data:post.body Machi 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HUU NDIO MUDA AMBAO MAMA ANATAKIWA KUSUBIRI KABLA YA KUZAA MTOTO MWINGINE.

Linapokuja swala la kuzaa watoto ni vizuri kukaa chini na kupanga ni idadi gani ya watoto unataka kuzaa, unataka kuwazaa lini na ukiwa na miaka mingapi?
Unaweza kua una changamoto nyingi labda uchumi wako sio mzuri, hujapata mtu rasmi wa kuzaa naye, mambo yako bado hayajakaa vizuri na kadhalika lakini ni vizuri ukazingatia haya mambo kwani yanachukua nafasi muhimu sana kwenye afya yako na watoto utakaozaa.
                                                                       
Kitaalamu mwanamke akiamua kuanza kuzaa basi anatakiwa ahikikishe siku akiacha basi ndio amealizana na mambo ya uzazi.
Watoto wote  wanatakiwa waachane miaka miwili na sio zaidi ya miaka mitano yaani ukiamua kuzaa hakikisha watoto hawaachani kwa upungufu wa miaka miwili na sio zaidi ya miaka mitano kwa maana nyingine hutakiwi kuzaa kila baada ya mwaka mmoja au ukazaa afu baada ya miaka 6 au 7 unasema unataka mwingine.
kuachisha watoto muda kitaalamu kama child spacing ni muhimu sana kwa sababu zifutazo.
muda wa kunyonya; maziwa ya mama hayana mbadala wa 100%, kuna virutubisho viingi sana mtaani kwa ajili ya kuwapa watoto lakini hakuna ambacho kinalingana ubora na maziwa ya mama.
Shirika la afya duniani(WHO) linashauri mtoto kunyonyeshwa mfululizo kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuachishwa kuendelea na vyakula vingine, hivyo kama mama atabeba mimba kabla ya miaka miwili basi maziwa yake yatapungua sana na ataishia kumuachisha mtoto.
Muda wa mwili kujijenga; kila kitu ambacho unakiona baada ya mtoto kuzaliwa kimetoka kwa mama, hivyo mama amepoteza madini na virutubisho vingi sana ili kumpa mtoto.
vitu hivyo vinataka muda ili viweze kujijenga kwenye mwili wa mama kwa kiasi cha kutosha ili kubeba mimba nyingine.
Matatizo ya kuzaa watoto ambao hawajakomaa; kufuatisha mimba haraka haraka kuna ambatana sana uwezekano wa mama kuzaa watoto kabla miezi tisa haijafika.
watoto hawa maarufu kama kabichi ni wagumu sana kuwalea mpaka wafike muda sahihi, wengi hufa na baadhi hudumaa.
muda wa mama kupona; haijalishi mama alizaa kwa njia ya kawaida au upasuaji, mama anahitaji muda wa kutosha kuacha sehemu ya kizazi iliyokua imeshika mtoto ipone kabisa na kua katika hali ya kawaida, kubeba mimba kabla ya kizazi kupona kabisa huweza kua chanzo cha mimba kuharibika mara kwa mara.
hatari ya magonjwa ya akili kwa watoto; tafiti mpya zinaonyesha kuongezeka kwa tatizo la magonjwa ya akili hasa ya mtoto kushindwa kukua kiakili nakushindwa  kuwasiliana na watu wanaomzunguka kitaalamu kama "autism".
magonjwa haya hayana matibabu ya kuponya kabisa na mtoto huyu atakua mlemavu maisha yake yote.
hatari ya kuzaliwa na upungufu wa viungo vya mwili; kitaalamu huu inaitwa congenital abnormality,
ni hali ambayo mtoto anazaliwa na mapungufuu kadhaa kama upungufu wa vidole, miguu mitatu, mkono mmoja, tundu kwenye moyo na kadhalika.
hatari ya kifo cha mama;  tafiti zinaonyesha kwamba kuna ongezeko la vifo la akina mama ambao wanazaa kwa tofauti ya umri wa miaka mitano na wale ambao wanazaa kabla ya miaka miwili, huku chanzo cha kifo cha akina mama wanaochanisha zaidi ya miaka mitano ikiwa kifafa cha mimba na vifo vya wanaozaa chini ya miaka miwili ikiwa kuishiwa damu sana.
mwisho; ili kuepusha matatizo ya kuzaa bila mpangilio mzuri wa kiafya basi ni vizuri kupanga uzazi jinsi unavyoweza ili kufuata mtiririko sahihi kwa maana kwamba kama hauko tayari kuanza kuzaa usizae kwanza na ukishaanza kuzaa maana yake usizae kwa tofauti ya chini ya miaka miwili au zaidi ya miaka mitano ili kupata matokeo bora ya uzazi.

                                                                   STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 
                                                   0769846183/0653095635

HIZI NDIO NJIA TATU ZA KUZAA NA MUATHIRIKA WA UKIMWI BILA KUPATA MAAMBUKIZI.

