data:post.body JINSI YA KUJUA KAMA MTU ALIKUFA MAJI AU ALIUAWA NA KUTUPWA MAJINI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JINSI YA KUJUA KAMA MTU ALIKUFA MAJI AU ALIUAWA NA KUTUPWA MAJINI.

Mtu anaweza ukamuua mtu kisha akamtupa kwenye maji ali aonekane amekufa maji, kama mtu huyo hakua na vidonda vya kupigwa ni ngumu sana kujua kama mtu huyu alikufa kwa kuzama kwenye maji au aliuawa kwanza kisha akatupwa kwenye maji.
                                                             
nini hufanyika kutambua mtu aliuawa kisha kutupwa kwenye maji?
Mtu akifa kwa kuzama kwenye majini, kwanza anavuta kiasi kikubwa sana cha maji ambacho kinaingia mapafuni na kuyafanya yapanuke na kuongezeka uzito.
Lakini mtu akitupwa kwenye maji baada ya kufa hawezi kuvuta tena hewa, kiasi kidogo cha maji kitaingia mapafuni.
Hivyo ukifungua kifua cha marehemu kisha ukakata kiasi cha mapafu na kukiweka kwenye ndoo ya maji basi kitazama kama marehemu alikufa maji ila kama marehemu alikufa kisha akatupwa kwenye maji, kipande hicho cha pafu kitaelea juu ya maji.

                                                                   STAY ALIVE


0 maoni:

Chapisha Maoni