data:post.body Julai 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JINSI YA KUJUA KAMA MTU ALIKUFA MAJI AU ALIUAWA NA KUTUPWA MAJINI.

Mtu anaweza ukamuua mtu kisha akamtupa kwenye maji ali aonekane amekufa maji, kama mtu huyo hakua na vidonda vya kupigwa ni ngumu sana kujua kama mtu huyu alikufa kwa kuzama kwenye maji au aliuawa kwanza kisha akatupwa kwenye maji.
                                                             
nini hufanyika kutambua mtu aliuawa kisha kutupwa kwenye maji?
Mtu akifa kwa kuzama kwenye majini, kwanza anavuta kiasi kikubwa sana cha maji ambacho kinaingia mapafuni na kuyafanya yapanuke na kuongezeka uzito.
Lakini mtu akitupwa kwenye maji baada ya kufa hawezi kuvuta tena hewa, kiasi kidogo cha maji kitaingia mapafuni.
Hivyo ukifungua kifua cha marehemu kisha ukakata kiasi cha mapafu na kukiweka kwenye ndoo ya maji basi kitazama kama marehemu alikufa maji ila kama marehemu alikufa kisha akatupwa kwenye maji, kipande hicho cha pafu kitaelea juu ya maji.

                                                                   STAY ALIVE


IMANI KWAMBA MGONJWA WA SIKOSELI AU SELI MUNDU HAWEZI KUZAA SIO ZA KWELI.TAFITI

 Sikoseli ni nini?
Huu ni ugonjwa wa upungufu wa damu wa kurithi ambao husabishwa na kuwepo Kwa protein ambayo sio ya kawaida kwenye seli nyekundu za damu.
Hali hii hupelekea kupinda wa seli hizi na kua kama mwezi pale zinapokosa hewa ya kutosha.
Ugonjwa huu huathiri zaidi watu weusi kuliko rangi nyingine yeyote duniani.
                                                            


Kwanini inaaminika mgonjwa wa siko seli hawezi kuzaa?
Kutokana na teknolojia duni ya miaka ya nyuma, wagonjwa wengi wa sikoseli walikua hawafiki umri wa kubeba mimba kwa kufa mapema, wasichana wengi walikufa baada ya kuvunja ungo sababu ya kupoteza damu ya hedhi na kufanya hali kua mbaya zaidi na hata waliobahatika kubeba mimba walikufa kabla ya uchungu, au kipindi cha uchungu au baada ya kujifungua.
Sasa kwasababu hakuna mtu aliwahi kuona mama mwenye siko seli amebeba mtoto basi ilionekana watu hawa hawawezi kuzaa.
Lakini pia Kwa wanaume moja ya madhara ya siko seli ni kuathirika Kwa mfumo wa utengenezaji wa mbegu za kiume ambao unaweza kumfanya kijana wa kiume kushindwa kumpa mtu mimba.

je mgonjwa wa sikoseli anaweza kubeba mimba?
kama binti akihudumiwa vizuri kwanzia utoto mpaka utu uzima basi anaweza kubeba mimba kama watu wengine kabisa japokua atahitaji uangalizi zaidi kuliko wajawazito wengine sababu ya hatari kubwa ya kupungukiwa damu ambayo ni moja ya chanzo kikuu cha vifo vya Akina mama hata ambao sio wagonjwa wa siko seli hapa nchini.

mambo ya kuzingatia mgonjwa wa sikoseli akiwa mjamzito.
Kulingana na unyeti wa tatizo hili hata madaktari wengi WA zamani hawakushauri watu hawa wabebe ujauzito na wengi waliolazimisha waliishia kufariki lakini Kwa sasa kuna mambo unaweza kuzingatia ili kuweza kujifungua kama ifuatavyo.
*Wanatakiwa hahudumiwe na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama kwenye hospitali kubwa ya rufaaa.
*Ahakikishe damu yake haishuki 9g/dl kipindi chote cha ujauzito.
*Aanze clinic mapema Sana angalau mwezi wa Kwanza au wa pili na awe anaenda kila baada ya wiki mbili mpka kujifungua.
*Apate virutubisho na dawa zote muhimu ambazo hutolewa Kwa wajawazito wa kawaida bila kukosa Hata moja.
*Crisis  za siko seli hua nyingi zaidi kipindi hiki hivyo awe tayari kulazwa na kutibiwa mara Kwa mara kipindi hiki.

Njia gani sahihi ya mgonjwa sikoseli kujifungua?

