusi hivi sio vikali, ni ngumu kumuambukiza mtu na huchukua muda mrefu sana kumfanya mtu awe hoi kitandani kwani hata kasi yake ya kusambaa ni ndogo.
Virusi hivi pia vinakua na na magroup yake makubwa na madogo madogo.

je unaweza kuathirika na aina zote mbili?
Ndio mgonjwa wa ukimwi anaweza kupata iana zote mbili za ukimwi au aina moja na magroup yake mengine kitaalamu kama HIV superinfection, na mara nyingi hatari ya maambukizi haya iko kwenye miezi michache ya kwanza baada ya kuambukizwa aina fulani ya virusi vya ukimwi.
Mara nyingi wagonjwa wenye virusi vya aina zote mbili huugua na kufa baada ya muda mfupi hata kama wakipewa dawa kwani dawa nyingi hukataa kuwatibu.

Kwanini wagonjwa wa ukimwi hushauriwa kuendelea kutumia condom?
Unaweza ukapata ukimwi kwa mara ya kwanza na kupata aina fulani ya virusi ambavyo vinatibika kirahisi ukitumia dawa.
Lakini ukiendelea kulala na watu bila kinga basi unaweza ukapata virusi vingine na vingine kiasi kwamba hata dawa ulizopewa mwanzoni zikashindwa kukusaidia.

                                                         
                                                          STAY ALIVE
                                           

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni