data:post.body IMANI KWAMBA MGONJWA WA SIKOSELI AU SELI MUNDU HAWEZI KUZAA SIO ZA KWELI.TAFITI ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

IMANI KWAMBA MGONJWA WA SIKOSELI AU SELI MUNDU HAWEZI KUZAA SIO ZA KWELI.TAFITI

 Sikoseli ni nini?
Huu ni ugonjwa wa upungufu wa damu wa kurithi ambao husabishwa na kuwepo Kwa protein ambayo sio ya kawaida kwenye seli nyekundu za damu.
Hali hii hupelekea kupinda wa seli hizi na kua kama mwezi pale zinapokosa hewa ya kutosha.
Ugonjwa huu huathiri zaidi watu weusi kuliko rangi nyingine yeyote duniani.
                                                            


Kwanini inaaminika mgonjwa wa siko seli hawezi kuzaa?
Kutokana na teknolojia duni ya miaka ya nyuma, wagonjwa wengi wa sikoseli walikua hawafiki umri wa kubeba mimba kwa kufa mapema, wasichana wengi walikufa baada ya kuvunja ungo sababu ya kupoteza damu ya hedhi na kufanya hali kua mbaya zaidi na hata waliobahatika kubeba mimba walikufa kabla ya uchungu, au kipindi cha uchungu au baada ya kujifungua.
Sasa kwasababu hakuna mtu aliwahi kuona mama mwenye siko seli amebeba mtoto basi ilionekana watu hawa hawawezi kuzaa.
Lakini pia Kwa wanaume moja ya madhara ya siko seli ni kuathirika Kwa mfumo wa utengenezaji wa mbegu za kiume ambao unaweza kumfanya kijana wa kiume kushindwa kumpa mtu mimba.

je mgonjwa wa sikoseli anaweza kubeba mimba?
kama binti akihudumiwa vizuri kwanzia utoto mpaka utu uzima basi anaweza kubeba mimba kama watu wengine kabisa japokua atahitaji uangalizi zaidi kuliko wajawazito wengine sababu ya hatari kubwa ya kupungukiwa damu ambayo ni moja ya chanzo kikuu cha vifo vya Akina mama hata ambao sio wagonjwa wa siko seli hapa nchini.

mambo ya kuzingatia mgonjwa wa sikoseli akiwa mjamzito.
Kulingana na unyeti wa tatizo hili hata madaktari wengi WA zamani hawakushauri watu hawa wabebe ujauzito na wengi waliolazimisha waliishia kufariki lakini Kwa sasa kuna mambo unaweza kuzingatia ili kuweza kujifungua kama ifuatavyo.
*Wanatakiwa hahudumiwe na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama kwenye hospitali kubwa ya rufaaa.
*Ahakikishe damu yake haishuki 9g/dl kipindi chote cha ujauzito.
*Aanze clinic mapema Sana angalau mwezi wa Kwanza au wa pili na awe anaenda kila baada ya wiki mbili mpka kujifungua.
*Apate virutubisho na dawa zote muhimu ambazo hutolewa Kwa wajawazito wa kawaida bila kukosa Hata moja.
*Crisis  za siko seli hua nyingi zaidi kipindi hiki hivyo awe tayari kulazwa na kutibiwa mara Kwa mara kipindi hiki.

Njia gani sahihi ya mgonjwa sikoseli kujifungua?

Kama akina mama wengine basi mama wa siko seli anaruhusiwa kujifungua kawaida kabisa kama Hajapata shida yeyote ambayo inamlazimu kujifungua kwa upasuaji.
Kulingana na mfumo wa ugonjwa wa siko seli wagonjwa wengi hua na nyonga ndogo sababu ya ukuaji duni kipindi cha kuvunja ungo na wengne hua na nyonga iliyoharibika sababu ya baadhi ya madhara ya siko seli kitaalamu kama avascular necrosis of the femur hivyo watahitaji upasuaji.
Ni vizuri familia kujiandaa kutoa damu kwani upungufu WA damu wa hata nusu kikombe cha chai wakati wa upasuaji utahitaji kuongezewa damu nyingine.
Kumbuka mgonjwa huyu hawez kuvimilia upungufu WA damu hata kidogo.

Changamoto anazoweza kuzipata mama kabla na baada ya kujifungua.
*Upungufu mkubwa wa damu na madin mwilini.
*Crises za mara Kwa mara.
*Mapacha, kuvuja damu, mtoto kukaa vibaya, kifafa cha mimba na mtoto mkubwa ni hatari Sana Kwa watu hawa.
*Kuharibika Kwa mimba.
*Mtoto kuzaliwa kabla ya Muda, kudumaa tumboni na kufa kabla au baada ya kuzaliwa.
*Kushindwa kulia baada ya kuzaliwa sababu ya kukosa hewa ya kutosha husabisha mtoto kuwa na mtindio wa ubongo au uwezo mdogo Sana darasani siku za usoni.
*Kifo cha mama na mtoto ambacho mara nyingi husababishwa na upungufu mkubwa wa damu, kushambuliwa na bacteria na mabonge ya damu ndani ya mwili wa mama.

mwisho;pamoja na changamoto nyingi ambazo zimetajwa kwenye makala hii, mama ambaye ni mgonjwa wa sikoseli kama alikuzwa vizuri na kufuata masharti yote ya ugonjwa huu anaweza kuzaa kawaida kama watu wengine.

                                                            STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183

Maoni 1 :

  1. Mimi sina maoni ila Nina mtoto mwenye ugonjwa huo na kapungua uzito

    JibuFuta