Kama akina mama wengine basi mama wa siko seli anaruhusiwa kujifungua kawaida kabisa kama Hajapata shida yeyote ambayo inamlazimu kujifungua kwa upasuaji.
Kulingana na mfumo wa ugonjwa wa siko seli wagonjwa wengi hua na nyonga ndogo sababu ya ukuaji duni kipindi cha kuvunja ungo na wengne hua na nyonga iliyoharibika sababu ya baadhi ya madhara ya siko seli kitaalamu kama avascular necrosis of the femur hivyo watahitaji upasuaji.
Ni vizuri familia kujiandaa kutoa damu kwani upungufu WA damu wa hata nusu kikombe cha chai wakati wa upasuaji utahitaji kuongezewa damu nyingine.
Kumbuka mgonjwa huyu hawez kuvimilia upungufu WA damu hata kidogo.

Changamoto anazoweza kuzipata mama kabla na baada ya kujifungua.
*Upungufu mkubwa wa damu na madin mwilini.
*Crises za mara Kwa mara.
*Mapacha, kuvuja damu, mtoto kukaa vibaya, kifafa cha mimba na mtoto mkubwa ni hatari Sana Kwa watu hawa.
*Kuharibika Kwa mimba.
*Mtoto kuzaliwa kabla ya Muda, kudumaa tumboni na kufa kabla au baada ya kuzaliwa.
*Kushindwa kulia baada ya kuzaliwa sababu ya kukosa hewa ya kutosha husabisha mtoto kuwa na mtindio wa ubongo au uwezo mdogo Sana darasani siku za usoni.
*Kifo cha mama na mtoto ambacho mara nyingi husababishwa na upungufu mkubwa wa damu, kushambuliwa na bacteria na mabonge ya damu ndani ya mwili wa mama.

mwisho;pamoja na changamoto nyingi ambazo zimetajwa kwenye makala hii, mama ambaye ni mgonjwa wa sikoseli kama alikuzwa vizuri na kufuata masharti yote ya ugonjwa huu anaweza kuzaa kawaida kama watu wengine.

                                                            STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183

JINSI YA KUTAMBUA MTU KAMA ALIYEJIUA AU ALIULIWA.[FORENSIC MEDICINE}

Ripoti ya shirika la afya duniani(WHO) mwaka 2014 inaonyesha kwamba kila baada ya sekunde 40 kuna mtu anajiua duniani, Tanzania ikiwa moja ya vinara wa shida hii.
Watu wakikuta mtu amening'inia kwenye mti huamini kwamba amejinyonga, wakikuta mtu kafa kwa majeraha huamini kwamba amechomwa visu na wakikuta mtu na jeraha la risasi huamini kwamba ampepigwa risasi...SIO KWELI.
         
Mauaji sehemu mbalimbali duniani hutegemea sana aina ya nchi huka marekani wakiongoza kwa kujipiga risasi sababu ya upatikanaji wa bunduki kirahisi, uingereza kujichoma visu sababu ya uhaba wa bunduki na afrika kujinyonga....
Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kukwambia kama mtu amejiua au amuawa.
makundi ya vidonda; kwa mtu aliyejiua kwa kujichoma kisu mara nyingi anakua anajikata huku akiwa ametulia kabisa na huenda amejipa na dawa za kuondoa maumivu hivyo utakuta vidonda vyake vimekatwa kwa kujipanga na kwa kueleweka lakini mtu aliyevamiwa kwa visu majeraha yake yanakua hayaeleweki kwani huchomwa huku akijaribu kupambana na muuaji.
maeneo yenye vidonda;  mtu akijichoma kisu mara nyingi hulenga maeneo ambayo anaweza kuyafikia kama mkononi, tumboni na mguuni lakini ukikuta mtu ana majeraha mgongoni, kifuani na maeneo ambayo mkono wake haufiki kirahisi basi huyo ameuwa.
uelekeo wa vidonda; mtu ambaye anatumia mkono wa kulia lazima atajikata kutoka kushoto kwenda kulia, na atajikata kwanzia juu kwenda chini lakini pia mtu mwenye mkono wa kushoto hukata kwanzia kulia kwenda kushoto... hi ni tofauti na mtu aliyechomwa visu kwani havina uelekeo maalumu.
alama za kusitasita; kujikata na kisu kuna maumivu makali sana, mtu ambaye anajikata kuna sehemu utaona alijaribu kujikata lakini akashindwa na kuhamia sehemu nyingine tofauti na mtu aliyechomwa kwani hakuna kusitasita.
urefu wa vidonda kwenda ndani; mtu akijiua kwa kujichoma kisu basi utakuta kisu hakijaingia sana ndani kutokana na maumivu makali amabayo alikua anasikia tofauti na yule aliyeshambuliwa na maadui.
sehemu na idadi ya risasi na zilizopigwa; mtu akijipiga risasi basi hawezi kujipiga zaidi ya moja lakini pia kama alikua mashoto basi atajipiga upande wa kushoto wa kichwa na kama alikua anatumia mkono wa kulia atajipiga upande wa kulia wa kichwa lakini pia kuna maeneo ambayo kulingana na mkono anaotumia ndio itakua rahisi kuyapiga kama tumbo, kichwa na kifua.
ukikuta mtu amepigwa risasi zaidi ya moja, kajipiga maeneo ambayo mkono wake hauwezi kulenga basi ujue ameuawa.
mazingira ya kujinyonga; mara nyingi watu wanaojinyonga wenyewe hawachukui maamuzi ya ghafla, lazima kuna mambo hayakua sawa kwa muda mrefu na huenda muhusika alikua ameomba msaada sehemu.
Hata kama imetokea akajinyonga ghafla lazima ataacha ujumbe wa kutoa malalamiko yake.
ukikuta mtu amejinyonga bila kuacha ujumbe, au ujumbe sio mwandiko wake, au tayari ana majeraha basi kuna watu walimnyonga halafu wakatengeneza mazingira ionekane amejinyonga.
Mwisho; Sio vizuri kuamua kumzika mtu tu baada ya kukuta amekufa, ni vizuri kutoa taarifa polisi kabla ya kumgusa ili waje waaangalie mazingira ya kifo.Kule kuna madaktari bingwa wataalamu wa hizi kazi.

