data:post.body Aprili 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

SABABU KWANINI ASALI HAIFAI KUTUMIKA KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO.

Kumekua na ongezeko la idadi kubwa ya watu wanaotumia asali kunywa chai kama mbadala wa sukari kwa sababu za kiafya zaidi lakini pia wapo wanaotumia kulamba.
Ni kweli asali ni nzuri kuliko sukari kwasababu ina madini mbalimbali kama potashiamu, sodium, calcium, magnesium, vitamin  B, copper na madini ya chuma.
                                                               
Lakini linapokuja kwenye swala la kupunguza uzito, matumizi ya asali yanahitaji umakini sana kwani unaweza kujikuta unaongezeka zaidi badala ya kupungua kwa sababu zifuatavyo.
wingi mkubwa wa nguvu au calorie; linapokuja swala la kupungua uzito, kiasi cha nguvu au calories zilizopo kwenye chakula ni muhimu sana kwani ndio zinamua kama unapungua au unaongezeka.
kwa kawaida kijiko kimoja cha asali kina nguvu au calories 64, wakati huohuo kijiko kimoja cha sukari kina calories 49.
Hivyo pamoja na kwamba asali ina vitamin nyingi lakini inatoa nguvu nyingi ambayo kimsingi inaongeza uzito zaidi kuliko sukari ya kawaida kwa kipimo kilekile.

utengenezaji mkubwa wa homoni ya insulini; insulini ni homoni inayotumika kuvunja sukari yeyote au chakula chochote cha jamii ya wanga kama wali, ugali, viazi, mihogo, na kadhalika.
sasa ukiwa mtumiaji wa vyakula hivi  wanga  haijalishi ni asili au sio asili, homoni hii lazima itengenezwe nyingi.
Bahati mbaya ni kwamba moja ya kazi ya homoni hii ni kuhifadhi mafuta mwilini.
kwa mtu anayetaka kupungua uzito lazima ahakikishe homoni hii iko chini muda wote kwa kuepuka vyakula vya wanga ikiwemo asali au kula kidogo sana vyakula hivi.
vyakula ambavyo vinaweka homoni hii kwenye kiwango kidogo ni vyakula vya mafuta na protini kama samaki, nyama, dagaa, mayai, matunda yasiyo na sukari nyingi kama parachichi na matango.
                                                             
matumizi makubwa ya asali; mara nyingi asali ili ishike kwenye chai lazima uweke zaidi ya vijiko viwili na kwasababu watu wameaminishwa kwamba asali ni salama basi wanatumia nyingi mno na kuendelea kuongeza uzito bila kujua.

mwisho; asali ni nzuri kuliko sukari kama uko kwenye uzito sahihi lakini kama wewe ni mnene na unataka kupungua uzito ujue asali haiwezi kukusaidia.
ni lazima uhakikishe vyakula vyote vya jamii ya wanga ikiwemo asali unavitumia kwa kiasi kidogo sana au kuachana navyo kabisa kwa muda.
                                                               
Kuna sukari mbadala unaweza kuzitumia ambazo ni tamu mdomoni lakini mwili hauna uwezo wa kuzitumia zikifika tumboni, ni mbadala mzuri zaidi kuliko sukari na husaidia sana kupunguza uzito.

                                                                    STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0769846183/0653095635

UFAHAMU UGONJWA WA DENGU, CHANZO CHA KIFO NA MATIBABU YAKE.

Kuvuja damu kwenye pua na fidhi za mdomoni mpaka kufa ndio chanzo kikuu cha kifo cha ugonjwa huu.
Shirika la afya duniani WHO linakadiria kwamba kila mwaka watu milion mia tatu na tisini huuugua ugonjwa wa dengu kwa kujua na wengine kutokujua.
                                                         
Ugonjwa huu hupatikana sana maeneo yenye joto hasa afrika na asia sababu maeneo yanaweza kutunza mbu wengi tofauti na maeneo yenye baridi kali ambapo mbu hakuna.
Ugonjwa wa dengu unaweza kua hatari mpaka kusababisha kifo hasa kwa watoto wadogo na wazee ambao kinga zo hua ziko chini.
Inakadiriwa kua katika kila wagonjwa 100 wa dengue basi wawili mpaka watatu hufariki wa ugonjwa huu.

chanzo cha ugonjwa ni nini?
Virusi vya dengu ndio chanzo kikuu cha ugonjwa huu, kuna aina nyingi za virusi hawa kama DEN-1, DEN-2,DEN-3 na DEn-4.
Virusi hawa husambazwa na mbu wa kike kwa jina la Aedes aegypti, Mbu hawa pia husambaza magonjwa mengine kama chikungunya, homa ya manjano na ugonjwa wa zika.

dalili za ugonjwa wa dengue.

