data:post.body Mei 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

SABABU NNE KWANINI UPUNGUZE KULA VYAKULA VILIVYOKUFA NA KULA VYAKULA HAI.

Historia ya dunia kwenye Biblia  inaonyesha kwamba kabla ya gharika ya nuhu watu waliishi miaka mingi sana sababu Mungu aliwakataza kula vyakula ambavyo sio hai na kuwaelekeza kula vyakula hai ambavyo vilikua na uhai ndani yake.

Kitabu cha mwanzo kinaonyesha kwamba Adam aliishi miaka 930  lakini baada ya gharika na vyakula mfu viliporuhusiwa umri wa kuishi ulipungua mpaka miaka 75.

vyakula hai ni vipi?
kitaalamu vyakula hai ni vile ambavyo vinaweza kuota tena kama vikirudishwa shambani, uwezo ule wa kuchepua na kuota tena ndio unaonyesha kwamba vyakula vile vina uhai ndani yake.
mfano wa vyakula hivyo ni matunda kama machungwa, matango, machenza, maparachichi, passion, mapapai, zabibu na mengine mengi unayojua, vingine ni mboga za majani na mboga kama mchicha, kisamvu, matembele, karoti, pilipili, bamia, nyanya chungu na kadhalika, vyakula vya jamii ya mizizi kama viazi, mihogo, karanga, na kadhalika.

Vyakula hivi kemikali au enzymes ambazo zinatakiwa mwili mzima ile kufanya uweze kua hai, ukosefu wa enzymes hizi ni hatari kwa afya yako na huporomosha kinga ya mwili kwa kiasi kikubwa.
Kumbuka kwamba vyakula hivi vinapaswa kuliwa katika hali ya ubichi au moto mdogo sana  ndio kipindi ambapo viko hai.

vyakula vilivyokufa ni vipi?
hivi ni vyakula ambavyo haviwezi kurudi shambani na kuota au vilikua na uwezo wa kuota lakini vimepikwa hivyo havina uwezo tena wa kuota shambani, mfano wa vyakula hivyo ni nyama, dagaa,  samaki, kuku, chips, mayai, viazi vilivyopikwa, sukari, soda, pombe, mihogo iliyopikwa, mikate, keki, maandazi, chapati, wali, ugali na kadhalika.
sio kwamba vyakula hivi vinatakiwa vitupwe,  hapana lakini ni vyakula vilivyokufa na vinatakiwa viliwe kwa kiasi kidogo sana.

ukichunguza vyakula vyote hivyo ndio vyakula vinavyoleta magonjwa sana kwa binadamu na kukatazwa sana kuliwa.
magonjwa kama ya moyo, kisukari, presha na saratani husababishwa sana na kula vyakula vilivyokufa.

nini faida ya kula vyakula hai?
Hupunguza unene; vyakula hai kama nilivotaja hapo huu hutumika sana na wataalamu wa lishe kuwasaidia watu ambao ni wanene sana wapungue uzito.
vyakula hivyo vina calories au nguvu kidogo na hufaa sana kwa kazi hiyo lakini pia vina enzymes nyingi ambazo ni muhimu katika kumeng'enya chakula haraka sana tumboni.
Huzuia magonjwa; vyakula hai huzuia magonjwa ambayo sio ya kuambukiza ambayo kwa sasa ndio yanaua watu wengi zaidi duniani.
matunda yana vitamini ambazo kitalaamu zinaitwa antoxidant, vitamin C na vitamin E ambazo hupambana sana na magonjwa ya saratani, presha na kuzuia magonjwa ya moyo.
mfano ukosefu wa enzyme kwa jina la lipase husababisha magonjwa ya figo, mifupa, kidole tumbo na saratani.
tiba ya magonjwa; vyakula hai vingi kama matunda hutumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali ambayo yanakua yameanza kushambulia mwili.
magonjwa kama kutokwa damu za kwenye fidhi, kuishiwa damu, kisukari, magonjwa ya moyo na saratani huweza kutibiwa au kudhibitiwa na vyakula hai.
ulaji wa vyakula vilivyokufa hupunguza kasi ya kumeng'enya chakula, choo ngumu sana na kuzua magonjwa mapya ambayo sio ya kuambukiza.
urefu wa maisha; kama nilivyoelezea kidogo kwenye historia yangu fupi ya kibiblia, vyakula hivi vina uhai na vitakuzuia wewe na magonjwa mengi sana na kukufanya uishi maisha marefu na yenye furaha bila kuugua magonjwa yeyote.
mwisho; Nawashauri wasomaji wote wa makala hii kuanza kula angalau 30% ya vyakula hai kila siku yaani bila kupitisha siku hata moja bila kula vyakula hai na wataona mabadiliko makubwa sana ya afya zao ndani ya kipindi cha muda mfupi sana.

                                                                STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0769846183/0653095635

FAHAMU UGONJWA WA VIDONDA VYA HOMA NA MATIBABU YAKE.(COLD SORE)

Vidonda vya homa ni vipi?
Hivi ni vipele vidogo vidogo vinavyotekea kwenye lips za mdomo kabla havijapasuka na kuleta vidonda mdomoni.
Watu wengi huviita vidonda vya homa sababu huwatokea watu baada ya kuugua homa za aina  mbalimbali lakini kitaalamu mtu anaweza kupata vipele hivi hata kama hajaugua homa.
                                                                 
chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa huu husababishwa na aina fulani ya virusi kitaalamu kama HPV-1 ambavyo huweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine lakini pia aina nyingine ya virusi kwa jina la HPV-2 huweza kusababisha ugonjwa huu.

ugonjwa huu unasambaa vipi?
kuna njia mbalimbali ugonjwa huu unaweza kusambaa kama ifuatavyo..

 • kubusu na mgonjwa mdomoni.
 • kuchangia vitu kama glass ya maji, taulo au urembo wowote wa kupaka mdomoni.
 • kulamba sehemu za siri zenye virusi hivi.


jinsi ya kugundua ugonjwa
Daktari hahitaji vipimo vyovyote kugundua ugonjwa huu, bali anaweza kuutambua kwa kuangalia kwa macho tu.

matibabu;
ugonjwa huu hautibiki ila unapona wenyewe ndani ya wiki moja mpaka wiki tatu lakini virusi hawafi, virusi vile vitabaki kwenye mwili wako vimejificha na siku ikitokea umepata homa, kinga yako imeshuka au msongo mkubwa wa mawazo basi virusi hawa watashambulia tena.
Wanawake wana hatari ya kupata vidonda hivi kabla na baada ya kuanza kwa siku zao za mwezi.
wakati mwingine ugonjwa hushambulia na kutoa vidonda vingi sana, dawa ya acyclovir huweza kutumika kupaka au kumeza mara tano kwa siku kupunguza makali hasa ikitumika siku ya kwanza kabisa ya ugonjwa huu.

jinsi ya kuzuia
kuzuia njia za ugonjwa kusambaa kwa njia rahisi zaidi...

 • usimbusu mgonjwa mwenye shida hii.
 • usichangie nae vitu vya mate kama glass, soda, au vitu vya kujifuta kama taulo na leso.
 • usikae kwenye jua kali.
 • usilambe sehemu za siri za mtu ambaye hujui kuhusu afya yake.
Baadhi ya watu hupata shida hii mara kwa mara sana hivyo ni vizuri kujua chanzo chako kinachofanya virusi hawa waamke na kushambulia mara kwa mara na kujiuzuia.

Kupata makala zetu mara kwa mara bonyeza kupakua au kudownload application yetu au nenda playstore andika "siri za afya bora" kupata application hiyo.

                                                                     STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0769846183/0653095635  

FAHAMU TATIZO UPUNGUFU AU ONGEZEKO LA HOMONI KWA WANAWAKE.(HORMONAL IMBALANCE)

homoni ni nini? 
Hizi ni kemikali ambazo zinatengenezwa na mwili wa binadamu kwa ajili ya kutoa amri ndani ya mwili kitu gani kifanyike na wakati gani kifanyike.
                                                             

homoni hizi zinahusika kufanya mambo mengi sana ya mwili kama uzazi, kujifungua, kupata hedhi, mapigo ya moyo, hamu ya kula, joto la mwili, ukuaji, usingizi, kumeng'enya chakula na kadhalika.