                                                                 STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                    0769846183/0653095635

IFAHAMU DAWA INAYOTUMIKA KUONDOA NGUVU ZA KIUME KABISA.

Kuna aina ya watu hufanya aina fulani ya makosa ambayo yanakua yamekiuka sheria ya nchi mbali mbali duniani.
Makosa hayo ni kama kubaka, kuingilia watu kinyume na maumbile, kuingilia watoto wadogo na kadhalika....baadhi ya nchi zina sheria ambazo ukifanya makosa hayo basi adhabu yako ni kuondolewa nguvu za kiume, nchi hizi ni kama ulaya, canada na nchi za kiarabu.

Lakini pia baadhi ya wanaume ambao wanakua na matatizo ya akili au mtindio wa ubongo hupewa dawa hizi ili kuepusha hatari ya kubaka watu.

dawa hii ni ipi?
Kitaalamu dawa hii inaitwa cyproterone acetate,  dawa hii hufanya kazi ya kupunguza nguvu za kiume, kupunguza msisimko kisha kuondoa nguvu za kiume kabisa.
Nguvu za kiume hupungua ndani ya wiki ya kwanza na baada ya wiki tatu nguvu za kiume zinakua zimeisha kabisa.
Dawa hizi hupatikana kwa mfumo wa sindano na vidonge na mara nyingi watuhumiwa huchowa sindano.

matumizi mabovu ya dawa hizi.
Mwanamke mmoja aliripotiwa kumewekea mwanaume dawa hizi kwenye kinywaji chake, hii ni baada ya kutumia pesa za mwanaume huyu usiku mzima akiwa na rafiki zake wa kike na baadae waliporudi nyumbani, mwanaume yule alishindwa kushiriki kabisa tendo la ndoa.
Wanawake wengi na makahaba  ambao huwatumia wanaume kifedha, hupenda kuwawekea wanaume dawa hii ili washindwe kushiriki nao tendo la ndoa.
Bahati nzuri dawa za kumeza huacha kufanya kazi zikiacha kutumika na kurudisha hali ya kawaida.

                                                                   STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0653095635/0769846183

UKIPOTEZA KIASI HICHI CHA DAMU LAZIMA UPOTEZE MAISHA.

Utangulizi.
Kifo cha kuvuja damu siku zote hua hakina maumivu hivyo ni hatari sana kupuuzia damu ambayo inavuja sehemu ya mwili wako.
Asilimia kubwa ya watu wanaofariki kwenye ajari mbalimbali na wamama wanaotoka kujifungua, wanaotoa mimba hufa kwa kupoteza damu nyingi.

Binadamu wa kawaida ana lita tano mpaka lita sita za damu tu, hata kama ana mwili mkubwa kiasi gani.
ukivuja damu kiasi gani unaweza kufa?
Mara nyingi mtu hupoteza maisha pale anapopoteza zaidi ya nusu ya kiwango cha damu alichokua nacho, kwa maana nyingine ni kwamba watu wawili wanaweza kuvuja damu kiasi sawa lakini mmoja akafa mwingine akabaki.
kama una damu lita sita basi ukipoteza lita tatu au tatu na zaidi unakufa, lakini mgonjwa ambaye ana upungufu wa damu tangu muda labda akawa na lita nne za damu basi huyu atakufa akipoteza lita mbili tu.

kifo kinakuja vipi?
Mgonjwa huanza na kuishiwa nguvu zote na baadae haunza kuhisi usingizi kisha atalala bila kuamka tena.
Kifo hichi husababishwa na moyo kukosa damu ya kutosha, kushindwa kazi na hatimaye kusimama kabisa.
Kwa mgonjwa ambaye anavuja damu kidogo kidogo kwa muda mrefu mwili unaweza kupata taarifa na kusababisha moyo wake kuanza kukimbia sana ili kujaribu kudhibiti hali ile, lakini anayevuja damu ghafla, mwili haupati nafasi kabisa ya kupata taarifa.

mwisho; ukiwa na mgonjwa yeyote ambaye anavuja damu basi kipaumbele kikubwa kwako inatakiwa iwe kuzuia damu isivuje.
njia za kuzuia damu ni kukandamiza sehemu inayofuja na nguo, kufunga kamba juu ya sehemu inayovuja kama mguuni, na kumtuliza mgonjwa asifurukute zaidi.

                                                     STAY ALIVE

                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          0769846183/0653095635

SABABU KWANINI JUISI ZOTE ZA MATUNDA SIO NZURI KAMA ZINAVYOTANGAZWA.

Kumekua na mlipuko mkubwa sana ya magonjwa ambayo sio ya kuambukizwa, yakiambatana na unene, uzito uliopitiliza, magonjwa ya moyo, sukari na presha.
magonjwa yote hayo tunafahamu yanasababishwa na mfumo wa maisha yaani aina ya vyakula na ukosefu wa mazoezi.
                                                             
kwa miaka mingi makampuni ya juisi yamekua yakijitapa kwamba wanatengeneza kitu kizuri cha afya kitu ambacho kimethibitika kutokua na ukweli hata kidogo kulingana na matokeo ambayo tumekua tukiyaona mtaani lakini pia hata juisi zinazotengenezwa nyumbani haziendani na jinsi mwili wa binadamu ulivyoumbwa maana yake hazifai kwa watumiaji kama ifuatavyo.
kukosa nyuzi nyuzi au fibre; Lengo la kula  chakula chochote ni kupata aina fulani ya sukari kwa jina la glucose na virutubisho ili uweze kuishi na kufanya kazi...ukiangalia vyakula vyote ambavyo viko kwenye hali ya asili, utakuta ladha au utamu wake unaambatana na maganda au nyuzi nyuzi fulani.
Yaani sukari iliyoko ndani ya ugali, wali, mihogo, ndizi, viazi na kadhalika hauipati moja kwa moja ni mpaka ule vyakula hivyo.
lakini pia  maembe yana nyuzi zake ndani, machungwa , machenza na malimao yana nyanda zake ndani, ndizi mbivu zina nyuzi nyuzi ndani, apple na mapera huwez kuyala bila kutafuna maganda yake, na kadhalika.
maana yake ni kwamba sukari ambayo iko ndani ya vyakula au matunda hayo inatakiwa iingie na maganda yake tumboni ili mwili uweze kuchukua sukari na virutubisho taratibu lakini vinapochujwa na kua juisi maana yake ukinywa juisi tu sukari inapanda ghafla mwilini hapo hapo kwa kiasi kikubwa sana.
unaweza usione madhara yake hapo hapo lakini baada ya miaka kadhaa utapata majibu ya kisukari, unene na magonjwa ya pressure.
sukari nyingi sana kwenye juisi; sukari ni sumu au madawa ya kulevya ambayo yamehalalishwa, juisi za viwandani zina sukari nyingi sana ambayo haifai kabisa kwenye mwili wa binadamu.
utakuta chupa moja tu ina vijiko 10 mpaka 20 vya sukari, juisi za kutengenezwa nyumbani pamoja kua zina sukari kutoka kwenye matunda yenyewe lakini bado nyingine huongezwa ambavyo vinakuletea uteja wa kutaka kunywa kila siku lakini pia inachosha kongosho yako ambayo inatakiwa kutoa homoni za kupambana na sukari kila siku.
lakini pia sukari hii ikiingia mwilini hubadilishwa kua mafuta na kuongeza matatizo mengine hasa ya moyo.
watu wengi bado wanaamini unene unatokana na ulaji wa mafuta kitu ambacho sio ukweli, unene mkubwa unaletwa na vyakula vya sukari na wanga, kwa maana nyingine mtu anayekula kuku, nyama ya ngombe, kitimoto na  na samaki kila siku hawezi kunenepa kama anayekunywa juisi tu kila siku.
mwisho; pamoja ya kwamba juisi zina virutubisho,sukari yake inangia mwilini kwa njia ambayo sio salama.
Ni vizuri kama wewe ni mdau au mpenzi wa matunda fulani basi yanunue uyale kama yalivyo bila kukamua chochote.
Kwanza utakula machache kama inavyotakiwa lakini pia sukari itangia bila kuakuathiri kabisa.

                                                         STAY ALIVE

                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            0653095635/0653095635