data:post.body ZIFAHAMU AINA KUMI ZA WATU KWENYE JAMII AMBAO SIO WA KAWAIDA.(PERSONALITY DISORDERS) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU AINA KUMI ZA WATU KWENYE JAMII AMBAO SIO WA KAWAIDA.(PERSONALITY DISORDERS)

Unaweza kusikia mtu kaua mpenzi wake ukashangaa sana, ukawaza  kwanini hakuachana naye tu?lakini duniani kuna aina za watu ambao wanachululia vitu tofauti na watu wengine.
huweza kufanya mambo ya ajabu sana ambayo mtu mwenye utu wa kawaida hawezi kufanya kabisa, ni vizuri kua makini sana kuanzisha mahusiano nayo kwani yanaweza kuishia pabaya sana.                           
                 
Personality ni nini?
personality au utu, ni ile hali au tabia inayomtambulisha mtu kwa watu, yaani ukitaja jina lake kwa watu wanajua huyu ni mpole, mkali, makarimu na kadhalika.
Kila mtu ana aina yake ya utu ambayo inakubalika kwenye jamii, kawaida kuna aina 16 za utu ambazo zote hizo ni za kawaida lakini kuna watu wachache ambao za kwao haziko sawa na kitaalamu ni wagonjwa wa akili lakini mtaani wanaonekana wanafanya kazi zao vizuri kabisa yaani sio watu wa kuokota makopo lakini mara nyingi wanakua wako tafauti sana na watu wa kawaida.
zifuatazo nia aina hizo kumi kama ifuatavyo.
paranoid personality; hawa ni aina ya watu ambao hawanaga imani na watu wengine, kila siku wana wasiwasi labda utafanya kitu cha kuwageuka au kuwaangamiza.
mara nyingi wanakua hawaamini hata ndugu zao ,wapenzi wao, rafiki zao au jamaa zao na siku zote hutumia muda mwingi kutafuta makosa kwao.
ukiwa kwenye mahusiano na mtu kama huyu, hua ana wivu sana na atakupigia simu muda wote au kupigia marafiki na watu walioko karibu kuhakikisha kwamba hauko unawasaliti lakini pia watakua na tuhuma za hapa na pale kwamba unawasaliti, watu kama hawa wanakua wakorofi sana kwenye mahusiano, huwafanya wapenzi wao watumwa na hata wakiachwa hawakubali, mwisho wa siku huweza kumuua mpenzi husika.
ukiwa na mtu wa aina hii na ukawa na hofu sana kwenye mahusiano ni vizuri kushtaki polisi kabla hajakudhuru.
schizoid personality; Ni aina ya watu ambao hawapendi kua karibu na watu wengine kabisa hata familia zao, hupenda kukaa peke yao na kufanya mambo.
mara nyingi hufikiri kwamba kua karibu na watu kunawanyima uhuru wao, watu hawa hua hawafurahii maisha sababu hawafurahii vitu vya ukaribu hasa mahuasiano na hua hawajali hisia za watu wengine.
ant social personality; hawa ni watu ambao hawajali kabisa jinsi watu wengine wanavyoumizwa na matendo yao, watafanya kila kitu au kitu chochote maisha yao yaende bila kujali kitu hicho kinaumiza watu wengine au vipi.
mara nyingi hupigana kirahisi na hawana ile roho ya kujisuta wenyewe yaani anaweza akaomba mkopo asilipe, akapita asisalimie jamaa zake, akajenga nyumba kwenye kiwanja sio chake, akadhulumu mali bila wasiwasi wowote.
borderline personality disorder;  hawa ni watu ambao hisia zao zinabadilika badilika sana, yaani anaweza kuamka asubuhi akiwa na furaha sana na mchana akawa hana furaha, hua wana wasiwasi sana kwamba watu wanataka wawaache peke yao na watafanya chochote kuzuia hilo.
hua na hasira sana na hutumia muda mwingi kupambana nazo, hujisikia wako peke yao muda mwingi, na hupata mawazo ya kujidhuru wakati mwingine,
hali hii huwafanya watu hawa kushindwa kukaa kwenye mahusiano na huishia kuachana.
histrionic personality disorder; hawa ni aina ya watu ambao hawawezi kukaa katikati ya watu bila kujaribu kupata macho ya kila mtu kwao au "attention", hujaribu kufanya chochote ili waweze kuongelewa na kila mtu.
mara nyingi tabia zao hutegemea watu ambao wako nao, na hawawezi kufanya kitu wao wenyewe bila kuapata mawazo kutoka kwa watu wengine.
narsissistic personality; hawa ni watu ambao wanaamini kwamba wao ni spesho sana kuliko watu wengine, hupenda kutambulika kila sehemu wanayoenda. ni wachoyo na wanapenda kuwashusha watu wengine imradi tu wao wawe juu.
hupenda kusifiwa kwa chochote wanachofanya na hujisikia vibaya sana kama mtu asipowatambua.
avoidant personality; hawa ni watu ambao wanapenda kujitenga sana na mikusanyiko ya watu au watu wachache, mara nyingi huogopa kukataliwa kwa chochote wanachofanya hivyo huogopa kufanya vitu vipya, kuomba kazi au kuomba mahusiano yeyote kwa kuogopa kukataliwa.
hufurahia kukaa peke yao bila kujichanganya na watu wengine.
dependant personality;  hawa ni watu ambao hawajiamini kabisa kwenye maisha yao na hawawezi kufanya maamuzi yeyote.
hupenda kuwategemea sana watu kwa kila kitu, kama kifedha, kufanya kazi, mahusiano na kadhalika.
watu wa aina hii hawawezi kua peke yao, yaani akitoka kwenye mahusiano haya huingia kwenye mahusiano mengine haraka.
obsessive compulsive personality disorder;  hawa ni watu wenye wasiwasi sana kuhusu kesho yao, hivyo hukaa wakijiandaa kwa lolote.
hupenda kuweka kila kitu kwenye mpangilio maaalumu yaani hawawezi kuvumilia kukaa sehemu ambayo haijapangwa au chafu.
lakini pia hawapendi kutumia pesa zao kwao au kwa watu wengine na muda mwingi wanaweza kukaa na vitu ambavyo vimeisha na hawana kazi navyo.
schizotypal personality; ni aina ya watu ambao hua wakua tofauti kabisa mbele za watu, wanaamini kwamba wana nguvu ya ziada ambayo ni tofauti na wengine kwamba wanaweza kusoma mawazo ya mtu, kutambua mchawi, kumtambua mwizi na kadhalika.
hutumia maneno ambayo sio ya kawaida kujitambulisha na kuwafanya watu wawashangae sana.
mwisho; hakuna matibabu maalumu ya aina hizi za watu kwani huweza kufanya mambo mengine kawaida kama watu wengine, sema baadhi yao wanakua na hatari ya kushtakiwa na kufungwa kwa kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida huku wakiona ni kawaida kwao.
Kwa nchi zilizoendelea huweza kutambuliwa na kupewa dawa za kuwatuliza kidogo.

                                                           STAY ALIVE
  
                                   KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni