data:post.body HII NDIO SARATANI YA UZAZI INAYOUA ZAIDI WANAWAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HII NDIO SARATANI YA UZAZI INAYOUA ZAIDI WANAWAKE.

Japokua saratani ya matiti, saratani ya shingo ya uzazi na saratani ya kizazi ndio zinashambulia zaidi wanawake, vifo vingi vinavyotakana na saratani havisababishwi na saratani hizo.
                                                                  
saratani ya mayai ya uzazi ni hatari kuliko saratani zote za uzazi ambazo unazifahamu, na ubaya wake ni kwamba huonekana ikiwa kwenye hatua za mwisho kabisa hivyo ukiona dalili zimeanza kutokea basi ujue ni hatua za mwisho za ugonjwa.

nini chanzo cha saratani ya mayai?
hakuna chamzo halisi kinachofahamika lakini vifuatavyo vinamuweka muhusika hatarini kuugua.
 • Historia ya saratani ya mayai kwenye familia yake.
 • kutozaa kabisa au kuzaa watoto wachache sana.
 • umri zaidi ya miaka 50
 • Rangi ya ngozi i.e wanawake weupe wanaugua zaidi kuliko weusi.

nini dalili za ugonjwa huu?
 • kuvimba tumbo
 • kupungua uzito
 • kukosa siku za hedhi
 • siku za hedhi kuvurugika
 • kukojoa mara kwa mara
 • kupata choo ngumu.
vipimo gani hufanyika kugundua tatizo?
 • utrasound
 • biopy i.e kukata sehemu ya nyama ya uvimbe na kupima maabara.
 • CT scan
 • MRI
 • X  RAY ya kifua
 • vipimo vya homoni na enzymes kama CA-125. Alpha fetoprotein, Human chorionic gonadotrophin hormone, lactate dehydrogenase.
 matibabu
 Matibabu ya ugonjwa huu ni upasuaji, mionzi na dawa...inategemea na hatua ya ugonjwa wenyewe.
Kwasababu wagonjwa wengi hupatikana kwenye hatua za mwisho basi wengi hufariki ndani ya miezi sita mpaka miaka mitano.

Jinsi ya kujizuia na ugonjwa huu.
Bahati mbaya hakuna njia iliyothibitishwa kuzuia ugonjwa huu, hivyo watu wengi ambao wana historia ya ugonjwa huu kwenye familia zao huamua kuondoa mayai na kizazi wakishamaliza uzazi.
Lakini pia matumizi ya dawa za uzazi wa mpango, kupunguza uzito, mazoezi na kula vizuri hupunguza hatari.

                                                         STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                         0769846183/0653095635

0 maoni:

Chapisha Maoni