data:post.body FAHAMU TATIZO LA KUPATA CHOO NGUMU SANA NA MATIBABU YAKE.(CONSTIPATION) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU TATIZO LA KUPATA CHOO NGUMU SANA NA MATIBABU YAKE.(CONSTIPATION)

constipation ni nini?
Hii ni hali ya kupata choo kubwa chini ya mara tatu kwa wiki, mara nyingi huweza  huambatana na dalili kama kupata choo kigumu sana, maumivu ya tumbo, tumbo kujaa,  au kuchukua mda mrefu sana kupata ukiwa chooni.
                                                       

chanzo ni nini?
sababu mbalimbali zinaweza kuchangia mtu kupata hali hii kama ifuatavyo.
chakula; kutokunywa maji ya kutosha na kutokula vyakula vyenye nyuzi nyuzi ni moja ya vyanzo vikuu vya tatizo hili, vyakula vyenye nyuzi nyuzi au fibre hufanya kazi ya kulainisha choo na kukifanya kisafiri kirahisi.
vyakula hivi ni kama mboga za majani, matunda kama maembe, papai, machungwa, machenza na kadhalika.
dawa; dawa nyingi sana zinasababisha mtu kupata choo ngumu, hivyo kama unapata choo ngumu huku unatumia dawa fulani ni vizuri kufuatilia ili kujua moja ya madhara yake,  dawa za maumivu, dawa za msongo wa mawazo, dawa za presha, dawa za kuzuia kuharisha, dawa za moyo na kadhalika.
kuzuia choo; ukijisikia kwenda chooni afu ukapuuzia kwa uvivu au kukosa sehemu ya kujisaidia basi choo kile kinaendelea kupungua maji kikiwa bado kwenye utumbo na siku ukipata muda wa kwenda chooni utakuta choo ni kigumu sana.
magonjwa; baadhi ya magonjwa huja na na asilia ya kusababisha choo ngumu, magonjwa ya utumbo mkubwa, kisukari, magonjwa ya figo na magonjwa ya mishipa ya fahamu huweza kusababisha mgonjwa kupata matatizo ya kupata choo.
magonjwa ya kuzaliwa nayo; kama mtoto mdogo akizaliwa akawa hapati choo basi kuna magonjwa ambayo yanapelekea hali hii, magonjwa hayo ni kama kuziba kwa sehemu ya haja kubwa kitaalamu kama impaforate anus na magonjwa ya mishipa ya fahamu ya utumbo mkubwa.

vipimo vinavyofanyika.
mara nyingi dakatari anaweza kuufahamu ugonjwa kwa maelezo utakayotoa tu lakini kama hupati choo kabisa vipimo kama x ray na colonoscopy hufanyika ili kuona chanzo cha kuziba kabisa kwa njia ya haja kubwa.

matibabu
matibabu ya hali hii mara nyingi hutegemea chanzo husika kama ifuatavyo.
kula vyakula sahihi; kama milivyoeleza hapo kwenye chanzo cha ugonjwa huu basi mgonjwa anatakiwa afuate mlo sahihi wa vyakula vya nyuzi nyuzi na maji mengi kupunguza tatizo hili.
dawa; baadhi ya dawa hutolewa kwa wagonjwa wa hali hii ili kuondoa dalili haraka, dawa hizo ni kama ducolax, lactulose na lubiprostone.
ukitumia dawa hizi ni vizuri ukakaa nyumbani kwani huweza kusababisha kuharisha.
enema; hii ni aina ya matibabu ambayo yanafanyika hospitali ambapo choo kilichokakamaa ndani ya tumbo huondolewa kwa kutumia vifaa maalumu, kiswahili wanaita kuinika.
upasuaji; lkiwa wagonjwa ambao hawapati choo sababu ya utumbo kujikunja tumboni kitaalamu kama intestinal obstruction basi upasuaji hufanyika ili kuuweka utumbo huo sawa, hali hii huambatana na kuvimba tumbo na kutapika sana,

madhara; 
madhara makubwa ya hali hii ni kupata bawasiri, michubuko ya sehemu ya haja kubwa na kudondoka kwa puru kitaalamu kama rectal prolapse.

                                                                           STAY ALIVE
                                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                             0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni