data:post.body UKIPOTEZA KIASI HICHI CHA DAMU LAZIMA UPOTEZE MAISHA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UKIPOTEZA KIASI HICHI CHA DAMU LAZIMA UPOTEZE MAISHA.

Utangulizi.
Kifo cha kuvuja damu siku zote hua hakina maumivu hivyo ni hatari sana kupuuzia damu ambayo inavuja sehemu ya mwili wako.
Asilimia kubwa ya watu wanaofariki kwenye ajari mbalimbali na wamama wanaotoka kujifungua, wanaotoa mimba hufa kwa kupoteza damu nyingi.

Binadamu wa kawaida ana lita tano mpaka lita sita za damu tu, hata kama ana mwili mkubwa kiasi gani.
ukivuja damu kiasi gani unaweza kufa?
Mara nyingi mtu hupoteza maisha pale anapopoteza zaidi ya nusu ya kiwango cha damu alichokua nacho, kwa maana nyingine ni kwamba watu wawili wanaweza kuvuja damu kiasi sawa lakini mmoja akafa mwingine akabaki.
kama una damu lita sita basi ukipoteza lita tatu au tatu na zaidi unakufa, lakini mgonjwa ambaye ana upungufu wa damu tangu muda labda akawa na lita nne za damu basi huyu atakufa akipoteza lita mbili tu.

kifo kinakuja vipi?
Mgonjwa huanza na kuishiwa nguvu zote na baadae haunza kuhisi usingizi kisha atalala bila kuamka tena.
Kifo hichi husababishwa na moyo kukosa damu ya kutosha, kushindwa kazi na hatimaye kusimama kabisa.
Kwa mgonjwa ambaye anavuja damu kidogo kidogo kwa muda mrefu mwili unaweza kupata taarifa na kusababisha moyo wake kuanza kukimbia sana ili kujaribu kudhibiti hali ile, lakini anayevuja damu ghafla, mwili haupati nafasi kabisa ya kupata taarifa.

mwisho; ukiwa na mgonjwa yeyote ambaye anavuja damu basi kipaumbele kikubwa kwako inatakiwa iwe kuzuia damu isivuje.
njia za kuzuia damu ni kukandamiza sehemu inayofuja na nguo, kufunga kamba juu ya sehemu inayovuja kama mguuni, na kumtuliza mgonjwa asifurukute zaidi.

                                                     STAY ALIVE

                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          0769846183/0653095635

Maoni 2 :

  1. Mm sai Nina miezi miwili navuja damu sababu ya depo provera.ntasaidika vp

    JibuFuta
    Majibu
    1. kuvuja damu baada ya kuchoma hiyo sindano hua ni kawaida, ni vizuri kuhudhuria semina kabla hujaamua kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango.
      cha msingi ni kujua ni kiasi gani kinavuja kwa siku kujua kama ni hatari au sio hatari.
      nenda hospitali.

      Futa