data:post.body FAHAMU RANGI 6 ZA UCHAFU WA SEHEMU ZA SIRI NA TAFSIRI YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU RANGI 6 ZA UCHAFU WA SEHEMU ZA SIRI NA TAFSIRI YAKE.

Uke wa mwanamke sio mkavu, kuna maji maji ambayo yanatoka kila siku kuulainisha na kuulinda na mashambulizi ya magonjwa mbalimbali.
                                                                 

Sasa majimaji haya ukeni yani rangi mbalimbali ambazo zinakufanya wewe uweze kujua kama ni salama au sio salama kama ifuatavyo.
rangi ya maji; hii hutoka mara kwa mara sana kwa wanawake, rangi hii ni kawaida kabisa ambayo hutoka kufanya usafi, pia inaweza kutoka mwanamke akiwa kwenye siku zake za hatari, kipindi cha ujauzito au kukiwa kuna tatizo la homoni.
lakini kukiwa kuna tatizo la homoni kitaalamu kama hormonal imbalance maji haya huja na dalili zingine kama kukosa hedhi na kadhalika.

rangi ya kijivu; haya majimaji hutoka mwanamke anapokua ameshambuliwa na ugonjwa wa bacteria kitaalamu kama bacteria vaginosis, huambatana na dalili ya harufu kama kali ya samaki, kuwashwa sehemu za siri na maumivu wakati wa kukojoa.
kutokwa na majimaji haya huhitaji matibabu.

rangi nyeupe; uchafu wa rangi nyeupe kwenye uke unaweza usiwe dalili ya ugonjwa wowote ni kawaida kabisa kupata, lakini wakati mwingine majimaji meupe ni dalili za za fangasi lakini huambatana na kuwashwa sana sehemu za siri.

kijani na njano;  mara nyingi uchafu huu ni dalili ya magonjwa ya zinaa kama kisonono na trichomona, uchafu huu mara nyingi huabatana na harufu kali sana na maumivu wakati wa kukojoa na mgonjwa anahitaji matibabu kwani huweza kuleta ugumba siku za usoni.
                                                     
     
rangi ya pink; mara nyingi pink hua ni damu ambayo inatoka kidogo baada ya mimba kupadikizwa kwenye ukuta wa uzazi na  inaweza kua ni damu inayotoka kwenye mlango wa uzazi.
                             
rangi nyekundu; mara nyingi hii hua ni damu, inaweza kua damu ya hedhi, damu kutokana na ugonjwa kwenye mlango wa uzazi hasa bacteria,  saratani ya kizazi au mlango wa uzazi.
damu ya saratani ya mlango wa uzazi mara nyingi hutoka wakati wa tendo la ndoa.

mwisho; ni vizuri kuchukua hatua na kwenda hospitali pale unapoona majimaji au uchafu ambao hujawahi kuuona kwenye uke wako, kujitibu mwenyewe mara nyingi huchelewesha matibabu ya kweli na kufanya ugonjwa uwe mkubwa zaidi.

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                        0769846183/0653095635

0 maoni:

Chapisha Maoni