Hormonal imbalance ni nini?
Hili ni tatizo la homoni ambalo linatokea pale kiasi cha homoni zinapokua nyingi sana au kidogo sana, tatizo hili huweza kutokea kwa jinsia zote lakini waathirika wakubwa ni wanawake hivyo tutawazungumzia wao zaidi.
Mabadiliko hayo ya homoni yanaweza kuleta madhara mbalimbali kwenye mwili wa mwanamke kutokana na umuhimu mkubwa sana wa homoni hizo kwenye mwili wa mwanamke.
Wanawake wengi wanaathirika sana shida ya homoni za oestrogen na progesterone wakati wanaume wanaathirika na homoni za testosterone.
wanawake wanapata sana shida hii kipindi cha ujauzito, hedhi, kubalehe, na kipindi wanapofikia umri wa kushindwa kuona hedhi zao(menopause).

chanzo cha tatizo hili ni nini?
kuna vyanzo vingi vya matatizo ya homoni kama msongo mkubwa wa mawazo, lishe duni au lishe aisiyo sahihi, uzito mdogo, uzito uliopitiliza, saratani za sehemu za uzazi, magonjwa ya vizalishaji vya mayai mfano polycystic ovarian syndrome,  magonjwa ya kizazikwa ujumla, mwisho wa hedhi(menopause)  na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.

dalili za tatizo hili ni zipi?
dalili zipo nyingi na mara nyingi hutegemea chanzo husika cha tatizo lako na sio lazima upate dalili zote, kama ifuatavyo.
 • maumivu makali na damu nyingi siku ya hedhi.
 • kukosa hedhi.
 • mifupa laini na inayovunjika
 • kusikia upepo wa joto na kutokwa jasho usiku.(hot flashes)
 • uke mkavu.
 • maumivu ya chuchu.
 • choo ngumu na kuharisha wakati mwingine.
 • chunusi kabla au kipindi cha hedhi.
 • kutokwa na damu siku ambazo sio za hedhi.
 • nywele nyingi kuota kifuani, uso, kifua na mgongo.
 • kunenepa.
 • kushindwa kushika mimba.
 • sauti nzito.
 • kuongezeka kwa ukubwa wa kinembe.
 • kukosa hamu ya tendo la ndoa.
 • Kuchoka sana.
 • kusahau sana
 • kubadilika kwa hisia mara kwa mara.
 • wasiwasi
vipimo vinavyofanyika ni vipi?

 • kipimo cha hormonal assay huweza kufanyika ili kuhakiki kama kweli kuna shida ya homoni kabla ya matibabu.
matibabu ambayo hufanyika.

Matibabu mbalimbali hufanyika kutokana na chanzo cha ugonjwa husika, kama ifuatavyo.
dawa za uzazi wa mpango; kwa watu ambao hawana mpango wa kubeba mimba kwa kipindi hicho wanaweza kutumia dawa hizi ili kujaribu kuweka homoni sawa, inaweza kua vidonge, kijiti, kitanzi na kadhalika.
vagina oestrogen; hizi dawa hutumika moja kwa moja na watu ambao wana uke mkavu kwa kuchomeka ndani ya uke ili uweze kulainika.
clomiphene; dawa hizi hutumika kusaidia kushusha mayai kwa watu ambao wana matatizo ya kubeba mimba lakini zinaweza kusababisha mayai mengi kushuka na kuleta mapacha.
hormonal replacement therapy; dawa hizi hutumiaka na watu amabo umri umeenda na hawaoni hedhi tena, huwasaidia kuweka homoni sawa na wao kupata nafuu.
antri-androgen medication; hizi dawa hutolewa kwa kuzuia kutengenezwa kwa homoni za kiume ndani ya mwili wa mwanamke.

matibabu asilia;
kwa miaka mingi dawa asilia zimekua zikitumika kutibu tatizo hili la homoni, mfano wa dawa hizo ni black cohosh, ginseng,  na maca.