  • maumivu ya ghafla ya kichwa.
  • homa kali ya ghafla.
  • maumivu ndani ya macho
  • maumivu makali ya jointi na mifupa
  • kuchoka sana
  • kutapika
  • vipele vya ngozi.
  • kutoka damu puani na kwenye fidhi.
vipimo vya maabara
kipimo maalumu kitaalamu kama antibody test hufanyika kugundua ugonjwa huu.


matibabu ya ugonjwa wa dengu.
hakuna matibabu ya ugonjwa huu ila kuna jinsi ya kutuliza makali ya ugonjwa huu.
ikithibitika una ugonjwa wa dengue unatakiwa unywe maji mengi na kutumia dawa ya paracetamol tu.
epuka dawa zote za jamii ya aspirini kama diclofenac, diclopa, meloxicam, peroxicam, ibuprofen na kadhalika kwani zinaongeza uvujajaji wa damu.

jinsi ya kuzuia ugonjwa huu.
Njia bora ya kuzuia ugonjwa huu ni kuepuka kung'atwa na mbu ambao wanasababisha ugonjwa dengu kama ifuatavyo.

  • usiishi sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu.
  • tumia dawa za mbu za kupaka kwenye ngozi au kupuliza.
  • vaa ngo ndefu na za kufunika miguu na mikono.
  • funga madirisha na milango jioni kuzuia mbu wasiingie.
  • ukipata dalili za ugonjwa huo nenda hospitali.


                                                   STAY ALIVE 

                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                     0769846183/0653095635

HIVI NDIO VYAKULA 6 VINAVYOZEESHA MAPEMA.

Kuzeeka ni hali ya kawaida kwa binadamu ambaye amezaliwa na mwanamke, lakini kuzeeka kabla ya wakati sio kawaida.
sababu kuu za kuzeeka mapema kwa watu wengi ni uvutaji wa sigara na kupigwa na jua kwa muda mrefu.
                                                                       
mtu akipigwa na jua kwa muda mrefu hubadilika na kua mweusi zaidi na ngozi yake kuonekana chakavu lakini pia watu wanaovuta sigara hufika hatua wanaanza kuonekana wakubwa kuliko umri wao hasa usoni kuokana na kemikali ya nikotini iliyomo kwenye sigara.
Leo ntazungumzia vyakula ambavyo vinazeesha mapema na huenda watu hawavijui kwenye milo yao kama ifuatavyo.
kahawa; kahawa inaweza kukupa nguvu za kufanya kazi kwa muda mrefu na kukufanya ujisikie una nguvu sana lakini kahawa ina tabia ya kupunguza maji mwilini na kumfanya mtu akojoe mara kwa mara, hii hupunguza maji kwenye ngozi na kuifanya kavu sana lakini pia kahawa hukunyima usingizi wa kutosha.
mtu ambaye hapati usingizi wa kutosha hawezi kua na mwili na ngozi zenye afya hivyo huanza kuzeeka.
nyakula vya viwandani(processed meat); nyama kama soseji na bacon zinahifadhiwa na kemikali nyingi na chumvi ili ziweze kudumu bila kuharibika, hii  huingilia utengenezaji wa collagen.
collagen ni aina ya protini ya ngozi ambayo hutengenezwa tangu ukiwa mdogo kuweka ngozi yako laini, lakini unavyozidi kukua collagen hii inatengenezwa kidogo ndio maana makunyazi hutokea wa watu wazee.
sasa ulaji wa vyakula hivi hupunguza collagen hata kama hujazeeka bado.
pombe; kama ilivyo kwa kahawa, pombe ina tabia ya kupunguza sana maji mwilini na kukuacha mkavu wa ngozi, pombe huharibu mfumo wako wa kulala na kujikuta unalala tofauti na mwanzo, pombe hupunguza vitamin muhimu za mwili kama vitami A na vitamin c ambazo ni muhimu sana kwa mwili, pombe huharibu maini ambayo kazi yake kubwa ni kuondoa sumu mwilini.
sumu zikishindwa kuondolewa vizuri na maini basi zinakufanya wewe uendelee kuzeeka.
kupunguza madhara ya pombe ni vizuri kunywa kidogo na kunywa maji mengi sana ili kuzuia kuishiwa maji.
vyakula vya chumvi nyingi: kama wewe ni mpenzi wa chumvi nyingi sana kwenye chakula basi ujue uko unazeeka haraka kuliko unavyofikiri, chumvi ina kiasi kikubwa cha sodium ambacho hujaza maji kwenye mwili na kukufanya uonekane na sura iliyojaa kama umepigwa.
kama huwezi kuvumilia basi unaweza ukatumia chumvi maalumu zenye kiwango kidogo sana cha sodium kwa ladha ileile.

ulaji mkubwa wa sukari; sukari inayopatikana kwenye chai, soda, keki, ice cream, biskuti, chocolate na kadhalika ni hatari sana kwa ngozi yako.
ukila sukari nyingi huenda kwenye ngozi na kujichanganya na protini za collagen kwenye ngozi yako kitaalamu kama glycation.
hii huharibu ngozi na kuleta makunyazi.
ulaji wa mafuta mabaya; mafuta mabaya ni yale ambayo mara nyingi yanaliwa yakiwa kwenye mfumo wa mgando, mara nyingi kwa kutumia njia inayoitwa hydrogenation mafuta hayo hubadilishwa kutoka kwenye mafuta ya kimiminika na kua mgando. mfano blue band au siagi.
mafuta yeyote ambayo unayatumia yakiwa yameganda hayafai kwa ngozi yako na afya kwa ujumla lakini pia mafuta haya hupatikana kwenye vyakula vya kukaangwa kama chips,piza na maandazi, vitumbua na mikaango yote.
                                                         
mwisho; madhara ya vitu mbalimbali kwa mwili wa binadamu husababishwa na matumizi ya muda mrefu wa vitu hivyo, sio dhambi kuvitumia mara moja moja sana lakini vitu hivyo vikiwa sehemu ya maisha yako basi kuzeeka hata kabla hujafika umri wa kuzeeka itakua kitu cha kawaida.

HIZI NDIO SABABU KUU TATU KWANINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA UKIMWI.

Mbu ni mmoja ya wadudu wanaosambaza magonjwa mbalimbali kama malaria, matende, virusi vya homa ya dengu, virusi vya yellow fever na kadhalika lakini kumekua na maswali mengi kutoka kwa wadau kwamba ni kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi wakati ananyonya damu kutoka kwa mtu mmoja na kwenda kuitema kwa mtu mwingine?
                                                               
Kimsingi mbu hawezi kuambukiza ukimwi na hii ni kama bahati kwa wanadamu kwani hakuna ambaye angepona kama kweli mbu anefanikiwa kufanya kazi hiyo.
pamoja na udogo wa mbu, yeye ndio mdudu ambaye anasambaza magonjwa yanayoua watu wengi zaidi duniani kila mwaka huku malaria ikiwa inaongoza,
zifuatazo ni sababu kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi.
mfumo anaotumia kunyonya damu; sindano anayotumia mbu kunyonya damu ina sehemu kuu sita, sindano nne hutumika kuchoma ngozi ya binadamu, sindano ya tano  inatumika kuvuta damu kutoka kwa binadamu kwenda kwa mbu na sindano ya sita inatumika kuingiza mate ya mbu  kwenda binadamu.
Hivyo mwisho wa siku ni mate tu ya mbu ndio yanaingia kwa binadamu wala sio damu, hivyo hata kama mbu ametoka kunyonya damu ya muathirika akaenda kwa ambaye sio muathirika atamuingizia mate na sio damu.
virusi vya ukimwi vinakufa ndani ya tumbo la mbu: tofauti na magonjwa mengine kama malaria ambayo wadudu wa malaria kitaalamu kama plasmodium wakifika ndani ya mbu huanza kuzaliana na kujiandaa kuingia kwa binadamu basi kwa virusi vya ukimwi ni tofauti.
Virusi vya ukimwi vikifika tumboni mwa mbu vinakufa kwasababu zile seli ambazo virusi huzitumia kusambaa kwenye mwili wa binadamu kitaalamu kama T HELPER CELLS hazipatikani ndani ya mbu, hivyo wakati damu  inameng'enywa tumboni mwa mbu kama chakula na virusi vya ukimwi huharibiwa kabisa.
damu anayonyonya mbu ni kidogo sana; hata kama mbu angekua anaingiza damu ndani ya mwili wa binadamu bado kiasi anachoingiza ni kidogo sana kiasi kwamba hakiwezi kuambukiza ukimwi.
kwa maana nyingine ni kwamba inahitajika damu ya kutosha ili mbu aweze kumuambukiza mtu mwingine virusi vya ukimwi.

