Kumekua na ongezeko la idadi kubwa ya watu wanaotumia asali kunywa chai kama mbadala wa sukari kwa sababu za kiafya zaidi lakini pia wapo wanaotumia kulamba.
Ni kweli asali ni nzuri kuliko sukari kwasababu ina madini mbalimbali kama potashiamu, sodium, calcium, magnesium, vitamin B, copper na madini ya chuma.
Lakini linapokuja kwenye swala la kupunguza uzito, matumizi ya asali yanahitaji umakini sana kwani unaweza kujikuta unaongezeka zaidi badala ya kupungua kwa sababu zifuatavyo.
wingi mkubwa wa nguvu au calorie; linapokuja swala la kupungua uzito, kiasi cha nguvu au calories zilizopo kwenye chakula ni muhimu sana kwani ndio zinamua kama unapungua au unaongezeka.
kwa kawaida kijiko kimoja cha asali kina nguvu au calories 64, wakati huohuo kijiko kimoja cha sukari kina calories 49.
Hivyo pamoja na kwamba asali ina vitamin nyingi lakini inatoa nguvu nyingi ambayo kimsingi inaongeza uzito zaidi kuliko sukari ya kawaida kwa kipimo kilekile.
utengenezaji mkubwa wa homoni ya insulini; insulini ni homoni inayotumika kuvunja sukari yeyote au chakula chochote cha jamii ya wanga kama wali, ugali, viazi, mihogo, na kadhalika.
sasa ukiwa mtumiaji wa vyakula hivi wanga haijalishi ni asili au sio asili, homoni hii lazima itengenezwe nyingi.
Bahati mbaya ni kwamba moja ya kazi ya homoni hii ni kuhifadhi mafuta mwilini.
kwa mtu anayetaka kupungua uzito lazima ahakikishe homoni hii iko chini muda wote kwa kuepuka vyakula vya wanga ikiwemo asali au kula kidogo sana vyakula hivi.
vyakula ambavyo vinaweka homoni hii kwenye kiwango kidogo ni vyakula vya mafuta na protini kama samaki, nyama, dagaa, mayai, matunda yasiyo na sukari nyingi kama parachichi na matango.
matumizi makubwa ya asali; mara nyingi asali ili ishike kwenye chai lazima uweke zaidi ya vijiko viwili na kwasababu watu wameaminishwa kwamba asali ni salama basi wanatumia nyingi mno na kuendelea kuongeza uzito bila kujua.
mwisho; asali ni nzuri kuliko sukari kama uko kwenye uzito sahihi lakini kama wewe ni mnene na unataka kupungua uzito ujue asali haiwezi kukusaidia.
ni lazima uhakikishe vyakula vyote vya jamii ya wanga ikiwemo asali unavitumia kwa kiasi kidogo sana au kuachana navyo kabisa kwa muda.
Kuna sukari mbadala unaweza kuzitumia ambazo ni tamu mdomoni lakini mwili hauna uwezo wa kuzitumia zikifika tumboni, ni mbadala mzuri zaidi kuliko sukari na husaidia sana kupunguza uzito.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0769846183/0653095635

0 maoni:
Chapisha Maoni