Katika hali ambayo sio ya kawaida, watu wawili wanaweza wakakutana na kupendana huku mmoja wao ni muathirika wa ukimwi na mwingine asiwe muathirika wa ukimwi.
Hali hii inaweza kuleta ugumu kidogo kwenye mitazamo ya watu wa nje kama ndugu, jamaa na marafiki.                                                             
Lakini linapokuja swala la mapenzi hua ni vigumu sana kulizuia, kwani kuna ushahidi wa watu waliofunga ndoa na waathirika bila kujali afya zao sababu ya mapenzi.
sasa kumekua na utata ni jinsi gani unaweza kuzaa na mtu ambaye ni muathirika kwani watu wengi ambao wana wapenzi waathirika wanatakiwa watumie kondom kujilinda na maambukizi.
Leo ntatoa njia tatu muhimu ambazo unaweza kutumia kulala na mwanamke muathirika bila kondom na ukawa salama.
mgonjwa kutumia dawa zake vizuri;  mgonjwa akitumia dawa zake vizuri kiasi kwamba majibu ya damu kitaalamu kama viral load yakafika hatua amabayo virusi havionekani kwenye vipimo vya damu{ sio vile vinavyotumika nyumbani kujipima} au undetectable basi mchumba wake ambaye sio muathirika anaweza kulala na muathirika huyo bila kutumia kondom na kumpa mimba.
tafiti zinaonyesha kwamba kulala na mtu kama huyu ni sawa na kulala mtu kwa kutumia kondom kwani hawezi kukuambukiza kabisa.

kupandikiza mbegu za kiume; hii ni njia ya kisasa ambayo hutumika kuchukua mbegu za mwanaume na kuzipandikiza kwa mwanamke bila kukutana naye kingono, hii inaweza kutumika mwanamke akiwa muathirika au mwanaume akiwa muathirika kama ifuatavyo.
kama mwanamke ni muathirika basi mbegu za mwanaume zinachukuliwa na kupandikizwa na kumbebesha mimba, kama ni mwanaume muathirika mbegu za zake zinachukuliwa na kusafishwa kitaalamu kabla ya kupandikizwa kupata ujauzito.
                                       
kutumia dawa za kujizuia na ukimwi: kuna dawa maarufu ambazo zinatumika sana siku hizi kwa ajili ya kuwapa watu ambao wamelala na waaathirika bahati mbaya ili kuzuia ukimwi, dawa zile ni maarufu kama PEP.
Zinaweza kutumika pia kama chanjo mtu ambaye anataka kuzaa na muathirika, yaani siku mwanaume au mwanamke ambaye sio muathirika anachukua dozi ya mwezi mmoja na kuanza kumeza huku akikutana na mtu wake ambaye ni muathirika bila kutumia kondomu, akishafanikisha kumpa mimba basi anaendelea kutumia kondom na kuacha dawa.
                                                             
mwisho; kama mama ndio muathirika basi jitihada za msingi za kuhakikisha mimba hiyo inakua chini ya uangalizi wa kliniki ya mama na mtoto inatkiwa zifanyike ili kuhakikisha mtoto mtarajiwa anazaliwa bila maambukizi ya virusi vya ukimwi.

  • Kupata makala zetu mara kwa mara ingia playstore kisha pakua au download application ya "siri za afya bora".

MGONJWA MWINGINE WA UKIMWI APONA KABISA NA KUACHA DAWA.

Mgonjwa mmoja ambaye alikua ni muathirika wa virusi vya ukimwi huko nchini uingereza amethibitika kupona kabisa ugonjwa huo na huu ni mwaka sasa na miezi sita hajatumia dawa tena.
Mgonjwa huyu aligunduliwa na ukimwi mwaka 2003 kisha alikutwa na ugonjwa saratani mwaka 2012.         
                                             
baada ya hapo mgonjwa alianzishiwa matibabu ya saratani kitaalamu kama chemotherapy na baadae alifanyiwa upandikizi wa seli ambazo zilizotoka kwa mtu ambaye seli zake hazipokei virusi vya ukimwi.
Nia na madhumuni ya matibabu haya ilikua ni kutibu ugonjwa wake wa saratani, lakini cha kushangaza matibabu yale yalitibu saratani lakini pia yakaondoa virusi vyote vya ukimwi kwenye mwili wake.
watafiti katika vyuo vikuu vyote maarufu nchini uingereza kama oxford, cambridge, imperial college of london na university college of london walihusika kwenye kazi hii.

je hii ni bahati tu imetokea?
Hapana, hii sio bahati kwani miaka kumi iliyopita mgonjwa mmoja kwa jina la Timothy Brown alikua wa kwanza kutibiwa ukimwi kwa njia hii hii lakini yeye akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya damu pamoja na upungufu wa kinga mwilini(UKIMWI).
wakati wa matibabu ya saratani yake alipewa mionzi, na kupandikizwa seli za mifupa kitaalamu kama bone marrow transplant kutoka kwa mtu ambaye alikua ana kinga ya ukimwi ya kuzaliwa nayo mgonjwa huyu alipona saratani yake na ukimwi kwa pamoja na ndio akawa mtu wa kwanza kabisa duniani kupona ugonjwa wa ukimwi.

matibabu haya yanafanya kazi vipi?
kuna baadhi ya watu duniani ambao hawawezi kuambukizwa ukimwi kabisa sababu walizaliwa hivyo, kitaalamu ni kwamba njia ambayo inatumika na virusi vya ukimwi kuingia kwa watu wengine au receptors kwao haipo.
sasa wagonjwa hawa walipona ukimwi baada ya kupandikiziwa seli kutoka kwa hawa watu ambao kinga zao haziwaruhusu kupata ukimwi kabisa.

je kuna matumaini ya dawa ya ukimwi hivi karibuni?
bahati mbaya njia hii haiwezi kutumika kutibu watu wote kwani gharama kubwa sana na upasuaji wake ni hatari unaweza kusababisha kifo, lakini kupitia matukio haya wataalamu wanazidi kujifunza kuhusu ugonjwa huu na wanazidi kuyakaribia matibabu.
Huenda sisi ndio tukawa kizazi cha mwisho kusumbuliwa na ugonjwa huu na ndani ya miaka 10 mpaka 20 ugonjwa wa ukimwi utabaki historia kama ugonjwa kwa ukoma ambao pamoja kwamba ulisumbua sana  kabla na baada ya kuja kwa yesu, sasa hivi imebaki historia tu.

                                                               STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0769846183/0653095635