data:post.body FAHAMU UGONJWA WA VIDONDA VYA HOMA NA MATIBABU YAKE.(COLD SORE) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU UGONJWA WA VIDONDA VYA HOMA NA MATIBABU YAKE.(COLD SORE)

Vidonda vya homa ni vipi?
Hivi ni vipele vidogo vidogo vinavyotekea kwenye lips za mdomo kabla havijapasuka na kuleta vidonda mdomoni.
Watu wengi huviita vidonda vya homa sababu huwatokea watu baada ya kuugua homa za aina  mbalimbali lakini kitaalamu mtu anaweza kupata vipele hivi hata kama hajaugua homa.
                                                                 
chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa huu husababishwa na aina fulani ya virusi kitaalamu kama HPV-1 ambavyo huweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine lakini pia aina nyingine ya virusi kwa jina la HPV-2 huweza kusababisha ugonjwa huu.

ugonjwa huu unasambaa vipi?
kuna njia mbalimbali ugonjwa huu unaweza kusambaa kama ifuatavyo..

 • kubusu na mgonjwa mdomoni.
 • kuchangia vitu kama glass ya maji, taulo au urembo wowote wa kupaka mdomoni.
 • kulamba sehemu za siri zenye virusi hivi.


jinsi ya kugundua ugonjwa
Daktari hahitaji vipimo vyovyote kugundua ugonjwa huu, bali anaweza kuutambua kwa kuangalia kwa macho tu.

matibabu;
ugonjwa huu hautibiki ila unapona wenyewe ndani ya wiki moja mpaka wiki tatu lakini virusi hawafi, virusi vile vitabaki kwenye mwili wako vimejificha na siku ikitokea umepata homa, kinga yako imeshuka au msongo mkubwa wa mawazo basi virusi hawa watashambulia tena.
Wanawake wana hatari ya kupata vidonda hivi kabla na baada ya kuanza kwa siku zao za mwezi.
wakati mwingine ugonjwa hushambulia na kutoa vidonda vingi sana, dawa ya acyclovir huweza kutumika kupaka au kumeza mara tano kwa siku kupunguza makali hasa ikitumika siku ya kwanza kabisa ya ugonjwa huu.

jinsi ya kuzuia
kuzuia njia za ugonjwa kusambaa kwa njia rahisi zaidi...

 • usimbusu mgonjwa mwenye shida hii.
 • usichangie nae vitu vya mate kama glass, soda, au vitu vya kujifuta kama taulo na leso.
 • usikae kwenye jua kali.
 • usilambe sehemu za siri za mtu ambaye hujui kuhusu afya yake.
Baadhi ya watu hupata shida hii mara kwa mara sana hivyo ni vizuri kujua chanzo chako kinachofanya virusi hawa waamke na kushambulia mara kwa mara na kujiuzuia.

Kupata makala zetu mara kwa mara bonyeza kupakua au kudownload application yetu au nenda playstore andika "siri za afya bora" kupata application hiyo.

                                                                     STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0769846183/0653095635  

Maoni 2 :

 1. Asante. Kila mm naomba mnambie Nina hizo dalilibila mm mdomo unavimba sana

  JibuFuta
 2. Hata Mimi Mimi pona tu homa yeyote razima vinitokee ninakelekwa sana jamani

  JibuFuta