data:post.body Agosti 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU AINA ZA VIRUSI VYA UKIMWI NA TOFAUTI ZA MAKALI YAKE MWILINI.

Unaweza kushangaa mtu anapata ukimwi leo lakini anakufa baada ya mwaka mmoja au miwili pamoja na kufuata masharti yote na kutumia dawa zote kwa uaminifu.
Hii ni kwasababu virusi vya ukimwi havifanani, kuna ambavyo vikikupata vinakushambulia na kusambaa kwa kasi lakini vingine haviwezi.

je kuna aina ngapi ya virusi vya ukimwi?
Kuna aina mbili za virusi vya ukimwi kwa jina la HIV-1 na HIV-2 vyote husababisha maambukizi ya ukimwi lakini hutofautiana.
HIV-1 ndio aina ya virusi ambavyo vinapatikana zaidi, zaidi ya asilimia tisini ya wagonjwa wameathirika na virusi hivi,ni vikali sana, vinaambukizwa kirahisi, huchukua muda mfupi kutoka kwenye HIV kwenda kwenye AIDS na vimeua watu wengi sana duniani, yaani kwa haraka haraka ukisikia mtu ni mgonjwa wa ukimwi basi uwezekano mkubwa yuko na hivi.
Virusi hivi vina makundi manne yaani M,N,O na P lakini pia vikundi hivi vimegawanyika katika vikundi vingine vidogo vidogo zaidi na mara nyingi daktari anaweza kukutibu vizuri kama akijua ni aina gani ya hivyo vikundi vidogo vidogo unavyo kwani baadhi ya vikundi havisikii kabisa dawa fulani na vingine vinasikia, na bahati mbaya ni nchi zilizoendelea tu  ndio zina uwezo wa kutambua iana ya ukimwi ulionao.

HIV-2 ni aina ya virusi ambavyo vinashambulia watu wachache sana, mara nyingi hupatikana maeneo ya ya afrika magharibi.
Virusi hivi sio vikali, ni ngumu kumuambukiza mtu na huchukua muda mrefu sana kumfanya mtu awe hoi kitandani kwani hata kasi yake ya kusambaa ni ndogo.
Virusi hivi pia vinakua na na magroup yake makubwa na madogo madogo.

je unaweza kuathirika na aina zote mbili?
Ndio mgonjwa wa ukimwi anaweza kupata iana zote mbili za ukimwi au aina moja na magroup yake mengine kitaalamu kama HIV superinfection, na mara nyingi hatari ya maambukizi haya iko kwenye miezi michache ya kwanza baada ya kuambukizwa aina fulani ya virusi vya ukimwi.
Mara nyingi wagonjwa wenye virusi vya aina zote mbili huugua na kufa baada ya muda mfupi hata kama wakipewa dawa kwani dawa nyingi hukataa kuwatibu.

Kwanini wagonjwa wa ukimwi hushauriwa kuendelea kutumia condom?
Unaweza ukapata ukimwi kwa mara ya kwanza na kupata aina fulani ya virusi ambavyo vinatibika kirahisi ukitumia dawa.
Lakini ukiendelea kulala na watu bila kinga basi unaweza ukapata virusi vingine na vingine kiasi kwamba hata dawa ulizopewa mwanzoni zikashindwa kukusaidia.

                                                         
                                                          STAY ALIVE
                                           

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183

TATIZO LA MTOTO KUNYONYA KIDOLE NA MATIBABU YAKE.

Kunyonya kitu chochote wakati wa kuzaliwa ni tabia ya kawaida kwa mtoto, na kama mtoto akizaliwa hawezi kunyonya basi ujue kuna tatizo sehemu.
watoto wengine huanza kunyonya vidole wakiwa tumboni mwa mama zao kabla hata ya kuzaliwa na hii ni kawaida kabisa na wakishazaliwa hupenda kunyonya vidole vyao kabla ya kwenda kulala kwani huwafanya wajisikie vizuri.

