data:post.body FAHAMU TATIZO UPUNGUFU AU ONGEZEKO LA HOMONI KWA WANAWAKE.(HORMONAL IMBALANCE) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU TATIZO UPUNGUFU AU ONGEZEKO LA HOMONI KWA WANAWAKE.(HORMONAL IMBALANCE)

homoni ni nini? 
Hizi ni kemikali ambazo zinatengenezwa na mwili wa binadamu kwa ajili ya kutoa amri ndani ya mwili kitu gani kifanyike na wakati gani kifanyike.
                                                             

homoni hizi zinahusika kufanya mambo mengi sana ya mwili kama uzazi, kujifungua, kupata hedhi, mapigo ya moyo, hamu ya kula, joto la mwili, ukuaji, usingizi, kumeng'enya chakula na kadhalika.

Hormonal imbalance ni nini?
Hili ni tatizo la homoni ambalo linatokea pale kiasi cha homoni zinapokua nyingi sana au kidogo sana, tatizo hili huweza kutokea kwa jinsia zote lakini waathirika wakubwa ni wanawake hivyo tutawazungumzia wao zaidi.
Mabadiliko hayo ya homoni yanaweza kuleta madhara mbalimbali kwenye mwili wa mwanamke kutokana na umuhimu mkubwa sana wa homoni hizo kwenye mwili wa mwanamke.
Wanawake wengi wanaathirika sana shida ya homoni za oestrogen na progesterone wakati wanaume wanaathirika na homoni za testosterone.
wanawake wanapata sana shida hii kipindi cha ujauzito, hedhi, kubalehe, na kipindi wanapofikia umri wa kushindwa kuona hedhi zao(menopause).

chanzo cha tatizo hili ni nini?
kuna vyanzo vingi vya matatizo ya homoni kama msongo mkubwa wa mawazo, lishe duni au lishe aisiyo sahihi, uzito mdogo, uzito uliopitiliza, saratani za sehemu za uzazi, magonjwa ya vizalishaji vya mayai mfano polycystic ovarian syndrome,  magonjwa ya kizazikwa ujumla, mwisho wa hedhi(menopause)  na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.

dalili za tatizo hili ni zipi?
dalili zipo nyingi na mara nyingi hutegemea chanzo husika cha tatizo lako na sio lazima upate dalili zote, kama ifuatavyo.
 • maumivu makali na damu nyingi siku ya hedhi.
 • kukosa hedhi.
 • mifupa laini na inayovunjika
 • kusikia upepo wa joto na kutokwa jasho usiku.(hot flashes)
 • uke mkavu.
 • maumivu ya chuchu.
 • choo ngumu na kuharisha wakati mwingine.
 • chunusi kabla au kipindi cha hedhi.
 • kutokwa na damu siku ambazo sio za hedhi.
 • nywele nyingi kuota kifuani, uso, kifua na mgongo.
 • kunenepa.
 • kushindwa kushika mimba.
 • sauti nzito.
 • kuongezeka kwa ukubwa wa kinembe.
 • kukosa hamu ya tendo la ndoa.
 • Kuchoka sana.
 • kusahau sana
 • kubadilika kwa hisia mara kwa mara.
 • wasiwasi
vipimo vinavyofanyika ni vipi?

 • kipimo cha hormonal assay huweza kufanyika ili kuhakiki kama kweli kuna shida ya homoni kabla ya matibabu.
matibabu ambayo hufanyika.

Matibabu mbalimbali hufanyika kutokana na chanzo cha ugonjwa husika, kama ifuatavyo.
dawa za uzazi wa mpango; kwa watu ambao hawana mpango wa kubeba mimba kwa kipindi hicho wanaweza kutumia dawa hizi ili kujaribu kuweka homoni sawa, inaweza kua vidonge, kijiti, kitanzi na kadhalika.
vagina oestrogen; hizi dawa hutumika moja kwa moja na watu ambao wana uke mkavu kwa kuchomeka ndani ya uke ili uweze kulainika.
clomiphene; dawa hizi hutumika kusaidia kushusha mayai kwa watu ambao wana matatizo ya kubeba mimba lakini zinaweza kusababisha mayai mengi kushuka na kuleta mapacha.
hormonal replacement therapy; dawa hizi hutumiaka na watu amabo umri umeenda na hawaoni hedhi tena, huwasaidia kuweka homoni sawa na wao kupata nafuu.
antri-androgen medication; hizi dawa hutolewa kwa kuzuia kutengenezwa kwa homoni za kiume ndani ya mwili wa mwanamke.

matibabu asilia;
kwa miaka mingi dawa asilia zimekua zikitumika kutibu tatizo hili la homoni, mfano wa dawa hizo ni black cohosh, ginseng,  na maca.

mambo mengine ya kuzingatia nje ya matumizi ya dawa na za hospitali na asilia.
 • hakikisha uko kwenye uzito sahihi kulingana na urefu wako.
 • fanya mazoezi mara kwa mara.
 • kula vyakula vya kiafya.
 • punguza msongo wa mawazo.
 • acha vyakula vya sukari na wanga ambao sio asili kitaalamu kama refined cabohydrates kama mikake, maandazi, keki na kadhalika.
 • epuka vyakula vya makopo.
 • usile vyakula kwenye plastic au microwave
 • epuka mboga za majani ambazo zimepuliziwa kemikali shambani.
 • epuka mafuta ya nywele au ngozi yenye kemilali nyingi za kuchububua au kuweka dawa kwenye nywele.
 • jithidi kuishi kiasili kwa uwezo wako wote.              

                                                                        STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni