Linapokuja swala la kuzaa watoto ni vizuri kukaa chini na kupanga ni idadi gani ya watoto unataka kuzaa, unataka kuwazaa lini na ukiwa na miaka mingapi?
Unaweza kua una changamoto nyingi labda uchumi wako sio mzuri, hujapata mtu rasmi wa kuzaa naye, mambo yako bado hayajakaa vizuri na kadhalika lakini ni vizuri ukazingatia haya mambo kwani yanachukua nafasi muhimu sana kwenye afya yako na watoto utakaozaa.
Kitaalamu mwanamke akiamua kuanza kuzaa basi anatakiwa ahikikishe siku akiacha basi ndio amealizana na mambo ya uzazi.
Watoto wote wanatakiwa waachane miaka miwili na sio zaidi ya miaka mitano yaani ukiamua kuzaa hakikisha watoto hawaachani kwa upungufu wa miaka miwili na sio zaidi ya miaka mitano kwa maana nyingine hutakiwi kuzaa kila baada ya mwaka mmoja au ukazaa afu baada ya miaka 6 au 7 unasema unataka mwingine.
kuachisha watoto muda kitaalamu kama child spacing ni muhimu sana kwa sababu zifutazo.
muda wa kunyonya; maziwa ya mama hayana mbadala wa 100%, kuna virutubisho viingi sana mtaani kwa ajili ya kuwapa watoto lakini hakuna ambacho kinalingana ubora na maziwa ya mama.
Shirika la afya duniani(WHO) linashauri mtoto kunyonyeshwa mfululizo kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuachishwa kuendelea na vyakula vingine, hivyo kama mama atabeba mimba kabla ya miaka miwili basi maziwa yake yatapungua sana na ataishia kumuachisha mtoto.
Muda wa mwili kujijenga; kila kitu ambacho unakiona baada ya mtoto kuzaliwa kimetoka kwa mama, hivyo mama amepoteza madini na virutubisho vingi sana ili kumpa mtoto.
vitu hivyo vinataka muda ili viweze kujijenga kwenye mwili wa mama kwa kiasi cha kutosha ili kubeba mimba nyingine.
Matatizo ya kuzaa watoto ambao hawajakomaa; kufuatisha mimba haraka haraka kuna ambatana sana uwezekano wa mama kuzaa watoto kabla miezi tisa haijafika.
watoto hawa maarufu kama kabichi ni wagumu sana kuwalea mpaka wafike muda sahihi, wengi hufa na baadhi hudumaa.
muda wa mama kupona; haijalishi mama alizaa kwa njia ya kawaida au upasuaji, mama anahitaji muda wa kutosha kuacha sehemu ya kizazi iliyokua imeshika mtoto ipone kabisa na kua katika hali ya kawaida, kubeba mimba kabla ya kizazi kupona kabisa huweza kua chanzo cha mimba kuharibika mara kwa mara.
hatari ya magonjwa ya akili kwa watoto; tafiti mpya zinaonyesha kuongezeka kwa tatizo la magonjwa ya akili hasa ya mtoto kushindwa kukua kiakili nakushindwa kuwasiliana na watu wanaomzunguka kitaalamu kama "autism".
magonjwa haya hayana matibabu ya kuponya kabisa na mtoto huyu atakua mlemavu maisha yake yote.
hatari ya kuzaliwa na upungufu wa viungo vya mwili; kitaalamu huu inaitwa congenital abnormality,
ni hali ambayo mtoto anazaliwa na mapungufuu kadhaa kama upungufu wa vidole, miguu mitatu, mkono mmoja, tundu kwenye moyo na kadhalika.
hatari ya kifo cha mama; tafiti zinaonyesha kwamba kuna ongezeko la vifo la akina mama ambao wanazaa kwa tofauti ya umri wa miaka mitano na wale ambao wanazaa kabla ya miaka miwili, huku chanzo cha kifo cha akina mama wanaochanisha zaidi ya miaka mitano ikiwa kifafa cha mimba na vifo vya wanaozaa chini ya miaka miwili ikiwa kuishiwa damu sana.
mwisho; ili kuepusha matatizo ya kuzaa bila mpangilio mzuri wa kiafya basi ni vizuri kupanga uzazi jinsi unavyoweza ili kufuata mtiririko sahihi kwa maana kwamba kama hauko tayari kuanza kuzaa usizae kwanza na ukishaanza kuzaa maana yake usizae kwa tofauti ya chini ya miaka miwili au zaidi ya miaka mitano ili kupata matokeo bora ya uzazi.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0769846183/0653095635

0 maoni:
Chapisha Maoni