data:post.body SABABU NNE KWANINI UPUNGUZE KULA VYAKULA VILIVYOKUFA NA KULA VYAKULA HAI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

SABABU NNE KWANINI UPUNGUZE KULA VYAKULA VILIVYOKUFA NA KULA VYAKULA HAI.

Historia ya dunia kwenye Biblia  inaonyesha kwamba kabla ya gharika ya nuhu watu waliishi miaka mingi sana sababu Mungu aliwakataza kula vyakula ambavyo sio hai na kuwaelekeza kula vyakula hai ambavyo vilikua na uhai ndani yake.

Kitabu cha mwanzo kinaonyesha kwamba Adam aliishi miaka 930  lakini baada ya gharika na vyakula mfu viliporuhusiwa umri wa kuishi ulipungua mpaka miaka 75.

vyakula hai ni vipi?
kitaalamu vyakula hai ni vile ambavyo vinaweza kuota tena kama vikirudishwa shambani, uwezo ule wa kuchepua na kuota tena ndio unaonyesha kwamba vyakula vile vina uhai ndani yake.
mfano wa vyakula hivyo ni matunda kama machungwa, matango, machenza, maparachichi, passion, mapapai, zabibu na mengine mengi unayojua, vingine ni mboga za majani na mboga kama mchicha, kisamvu, matembele, karoti, pilipili, bamia, nyanya chungu na kadhalika, vyakula vya jamii ya mizizi kama viazi, mihogo, karanga, na kadhalika.

Vyakula hivi kemikali au enzymes ambazo zinatakiwa mwili mzima ile kufanya uweze kua hai, ukosefu wa enzymes hizi ni hatari kwa afya yako na huporomosha kinga ya mwili kwa kiasi kikubwa.
Kumbuka kwamba vyakula hivi vinapaswa kuliwa katika hali ya ubichi au moto mdogo sana  ndio kipindi ambapo viko hai.

vyakula vilivyokufa ni vipi?
hivi ni vyakula ambavyo haviwezi kurudi shambani na kuota au vilikua na uwezo wa kuota lakini vimepikwa hivyo havina uwezo tena wa kuota shambani, mfano wa vyakula hivyo ni nyama, dagaa,  samaki, kuku, chips, mayai, viazi vilivyopikwa, sukari, soda, pombe, mihogo iliyopikwa, mikate, keki, maandazi, chapati, wali, ugali na kadhalika.
sio kwamba vyakula hivi vinatakiwa vitupwe,  hapana lakini ni vyakula vilivyokufa na vinatakiwa viliwe kwa kiasi kidogo sana.

ukichunguza vyakula vyote hivyo ndio vyakula vinavyoleta magonjwa sana kwa binadamu na kukatazwa sana kuliwa.
magonjwa kama ya moyo, kisukari, presha na saratani husababishwa sana na kula vyakula vilivyokufa.

nini faida ya kula vyakula hai?
Hupunguza unene; vyakula hai kama nilivotaja hapo huu hutumika sana na wataalamu wa lishe kuwasaidia watu ambao ni wanene sana wapungue uzito.
vyakula hivyo vina calories au nguvu kidogo na hufaa sana kwa kazi hiyo lakini pia vina enzymes nyingi ambazo ni muhimu katika kumeng'enya chakula haraka sana tumboni.
Huzuia magonjwa; vyakula hai huzuia magonjwa ambayo sio ya kuambukiza ambayo kwa sasa ndio yanaua watu wengi zaidi duniani.
matunda yana vitamini ambazo kitalaamu zinaitwa antoxidant, vitamin C na vitamin E ambazo hupambana sana na magonjwa ya saratani, presha na kuzuia magonjwa ya moyo.
mfano ukosefu wa enzyme kwa jina la lipase husababisha magonjwa ya figo, mifupa, kidole tumbo na saratani.
tiba ya magonjwa; vyakula hai vingi kama matunda hutumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali ambayo yanakua yameanza kushambulia mwili.
magonjwa kama kutokwa damu za kwenye fidhi, kuishiwa damu, kisukari, magonjwa ya moyo na saratani huweza kutibiwa au kudhibitiwa na vyakula hai.
ulaji wa vyakula vilivyokufa hupunguza kasi ya kumeng'enya chakula, choo ngumu sana na kuzua magonjwa mapya ambayo sio ya kuambukiza.
urefu wa maisha; kama nilivyoelezea kidogo kwenye historia yangu fupi ya kibiblia, vyakula hivi vina uhai na vitakuzuia wewe na magonjwa mengi sana na kukufanya uishi maisha marefu na yenye furaha bila kuugua magonjwa yeyote.
mwisho; Nawashauri wasomaji wote wa makala hii kuanza kula angalau 30% ya vyakula hai kila siku yaani bila kupitisha siku hata moja bila kula vyakula hai na wataona mabadiliko makubwa sana ya afya zao ndani ya kipindi cha muda mfupi sana.

                                                                STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0769846183/0653095635

0 maoni:

Chapisha Maoni