data:post.body HIZI NDIO SABABU KUU TATU KWANINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA UKIMWI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO SABABU KUU TATU KWANINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA UKIMWI.

Mbu ni mmoja ya wadudu wanaosambaza magonjwa mbalimbali kama malaria, matende, virusi vya homa ya dengu, virusi vya yellow fever na kadhalika lakini kumekua na maswali mengi kutoka kwa wadau kwamba ni kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi wakati ananyonya damu kutoka kwa mtu mmoja na kwenda kuitema kwa mtu mwingine?
                                                               
Kimsingi mbu hawezi kuambukiza ukimwi na hii ni kama bahati kwa wanadamu kwani hakuna ambaye angepona kama kweli mbu anefanikiwa kufanya kazi hiyo.
pamoja na udogo wa mbu, yeye ndio mdudu ambaye anasambaza magonjwa yanayoua watu wengi zaidi duniani kila mwaka huku malaria ikiwa inaongoza,
zifuatazo ni sababu kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi.
mfumo anaotumia kunyonya damu; sindano anayotumia mbu kunyonya damu ina sehemu kuu sita, sindano nne hutumika kuchoma ngozi ya binadamu, sindano ya tano  inatumika kuvuta damu kutoka kwa binadamu kwenda kwa mbu na sindano ya sita inatumika kuingiza mate ya mbu  kwenda binadamu.
Hivyo mwisho wa siku ni mate tu ya mbu ndio yanaingia kwa binadamu wala sio damu, hivyo hata kama mbu ametoka kunyonya damu ya muathirika akaenda kwa ambaye sio muathirika atamuingizia mate na sio damu.
virusi vya ukimwi vinakufa ndani ya tumbo la mbu: tofauti na magonjwa mengine kama malaria ambayo wadudu wa malaria kitaalamu kama plasmodium wakifika ndani ya mbu huanza kuzaliana na kujiandaa kuingia kwa binadamu basi kwa virusi vya ukimwi ni tofauti.
Virusi vya ukimwi vikifika tumboni mwa mbu vinakufa kwasababu zile seli ambazo virusi huzitumia kusambaa kwenye mwili wa binadamu kitaalamu kama T HELPER CELLS hazipatikani ndani ya mbu, hivyo wakati damu  inameng'enywa tumboni mwa mbu kama chakula na virusi vya ukimwi huharibiwa kabisa.
damu anayonyonya mbu ni kidogo sana; hata kama mbu angekua anaingiza damu ndani ya mwili wa binadamu bado kiasi anachoingiza ni kidogo sana kiasi kwamba hakiwezi kuambukiza ukimwi.
kwa maana nyingine ni kwamba inahitajika damu ya kutosha ili mbu aweze kumuambukiza mtu mwingine virusi vya ukimwi.

kimahesabu inatakiwa binadamu ang'atwe na mbu kama milioni kumi ili kuanzisha ugonjwa yaani unit moja ya virusi vya ukimwi.

                                                                    STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                              0766712711/0653095635
                                            

0 maoni:

Chapisha Maoni