data:post.body MGONJWA MWINGINE WA UKIMWI APONA KABISA NA KUACHA DAWA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MGONJWA MWINGINE WA UKIMWI APONA KABISA NA KUACHA DAWA.

Mgonjwa mmoja ambaye alikua ni muathirika wa virusi vya ukimwi huko nchini uingereza amethibitika kupona kabisa ugonjwa huo na huu ni mwaka sasa na miezi sita hajatumia dawa tena.
Mgonjwa huyu aligunduliwa na ukimwi mwaka 2003 kisha alikutwa na ugonjwa saratani mwaka 2012.         
                                             
baada ya hapo mgonjwa alianzishiwa matibabu ya saratani kitaalamu kama chemotherapy na baadae alifanyiwa upandikizi wa seli ambazo zilizotoka kwa mtu ambaye seli zake hazipokei virusi vya ukimwi.
Nia na madhumuni ya matibabu haya ilikua ni kutibu ugonjwa wake wa saratani, lakini cha kushangaza matibabu yale yalitibu saratani lakini pia yakaondoa virusi vyote vya ukimwi kwenye mwili wake.
watafiti katika vyuo vikuu vyote maarufu nchini uingereza kama oxford, cambridge, imperial college of london na university college of london walihusika kwenye kazi hii.

je hii ni bahati tu imetokea?
Hapana, hii sio bahati kwani miaka kumi iliyopita mgonjwa mmoja kwa jina la Timothy Brown alikua wa kwanza kutibiwa ukimwi kwa njia hii hii lakini yeye akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya damu pamoja na upungufu wa kinga mwilini(UKIMWI).
wakati wa matibabu ya saratani yake alipewa mionzi, na kupandikizwa seli za mifupa kitaalamu kama bone marrow transplant kutoka kwa mtu ambaye alikua ana kinga ya ukimwi ya kuzaliwa nayo mgonjwa huyu alipona saratani yake na ukimwi kwa pamoja na ndio akawa mtu wa kwanza kabisa duniani kupona ugonjwa wa ukimwi.

matibabu haya yanafanya kazi vipi?
kuna baadhi ya watu duniani ambao hawawezi kuambukizwa ukimwi kabisa sababu walizaliwa hivyo, kitaalamu ni kwamba njia ambayo inatumika na virusi vya ukimwi kuingia kwa watu wengine au receptors kwao haipo.
sasa wagonjwa hawa walipona ukimwi baada ya kupandikiziwa seli kutoka kwa hawa watu ambao kinga zao haziwaruhusu kupata ukimwi kabisa.

je kuna matumaini ya dawa ya ukimwi hivi karibuni?
bahati mbaya njia hii haiwezi kutumika kutibu watu wote kwani gharama kubwa sana na upasuaji wake ni hatari unaweza kusababisha kifo, lakini kupitia matukio haya wataalamu wanazidi kujifunza kuhusu ugonjwa huu na wanazidi kuyakaribia matibabu.
Huenda sisi ndio tukawa kizazi cha mwisho kusumbuliwa na ugonjwa huu na ndani ya miaka 10 mpaka 20 ugonjwa wa ukimwi utabaki historia kama ugonjwa kwa ukoma ambao pamoja kwamba ulisumbua sana  kabla na baada ya kuja kwa yesu, sasa hivi imebaki historia tu.

                                                               STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0769846183/0653095635
                                                      

0 maoni:

Chapisha Maoni