mambo mengine ya kuzingatia nje ya matumizi ya dawa na za hospitali na asilia.
 • hakikisha uko kwenye uzito sahihi kulingana na urefu wako.
 • fanya mazoezi mara kwa mara.
 • kula vyakula vya kiafya.
 • punguza msongo wa mawazo.
 • acha vyakula vya sukari na wanga ambao sio asili kitaalamu kama refined cabohydrates kama mikake, maandazi, keki na kadhalika.
 • epuka vyakula vya makopo.
 • usile vyakula kwenye plastic au microwave
 • epuka mboga za majani ambazo zimepuliziwa kemikali shambani.
 • epuka mafuta ya nywele au ngozi yenye kemilali nyingi za kuchububua au kuweka dawa kwenye nywele.
 • jithidi kuishi kiasili kwa uwezo wako wote.              

                                                                        STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

FAHAMU SABABU 7 ZINAZOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUCHELEWA KUPATA MIMBA.

Sio kila mwanamke ambaye hapati mimba ni mgumba, wengine hawana shida kabisa ila kuna sababu fulani fulani ambazo zinawafanya wasipate mimba.
Sasa ukipuuzia vitu kama hivi unaweza ukawa unaenda hospitali zote unaambiwa hauna shida lakini bado haupati mimba.
                                                           
Kama mwanamke ambaye unategemea kupata mimba siku za usoni au unasumbukiwa na mambo ya uzazi kwa sasa basi mambo haya unatakiwa uyazingatie sana.
umri: uwezo wa mwanamke kubeba mimba unapungua wenyewe anapofikisha miaka 35, hii ni kwasababu ya kupungua sana kwa ubora wa mayai yanayotolewa, sio kwamba hawezi kubeba mimba kabisa lakini mimba hazishiki kirahisi kama alivyokua na umri chini ya miaka 35.

uvutaji wa sigara; sigara inaharibu kwa kiasi kikubwa sana ubora wa mayai ya kike lakini pia huweza kusababisha mimba itungwe nje ya kizazi, sigara pia huharibu mbegu za kiume na kuzifanya kutokua na uwezo kama mwanzo.

ukubwa wa mwili; kuna mahusiano makubwa sana kati ya ukubwa wa mwili na uwezo wa kubeba mimba, wanawake wembamba sana na wanene sana wanapata shida sana kupata mimba sababu ya matatizo ya homoni, watu hawa hata kuona siku zao za mwezi hua ni shida sana,

tendo la ndoa; ili kujihakikishia kupata mimba, mwanamke anatakiwa akkutane na mwanaume angalau mara tatu kwa wiki au zaidi..
Hali ya kushiriki tendo mara moja moja hupunguza uwezekano wa kukutana na siku za hatari za kubeba mimba.
unywaji mkubwa wa pombe; ulevi wa kupindukia huathiri sana uwezo wa mbegu za kiume, lakini pia mwanamke ambaye ameshabeba mimba tayari akiwa mlevi basi huharibu mtoto ambaye yuko tumboni na kusababisha mimba kuharibika.
Ni vizuri mama kuacha pombe kabisa kipindi anatafuta mtoto na baba kupunguza pombe au kuacha kabisa.
dawa; kuna dawa nyingi sana ambazo zinapatikana kwenye maduka ya dawa mitaani lakini matumizi yake ni hatari kwa wanawake ambao wategemea au wanahitaji mimba.
mfano; dawa za maumivu jamii ya NSAID kama aspirin, diclofenac, ibuprofen, meloxicam, peroxicam, na diclopa huzuia yai kushuka.
dawa za kutibu saratani litaalamu kama chemotherapy huzuia ukuaji wa kijusi baada ya mbegu ya kiume na yai la mama kukutana.
Dawa za jamii ya sulpher, cimetidine na adrogens huharibu ubora wa mbegu za mwanaume.

mazingira; ni muhimu kua makini sana na mazingira ya kuishi na kazi tunazofanya, watu wanaofanya kazi za viwandani wako kwenye hatari sana ya kutana na mionzi ambayo huathiri uwezo wa mbegu zao na mayai yao.

mwisho; kama wewe ni mwanaume unatarajia kumpa mwanamke mimba au wewe ni mwanamke unategemea kupata mimba basi ni vizuri kua makini sana na mambo tajwa hapo juu.

