data:post.body HIVI NDIO VYAKULA 6 VINAVYOZEESHA MAPEMA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIVI NDIO VYAKULA 6 VINAVYOZEESHA MAPEMA.

Kuzeeka ni hali ya kawaida kwa binadamu ambaye amezaliwa na mwanamke, lakini kuzeeka kabla ya wakati sio kawaida.
sababu kuu za kuzeeka mapema kwa watu wengi ni uvutaji wa sigara na kupigwa na jua kwa muda mrefu.
                                                                       
mtu akipigwa na jua kwa muda mrefu hubadilika na kua mweusi zaidi na ngozi yake kuonekana chakavu lakini pia watu wanaovuta sigara hufika hatua wanaanza kuonekana wakubwa kuliko umri wao hasa usoni kuokana na kemikali ya nikotini iliyomo kwenye sigara.
Leo ntazungumzia vyakula ambavyo vinazeesha mapema na huenda watu hawavijui kwenye milo yao kama ifuatavyo.
kahawa; kahawa inaweza kukupa nguvu za kufanya kazi kwa muda mrefu na kukufanya ujisikie una nguvu sana lakini kahawa ina tabia ya kupunguza maji mwilini na kumfanya mtu akojoe mara kwa mara, hii hupunguza maji kwenye ngozi na kuifanya kavu sana lakini pia kahawa hukunyima usingizi wa kutosha.
mtu ambaye hapati usingizi wa kutosha hawezi kua na mwili na ngozi zenye afya hivyo huanza kuzeeka.
nyakula vya viwandani(processed meat); nyama kama soseji na bacon zinahifadhiwa na kemikali nyingi na chumvi ili ziweze kudumu bila kuharibika, hii  huingilia utengenezaji wa collagen.
collagen ni aina ya protini ya ngozi ambayo hutengenezwa tangu ukiwa mdogo kuweka ngozi yako laini, lakini unavyozidi kukua collagen hii inatengenezwa kidogo ndio maana makunyazi hutokea wa watu wazee.
sasa ulaji wa vyakula hivi hupunguza collagen hata kama hujazeeka bado.
pombe; kama ilivyo kwa kahawa, pombe ina tabia ya kupunguza sana maji mwilini na kukuacha mkavu wa ngozi, pombe huharibu mfumo wako wa kulala na kujikuta unalala tofauti na mwanzo, pombe hupunguza vitamin muhimu za mwili kama vitami A na vitamin c ambazo ni muhimu sana kwa mwili, pombe huharibu maini ambayo kazi yake kubwa ni kuondoa sumu mwilini.
sumu zikishindwa kuondolewa vizuri na maini basi zinakufanya wewe uendelee kuzeeka.
kupunguza madhara ya pombe ni vizuri kunywa kidogo na kunywa maji mengi sana ili kuzuia kuishiwa maji.
vyakula vya chumvi nyingi: kama wewe ni mpenzi wa chumvi nyingi sana kwenye chakula basi ujue uko unazeeka haraka kuliko unavyofikiri, chumvi ina kiasi kikubwa cha sodium ambacho hujaza maji kwenye mwili na kukufanya uonekane na sura iliyojaa kama umepigwa.
kama huwezi kuvumilia basi unaweza ukatumia chumvi maalumu zenye kiwango kidogo sana cha sodium kwa ladha ileile.

ulaji mkubwa wa sukari; sukari inayopatikana kwenye chai, soda, keki, ice cream, biskuti, chocolate na kadhalika ni hatari sana kwa ngozi yako.
ukila sukari nyingi huenda kwenye ngozi na kujichanganya na protini za collagen kwenye ngozi yako kitaalamu kama glycation.
hii huharibu ngozi na kuleta makunyazi.
ulaji wa mafuta mabaya; mafuta mabaya ni yale ambayo mara nyingi yanaliwa yakiwa kwenye mfumo wa mgando, mara nyingi kwa kutumia njia inayoitwa hydrogenation mafuta hayo hubadilishwa kutoka kwenye mafuta ya kimiminika na kua mgando. mfano blue band au siagi.
mafuta yeyote ambayo unayatumia yakiwa yameganda hayafai kwa ngozi yako na afya kwa ujumla lakini pia mafuta haya hupatikana kwenye vyakula vya kukaangwa kama chips,piza na maandazi, vitumbua na mikaango yote.
                                                         
mwisho; madhara ya vitu mbalimbali kwa mwili wa binadamu husababishwa na matumizi ya muda mrefu wa vitu hivyo, sio dhambi kuvitumia mara moja moja sana lakini vitu hivyo vikiwa sehemu ya maisha yako basi kuzeeka hata kabla hujafika umri wa kuzeeka itakua kitu cha kawaida.

Maoni 1 :