Ni umri gani mtoto anatakiwa aache kunyonya vidole?
Mtoto anatakiwa aache kujinyonya vidole alifika umri wa miezi 6 mpaka 7 na wakati mwingine mpaka miaka mitatu, lakini akiendelea kujinyonya baada ya miaka mitatu basi kuna hatari ya kuendelea kupata minyoo mara kwa mara ambayo huweza kuleta upungufu wa damu, na kuharibu mpangilio wa meno yake mpaka ukubwani.

mambo gani huweza kusaidia kuacha kunyonya vidole?
mpe zawadi; wazazi wengi hupenda kutumia adhabu kumbadilisha tabia mtoto kitaalamu kama negative reinforcement lakini unaweza kutumia njia tofauti au positive reinforcement kwa kuwapa zawadi pale wanapofanikiwa kuepuka makosa fulani.
mfano unaweza kumpa zawadi ya shilingi 200 akimaliza siku nzima bila kunyonya kidole badala ya kumchapa viboko.
weka tiki kwenye kalenda kwenye siku ambazo hakunyonya vidole na hii itampa nguvu sana.
angalia mambo yanayosababisha anyonye kidole; mara nyingi watoto hunyonya vidole wakiwa na msongo wa mawazo au wakikosa amani kwa muda fulani.
ukiliona hilo basi mkumbatie mtoto wako na kaa naye karibu au jaribu kutatua changamoto yake.
mkumbushe kiutaratibu; muonyeshe tu kwamba hupendezwi na tabia yake kwa sauti ya upole bila kufoka, binadamu ana asili ya kupingana na sheria hasa ukitumia nguvu sana kumzuia, ukimpa uhuru inakua rahisi yeye kuachana na tabia fulani.
vipi kama njia zote zikikwama?: usiwe na wasiwasi, haraka wala usitumie nguvu kubwa, endelea tu na utaratibu huo na mwishowe utafanikiwa tu kumrekebisha.

                                                                         STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                             0769846183/0653095635  
                                                          

makundi 8 ya watu wasioruhusiwa kunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume.

Huenda umesikia mara kwa mara kwamba kuna mwanaume amefia chumba cha kulala wageni baada au kabla ya kushiriki tendo la ndoa na huenda hujawahi kufuatilia ili kujua chanzo ramsi cha kifo hicho ni nini.
 Naomba nikwambie kwamba moja ya sababu ya kufia chumba cha wageni ni matumizi ya dawa hizi za viagra kiholela bila kujua kama afya yako inaruhusu matumizi ya dawa hii.
                                                                     
Leo ntaenda kuzungumzi makundi ya watu ambao hawaruhusiwi kutumia dawa hizi kama ifuatavyo.
wagonjwa wa moyo; wagonjwa wengi wa moyo hawaruhusiwi hata kushiriki tendo la ndoa kutokana na uwezo wao mdogo wa kuhimili mazoezi lakini pia dawa ya viagra inafanya kazi kwa kusukuma damu nyingi kwenda sehemu za siri na kupanua mishipa ya damu kitu ambacho hakiwezi kuvumilika kwa wagonjwa hawa.
Mshtuko wa moyo, kusimama kwa moyo na vifo vya ghafla vimeripotiwa sana sababu ya matumizi ya dawa hii ya viagra kwa wagonjwa wa moyo.
wagonjwa wa presha ya kushuka: dawa ya viagra ilitengenezwa mwanzoni kabisa kwa ajili ya kushusha presha ya kupanda lakini baadae ikaonekana kwamba madhara yake ni kuongeza nguvu za kiume hivyo ikabidi iondolewe kwenye dawa za presha.
Hivyo kama wewe presha yako ina tabia ya kushuka basi dawa hii inaweza kukushusha mpaka presha ya sifuri na huo ndio ukawa mwisho wako.
wanaotumia dawa za presha ya kupanda;  hawa wagonjwa hutumia dawa za kushusha presha kila siku, sasa kama nilivyosema hapo juu.
viagra pia inatabia ya kushusha presha hivyo kama ukiamua kuimeza basi dawa zako za presha ni vizuri usizimeze kwani presha itashuka sana na kuhatarisha maisha yako.
wagonjwa wa macho; kama una tatizo lolote la macho ukatumia dawa hii ukaona giza ghafla basi achana nayo kwani hiyo ni kengere ya hatari na unatakiwa uwahi hospitali kuonana na daktari kwani ukiendelea kutumia itakumaliza macho kabisa.
wagonjwa wa siko seli; moja ya matatizo ya siko seli ni kuzuia damu kwenye uume na kushindwa kutoka kitaalamu kama priapism.
Tatizo hili ni kubwa na huweza kusababisha kufanyika kwa upasuaji, sasa mgonjwa wa siko seli akimeza dawa hii anaongeza hatari ya kushikwa na hali hiyo kwa maana nyingine dawa hii sio salama kwake, wagonjwa wa saratani ya damu pia wana hatari hii.
wagonjwa wa chembe ya moyo;  huu ugonjwa kwa kitaalamu unaitwa angina pectoris, ni maumivu ya misuli ya moyo pale moyo unapokosa hewa ya kutosha sababu ya mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kuzibwa na mafuta au kukakamaa.
sasa wagonjwa hawa mara nyingi hupewa dawa zinaizwa isosorbide mononitrate or dinatrate, dawa hizi hupanua mishipa ya damu na kuwafanya wapate nafuu huku dawa hizo zikishusha presha kama moja ya madhara yake, hivyo zikitumika na viagra ambayo kazi yake ni kushusha presha pia huweza kumuua mgonjwa.
wanawake; kuna watu hufikiri dawa za viagra zinaweza kuwasaidia wanawake kupata hamu ya tendo la ndoa, kitu hicho sio kweli na hakuna utafiti ulionyesha kitu kama hicho.
matumizi ya dawa hii kwa wanawake haina faida yeyote zaidi ya kushusha presha bure.
kuchanganya na baadhi ya dawa; dawa ya viagra ikishafanya kazi mwilini inaondolewa na maini kwa kutumia enzyme moja inayoitwa cytchrome p450, sasa baadhi ya dawa kama erythromycin, ritonavir na cimetidine hufanya kazi kwa kuzuia enzyme hiyo na kinachotokea ni kwamba viagra haitoki mwilini na inazidi kua nyingi kwenye mfumo wa damu,
Hivyo kua makini usitumie dawa hizi na pamoja na viagra.
MWISHO: viagra ni dawa hatari sana na inatakiwa itolewe kwa kibali maalumu cha daktari pale anaothibitisha kweli hakuna mazingira yeyote yanaweza kuhatarisha afya yako wa matumizi ya dawa hizo.

                                                                       STAY ALIVE
                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          0653095635/0769846183

FAHAMU KWANINI MWILI WA BINADAMU UNAELEA BAADA YA KIFO.

Katika hali ya kawaida binadamu akiwa hai anakua ni mwepesi kuliko maji hivyo hawezi kuzama chini ya maji akiwa bado anapumua, naomba hilo lieleweke vizuri.
Misuli ni mizito kidogo kuliko maji, mifupa ni mizito kidogo kuliko maji, mafuta ni mepesi kuliko maji lakini pia mapafu ya binadamu ya hewa ambayo yanamfanya binadamu awe kama boya la kuogelea.

binadamu akifa inakuwaje?
Sasa binadamu akifia kwenye maji, basi maji mengi yataingia kwenye mapafu na kuupoteza ule uwezo wa binadamu kuelea yaani atakua mzito kuliko maji na matakeo yake atazama chini ya maji kwa muda.
baada ya masaa kadhaa binadamu huyo ataanza kuharibika, wakati wakuharibika binadamu hutoa hewa nyingi ambayo hutokana na kazi ya bacteria wanaomshambulia.
Hewa ile itajaa sehemu mbalimbali za mwili wake na kumfanya avimbe, sasa hapo ndio atakua mwepesi tena kama boya, kama alivyokua mwanzo kabla ya kufa hivyo mwili utarudi juu na kuelea.

mwili unachukua masaa mangapi mpaka kuelea?
kutokana na hali ya hewa ya eneo husika, sehemu yenye joto mwili unaharibika haraka hivyo utaelea ndani ya masaa 24, lakini sehemu yenye baridi kali sana ambapo kuoza kunachelewa basi mwili unaweza kukaa chini hata wiki kadhaa bila kuelea.

                                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

                                                           STAY ALIVE.