pakua au download bure application yetu ya sizi za afya bora kwa kubonyeza link hii, ili kupata makala zetu kila wiki kwa ajili ya afya yako na familia yako  https://play.google.com/store/apps/details?id=com.siri.za.afya.bora&fbclid=IwAR3OdjOUd8sdoIWoV1YhNjS79rKobNtzGSX_K_JkL0W30ZlW6Ik-CjvefFk

                                                                         STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                               0653095635/0769846183

FAHAMU TATIZO LA KIZAZI KUGEUKA NA MATIBABU YAKE.(RETROVERTED UTERUS)

Kwa kawaida zaidi ya 80% ya wanawake wana vizazi ambavyo vimelalia upande mbele yaani kwenye ukuta wa tumbo lakini baadhi ya wanawake wachache vizazi vyao vimelalia nyuma yaani kwa upande wa mgongoni.               
                                                       

Kizazi kugeuka au kulalia mgongo hua sio tatizo kubwa sana wala haliwezi kuzuia mtu kupata mimba japokua linaweza kusababisha dalili mbalimbali kama maumivu wakati wa tendo la ndoa.

kitu gani kinafanya kizazi kinageuka?
hali ya kuzaliwa nayo; kuna wanawake ambao wamezaliwa hivyo wala hakuna tatizo lolote ambalo limetokea kuleta hali hiyo.
makovu(adhehesions); wakati mwingine mwanamke huhitaji upasuaji kutibu magonjwa mbalimbali  au kujifungua sasa baadhi ya wanawake hupata makovu baada ya upasuaji ambayo huweza kupelekea kizazi kukosa nafasi ya kukaa vizuri na kugeuka,
uvimbe wa kizazi; baadhi ya vimbe zinazotokea kwenye kizazi huweza kuingilia ukaaji halisi wa kizazi na kufanya kizazi kigeuke.
Vimbe kama hizo zinaweza kua za saratani au ambazo sio za saratani, mfano fibroids.
endometriosis; huu ni ugonjwa unaosababishwa na seli za ndani ya ukuta wa kizazi kuota sehemu zingine ambazo seli hizo hazikutakiwa kuwepo, seli hizo huwezi kubana kizazi kama gundi na  kukigeuza.
uzazi; kwa kawaida kizazi kinashikwa kwenye sehemu yake na kamba maalumu kitaalamu kama ligament, mwanamke akibeba ujauzito ligament zile zinavutika sana na kushindwa kushika kizazi vizuri.
sasa baada ya kujifungua kizazi kinaweza kurudi kwenye hali yake ya zamani au kisirudi tena na kubaki kimegeuka.

dalili za kizazi kugeuka.
mara nyingi mwanamke hapati dalili yeyote hasa kama amezaliwa hivyo lakini maumivu huweza kutokea wakati wa tendo la ndoa hasa mwanamke akikaa kwa juu wakati wa tendo la ndoa lakini pia mwanamke anaweza kupata maumivu ya tumbo na dalili zingine  kutokana na chanzo husika cha ugonjwa kama nilivyotaja hapo juu.

mahusiano ya ugumba na kizazi kugeuka
kwa kawaida kama mwanake amezaliwa na kizazi kilichogeuka basi hawezi kupata shida ya uzazi lakini kama kizazi kiligeuzwa na matatizo mengine ya uzazi basi kizazi kinaweza kuleta shida ya uzazi japo sio kwa watu wote.

jinsi ya kugundua kama kizazi kimegeuka.
mara nyingi madaktari huweza kugundua kizazi kimegeuka wakati wa uchunguzi wa kawaida au wakati wa vipimo vya picha kitaalamu kama utrasound.

matibabu ya kizazi kilichogeuka;
kuna matibabu aina mbaimbali kama mazoezi, vidonge maalumu kwenye kizazi, na kujaribu kutibu chanzo cha ugonjwa lakini yote hua hayatoi suluhisho la moja kwa moja.
suluhisho la moja kwa moja ni upasuaji tu, ambao huweza kurekebisha kizazi na kukiweka sawa.

                                                                    STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0769846183/0653095635