kimahesabu inatakiwa binadamu ang'atwe na mbu kama milioni kumi ili kuanzisha ugonjwa yaani unit moja ya virusi vya ukimwi.

                                                                    STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                              0766712711/0653095635
                                            

HIZI NDIO FAIDA 5 ZA KUNYWA SODA AMBAZO HAZINA SUKARI ASILIA.(SUGAR FREE DRINKS)

Soda ambazo hazina sukari asilia ziligunduliwa mwaka 1960 kwa ajili ya kuwapa watu wenye kisukari kwasababu zilikua zimetengenezwa na sukari feki kitaalamu kama artificial sweetener ambayo ukinywa mdomoni inaonekana ni tamu kabisa kama soda lakini, ikifika tumboni ni kama maji tu yaani haiwezi kukupa nguvu wala kuongeza kiasi cha sukari mwilini mwako.


miaka michache baadae soda hizi zilianza kutangazwa zitumike kwa ajili ya watu wote baada ya faida zake kuanza kuonekana ndio maaana siku hizi unazioana nyingi sana mtaani ili kila mtu aweze kutumia kama mbadala wa soda za zenye sukari asilia.
faida zake ni kama ifuatavyo.
husaidia kupunguza uzito; soda za kawaida zina vijiko kumi vya sukari kwa kila moja, kipimo ambacho ni kikubwa sana kwa matumizi ya binadamu na huongeza uzito kwa kiasi kikubwa.
Kawaida mwanaume hatakiwi kutumia zaidi ya vijiko tisa vya sukari kwa siku nzima yaani kwanzia chai na chakula utakachokula mchana huki mwanamke akitakiwa vijiko sita tu.
Hivyo ukinywa soda moja tu ushapita kiwango na hapo hujaongezea biskuti, ndizi mbivu,keki,chocolate, sukari ya chai na vyakula vingine vya jamii ya sukari.
Hivyo wakati soda ya kawaida pekee inakupa calories 150 kwa siku ambayo ni sawa na kilo mbili za unene kila mwezi, soda ambazo hazina sukari asilia hazikuongezi calorie yeyote wala uzito wowote mwilini.
nzuri kwa afya ya meno; sukari za kwenye soda za kawaida hutengeneza tindikali mdomoni ambazo hubandua na kutoboa meno kwa watumiaji, ndio maana wagonjwa wote wa meno hawashauriwi sana kula vyakula vya sukari nyingi.
lakini soda hizi sababu sukari yake sio asilia basi hazina uwezo wa kukuunguza au kukutoboa meno.
nzuri kwa wagonjwa wa kisukari;mgonjwa wa kisukari anaweza kunywa soda hizi bila wasiwasi kama watu wengine na bila kuhofia uwezekano wowote wa sukari yake kupanda, ukilinganisha na soda za zamani ambazo zilikua zina sukari asilia ambazo zilikua zinapandisha sukari kwa kiasi kikubwa sana.
nzuri kwa vyakula vingine pia; siku hizi jamii ya sukari hii inapatikana madukani hivyo ili kupunguza matumizi makubwa sana ya sukari ambayo ni hatari kwa afya yako basi unaweza kuitumia kwenye chai na vyakula vyote ambavyo huhitaji sukari kwenye mapishi kama keki, maandazi na kadhalika.
hupunguza hatari ya saratani mbalimbali; kutokana na kiwango kikubwa sana cha sukari kwenye soda za kawaida, soda hizo zimehusishwa sana na kuugua ugonjwa wa saratani ya kongosho.
Ukilinganishwa na soda hizi mpya ambazo hazina sukari asilia ambazo tafiti zake zomeonyesha kwamba hakuna hatari yeyote ya saratani kwenye soda hizo.

                                                                          STAY ALIVE
                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                             0653095635/0769846183