data:post.body FAHAMU SABABU 7 ZINAZOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUCHELEWA KUPATA MIMBA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU SABABU 7 ZINAZOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUCHELEWA KUPATA MIMBA.

Sio kila mwanamke ambaye hapati mimba ni mgumba, wengine hawana shida kabisa ila kuna sababu fulani fulani ambazo zinawafanya wasipate mimba.
Sasa ukipuuzia vitu kama hivi unaweza ukawa unaenda hospitali zote unaambiwa hauna shida lakini bado haupati mimba.
                                                           
Kama mwanamke ambaye unategemea kupata mimba siku za usoni au unasumbukiwa na mambo ya uzazi kwa sasa basi mambo haya unatakiwa uyazingatie sana.
umri: uwezo wa mwanamke kubeba mimba unapungua wenyewe anapofikisha miaka 35, hii ni kwasababu ya kupungua sana kwa ubora wa mayai yanayotolewa, sio kwamba hawezi kubeba mimba kabisa lakini mimba hazishiki kirahisi kama alivyokua na umri chini ya miaka 35.

uvutaji wa sigara; sigara inaharibu kwa kiasi kikubwa sana ubora wa mayai ya kike lakini pia huweza kusababisha mimba itungwe nje ya kizazi, sigara pia huharibu mbegu za kiume na kuzifanya kutokua na uwezo kama mwanzo.

ukubwa wa mwili; kuna mahusiano makubwa sana kati ya ukubwa wa mwili na uwezo wa kubeba mimba, wanawake wembamba sana na wanene sana wanapata shida sana kupata mimba sababu ya matatizo ya homoni, watu hawa hata kuona siku zao za mwezi hua ni shida sana,

tendo la ndoa; ili kujihakikishia kupata mimba, mwanamke anatakiwa akkutane na mwanaume angalau mara tatu kwa wiki au zaidi..
Hali ya kushiriki tendo mara moja moja hupunguza uwezekano wa kukutana na siku za hatari za kubeba mimba.
unywaji mkubwa wa pombe; ulevi wa kupindukia huathiri sana uwezo wa mbegu za kiume, lakini pia mwanamke ambaye ameshabeba mimba tayari akiwa mlevi basi huharibu mtoto ambaye yuko tumboni na kusababisha mimba kuharibika.
Ni vizuri mama kuacha pombe kabisa kipindi anatafuta mtoto na baba kupunguza pombe au kuacha kabisa.
dawa; kuna dawa nyingi sana ambazo zinapatikana kwenye maduka ya dawa mitaani lakini matumizi yake ni hatari kwa wanawake ambao wategemea au wanahitaji mimba.
mfano; dawa za maumivu jamii ya NSAID kama aspirin, diclofenac, ibuprofen, meloxicam, peroxicam, na diclopa huzuia yai kushuka.
dawa za kutibu saratani litaalamu kama chemotherapy huzuia ukuaji wa kijusi baada ya mbegu ya kiume na yai la mama kukutana.
Dawa za jamii ya sulpher, cimetidine na adrogens huharibu ubora wa mbegu za mwanaume.

mazingira; ni muhimu kua makini sana na mazingira ya kuishi na kazi tunazofanya, watu wanaofanya kazi za viwandani wako kwenye hatari sana ya kutana na mionzi ambayo huathiri uwezo wa mbegu zao na mayai yao.

mwisho; kama wewe ni mwanaume unatarajia kumpa mwanamke mimba au wewe ni mwanamke unategemea kupata mimba basi ni vizuri kua makini sana na mambo tajwa hapo juu.

pakua au download bure application yetu ya sizi za afya bora kwa kubonyeza link hii, ili kupata makala zetu kila wiki kwa ajili ya afya yako na familia yako  https://play.google.com/store/apps/details?id=com.siri.za.afya.bora&fbclid=IwAR3OdjOUd8sdoIWoV1YhNjS79rKobNtzGSX_K_JkL0W30ZlW6Ik-CjvefFk

                                                                         STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                               0653095635/0769846183

Maoni 2 :

 1. Hongera kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii

  JibuFuta
 2. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
  * upendo
  inaelezea * inaelezea kivutio
  * kama unataka ex wako nyuma
  *acha talaka
  * kuvunja obsessions
  * huponya viharusi na magonjwa yote
  * uchawi wa kinga
  *Ugumba na matatizo ya ujauzito
  * bahati nasibu
  * uchawi wa bahati
  Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
  Whatsapp:+2349046229159

  JibuFuta