data:post.body FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA UGONJWA WA MAWE YA FIGO.(KIDNEY STONES) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA UGONJWA WA MAWE YA FIGO.(KIDNEY STONES)

Mawe ya figo ni nini?
Hivi ni vitu vigumu kama mawe ambavyo vinatengenezwa na madini mbalimbali yanayopatikana mwilini na kujihifadhi kwenye figo.
madini haya yanaweza kua ya kashiamu, uric acid, struviate na cystine.
                                 
chanzo cha mawe ya figo.
Hakuna chanzo cha moja kwa moja cha mawe ya figo kinachofahamika lakini sababu mbalimbali zinaweza kuchangia kuwepo kwa mawe haya.
mawe ya figo mara nyingi hutokea pale ambapo madini niliyotaja hapo juu yanakua mengi kwenye mkojo kuliko kiasi cha maji ambacho kinatakiwa kuyayeyusha madini hayo, wakati huo huo njia ya mkojo inaweza kukosa vitu ambavyo kibailojia hufanya kazi ya kuondoa  madini hayo.

mambo ambayo yanaweza kuchangia kutokea kwa mawe ya figo.
familia; kama kuna ndugu yako ambaye ana mawe ya figo basi hata wewe uko kwenye hatari ya kuugua ugonjwa huu, na kama ushapata jiwe moja la figo ukatibiwa basi uwezekano wa kuendelea kupata mengine ni mkubwa sana.
kuishiwa na maji mwilini; kutokunywa maji ya kutosha kunaweza kuchangia sana mtu kupata tatizo hili la mawe ya figo, watu ambao wanaishi maeneo ya joto sana na watu ambao wanatokwa sana na jasho wako kwenye hatari sana ya kuugua ugonjwa huu.
baadhi ya vyakula; kula sana vyakula vya protini kama nyama, samaki, karanga, korosho huchaagia kupata mawe ya figo, lakini pia vyakula vyenye sukari na chumvi nyingi ni moja ya vihatarishi vya mawe ya figo.
kua mnene; uzito uliopitiliza, kiuno kikubwa na kitambi ni moja ya sababu zinazoweza kukupelekea kuugua ugonjwa huu wa mawe ya kwenye figo.
magonjwa ya tumbo;  baadhi ya magonjwa ya tumbo yanaweza kuzuia uwezo wa tumbo kumeng'enya madini ya kashiumu yanapofika tumboni na kuyafanya madini hayo yaende moja kwa moja kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa, hii inaweza kupelekea kutengenezwa kwa mawe hayo.
mfano wa magonjwa hayo ni kuharisha sana, na baadhi ya upasuaji wa kuondoa sehemu ya tumbo.
magonjwa mengine; magonjwa mengine kama ya figo, baadhi ya dawa na magonjwa ya njia ya mkojo huweza kupelekea mtu kupata mawe ya figo.

dalili ya mawe ya figo.
 • maumivu wakati wakukojoa.
 • maumivu yanyobadilika ukali.
 • maumivu mgongoni na chini ya mbavu.
 • maumivu tumbo la chini na sehemu za siri.
 • mkojo mwekundu.
 • mkojo unaotoa harufu kali.
 • kichefuchefu na kutapika.
 • kukojoa mara kwa mara.
 • kukojia mkojo mdogo sana.
*maumivu ya mawe ya figo huweza kuhama hama kutokana na mawe ya figo yenyewe kuhama ovyo kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

vipimo vinavyofanyika kwa wagonjwa hawa.
 • vipimo vya damu; vipimo vya damu huweza kuonyesha kiasi kikubwa sana cha madini ya kashiamu na uric acid.
 • vipimo vya mkojo; hivi huweza kuonyesha kwamba mkojo wako unatoa madini mengi sana ambayo yanatengeneza mawe.
 • vipimo vya picha:vipimo vya utrasound, ct scan, xray na mri huweza kutumika kugundua mawe ya aina mbalimbali ambayo yanatokea kwenye figo.
Matibabu ya mawe ya figo.
mawe madogo: Haya yanaweza kutibiwa kwa kunywa maji mengi angalau lita tatu kwa siku na kutumia dawa za maumivu ili kupunguza uchungu wakati mawe hayo yanatoka.

mawe makubwa; kuna njia mbali mbali za kuondoa mawe makubwa lakini njia ya uhakika ni upasuaji ambapo mgonjwa hupewa dawa ya usingizi na  mawe kuondolewa.

jinsi ya kujizuia na ugonjwa huu.
kunywa maji mengi angalau lita tatu kwa siku, kula chakula chenye chumvi kidogo, punguza vyakula ambavyo vina mahusiano na kuugua ugonjwa huu kama bamia, spinachi, viazo vitamu, karanga, chai, chocolate na bidhaa za soya.

                                                                                STAY ALIVE

                                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                      0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni